Makamba amwinda Mengi, yeye awataja mafisadi rasmi! - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Jamii Intelligence


Jamii Intelligence Serious reports & Discussions on Corruption, Politics etc recommended to our clients! Detailed discussions which you need not to miss


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 23rd April 2009, 07:10 PM   #1
Makamba amwinda Mengi, yeye awataja mafisadi rasmi!
Bubu Ataka Kusema Bubu Ataka Kusema is offline 23rd April 2009, 07:10 PM

Makamba amwinda Mengi
  • Ahoji safari za mikoani

Mwandishi Wetu Aprili 22, 2009
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

HUKU kukiwa na shinikizo la kutaka kumuondoa katika nafasi yake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, mwanasiasa huyo machachari, ametajwa sasa kumfuatilia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.

Makamba ameelezwa kupendekeza ndani ya vikao vya chama hicho kuchunguzwa kwa uhusiano wa Mengi na wanasiasa waandamizi wa CCM wakiwamo wabunge, wengi wao wakiwa ni wale wanaofahamika kwa kuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi.

Habari za ndani ya vikao vya juu vya CCM vilivyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na baadaye mjini Dodoma, zinaeleza kwamba Makamba alitoa hoja hiyo katika vikao vya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM na katika Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho tawala.

Wakati Makamba akiwasilisha hoja hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alikuwa mmoja wa wageni wazito walioshiriki sherehe za miaka 75 ya kuzaliwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Mtera, John Malecela, mahali ambapo anaelezwa kusifia juhudi za wabunge wanaopinga ufisadi.

Miongoni mwa wabunge ambao Makamba anahisi wanaivuruga CCM wakiungwa mkono na Mengi ni pamoja na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, ambaye pamoja na kupongezwa na Kikwete kupata zawadi ya mwanamke shujaa, alikuwa mmoja wa washiriki wa sherehe ya kuzaliwa mumewe mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Makamba anadaiwa kuhoji sababu ya Mengi kuingilia mambo ya CCM kwa kushirikiana na baadhi ya wanasiasa wa ndani ya chama hicho, hali ambayo Katibu Mkuu huyo wa CCM anaielezea ndani ya vikao kama inaashiria hatari kwa chama hicho siku za usoni.

Hatua ya Makamba kumgusa Mengi katika vikao rasmi vya chama, vimeelezwa kuwa sehemu ya mkakati maalumu wa kupunguza kasi kubwa ya mfanyabiashara huyo kuonekana akishirikiana na baadhi ya wabunge katika baadhi ya shughuli mbalimbali za kijamii, huku wakibainisha wazi kumuunga mkono Rais Kikwete.

Ingawa haijawekwa bayana lengo hasa la mapendekezo ya Makamba ni kuhoji pia hatua ya hivi karibuni ya Mengi kutoa misaada ya fedha kwa ajili ya kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii kujiinua kiuchumi katika baadhi ya majimbo ya wabunge mbalimbali wa CCM bila kuyahusisha makao makuu ya chama hicho.

Mengi pia amekuwa mstari wa mbele katika vita ya ufisadi, vita ambayo inaungwa mkono na baadhi ya wabunge wa CCM akiwamo Anne Kilango - Malecela, ambaye hivi karibuni alitunukiwa Tuzo ya Mwanamke Jasiri na Serikali ya Marekani, kupitia ubalozi wake nchini.

Hata hivyo, habari zinaeleza kwamba hatua hiyo ya Makamba ni mkakati wa kujihami ama kulipiza kisasi kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wakiwamo wabunge wanaopinga ufisadi ambao wamekuwa wakitaka kiongozi huyo kuondolewa katika nafasi yake kutokana na kushindwa kukisaidia chama hicho.

Tayari Makamba alitengwa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini, ambako CCM ilishinda baada ya kuelezwa kwamba kiongozi huyo wa CCM alikuwa chanzo cha chama hicho kushindwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime.

Imefahamika kwamba sasa hata uchaguzi mdogo wa jimbo la Busanda, Makamba hatoshiriki kikamilifu, kukitolewa sababu kwamba ana majukumu mengi ya kitaifa na sababu nyingine za kiafya. CCM wanatarajiwa kumteua Lolesia Bukwimba, kuwania ubunge jimbo la Busanda.

