Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

    Report Post
    Page 4 of 6 FirstFirst ... 23456 LastLast
    Results 61 to 80 of 119
    1. #1
      Mongoiwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Posts : 478
      Rep Power : 668
      Likes Received
      51
      Likes Given
      23

      Default Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Utangulizi

      Mfanyabiashara Said Mohammed Saad anamiliki Kampuni ya Home Shopping Center iliyopo Kariakoo Mtaa wa Swahili na Msimbazi katika Jengo la Ghorofa lenye vioo vilivyochorwa picha za waigizaji wa Kikundi cha Orijino Commedy kinachorusha vipindi vyake Televisheni ya taifa ya TBC1.

      Mfanyabiashara huyu ambaye ana uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Saud Arabia, anafanya uhalifu na kuhujumu uchumi nchi kwa kushirikiana na wafanyabiashara wengine wakubwa

      Tuhuma

      Mfanyabiashara Said Mohammed ameshiriki katika matukio mengi ya kihalifu yakiwamo ya kupiga risasi watu na kesi zake zimekuwa zikifunguliwa na baadaye anazizima kwa kutoa rushwa polisi.

      Moja ya matukio hayo ni kumpiga risasi mfanyakazi wake mwaka 2005 wakati akishusha bidhaa za kuuza dukani kutoka katika gari lake, kumpiga risasi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Vingunguti, Deo Vicent Agosti 15, 2006 saa 1:00 usiku Mtaa wa Msimbazi na Swahili Kariakoo jijini Dar es Salaam.

      Mfanyakazi wake alimpiga baada ya kumbishia Said kwamba hawezi kumpiga risasi kwa sababu anajua sheria za nchi haziruhusu kufanya hivyo. Alimpiga kuonyesha kwamba yeye yupo juu ya sheria za nchi. Kesi hiyo nayo aliimaliza kimya kimya kwa kumpa hela mfanyakazi huyo na ndugu zake na polisi.

      Mtoto Vicent yeye baada ya kupigwa risasi aliliripoti Polisi na baadaye alilazwa katika Wodi namba 17 Moi kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Alipigwa risasi ya mguuni wakati akipita karibu na duka la Said baada ya mashabiki wa Simba waliokuwa wakisherekea ushindi wa timu yao kupita katika eneo hilo.

      Hata hivyo, alimaliza kesi hiyo nje ya mahakamani kwa kuwapa hela wazazi wa mtoto huyo.

      Pia anamiliki genge la Wahalifu ambalo analitumia kumlinda na kuwaadhibu wapinzani wake au maadui zake akishirikiana na mdogo wake Ghalib Mohammed Saad.

      Kundi hilo linalojulikana kama Ze Popobawa ndilo ambalo Agosti mwaka huu lilitumika kumteka nyara Mlebanoni mfanyabiashara ambaye ana duka la vitu vya ndani Mtaa wa Morogoro karibu na makutano ya barabara za Morogoro na Bibi Titi na baadaye kumwingilia kinyume cha maumbile kisha kumpeleka kwa nguvu Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kumrejesha kwao Yemen kinyume cha taratibu.

      Kisa kilichofanya mfanyabiashara huyo ambaye yupo nchini kisheria ni kumpa mimba mdogo wa Said anayeitwa Salha bila ya kuoana kama zilivyotaratibu za mila zao za Yemeni.

      Mfanyabiashra huyo wa Mlebanoni ambaye awali alikuwa rafiki yake mkubwa na Said, amemfanya tangu tukio hilo litokee kuishi kwa kujificha kwa kuhofia kufanyiwa unyama mwingine na Said ambaye anaendelea kumtisha.

      Unyama mwingine

      Baada ya kumfanyia unyama mfanyabiashra Mlebanoni , Said hakuishia hapo bali aliamua kumwadhibu dada yake Salha kwa kumpiga. kumnyoa nywele zake zote na kumnywesha vidonge ambavyo havijulikani aina yake na alimpa kwa sababu zipi?

      Salha baada ya kufanyiwa nyama huo nyumbani kwao Msasani wilaya Kinondoni aliamua kwenda kuripoti polisi kituo cha Osterbay ambako lilifunguliwa jalada la kesi namba OB/RB/13915 ambayo ilifunguliwa Agosti 5 mwaka huu.

