Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

    Report Post
    Page 1 of 6 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 119
    1. #1
      Mongoiwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Posts : 478
      Rep Power : 669
      Likes Received
      51
      Likes Given
      23

      Default Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Utangulizi

      Mfanyabiashara Said Mohammed Saad anamiliki Kampuni ya Home Shopping Center iliyopo Kariakoo Mtaa wa Swahili na Msimbazi katika Jengo la Ghorofa lenye vioo vilivyochorwa picha za waigizaji wa Kikundi cha Orijino Commedy kinachorusha vipindi vyake Televisheni ya taifa ya TBC1.

      Mfanyabiashara huyu ambaye ana uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Saud Arabia, anafanya uhalifu na kuhujumu uchumi nchi kwa kushirikiana na wafanyabiashara wengine wakubwa

      Tuhuma

      Mfanyabiashara Said Mohammed ameshiriki katika matukio mengi ya kihalifu yakiwamo ya kupiga risasi watu na kesi zake zimekuwa zikifunguliwa na baadaye anazizima kwa kutoa rushwa polisi.

      Moja ya matukio hayo ni kumpiga risasi mfanyakazi wake mwaka 2005 wakati akishusha bidhaa za kuuza dukani kutoka katika gari lake, kumpiga risasi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Vingunguti, Deo Vicent Agosti 15, 2006 saa 1:00 usiku Mtaa wa Msimbazi na Swahili Kariakoo jijini Dar es Salaam.

      Mfanyakazi wake alimpiga baada ya kumbishia Said kwamba hawezi kumpiga risasi kwa sababu anajua sheria za nchi haziruhusu kufanya hivyo. Alimpiga kuonyesha kwamba yeye yupo juu ya sheria za nchi. Kesi hiyo nayo aliimaliza kimya kimya kwa kumpa hela mfanyakazi huyo na ndugu zake na polisi.

      Mtoto Vicent yeye baada ya kupigwa risasi aliliripoti Polisi na baadaye alilazwa katika Wodi namba 17 Moi kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Alipigwa risasi ya mguuni wakati akipita karibu na duka la Said baada ya mashabiki wa Simba waliokuwa wakisherekea ushindi wa timu yao kupita katika eneo hilo.

      Hata hivyo, alimaliza kesi hiyo nje ya mahakamani kwa kuwapa hela wazazi wa mtoto huyo.

      Pia anamiliki genge la Wahalifu ambalo analitumia kumlinda na kuwaadhibu wapinzani wake au maadui zake akishirikiana na mdogo wake Ghalib Mohammed Saad.

      Kundi hilo linalojulikana kama Ze Popobawa ndilo ambalo Agosti mwaka huu lilitumika kumteka nyara Mlebanoni mfanyabiashara ambaye ana duka la vitu vya ndani Mtaa wa Morogoro karibu na makutano ya barabara za Morogoro na Bibi Titi na baadaye kumwingilia kinyume cha maumbile kisha kumpeleka kwa nguvu Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kumrejesha kwao Yemen kinyume cha taratibu.

      Kisa kilichofanya mfanyabiashara huyo ambaye yupo nchini kisheria ni kumpa mimba mdogo wa Said anayeitwa Salha bila ya kuoana kama zilivyotaratibu za mila zao za Yemeni.

      Mfanyabiashra huyo wa Mlebanoni ambaye awali alikuwa rafiki yake mkubwa na Said, amemfanya tangu tukio hilo litokee kuishi kwa kujificha kwa kuhofia kufanyiwa unyama mwingine na Said ambaye anaendelea kumtisha.

      Unyama mwingine

      Baada ya kumfanyia unyama mfanyabiashra Mlebanoni , Said hakuishia hapo bali aliamua kumwadhibu dada yake Salha kwa kumpiga. kumnyoa nywele zake zote na kumnywesha vidonge ambavyo havijulikani aina yake na alimpa kwa sababu zipi?

      Salha baada ya kufanyiwa nyama huo nyumbani kwao Msasani wilaya Kinondoni aliamua kwenda kuripoti polisi kituo cha Osterbay ambako lilifunguliwa jalada la kesi namba OB/RB/13915 ambayo ilifunguliwa Agosti 5 mwaka huu.

      Hata hivyo, mbali ya polisi kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini wanashangaa tangu Salha aripoti tukio hilo, hajarudi kituoni hapo wala simu yake mkononi ambayo aliicha namba zake kituoni hapo wakati akiandikisha maelezo haipatikani, kitu ambacho kinawapa wasiwasi.

      Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye anasema huenda suala hilo wamelimaliza kifamilia. Ingawa kuna tariafa kuwa msichana huyo amewekwa kizuizini chumbani ambako haruhusiwi kutoka nje. Polisi kituo cha Oysterbay hawajafuatilia suala hilo kutokana na kupozwa kwa kupewa kitu kidogo rushwa na Said ili kuzima suala hilo.

      Ushirika wa kihalifu

      Kutokana na kushirikiana vyema katika shughuli za dawa za kulevya na kutorosha nyara za taifa wakimtumia Mfanyabiashara huyu, Said, Manji ameamua kumpa vijana wake wa Orijino Commedy kuwapa ufadhili wa kutangaza bidhaa zake anazoingiza nchini za mashuka na nguo.

      Hivi karibuni baada ya Manji kushiriki katika kuigiza mchezo wa kikundi cha Orijino Comedy kama mfanyabishara ambaye alikuwa akihitaji msaada wa kupata fedha za kufadhili Klabu ya Yanga na kuwapa wagizaji wa kikundi hicho kutumia ofisi yake kuigiza, Said naye wiki iliyofuatia aliwapa wana kikundi hicho nafasi kuingiza katika ofisi yake na kuwapa gari lake kulitumia.

      Wizi wa makontena bandarini

      1. Mfanyabiashara huyu anamiliki kampuni nyingi za Clearing and Forwarding ambazo hutumika kuiba makontena ya bidhaa anazoziingiza nchini kutoka nje na akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa TRA.

      Hata hivyo, Kampuni hizi zimefungiwa baada ya kubaini kuhusika na wizi huo wa makontena, lakini kila inayofungiwa husajili nyingine Brela akitumia majina feki.

      Kampuni ambazo zimefungiwa na TRA kwa kuhusika na wizi wa makontena zaidi ya 30 kila moja ni Mbasi Clearing and Fowarding, Clinton Clearing and Forwarding, London Freight Forwarding, Exceptional Freight Forwaders na Upland Clearing and Forwarding.

      TRA imethibitisha kuzifungia kampuni hizo kufanya kazi ya Clearing and Fowading, kwa kutumia kifungu 145 (3) cha sheria ya Jumuia ya Afrika Mashariki ya utawala wa Forodha ya mwaka 2004.

      Hata hivyo, wamekataa kutaja majina ya wamiliki wa kampuni hizo wakisema Brela ndio wenye jukumu hilo. Ingawa wamekuwa wakikubali kuendelea kumhudumia mteja huyo huyo ambaye anaiba makontena na kufungiwa kampuni zake kisha anafungua nyingine chap chap kama uyoga.

      Hata hivyo, Brela kuna kumbukumbu ya kampuni mbili tu ambazo ni London Freight Fowarders Ltd yenye usajili namba 39834 iliyosajiliwa Agosti 15, 2000 ikionyesha wamiliki wake ni Angelo Peter mwenye hisa 2000, Richard Mulenga mwenye hisa 1500 na Abdulkarim Zaharan Salim mwenye hisa 1500. Kampuni hiyo ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

      Kampuni nyingine za kwake zenye kumbukumbu Brela ni Exceptional Freight Fowarders Ltd ambayo wamiliki wake ni Lumba Nguku mwenye hisa 5,000 na Salim Suleiman mwenye hisa 5,000. Kampuni ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

      Dawa za kulevya na kutorosha nyara

      Mfanyabiashara huyu anajihusisha na uingizaji wa dawa za kulevya nchini kwa kushirikiana na mfanyabiashara Manji wakitumia kampuni zake za Clearing and Fowarding ambazo huiba makontena yenye dawa hizo yanapoingia bandarini.

      Mfanyabiashara huyu ni mmoja wa watu waliotajwa katika orodha ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya iliyowasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2006 akitajwa kama Said Abuu mfanyabiashra wa Kariakoo.

      Nyara za taifa

      Mfanyabiashara huyu amekuwa akitumia kampuni zake kusafirisha makontena yenye nyara za taifa kwenda Vietnam, Philipiness na Malaysia akishirikiana Manji na Rostam Aziz ambaye pia ni mmiliki vitalu vya uwindaji. Kampuni ya Rostam ya Uwindaji inaendeshwa na mdogo wake anayeitwa Akram.

