Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mashangingi yaitafuna serikali Tanzania

    Report Post
    Page 9 of 9 FirstFirst ... 789
    Results 161 to 162 of 162
    1. #1
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,020
      Rep Power : 2562
      Likes Received
      788
      Likes Given
      28

      Default Mashangingi yaitafuna serikali Tanzania

      Mashangingi yaitafuna serikali Tanzania

      *Yatumia Sh33bilioni kwa mwaka

      Na Ramadhan Semtawa

      WAKATI matumizi ya Serikali yakiwa yamezidi bajeti kwa Sh 900 bilioni, imebainika gharama kubwa za kuendesha magari ya kifahari maarufu kama mashangingi ni moja ya chanzo kinachochangia hali hiyo.

      Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba, mashangingi yanayotumiwa na viongozi wa serikali yapo 800 yanatumia zaidi ya Sh33 bilioni kwa mwaka ikiwa ni matumizi ya mafuta na gharama za kuyafanyia mategenezo.

      Kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana, magari hayo yanatumia wastani wa lita 300 kila moja kwa wiki, hivyo hutumia lita za mafuta 240,000 kwa kipindi hicho kwa magari yote hayo. Kwa wastani bei ya sasa ya mafuta ya diseli ni sh 1200 kwa lita hivyo magari hayo yanatumia Sh1.152 bilioni kwa mwezi. Uchunguzi umegundua kuwa gharama za kulifanyia mategenezo kwa mwezi ni Sh2 milioni kila gari hivyo gharama za kuhudumia magari hayo kwa mwezi ni Sh1.6 bilioni.

      Ukijumlisha gharama za mafuta na mategenezo kwa mwezi ni Sh 2.752 bilioni na kwa mwaka ni kiasi cha Sh33 bilioni. Kiasi hicho cha matumizi kingepungua iwapo baadhi ya viongozi ukiachia rais, waziri mkuu na makamu wa rais wangetumia magari ya kawaida.

      Kati ya magari hayo, 540 ni ya viongozi wa Serikali Kuu wakiwamo ofisi ya rais, ofisi ya waziri mkuu, makamu wa rais, mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu. Orodha hiyo ya serikali kuu imezingatia, makatibu wakuu 27, manaibu wao 27, maafisa utumishi (Ma Dap) 27, na wakurugenzi wanne kila wizara na sehemu nyingine wakurugenzi wasaidizi, huku Ikulu, ofisi ya makamu wa rais na ya waziri mkuu, kwa pamoja zikiwa na magri hayo yasiyopungua 40.

      Mengine hutumiwa na watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za serikali, wakati kwa upande wa Tamisemi ni kuanzia wakuu wa mikoa 22, makatibu tawala wa mikoa 22, makatibu tawala wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa wilaya na wakuu wa wilaya 104.

      Wakati gharama hizo zikionekana kuwa mzigo kwa walipa kodi, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, ameliambia Mwananchi: "Tena naomba uninukuu vizuri, mawaziri wataendelea kutumia magari yanayoendana na hadhi yao, waziri hawezi kutembelea Vokswagen (Bito)".

      Uchunguzi umebaini kuwa gharama hizo zimekuwa zikiongezeka maradufu katika siku za hivi karibuni kutokana mawaziri, manaibu mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala wa mikoa na wilaya kutotulia ofisini kutokana na ziara wanazofanya katika maeneo mbalimali.

      Pia imebainika kwamba, gharama za kuendesha magari hayo zimekuwa ni mzigo kwa walipa kodi kutokana na baadhi ya mawaziri kutofanya kazi vizuri huku baadhi ya magari yakionekana kuranda randa kwenye mabaa nyakati za usiku na mwisho wa wiki. Akizungumzia zaidi kuhusu magari hayo, Chenge alisema serikali haijafikia uamuzi wowote wa kupiga marufuku magari hayo ya kifahari ambayo yeye anayaita kuwa ni ya kawaida.

      "Kwanza si magari ya kifahari, wewe ndiye unayeyaita hivyo, ni kwa sababu ya umasikini wetu tu, lakini lazima waziri atembelee gari lenye hadhi yake," alisisitiza Chenge.

      Hata hivyo, aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo kabla ya Chenge, Basil Mramba aliwahi kukaririwa na gazeti hili kuwa mashangingi ni mzigo mkubwa kwa serikali na kwamba inafanya mipango ya kusitisha ununuzi wa magari hayo.

      Alipoulizwa haoni huo umasikini wa nchi yetu ndiyo ambao ulitupasa kuacha kununua magari hayo, alijibu, " kwanza, matumizi ya serikali hayawezi kuzidi kwa ajili ya magari haya", na kuhoji:

      "Hivi siku za nyuma katika serikali zilizopita mafuta yalikuwa yakitolewa lita 50 kwa wiki, nchi yetu ilipiga hatua gani kubwa katika nyanja za maendeleo?" Chenge alipoelezwa mfano, wa serikali ya Mwalimu Nyerere kwamba iliweza kujenga viwanda na mashirika makubwa ambavyo watawala wa sasa wanayauza ovyo, alijibu tena, " wewe sikia, haya mafuta ya magari hayawezi kukuza uchumi, cha msingi watu fanyeni kazi kwa bidii, tushirikiane kutekeleza ilani ya chama na mipango ya maendeleo ya serikali."