Hayo yakiendelea, huko Mbeya, hali si shwari ndani ya chama hicho baada ya kuwapo mtafaruku miongono mwa viongozi wa CCM katika wilaya hiyo.

Katika moja ya matoleo yake, Raia Mwema ilikuwa na makala yenye kuelezea tahadhari iliyotolewa na wananchi wilayani Kyela kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu mwenendo wa kisiasa wilayani humo, sasa imedhihiri kwamba kilio cha wananchi wale kilikuwa ni cha kweli na kilipaswa kufanyiwa kazi na si kupuuzwa kama ilivyojidhihirisha.

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilayani Kyela sasa wamefikia hatua inayoipeleka wilaya hiyo kwenye machafuko makubwa zaidi, kwani kitendo cha makatibu kata wanne wa Chama hicho kuwavamia viongozi wao wa Kamati ya Maadili ya Wilaya hiyo na kuwapiga wakitumia mateke na ngumi, kinazidi kuongeza chumvi kwenye kidonda.

Makatibu kata hao wanne wanaodaiwa kuwatwanga viongozi wao ni pamoja na Josephat Mwakajinga kutoka kata ya Kajunjumele, Grayson Mwaikambo wa kata ya Kyela mjini, Alex Mwaisombwa wa kata ya Lusungo na Ipyana Mwangunga ambaye ni Katibu Mwenezi wa kata ya Makwale

Hali ya kimazingira inaonyesha kuwa vurugu hizo zilimlenga zaidi Katibu wa Chama hicho wilayani Kyela, Maria Mwambanga ambaye kwa mujibu wa mjumbe mmoja wa Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, inaelezwa kuwa wanataka kumuondoa kwa madai kuwa yuko upande wa Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Harrison Mwakyembe.

Pamoja na madai hayo kuna taarifa vile vile kuwa Katibu huyo hatakiwi na baadhi ya viongozi wa chama hicho wilayani humo kwa madai kuwa hashindi ofisini na muda mwingi amekuwa akiutumia jijini Mbeya, hivyo kuunda genge la kumuondoa kwa nguvu.

Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kyela, Japheth Mwakasumi anaelezea kushangazwa kwake na hatua ya makatibu kata hao kumvamia na kumpiga Mtendaji Mkuu wa Chama wilayani humo kwa madai yasiyo na kichwa wala miguu.

“Dhamira yao wanataka mtu anayepokea mawazo yao, hapo ndipo ninaposhindwa kuwaelewa kwani si unayaleta kwenye vikao, ni wazi kuwa there is someone behind, maana miongoni mwa madai yao ni kwamba Katibu ni mtu wa Mbunge, kwa kweli siwaelewi,” anaelezea kwa masikitiko Mwenyekiti huyo katika mahojiano maalumu na Raia Mwema.

Akizungumzia hali ya Katibu wake anasema sio nzuri na kwamba anaendelea na matibabu ikiwemo kupigwa picha.

“Wee unafanya mchezo midume mizima inamshambulia mwanamke, hapana tumefika pabaya kama siasa zenyewe ndio hizi za majungu yasiyo na kichwa wala miguu halafu mnamshambulia mwamamke asiye na hatia,” anazidi kushangaa Mwenyekiti huyo.

Aidha akizungumzia kinachoendelea ndani ya Chama hicho, Mwakasumi alisema kuwa Kamati ya Siasa ya Wilaya itaketi kesho Alhamis kulijadili suala hilo na kutoa maamuzi.

Hata hivyo, duru za ndani ya chama hicho wilayani humo zinabaisha kwamba vurugu hizo zilizosababisha Katibu huyo wa Wilaya kuumizwa vibaya, zinafadhiliwa na mmoja wa madiwani wilayani humo na kiongozi wa moja ya jumuiya za chama hicho mkoani Mbeya.

Ni wazi kwamba kwa taarifa hizo ni kwamba kuna kila dalili ya kuwepo kwa kambi mbili zenye mielekeo tofauti ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani.

Katika mahojiano na baadhi ya viongozi wa juu wa Chama hicho katika Wilaya ya Kyela pamoja na mkoani, wanazihusisha vurugu hizo moja kwa moja na harakati za kampeni za uchaguzi ujao mwakani na kwamba mbinu inayotumiwa na wafanya vurugu hao katika kukabiliana na Mbunge aliyepo haitofautiani na ile iliyotumika katika uchaguzi uliopita, kumtenganisha na uongozi wa juu wa chama hicho wilayani humo.