      Ili kufanikisha mtandao wao huo wana watu wao katika sehemu nyeti za TRA, bandari, Polisi na usalama wa taifa unaowalinda kwa hali na mali.

      Utajiri wa kutisha

      Kutokana na Said kujihusisha na biashara hizo haramu kwa muda mfupi tangu mwaka 2004 alipoanza hivi sasa ana utajiri wa kutisha. Anamiliki nyumba sita eneo la Kariakoo pekee.

      1. Moja ipo Swahili na Msimbazi, Ghorofa saba ambayo ameamua kuipangisha watu sehemu ya juu, lakini TRA akidaganya kwamba ni hoteli ili kukwepa kulipa kodi. 2. Congo na Agrey ghorofa sita, 3. Uhuru mkabala na shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa bado inajengwa ni ya ghorofa, 4. Livingstone na Uhuru ipo, 5. Mkunguni Kariakoo Sokoni karibu na dula la Azam Ice Cream ghorofa sita, 6. Lumumba karibu na CCM makao makuu limepakana na Hospitali ya Burhan.
      Nchi yangu inaangamia kwa kukosa maarifa ya Viongozi

    2. RukaaJuu Final

    3. #2
      Shilinde Nicholaus's Avatar
      Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Posts : 18
      Rep Power : 360
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      aisee!
      Papizo likes this.

    4. tz1
      #3
      tz1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th March 2011
      Posts : 2,049
      Rep Power : 827
      Likes Received
      406
      Likes Given
      319

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Mongoiwe,Well done.
      Wote Jf tungekuwa tuna andika kwa ufafanuzi na uhakika namna hii Jf ingeshwa fungwa na serikali siku nyingi.
      Papizo, Mongoiwe, Yo Yo and 3 others like this.
      [email protected]

    5. #4
      Kizamani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th September 2011
      Posts : 390
      Rep Power : 467
      Likes Received
      98
      Likes Given
      3

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Du!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    6. #5
      saragossa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd January 2011
      Location : Mkunazini
      Posts : 1,411
      Rep Power : 707
      Likes Received
      344
      Likes Given
      74

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Shughuli pevu iyo! Kwa mantiki nyingine HSC ni biashara anayoitumia kusafisha hela sio?

      Je records zake zinasema hana mkopo benki yoyote?

      Mtaji wa biashara yake ambayo inaonekana ni legit, ambayo ni HSC alipata wapi?

      Idara za juu za TISS zinampango gani na mtu huyu?

      Nzowa anasemaje pia?

      Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo, ila za mwizi arobaini, lazma atanasa tu siku moja!
      Yo Yo, Ndahani, KOMBESANA and 1 others like this.

    7. Miaka 50

    8. #6
      Elisha Ray's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th March 2012
      Posts : 262
      Rep Power : 414
      Likes Received
      64
      Likes Given
      51

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      si mchezo duh!!

    9. #7
      njiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2009
      Location : ax^2+bx+c=0
      Posts : 4,956
      Rep Power : 2369
      Likes Received
      959
      Likes Given
      172

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      mhh mleta mada inaelekea unamjua sana bwana said baadhi ya habari ni kweli ila mbona bado kampuni yake inahusika na kusafirisha makontena kutoka china .. hiii hii ya home shoping center ana branch zake guanzhou na yiwu .. bwana mdogo riziwani ana shere katika hii kampuni .. kuhusu madawa ya kulevya bado sijasikia..! ila the guy he is loaded ...
      Pure Matrimony >> Purity starts here (Quran 24:26)
      My loyalty is to reason,and as a reasonable person I reserve the right to change my mind when presented with new information that alters my perspective" Njiwa"ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯


    10. #8
      Kidogo chetu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2009
      Location : DAR ES SALAAM
      Posts : 478
      Rep Power : 577
      Likes Received
      53
      Likes Given
      130

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      wacha nikagonge castle lite nimeechanganyikiwa vibaya

    11. #9
      mmbangifingi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2011
      Posts : 2,569
      Rep Power : 858
      Likes Received
      452
      Likes Given
      2908

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Nimeshindwa kupata idea,anataja matukio kadhaa kufanyika August, Rpc Mark Kalunguyeye,, leo hii ni June 2, Kalunguyeye alishaondoka zamani sana Kinondoni na kama sikosei kashastaafu
      Who Jah bless, No one Curse!