      Hata hivyo, mbali ya polisi kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini wanashangaa tangu Salha aripoti tukio hilo, hajarudi kituoni hapo wala simu yake mkononi ambayo aliicha namba zake kituoni hapo wakati akiandikisha maelezo haipatikani, kitu ambacho kinawapa wasiwasi.

      Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye anasema huenda suala hilo wamelimaliza kifamilia. Ingawa kuna tariafa kuwa msichana huyo amewekwa kizuizini chumbani ambako haruhusiwi kutoka nje. Polisi kituo cha Oysterbay hawajafuatilia suala hilo kutokana na kupozwa kwa kupewa kitu kidogo rushwa na Said ili kuzima suala hilo.

      Ushirika wa kihalifu

      Kutokana na kushirikiana vyema katika shughuli za dawa za kulevya na kutorosha nyara za taifa wakimtumia Mfanyabiashara huyu, Said, Manji ameamua kumpa vijana wake wa Orijino Commedy kuwapa ufadhili wa kutangaza bidhaa zake anazoingiza nchini za mashuka na nguo.

      Hivi karibuni baada ya Manji kushiriki katika kuigiza mchezo wa kikundi cha Orijino Comedy kama mfanyabishara ambaye alikuwa akihitaji msaada wa kupata fedha za kufadhili Klabu ya Yanga na kuwapa wagizaji wa kikundi hicho kutumia ofisi yake kuigiza, Said naye wiki iliyofuatia aliwapa wana kikundi hicho nafasi kuingiza katika ofisi yake na kuwapa gari lake kulitumia.

      Wizi wa makontena bandarini

      1. Mfanyabiashara huyu anamiliki kampuni nyingi za Clearing and Forwarding ambazo hutumika kuiba makontena ya bidhaa anazoziingiza nchini kutoka nje na akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa TRA.

      Hata hivyo, Kampuni hizi zimefungiwa baada ya kubaini kuhusika na wizi huo wa makontena, lakini kila inayofungiwa husajili nyingine Brela akitumia majina feki.

      Kampuni ambazo zimefungiwa na TRA kwa kuhusika na wizi wa makontena zaidi ya 30 kila moja ni Mbasi Clearing and Fowarding, Clinton Clearing and Forwarding, London Freight Forwarding, Exceptional Freight Forwaders na Upland Clearing and Forwarding.

      TRA imethibitisha kuzifungia kampuni hizo kufanya kazi ya Clearing and Fowading, kwa kutumia kifungu 145 (3) cha sheria ya Jumuia ya Afrika Mashariki ya utawala wa Forodha ya mwaka 2004.

      Hata hivyo, wamekataa kutaja majina ya wamiliki wa kampuni hizo wakisema Brela ndio wenye jukumu hilo. Ingawa wamekuwa wakikubali kuendelea kumhudumia mteja huyo huyo ambaye anaiba makontena na kufungiwa kampuni zake kisha anafungua nyingine chap chap kama uyoga.

      Hata hivyo, Brela kuna kumbukumbu ya kampuni mbili tu ambazo ni London Freight Fowarders Ltd yenye usajili namba 39834 iliyosajiliwa Agosti 15, 2000 ikionyesha wamiliki wake ni Angelo Peter mwenye hisa 2000, Richard Mulenga mwenye hisa 1500 na Abdulkarim Zaharan Salim mwenye hisa 1500. Kampuni hiyo ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

      Kampuni nyingine za kwake zenye kumbukumbu Brela ni Exceptional Freight Fowarders Ltd ambayo wamiliki wake ni Lumba Nguku mwenye hisa 5,000 na Salim Suleiman mwenye hisa 5,000. Kampuni ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

      Dawa za kulevya na kutorosha nyara

      Mfanyabiashara huyu anajihusisha na uingizaji wa dawa za kulevya nchini kwa kushirikiana na mfanyabiashara Manji wakitumia kampuni zake za Clearing and Fowarding ambazo huiba makontena yenye dawa hizo yanapoingia bandarini.

