Jamii IntelligenceSerious reports & Discussions on Corruption, Politics etc recommended to our clients! Detailed discussions which you need not to miss
Mbunge wa Igunga na Mweka hazina wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, hatimaye amejibu rasmi madai mazito yaliyotolewa na Reginald Mengi kuhusu "mafisadi papa". Tamko hilo rasmi linapatikana katika ukurasa wa 6 wa gazeti la 'The Citizen' la leo Alhamisi, tarehe 30 Aprili 2009. Wakati tunamsubiri nakala yake tupate dondoo hii kutoka kwenye hitimisho la tamko hilo:
"I am therefore calling upon Mr. Mengi to either surrender whatever evidence he has to support his wild accusations and to appoint the appropriate legal bodies or state organs to act accordingly. Alternatively he is it to apologize to me personally within 48 hours, failing all of which, I reserve the right to exercise any appropriate actions in order to expose his wrongdoings"
Wakati huo huo gazeti hilo linaripoti kuwa mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji, yeye ameshachukua hatua ya kufungua kesi dhidi ya Reginald Mengi ambapo anadai fidia. Maswali ya msingi ya kujiuliza ni : Je, katika mpambano huu ile methali ya "wapiganapo tembo nyasi huumia" itatimia au nyasi ndio zitapata fursa ya kustawi zaidi? Je, mpambano huu utaishia kuwa mchezo wa kuigiza au utazitimizia hizo nyasi methali ya "avumaye baharini papa kumbe wengi wapo"?
TAMKO LAKE HILI HAPA:
__________________
"Each generation must, out of relative obscurity, discover its mission, fulfil it, or betray it"/Kila kizazi, katika utata wa kipindi chake, lazima kiutambue wajibu wake na kiutekeleze au kiusaliti - Frantz Fanon
Last edited by Invisible; 30th April 2009 at 11:36 AM..
Reason: Enclosed the doc
Ni TANZANIA TU, HUWA HAIWASHTAKI WATU, LA INASUBIRI MTU ALIYEAMBIWA MWIZI NDIYE AENDE MAHAKAMANI!!!
wote mnaotaka wezi waende kushtaki mahakamani, ni kipimo tosha kuwa hamna la kuwafanya mafisadi! na haya ni mawazo mabaya kabisa,
Mengi alitakiwa aende mahakamani! la akae kimya, maana hakuwa na jipya, pili tabia hii ni sawa na kuwapiga mawe vibaka, tunaposema utwala wa sheria nadhani JF tuwe tunaongoza, tunapokuwa na double standard, kuna siku tutaULIZWA!
Waberoya,
Tumeeleza mara nyingi kwa nini hatuendi mahakamani. Aidha huelewi au hutaki kuelewa kwa sababu unazoelewa mwenyewe. Kesi ya Uwizi ni kesi ya Jinai, na hivyo anayelalamika anayotakiwa ni kutoa taarifa polisi na kesi inageuka kuwa ya Jamhuri na aliyetoa taarifa anabaki kuwa shahidi. Tumeeleza mara nyingi kuwa iwapo utapeleka polisi ndio wanaoamua kuipeleka kesi hiyo mahakamani lini au hata kutoipeleka kabisa. Kwa msingi huo kesi hizi, mahakama yake ni wananchi, kwani pressure ya wenye mali yaani raia ndio inayosukuma kesi hizi kupelekwa mahakamani. Nadhani sasa unaelewa kwanini wanaotuhumu hawaendi mahakamani, na wewe na wale wote wanaoshikilia msimamo huo watakuwa wameelewa. Mahakama ya wananchi ndio njia pekee kwa tuhuma hizi kuweka pressure kwa Serikali, kwani vinginevyo kunakukingiana kifua kama wote mnavyojua.

Kuna watu sijui wamepewa posho kumtetea huyu jamaa!!! Maana hivi vitu viko wazi kabisa....Mengi has mislead Tanzanians na alipaswa aanzie kwanza mahakamani afu aje kutuambia kuwa amekabidhi ushahidi unaowatuhumu watu 10 kuwa mafisadi papa...na yeye atakuwa SHAHIDI wa kwanza, then aombe wengine wenye ushahidi kama wake wakijitokeze. Badala yake kaanza kuhukumu eti mwenye kosa ndo akashtaki, je wananchi wenye hasira wakimsubiri barabarani kwa mawe si atafia njiani kabla kujitetea???....Hatutaki utaratibu wa kihuni kama huo, mbona humu ndani watu hufungiwa kwa kuvunja baadhi ya kanuni??? Hapa bwana tutakesha hadi mtie akili waendelee kuwapa hizo posho za sitting allowance....ukweli utabaki pale pale nao ni KUHESHIMU UTAWALA WA SHERIA.