Katika mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, viongozi wa juu wa wilaya wa Chama hicho hawakumtaka kabisa Mbunge wa sasa na badala yake waliegemea kwa Mbunge aliyekuwapo madarakani wakati ule, na hata Dk. Mwakyembe aliposhinda kwenye mchujo huo bado viongozi hao hawakumpa ushirikiano hivyo kutegemea zaidi nguvu ya wapiga kura ambako hadi sasa ndiko nguvu yake iliko.

Inaelezwa kuwa vurugu hizo za Jumamosi iliyopita zilitokea kwenye Kikao cha Kamati Maadili kilichoitishwa maalumu na kwa ajili ya kuwahoji baadhi ya makatibu kata, pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya hiyo, Visk Mahenge wanaotuhumiwa kuhusiana na vurugu zilizosababishwa na baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama ya Wilaya hiyo Machi 31, mwaka huu.

Pamoja na tuhuma hiyo, Mwenyekiti wa Chama hicho Wilayani Kyela, Mwakasumi anaitaja tuhuma nyingine iliyokuwa wahojiwe makatibu hao ni kwa baadhi ya makatibu hao kudaiwa kuendesha kikao chenye mlengo wa kampeni za uchaguzi mwakani huku kikihusishwa na utoaji posho nje ya taratibu za chama hicho.

Wakizungumzia suala hilo la kampeni viongozi wa Chama hicho mkoani hapa walibaisha kuwa wanaelewa kuwepo kwa kampeni zinazoendelea chini kwa chini, lakini wakasisitiza haziwezi zikahalalishwa kuudharau uongozi uliopo madarakani kwani kwa kufanya hivyo ni kuruhusu vurugu na matumizi ya rushwa.

Mmoja wa viongozi wa chama hicho mkoani hapa alifikia hatua ya kusema, “Kinachonisikitisha ni hatua ya baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali kuchochea vurugu ndani ya chama wilayani Kyela, Katibu anatekeleza wajibu wake kwa kufuata kanuni na taratibu za chama zilizopo, hawezi kutoshirikiana na Mbunge wa jimbo la wilaya yake, hata kama mbunge ni kutoka chama cha upinzani bado angeshirikiana naye, ila tu asingeruhusiwa (mbunge wa upinzani) kuingia kwenye vikao vyetu vya chama, lengo ni maendeleo kwa wananchi na sio watu binafsi.”

Moja ya matatizo yanayozikabili siasa za mkoa wa Mbeya ni kwa baadhi ya wanasiasa kuendelea kuishi katika ndoto za mtandao uliomwingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete, wakiamini kwamba bado unazo nguvu zile zile za mwaka 2006 kurudi nyuma.

Pamoja Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Nawab Mulla kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akielezea kuchukuliwa kwa hatua za nidhamu kwa waliosababisha vurugu hizo iwapo suala hilo litatuliwa nje ya mahakama, baadhi ya wanachama wameelezea kupingana naye katika hilo kwa maelezo kuwa Chama hicho siku hizi hakina uwezo huo wa kuwajibishana.

Wanautaja mgogoro ulioibuka kwenye kikao kimoja cha CCM Mkoa ambapo kiongozi mwanamke alitaka kumvalisha sidiria kiongozi mwenzake mwanaume kwa madai kwamba anaingilia mambo ya wanawake, lakini duru za kisiasa mkoani humo zikidai kuwa sababu hasa ni kutoungwa mkono kwenye kampeni zake kuwania uongozi wa juu wa chama hicho kwenye moja ya jumuiya zake.


Quote:
View Post
Au ndio maana na Mengi leo kaamua kuwalipua mafisadi? Maana nasikia kwenye Press conference yake amewataja akina Rostam, Jeetu, Somaiya na Manji kuwa ndio mafisadi wakuu nchini
Quote:

Alichokiongea Mengi:

``Our country is currently facing a huge problem of corruption and is troubled by the fact that the people involved in acts of corruption do not what to be touched.
The resolve by our President, His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, to fight corruption and all other evils has shaken these people and they are now determined more than ever to combat all the people who are supporting the President in stopping further plunder of our country`s resources.

``Tanzanians should know that people who are being accused of being corrupt in our country do not exceed ten, and out of the ten, five are being accused of being notoriously corrupt - ``corrupt sharks``.