      Mfanyabiashara huyu ni mmoja wa watu waliotajwa katika orodha ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya iliyowasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2006 akitajwa kama Said Abuu mfanyabiashra wa Kariakoo.

      Nyara za taifa

      Mfanyabiashara huyu amekuwa akitumia kampuni zake kusafirisha makontena yenye nyara za taifa kwenda Vietnam, Philipiness na Malaysia akishirikiana Manji na Rostam Aziz ambaye pia ni mmiliki vitalu vya uwindaji. Kampuni ya Rostam ya Uwindaji inaendeshwa na mdogo wake anayeitwa Akram.

      Ili kufanikisha mtandao wao huo wana watu wao katika sehemu nyeti za TRA, bandari, Polisi na usalama wa taifa unaowalinda kwa hali na mali.

      Utajiri wa kutisha

      Kutokana na Said kujihusisha na biashara hizo haramu kwa muda mfupi tangu mwaka 2004 alipoanza hivi sasa ana utajiri wa kutisha. Anamiliki nyumba sita eneo la Kariakoo pekee.

      1. Moja ipo Swahili na Msimbazi, Ghorofa saba ambayo ameamua kuipangisha watu sehemu ya juu, lakini TRA akidaganya kwamba ni hoteli ili kukwepa kulipa kodi. 2. Congo na Agrey ghorofa sita, 3. Uhuru mkabala na shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa bado inajengwa ni ya ghorofa, 4. Livingstone na Uhuru ipo, 5. Mkunguni Kariakoo Sokoni karibu na dula la Azam Ice Cream ghorofa sita, 6. Lumumba karibu na CCM makao makuu limepakana na Hospitali ya Burhan.
      Nchi yangu inaangamia kwa kukosa maarifa ya Viongozi

    2. FemaTV & Radio

    3. #61
      Masabaja's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th March 2012
      Posts : 139
      Rep Power : 390
      Likes Received
      18
      Likes Given
      13

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Wana JF mimi niliwahi kuandika hapa JF kuhusu huyu jamaa amefanya mambo mengi shida ni kuwa anapata sapoti kubwa kutoka kwa RIZ1 naombeni mfuatilie. Amefanya uhalifu wa kupindukia na serikali hii pamoja na viongozi wakuu wa taasisi muhimu kama TRA commissioner anamfahamu vizuri huyu jamaa na anamsupport, IGP anamsupport na wengine katika idara nyeti. Labda wana JF tuambiane nini tufanye kukabiliana na uhalifu wa huyu jamaa maana TRA hawawezi kumfuata maana commissioner general ni mtu wake IGP hivyo hivyo sasa tunafanyaje.

    4. #62
      zumbemkuu's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Location : street dweller
      Posts : 5,317
      Rep Power : 1998
      Likes Received
      2114
      Likes Given
      7783

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By Edward Teller
      Huyu bwana bado tu anadunda mtaani-hivi uchafu kama huu kwa mtanganyika kama mimi mweusi unaweza kuufanya Yemen au sehem nyingine/na ukawa bado upo tu-kama si kiuwa na viongozi wabovu kwenye kila sekta hapa nchini
      sijui ni kwanini kuna baadhi ya watz wanapenda kunyanyaswa na wageni??? ngoja siku aingie kwenye anga zangu, wahindi wananijua.....
      Edward Teller likes this.
      "watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema

    5. #63
      flora msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : under a coconut tree
      Posts : 4,120
      Rep Power : 1258
      Likes Received
      499
      Likes Given
      371

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      uwiiiii kwanini nilizaliwa kwenye linji hili aghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh

      Never hate people who are jealous of you,
      Instead love them because they're the ones,
      who think you are better than them…

    6. #64
      BADILI TABIA's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Location : DUNIANI
      Posts : 14,547
      Rep Power : 5611
      Likes Received
      6208
      Likes Given
      2281

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      halafu nchi itaendekae hii?
      Imejaa wachumia tumbo????