__________________
:twisted: Become like your enemy to deceive your enemy
Mkuu nafikiri umemsikia Prof. Lipumba alivyompa somo Mengi, vp alitakiwa afanye na siyo ku behave kama "juha" au punguwani vile vyombo vya kushughulikia mambo hayo si vipo, angelikwenda TAKUKURU akawapa ushahidi na vielelezo vya madai yake, kama hatua singelichukuliwa ndo angekuja akawambia watu kupitia vyombo vya habarik, tungemuelewa.
Na kutoa maoni ni haki ya kila mtu lakini ina taratibu zake,zinafahamika, si kila maoni yoyote yanasemwa popote, kama Mengi angelijua pa kusemea maneno yake(on the right forum) asingelaumiwa na yeyote.
Hivi wewe na GT mnalipwa na nani?Ulikunywa maji ya bendera nini?Au na wewe ni wale wale wliotoka tabora kuja maelezo,au mwenzetu unatumia komputa ya RA?Mbona unakuwa mwingi wa kutetea bila kuchambua hoja?Nna hasira ya watu kama nyie mnaotupotezea muda humu ndani kuchangia tapu tapu.Ushaambiwa mkuu wa TaKOKUU alikuwamo RichadMonduli,Yule Felesi ndo wale wale,UWT walimklia RMond,Mkululu kawa Bubu,HIVI WE NANI#%6§
Kipengele cha Tano cha kanuni za JF
"Kutoa maelezo au shutuma dhidi ya mwanachama mwenzako, kiongozi wa au watu wenye hadhi kijamii bila kuwa na ushahidi wa kutosha kwa lengo la kuchafua rekodi safi ya mhusika kijamii."
Sasa kama Mengi angekuja humu ndani angepewa adhabu gani. Tuache kula matapishi yetu jamani...Huyo Mzee wenu kakosea mikakati yake. Hata hapa kwetu angeshughulikiwa au hii kanuni nayo haitekelezeki??? Watu wengine wabishi tu ila ukweli wanao.
__________________
:twisted: Become like your enemy to deceive your enemy
Fair point.
Inamaana leo hii nikija kumwuiba yule ng'ombe wako uliye mfunga kule malishoni na ukanione na pepea na ng'ombe wako ,kwa mtanzamo wako wewe itakubidi utafute organ husika ikupe mamlaka ya kuniita mwizi wa ng'ombe wako ?????????????
Na ukmenikamata na ng'ombe wako hivyo huruhusiwi kuniita mwizi kwa sababu huna mamlaka hayo maana vinginevyo nitakushitaki????????????
hakuna chombo kinachotoa ruhusa hiyo ila ni ushaidi ulionao ndio utabainisha.
Mengi kama mtanzania kaibiwa pesa zake na wezi wake anawafahamu kwa sababu anaushaidi wa kutosha hivyo mwacheni atatoa ushaidi gani jinsi fisadi papa lilivyopapua fedha.
Kama hana huo ushaidi ama hakumuona mwizi akikwapuwa ng'ombe hiyo basi itakuwa stori nyingine.
Ndio maana yake ,Na unaona watu wakimpa kisago mwizi kwa ujumla na sio alieibiwa pekee ,na wakati mwengine hata alieibiwa hajulikani baada ya mwizi kuuliwa,tabu anayoipata Mengi ni kujitenga na jamii na kujaribu kumpiga mwizi kwa kutumia zana zake kwa maana nyingine ,serikali imemwona kuwa yeye ndie aliempiga mwizi na kumsababishia maumivu makali wakati angeliweza kupeleka ushahidi wake katika vyombo husika au Mengi hana imani na vyombo vya serikali kama akina Slaa ?
Mafisadi wamo ndani ya serikali hivyo vita hii haitaki mmoja mmoja kupambana nakumpiga mwizi ni lazima kupatikane ujumla kwa maana wananchi wote waungane ili kuwafukuza wezi hawa na kuwaua na hivyo serikali na akina Sophia hawatakuwa na ubavu wa kusema Mengi amekiuka sheria kwa kujichukulia hatua mikoni mwake.
__________________
Light travels faster than sound. This is why some people appear bright until you hear them speak.
Unataka tuwatetemekee mabwana wako 'Watanzania wenye asili ya kiasia' ndani ya nchi yetu?