``These are: Rostam Aziz, Tanil Somaiya, Yusuf Manji, Jeethu Patel and Subash Patel.

These people are being accused of stealing billions of public money, and to make this worse, the billions have been transferred out of the country.

``These notoriously corrupt people are involved in almost all scandals that have happened in our country, including those concerning Richmond, EPA, Dowans, Army helicopters and vehicles, the Presidential Jet, Radar, NSSF, PSPF, National Lottery etc, etc.

``The great efforts of His Excellency the President to hasten economic development and better living for every Tanzanian are weakened by the horrendous theft of national resources.

A great majority of Tanzanians still face extreme poverty; they are unable to determine where the one meal a day is going to come from.

To make things worse, where a Tanzanian with better means provides assistance to lessen hardship within the society and to eradicate poverty, these people involved in corruption allege that such assistance has political agenda. They want Tanzanians to starve or die as a result of other problems.

``It seems that their aim now is to cause national havoc; it will not be surprising to learn that these people support what is behind DECI while Tanzanians remain chasing Pastors instead of asking themselves the real source of the havoc.

``These notoriously corrupt people are not only stealing our national resources; they are also stealing our precious time.

Instead of using our time for economic development we are using most of it to combat corruption.

``Our efforts have failed to even cause a dent; instead these corrupt people have been hardened in their determination.

They have established newspapers that are abusive and treat Tanzanians with contempt.

``They have created a scenario where the thief chases and attacks the person from whom he has stolen.

Even as Tanzanians continue to cry foul, the notoriously corrupt people continue to use their ill-obtained wealth to influence the granting of big contracts to them often in different names.

``Millions of Tanzanians are combating corruption, but there are a few who have come forward vehemently and are known by their names.

The notoriously corrupt people have been heard to say that they will annihilate these vehement combatants.

``The notoriously corrupt people should know that if the combatants are harmed in any way in this country or any other country, they will be answerable to the people of Tanzania.

``We Tanzanians must now ask ourselves - what gives these notoriously corrupt people the audacity to treat Tanzanians with contempt?

``I would like to conclude by saying that all corrupt people and especially those who are being accused of notorious corruption must be dealt with conclusively, otherwise they will rock the stability of our nation. We must realise that we have now reached the stage when we must say enough is enough.``
Videos:



__________________
~*~Life is Good~*~

 
Bubu Ataka Kusema's Avatar
Bubu Ataka Kusema
JF Premium Member
Points: 12,625,589, Level: 100 Points: 12,625,589, Level: 100 Points: 12,625,589, Level: 100
Activity: 67% Activity: 67% Activity: 67%
Join Date: Sun Feb 2007
Location: Mfaranyaki
Posts: 12,577
Thanks: 990
Thanked 1,129 Times in 655 Posts
Views: 14295
Reply With Quote
  #2  
Old 23rd April 2009, 07:15 PM
Bluray's Avatar
Bluray Bluray is offline
Bluray is the one talked about by the fashion bloggers
JF Senior Expert Member
Points: 224,597, Level: 100 Points: 224,597, Level: 100 Points: 224,597, Level: 100
Activity: 4% Activity: 4% Activity: 4%
 
Join Date: Tue Mar 2008
Posts: 3,453
Thanks: 55
Thanked 948 Times in 514 Posts
Rep Power: 29
Bluray will become famous soon enoughBluray will become famous soon enoughBluray will become famous soon enoughBluray will become famous soon enoughBluray will become famous soon enoughBluray will become famous soon enoughBluray will become famous soon enoughBluray will become famous soon enough
Default Re: Makamba amwinda Mengi

Makamba is a disgrace, of feeble mind, senile, and now like an unimaginative comedian out of jokes, is shooting himself in the foot, continuously, repeatedly.

His only salvation is the personal relationship he has with that other loser,Kikwete.