    7. #65
      Edward Teller's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Location : Area 51
      Posts : 3,431
      Rep Power : 1119
      Likes Received
      570
      Likes Given
      612

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By zumbemkuu
      sijui ni kwanini kuna baadhi ya watz wanapenda kunyanyaswa na wageni??? ngoja siku aingie kwenye anga zangu, wahindi wananijua.....
      ni ajabu kwa wagen kuleta zengwe kwa indigenous-hata hao indigenous wanaoteswa ni wajinga
      “Talk slowly but think quickly”

    8. Study Abroad

    9. #66
      King2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2011
      Posts : 1,280
      Rep Power : 635
      Likes Received
      159
      Likes Given
      0

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Serikali yenyewe inaongozwa na Wahalifu Sasa unafikiri kutakuwa na haki kweli. Tumeona yaliyomsibu ulimboka, babu seya, wafanyabiashara wa mahenge N.k.

    10. #67
      Borat69's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th June 2012
      Location : Global Citizen
      Posts : 698
      Rep Power : 487
      Likes Received
      279
      Likes Given
      77

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By Ritz
      Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu.

      Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.
      Polisi gani unaozungumzia hapa??? Interpol au!!??
      "Our Lives begin to End the Day We Become Silent About Things that Matter"-Dr Martin Luther King Jr.

    11. #68
      Zinedine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2011
      Posts : 485
      Rep Power : 508
      Likes Received
      174
      Likes Given
      230

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By saragossa
      Shughuli pevu iyo! Kwa mantiki nyingine HSC ni biashara anayoitumia kusafisha hela sio?

      Je records zake zinasema hana mkopo benki yoyote?

      Mtaji wa biashara yake ambayo inaonekana ni legit, ambayo ni HSC alipata wapi?

      Idara za juu za TISS zinampango gani na mtu huyu?

      Nzowa anasemaje pia?

      Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo, ila za mwizi arobaini, lazma atanasa tu siku moja!
      Hapo kwenye red labda utawala wa ccm uondoke, lakini chini ya ccm, labda za mwizi ziwe 400000000000 na wala si 40.

    12. #69
      Njilembera's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2008
      Posts : 781
      Rep Power : 723
      Likes Received
      88
      Likes Given
      155

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By MTANGANYIKA ORIGINAL
      Majungu tuu na fitina ilovuka mipaka! Kama una ushahidi kwa nini usipeleke kunapohusika ili hatua za isheria zikafuatwa au unatumiwa na mshindani wake wa kibiashara?

      Imekuwa majungu tena! Hii taarifa mefanyiwa kazi na ningekuwa na madaraka ningewalazimisha wote wenye kuleta habari wazitafiti kwa kina cha kiasi hiki walau. Kama una hoja inabidi na wewe ukatafiti. Kuna maeneo yametajwa kama ya huyo mtoto Vincenti, dada mtu na makampuni. Bila utafiti kaa kimya- huna la kusema au la kusimulia.

    13. #70
      Mingoi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st July 2012
      Location : Not reachable
      Posts : 2,135
      Rep Power : 609
      Likes Received
      241
      Likes Given
      213

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By Ritz
      Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu.

      Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.

      Ujumbe umefika hata jamvini kuna polisi, maafisa wa TRA, TISS, anti corruption wana sehemu ya kuanzia toka kwa mtoa habari

    14. #71
      Ndukidi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 372
      Rep Power : 575
      Likes Received
      141
      Likes Given
      327

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By Bufa
      U so deep man, umemuanika jamaa live bila chenga chaajabu serikali inamjua, Kikwete alipewa list ya wauza unga na huyu akiwa mmoja wao ila bado hamna kinachofanyika.
      Jamani lazima mtumie akili... hivi mnadhani yeye ni mjinga, ukiwa na ile list na ukajua jinsi ya kuitumia lazima uachane na umasikini. Nadhani wenyewe mnaweza ku conect dots ... wale kwenye list ndio wafadhili wa CCM, ndio wabia kwenye biashara na ndio wasafishaji hela chafu... unaambiwa tu tuna taarifa zako uko kwenye list hivyo angalia bana unatutoa vipi...