Kojozi bado unapigana na kivuli chako kwa maana inaonyesha na wewe unataka tumkubali bwana wako mwenye asili ya Msumbiji kwa kuvunja na kuvuruga sheria ?
__________________
Light travels faster than sound. This is why some people appear bright until you hear them speak.
Jamani mbona mnashindwa kuconnect the dots. Huu ubavu wa Manji kwenda mahakamani kufungua kesi na hii sasa ya Rostam kutoa vitisho wanaupata wapi ? Jibu liko wazi - ni baada ya Sophia na Mkuchika kuiingiza serikali ya Jamhuri kwenye utetezi wa mafisadi. Hawa wawili ni mawaziri - je walitumwa ? Je ni uchungu wa mwana, aujuaye baba ?
Usemi wa Rostam umenikumbusha ule wa waziri moja anayeitwa Masha, aliyeamua kumshughulikia Mengi na kutoa siku saba - sasa naye Rostam katoa masaa 48. Huu ni muda mwafaka wa kujipanga kuingia vitani - ama upo upande wa mafisadi au dhidi yao - wazungu husema, the daggers are drawn, na sasa hakulaliki mpaka kieleweke, mafisadi kaeni chonjo.
Mafisadi wameiweka serikali nzima ya CCM mfukoni.
Mzee do not underestimate RA, ni mhuni, mtoto wa mjini, tajiri ,anjeng hoja, wala hategemei mtu yeyote, RA hategemei Sofia Simba! kama humjui kamuulize salmin Amour! enzi zake ameshakuwa kama Zito vile!
Nadhani ifike wakati tu serikali itoe tamko kuwa haitawashtaki, na watu wachukue sheria mkononi, hii sema, sema hii , haina kitu !
__________________
‘’I have come to the conclusion that politics are too serious a matter to be left to the politicians’’. Charles De Gaulle (1890 - 1970)
Katika nchi ambayo sheria hufuatwa tu kama mdogo na mnyonge kakosea, kufuata sheria kumhukumu mkubwa na mwenye nguvu ni ujinga.
Mkubwa anaua hadharani mchana kwa kumpiga mtu risasi ya kichwa huku akihatarisha usalama wa raia wengi wema, lakini bado polisi wanashindwa kuchukua hatua kwa kisingizio cha kukosa ushahidi mpaka Mungu mwenyewe aingilie.
Mkubwa anajiuzia Kampuni ya kuchimba madini kwa bei ya kutupa kwa kutumia madaraka yake, kila mtu anagwaya hata kumtaja jina. Polisi ndo kabisaa wako kimya na mikia yao wamefyata. Rais wa nchi anasema Tumuache apumzike baada ya kuiba kwa muda mrefu.
Ndiyo hakuna msafi.
Wako wanukao jasho japo mashati yao yaonekana masafi.
Wako walao siku zote na kamwe hawaoshi mikono yao.
Wako walo jipakaa michuzi na mabaki ya chakula kwenye mashati yao na kutoa shombo kali.
Wako wasopiga mswaki.
Wako walojipakaa matope bokoboko ya kunuka hata rangi za mashati yao hazijulikani.
Lakini wako walojipakaa mavi, mikojo na aina zote za uchafu na midomo mwao wamejaa maneno ya ufedhuri. Hawa wakiambiwa wachafu wakaoge, radi za masika hutoka midomoni mwao na hawakubali kuoga kuogeshwa wala nini, watafanya kila njama ili kila mmoja anuke kama wao japo hana shombo.
Watu wachafu wa kunuka,wakijuacho ni kuchafuka na kunuka tu.
Kwa kutumia uchafu waliojilimbikizia kwa muda mrefu hujenga ngome imara na kujificha ndani yake, ili kila msasi awasakaye tunduni mwao achafuke na kunuka kama wao na hatima yake iwe kushindwa kwa jamii ya Tanzania kutofautisha Msasi na Msaswa(Prey and Predator).
Wachafu wako wengi lakini wapo walochafuka zaidi.
__________________
Jamii ya Kitanzania itazidi dumu mkiani kwa kuenzi UTEGEMEZI.Maendeleo ya kweli yatakuja Tanzania kwa KUIMARISHA UWEZO WETU WENYEWE na kufuta kabisa tabia ivizayo ya kuOMBAOMBA
Last edited by Madela Wa- Madilu; 30th April 2009 at 11:44 PM..