    12. #10
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Huyu bwana si ndio alikuwa mstari wa mbele kuwasaidia wahanga wa mafuriko uya jangwani? Hizi tuhuma naona zinaletwa karibu kila wakati lakini hakuna linaloendelea...si unajua tena tumelala usingizi wa pono
      Maundumula likes this.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    13. #11
      Mahesabu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2008
      Location : manzese
      Posts : 3,034
      Rep Power : 1318
      Likes Received
      218
      Likes Given
      677

      Default

      Quote By mmbangifingi
      Nimeshindwa kupata idea,anataja matukio kadhaa kufanyika August, Rpc Mark Kalunguyeye,, leo hii ni June 2, Kalunguyeye alishaondoka zamani sana Kinondoni na kama sikosei kashastaafu
      Nimtetee mwandishi!!!! Huenda ameiandika mda mrefu huku akiendelea kutafuta taarifa zaidi!!!
      Ukweli wa mwandishi huenda ukazidi uwongo kwa mbali sana!!! Ila ni kwa nini sasa?
      Kassim Awadh likes this.

    14. #12
      King Kong III's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Enaboishu-Umenyeni
      Posts : 11,920
      Rep Power : 5062
      Likes Received
      3200
      Likes Given
      2654

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Twanga twanga mpe makavu mpe makavu jamaa fisadi.

    15. #13
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,297
      Rep Power : 12584
      Likes Received
      5843
      Likes Given
      771

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu.

      Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.
      MziziMkavu and Maundumula like this.

    16. #14
      MTANGANYIKA ORIGINAL's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Posts : 12
      Rep Power : 361
      Likes Received
      9
      Likes Given
      1

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Majungu tuu na fitina ilovuka mipaka! Kama una ushahidi kwa nini usipeleke kunapohusika ili hatua za isheria zikafuatwa au unatumiwa na mshindani wake wa kibiashara?
      antoniozagarino and jamiif like this.

    17. #15
      Macos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th May 2008
      Posts : 777
      Rep Power : 718
      Likes Received
      167
      Likes Given
      13

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      majungu mengine bwana ...sasa huu ni wivu,uchiyo,kijiba cha roho ...ukimuona mwenzio ana pata basi wewe majungu,....
      wewe unasema hapo juu mwezi AUGUST Mwaka huu!! popobawa sijui nani wameteka ....sasa August hatujafika Majunguman...
      unasema rafiki yake mlebanon kamfiyini mpaka kamrejesha kwa Yemen!! yemen na lebanon wapi na wapi?
      wacha uchoyo..wenzako wanachapa kazi kupata,bongo kuna nafasi nyingi za kupata ..oppurtunity zipo tele ngugu yangu...fanya kazi,tumia bongo yako,utafanikiwa..uchoyo utakuumiza moyo tu....

    18. #16
      salito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 971
      Rep Power : 568
      Likes Received
      215
      Likes Given
      138

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      mhh..naona chenga..

    19. #17
      mathematics's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st February 2012
      Location : MY PLACE
      Posts : 1,964
      Rep Power : 1078
      Likes Received
      464
      Likes Given
      574

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Watu wanamiliki vikampuni uchwara lakini ni matajiri wa kutupwa, kumbe hivyo vikampuni wanatuzuga, na kumbe wanavitumia kusafishia pesa zao chafu...

    20. #18
      Ally Kombo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th November 2010
      Location : Dar es salaam
      Posts : 5,625
      Rep Power : 1359
      Likes Received
      790
      Likes Given
      169

      Default

      Quote By salito
      mhh..naona chenga..
      .....................mwenzangu !!!!

    21. #19
      Ally Kombo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th November 2010
      Location : Dar es salaam
      Posts : 5,625
      Rep Power : 1359
      Likes Received
      790
      Likes Given
      169

      Default

      Quote By ritz
      Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu.

      Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.
      ............. mbona imeelezwa hapo kuwa "Ameir Jeshi" anazo taarifa ! Au kuna Polisi anakizidi hicho cheo !? Msiingie humu na "mning'inio"

    22. #20
      bob68's Avatar
      Member Array
      Join Date : 4th February 2012
      Posts : 35
      Rep Power : 375
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Umeshaandikiwa hapo kwa ufafanuzi wote mtz badala uje na hoja yako ya msingi unasema wivu,majungu,kwa kuangalia typing error tu,si lazima upinge kila kitu na maelezo yameeleka hapo!!

    Page 1 of 6 123 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...