    15. #72
      brazilian's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th February 2012
      Posts : 609
      Rep Power : 1358
      Likes Received
      101
      Likes Given
      5

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Ndugu chunga sana wasije Wakakulimboka

    16. #73
      jamiif's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th April 2012
      Posts : 956
      Rep Power : 546
      Likes Received
      242
      Likes Given
      511

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad


    17. #74
      Bufa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st March 2012
      Posts : 337
      Rep Power : 427
      Likes Received
      56
      Likes Given
      161

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By Ndukidi
      Jamani lazima mtumie akili... hivi mnadhani yeye ni mjinga, ukiwa na ile list na ukajua jinsi ya kuitumia lazima uachane na umasikini. Nadhani wenyewe mnaweza ku conect dots ... wale kwenye list ndio wafadhili wa CCM, ndio wabia kwenye biashara na ndio wasafishaji hela chafu... unaambiwa tu tuna taarifa zako uko kwenye list hivyo angalia bana unatutoa vipi...
      True that.

    18. #75
      Lambardi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th February 2008
      Location : KITAANI ZAIDI
      Posts : 4,507
      Rep Power : 1793
      Likes Received
      653
      Likes Given
      0

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      CDM wajipange sana sana la sivyo watavurugwa na kusambaratika!!kuna mamluki wengi sana ndani CDM kazi kuvuruga chama!!wakiweza kusimama vizuri wanachukua nchi bila ubishi!

    19. #76
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,732
      Rep Power : 1916
      Likes Received
      1163
      Likes Given
      941

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Mimi ningekusifia sana kama maelezo haya ungeyapeleka vyombo husika kama Polisi, PCCB na hata kwa mwanasharia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi na kisha suala hilo kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

      Kuweka hapa ambapo watu makini wanajua fika una choyo na husda ya mafanikio ya Bw Said Saad.

      Kumbuka kuwa NI wajibu wa kila Mtanzania kutii sharia zenu. Ukipitia Katiba yenu Sharia namba 15 ibara ya 6 ya mwaka 1984 kifungu cha 26 imeweka wazi kabisa na inasema hivi
      26
      .-(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na
      sheria za Jamhuri ya Muungano.(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa nasheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba
      na sheria za nchi.
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    20. #77
      altaaf's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 15th September 2009
      Posts : 104
      Rep Power : 512
      Likes Received
      19
      Likes Given
      43

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By MTANGANYIKA ORIGINAL
      Majungu tuu na fitina ilovuka mipaka! Kama una ushahidi kwa nini usipeleke kunapohusika ili hatua za isheria zikafuatwa au unatumiwa na mshindani wake wa kibiashara?
      ipo harufu ya majungu ni mlebanon akarejeshwa kwao yemen. alimpa mimba kabla ya ndowa kinyume na utaratibu wao wa yemen , uraia mtanzania na saudi arabia kaatuwacha kwenye mataa hapo !

    21. #78
      Jiwe Linaloishi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th May 2008
      Location : Mlimani
      Posts : 3,106
      Rep Power : 17238
      Likes Received
      1622
      Likes Given
      1122

      Default Re: Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

      Quote By MTANGANYIKA ORIGINAL
      Majungu tuu na fitina ilovuka mipaka! Kama una ushahidi kwa nini usipeleke kunapohusika ili hatua za isheria zikafuatwa au unatumiwa na mshindani wake wa kibiashara?
      WE ushaambiwa polisi wakienda wanapewa posho wanatambaa sasa huo ushahidi aupeleke wapi labda kwa kikwete ndio mtu wa mwisho lakini kwa mtazamo tu inaonekana system yote kaiweka mfukoni
      SEMA UKWELI UMWAIBISHE SHETANI

    22. #79
      salito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 971
      Rep Power : 567
      Likes Received
      215
      Likes Given
      138

      Default

      Huyu mtu acha tumuundie kamati sasa ya ufundi...amezidi..

    23. #80
      Suzie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2010
      Posts : 1,084
      Rep Power : 0
      Likes Received
      339
      Likes Given
      309

      Default

      Quote By Ritz
      Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu.

      Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.
      Yeye kafanya uchunguzi na kutuletea hapa akiwa anajua kabisa hapa JF kuna watu wenye upeo zaidi. Kuliko kumbeza na kumkatisha tamaa ni bora ikajadiliwa nini kifanyike, na hii itasaidia hata wengine wenye tetesi kutokukaa nazo

    24. Miaka 50
    Page 4 of 6 FirstFirst ... 23456 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...