Kuna watu sijui wamepewa posho kumtetea huyu jamaa!!! Maana hivi vitu viko wazi kabisa....Mengi has mislead Tanzanians na alipaswa aanzie kwanza mahakamani afu aje kutuambia kuwa amekabidhi ushahidi unaowatuhumu watu 10 kuwa mafisadi papa...na yeye atakuwa SHAHIDI wa kwanza, then aombe wengine wenye ushahidi kama wake wakijitokeze. Badala yake kaanza kuhukumu eti mwenye kosa ndo akashtaki, je wananchi wenye hasira wakimsubiri barabarani kwa mawe si atafia njiani kabla kujitetea???....Hatutaki utaratibu wa kihuni kama huo, mbona humu ndani watu hufungiwa kwa kuvunja baadhi ya kanuni??? Hapa bwana tutakesha hadi mtie akili waendelee kuwapa hizo posho za sitting allowance....ukweli utabaki pale pale nao ni KUHESHIMU UTAWALA WA SHERIA.
Nadhani hukumwelewa Dr Slaa,tafadhali soma kwa mara nyingine tena labda utaweza kuelewa.
__________________ Res Ipsa Loquitur- "Our POVERTY is the EVIDENCE to the NEGLIGENCE of OURLEADERS" The facts speaks for themselves.
Waberoya,
Tumeeleza mara nyingi kwa nini hatuendi mahakamani. Aidha huelewi au hutaki kuelewa kwa sababu unazoelewa mwenyewe. Kesi ya Uwizi ni kesi ya Jinai, na hivyo anayelalamika anayotakiwa ni kutoa taarifa polisi na kesi inageuka kuwa ya Jamhuri na aliyetoa taarifa anabaki kuwa shahidi. Tumeeleza mara nyingi kuwa iwapo utapeleka polisi ndio wanaoamua kuipeleka kesi hiyo mahakamani lini au hata kutoipeleka kabisa. Kwa msingi huo kesi hizi, mahakama yake ni wananchi, kwani pressure ya wenye mali yaani raia ndio inayosukuma kesi hizi kupelekwa mahakamani. Nadhani sasa unaelewa kwanini wanaotuhumu hawaendi mahakamani, na wewe na wale wote wanaoshikilia msimamo huo watakuwa wameelewa. Mahakama ya wananchi ndio njia pekee kwa tuhuma hizi kuweka pressure kwa Serikali, kwani vinginevyo kunakukingiana kifua kama wote mnavyojua.
Mh. ulipotoa ile list pale MY, ulikuwa na vithibitisho, na hata wale waliokuona unakosea baadae walikubali kuwa umesema sahihi, Kwa kifupi katika historia ya kupigana na ufisadi vizazi vyote vijavyo lazima vitalitaja jina lako!
Ishu ya Mengi ni tofauti kabisa na yako!, kasema kama yuko kijiweni! wakati kumbuka kwa nafasi na uezo wake angeweza kwenda mbali kabisa! najua CHADEMA mnatetea Mengi, wasiwasi wangu na wazo langu ni kuwa hajafanya jipya! amesema kitu ambacho kila mtu anajua, swali ni kuwa kasema kwa manufaa ya nani?? PERSONAL ISSUES AU??
PILI MH.katika list yako hukumkwepesha JK, Mengi yeye anataka kutuonyesha kuwa JK ni safi ila hawa wengine ni wachafu!!!!!!!!!! which will never be true! na logically haiingii akilini! JK ana usalama wa taifa, Jeshi n.k, anauwezo wa kumaliza ufisadi akitaka, ngau kwa asilimia 90% tukaacha ufisadi wa mamesenja nawafagizi!
Mahakama ya wananchi ni hipi hiyo? pressure?? RA angekuwa amekimbia nchi kwa jinsi anavyosemwa! lakini PIA NA SISI WENYEWE TUNAENDA KUMPA POLE, WENGINE WANATANDIKIWA MAZURIA MARA WANAPOTUHUMIWA UFISADI! so they can not feel that pressure, never In Tz!
Na hii ni changamoto hata kwa CHADEMA, kuwa kuna haja ya kubadilisha mitazamo kuhusu kupigania haki ya taifa, watu bado wamelala! na mmoja wao Mengi! kama kwa nguvu aliyonayo akiishia kusema kama mimi! amesaidia nini??.
Mh. mimi niko tayari kwa lolote hasa CCM wote waondoke madarakani.
I am sick and tired pale mnapojifanya kuwasifia baadhi ya watu kama akina Mwakyembe, Mwandosya, n.k wote hawa wachafu TU! n wanaishi kwenye dampo linaloitwa CCM
__________________
‘’I have come to the conclusion that politics are too serious a matter to be left to the politicians’’. Charles De Gaulle (1890 - 1970)