It is only a matter of time before they are both exposed for the corrupt failures that they truly are.
Reply With Quote
  #3  
Old 23rd April 2009, 07:57 PM
Mpita Njia Mpita Njia is offline
Mpita Njia has no status.
JF Premium Member
Points: 738,469, Level: 100 Points: 738,469, Level: 100 Points: 738,469, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Mon Mar 2008
Posts: 3,143
Thanks: 79
Thanked 89 Times in 58 Posts
Rep Power: 29
Mpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enough
Default Re: Makamba amwinda Mengi

Au ndio maana na Mengi leo kaamua kuwalipua mafisadi? Maana nasikia kwenye Press conference yake amewataja akina Rostam, Jeetu, Somaiya na Manji kuwa ndio mafisadi wakuu nchini
Reply With Quote
  #4  
Old 23rd April 2009, 08:06 PM
Mzee Mwanakijiji's Avatar
Mzee Mwanakijiji Mzee Mwanakijiji is online now
Mzee Mwanakijiji anawashangaa wanaoitetea sheria mbovu
JF Premium Member
Points: 12,793,973, Level: 100 Points: 12,793,973, Level: 100 Points: 12,793,973, Level: 100
Activity: 90% Activity: 90% Activity: 90%
 
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 18,271
Thanks: 7,904
Thanked 4,237 Times in 1,187 Posts
Rep Power: 44
Mzee Mwanakijiji is on a distinguished roadMzee Mwanakijiji is on a distinguished road
Send a message via MSN to Mzee Mwanakijiji Send a message via Skype™ to Mzee Mwanakijiji
Default Re: Makamba amwinda Mengi

Quote:
View Post
Au ndio maana na Mengi leo kaamua kuwalipua mafisadi? Maana nasikia kwenye Press conference yake amewataja akina Rostam, Jeetu, Somaiya na Manji kuwa ndio mafisadi wakuu nchini
eh.. alikuwa na press conference?
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Reply With Quote
  #5  
Old 23rd April 2009, 08:16 PM
Kakalende's Avatar
Kakalende Kakalende is offline
Kakalende just around
JF Senior Expert Member
Points: 429,306, Level: 100 Points: 429,306, Level: 100 Points: 429,306, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Fri Dec 2006
Location: Itoma
Posts: 1,141
Thanks: 26
Thanked 33 Times in 17 Posts
Rep Power: 26
Kakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enough
Default Re: Makamba amwinda Mengi

Quote:
View Post
Au ndio maana na Mengi leo kaamua kuwalipua mafisadi? Maana nasikia kwenye Press conference yake amewataja akina Rostam, Jeetu, Somaiya na Manji kuwa ndio mafisadi wakuu nchini
MN hebu malizia kuhusu hiyo press conference, alizungumzia nini hasa?
Reply With Quote
  #6  
Old 23rd April 2009, 08:22 PM
Kituko Kituko is offline
Kituko has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 87,723, Level: 100 Points: 87,723, Level: 100 Points: 87,723, Level: 100
Activity: 23% Activity: 23% Activity: 23%
 
Join Date: Mon Jan 2009
Posts: 980
Thanks: 42
Thanked 145 Times in 107 Posts
Rep Power: 23
Kituko will become famous soon enoughKituko will become famous soon enoughKituko will become famous soon enoughKituko will become famous soon enoughKituko will become famous soon enoughKituko will become famous soon enoughKituko will become famous soon enoughKituko will become famous soon enough
Default Re: Makamba amwinda Mengi

Huu ndio mwanzo wa mwisho wa ccm, mpaka sasa katibu mkuu ajuhi aanzie wapi, kwa kilango, kwa mwakyembe kwa sitta, kwa shelukindo na pia ana kazi ya kuhakikisha ni kikwete pake yake ndio anasimama kwa uraisi bila kuwa na upinzani wa maana.

Kwa kweli hii kazi ni ngumu sana kwa makamba hipo juu ya uwezo wake
Reply With Quote
  #7  
Old 23rd April 2009, 08:30 PM
Mpita Njia Mpita Njia is offline
Mpita Njia has no status.
JF Premium Member
Points: 738,469, Level: 100 Points: 738,469, Level: 100 Points: 738,469, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Mon Mar 2008
Posts: 3,143
Thanks: 79
Thanked 89 Times in 58 Posts
Rep Power: 29
Mpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enough
Default Re: Makamba amwinda Mengi

Quote:
View Post
MN hebu malizia kuhusu hiyo press conference, alizungumzia nini hasa?
Ndio, alikuwa na press conference ofisini kwake leo na ametoa statement ya kurasa mbili, nashangaa kuwa hili halijafika humu hadi saa hizi!

Katika statement yake amesema kuwa mafisadi wakubwa wanaoimaliza Tanzania hawazidi kumi. Na yeye akaamua kuwataja watano ambao amewaita 'mafisadi papa' - Rostam Aziz, Tonil Somaiya, Yusuf Manji, Subash Patel na Jeetu Patel.

Amesema hawa wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya wananchi na mbaya zaidi fesha hizo wamezihamishia nje ya nchi.

Amesema wanaotuhumiwa kuwa 'mafisadi papa' wanahusishwa na kashfa kubwa zikiwemo Richmond, EPA, Dowans, helikopta na magari ya jeshi, ndege ya rais, rada, NSSF, NSPF, bahati nasibu ya taifa, mradi wa Mchuchuma na kadhalika.

Amesena jitihada kubwa za JK kuleta maisha bora kwa wananchi zinkwamishwa na hawa.

Amesena kuna uwezekano kuwa mabwana hawa naahusika pia na suala la DECI na si ajabu wakaunga mkono matatizo yanayotokana na DECI na watanzania wabaki wakifukuzana na wachungaji bila kujiuliza ni kina nai hasa wanachochea vurugu hizi.

kwa ufupi nawasilisha
Reply With Quote
  #8  
Old 23rd April 2009, 08:31 PM
Invisible's Avatar
Invisible Invisible is offline
Invisible is around but busy!
Robot
Points: 6,287,005, Level: 100 Points: 6,287,005, Level: 100 Points: 6,287,005, Level: 100
Activity: 18% Activity: 18% Activity: 18%
 
Join Date: Sat Feb 2006
Location: Here...!
Posts: 6,043
Thanks: 503
Thanked 1,429 Times in 427 Posts
Rep Power: 100000
Invisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of lightInvisible is a glorious beacon of light
Send a message via MSN to Invisible
Default

Quote:
View Post
Au ndio maana na Mengi leo kaamua kuwalipua mafisadi? Maana nasikia kwenye Press conference yake amewataja akina Rostam, Jeetu, Somaiya na Manji kuwa ndio mafisadi wakuu nchini
Hii list ya G4 we acha tu... Kawataja directly mkuu?

I see, basi kasheshe ipo!
__________________
Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!

Thank you for supporting JF! <---(click to support us)
Waliochangia 2010: <--- (click to read)
JINSI YA KUCHANGIA JF<---(click to read)

24/7 Email SUPPORT: support@jamiiforums.com

Reply With Quote
  #9  
Old 23rd April 2009, 08:37 PM
Mzee Mwanakijiji's Avatar
Mzee Mwanakijiji Mzee Mwanakijiji is online now
Mzee Mwanakijiji anawashangaa wanaoitetea sheria mbovu
JF Premium Member
Points: 12,793,973, Level: 100 Points: 12,793,973, Level: 100 Points: 12,793,973, Level: 100
Activity: 90% Activity: 90% Activity: 90%
 
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 18,271
Thanks: 7,904
Thanked 4,237 Times in 1,187 Posts
Rep Power: 44
Mzee Mwanakijiji is on a distinguished roadMzee Mwanakijiji is on a distinguished road
Send a message via MSN to Mzee Mwanakijiji Send a message via Skype™ to Mzee Mwanakijiji
Default Re: Makamba amwinda Mengi

invisible.... wasiliana na jamaa nadhani watakuwa na audio.
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Reply With Quote
  #10  
Old 23rd April 2009, 08:38 PM
Mpita Njia Mpita Njia is offline
Mpita Njia has no status.
JF Premium Member
Points: 738,469, Level: 100 Points: 738,469, Level: 100 Points: 738,469, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Mon Mar 2008
Posts: 3,143
Thanks: 79
Thanked 89 Times in 58 Posts
Rep Power: 29
Mpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enoughMpita Njia will become famous soon enough
Default Re: Makamba amwinda Mengi

Quote:
View Post
Kawataja directly mkuu?...
Kawataja bila kumung'unya majina
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
amwinda, awataja, criminal libel, grand oruption, mafisadi, makamba, mengi, rasmi, reginald mengi, tanzania, yeye


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Mengi vs Manji: Ukweli ni upi? Mzee Mwanakijiji Jamii Intelligence 664 30th April 2009 06:43 PM
Vita Kali Ndani Ya Chadema Mtoto wa Mkulima Jukwaa la Siasa 182 17th October 2007 12:34 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 04:53 AM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com