      Hata hivyo, Chenge alisema serikali itachukua hatua kwa wale watakaobainika kutumia magari hayo katika mabaa na nyakati zisizo za kazi.

      Wakati huo huo; Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeishauri Serikali ya Tanzania kubana matumizi yake kwa kuyaelekeza fedha kwenye vipaumbele muhimu vya nchi kama afya, miundombinu, elimu na maji.

      Ushauri huo ulitolewa jana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa IMF nchini, Dk David Robinson, alipokuwa akijitambulisha kwa wanahabari jijini Dar es Salaam, katika ofisi ya shirika hilo.

      "Siwezi kulitolea maoni kwa undani kwani nahitaji muda wa kujifunza zaidi, lakini ni muhimu Serikali ikadhibiti matumizi yake ya fedha na kuzielekeza katika sekta muhimu kama afya, miundombinu, elimu na maji," alishauri Mwakilishi huyo wa IMF.

      Dk Robinson alisema hayo wakati akijibu hoja ya wanahabari juu ya ripoti ya IMF kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania, ambayo imeifagilia Serikali kuwa iko makini katika udhibiti wa fedha, wakati ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeonyesha kuwepo kwa mushkeli katika matumizi.

      Ripoti hiyo ya CAG ya hivi karibuni inaonesha kwamba Serikali imekuwa na matumizi makubwa kwa kutumia ziada ya sh900 bilioni miezi minne kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha. Taarifa ya CAG kwa mwaka 2005/06, inaonesha kuongezeka kwa matumizi ya kawaida kutoka Sh2,138,860,343,786 mwaka 2004/05 hadi Sh2,732,455,841,323 mwaka 2005/06.

      Taarifa hiyo inasema, fedha za matumizi ya miradi ya maendeleo zimepungua kutoka Sh850,533,139,955 mwaka 2004/05 hadi Sh844,103,204,420, huku deni la taifa la nje likikua hadi kutokaSh5,548,446,077 hadi Sh5,772,620,992 katika kipindi hicho na kumfanya Rais Jakaya Kikwete kuitisha mkutano na watendaji waandamizi wa serikali kuijadili katika kikao hicho kilichofanyika Dodoma, ambapo aliwatahadharisha watendaji watakaorudia makosa hayo watatimuliwa kazini.

      Takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Machi mwaka huu, zinaonesha tayari katika matumizi hayo kuna ongezeko la asilimia 5.6 ya pato la taifa, badala ya asilimia 5.1 ya pato la taifa kama ilivyokuwa imekadiriwa kwenye bajeti ya mwaka 2006/07.

      Kutokana na kuongezeka kwa matumizi hayo, taarifa ya hiyo ya BoT inaonyesha mpaka Februari mwaka huu, tayari kumekuwa na pengo la Sh978.8 bilioni.

      Akizungumza zaidi, Dk. Robinson alieleza kwamba kwa sasa jumuiya ya nchi wahisani imekuwa ikielekeza zaidi misaada yake ya fedha kwenye bajeti kuu za Serikali ili ziwe na uhuru wa kupanga vipaumbele vyake badala ya kuamuliwa.

      Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo ya Februari mwaka huu Bodi tendaji ya IMF imeridhia kuipa Tanzanai fedha zaidi baada ya kuridhishwa na inavyotekeleza Mkakati wake wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini (MKUKUTA) katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita .

      Kwa hali hiyo Tanzania imefunzu kupewa dola za kimarekani 4.2 milioni kwa ajili ya kuendeleza jitihada hizo. Kiasi hivyo kinafanya jumla ya fedha ambazo Serikali ya Tanzania itazipata kwa ajili ya mpango huo kufikia dola za kimarekani 29.4 milioni.

      Lengo la wahisani hao ni kuona kwamba uchumi wa Tanzania unakuwa hasa katika kujenga uwezo wa matumizi bora ya fedha, kuimarisha mchango wa sekta ya fedha katika maendeleo, kuwa na sera za fedha zinazotekelezeka na mazingira bora ya biashara.

      Ripoti hiyo imeonesha kwamba katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikuwa vizuri na kufanikiwa kushusha mfumko wa bei pamoja na kujiwekea hakiba kubwa ya fedha.
      Last edited by Ole; 18th April 2007 at 23:48.
      Kennedy likes this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #161
      Tumbomoto's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 2nd August 2012
      Posts : 5
      Rep Power : 344
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Kaazziii kweli kweli

      Mashangingi! Mashangingi! Mashangingi!

      Naafikiana na huyu mzee wa maoni - Ramadhan Semtawa! Yaani kama kuna kitu kinachoishangaza hii dunia ni hicho! Nchi ni ya walala hoi; huduma za jamii kama Hosipitali, Elimu, maji na hata barabara za kuyabiringisha hayo mashangingi ndiyo hizoo zimedorora kabisaa!
      Hayo majangili hapo Dar es salaamu, ukianzia na Kikwete mwenyewe, Mawaziri na hata hivyo vikaragosi vinavyojiita wabunge wanchojua ni kufuja mali na kunywa damu ya watanzania kwa kubiringisha hayo Mashangingi ambayo hata ukienda kule Marekani kamwe hayawezi kutumika kama magari la kiongozi yeyote wa serikali au shirika lolote la Uma. Hayo ni magari ya wauza madawa ya kulevya! Rais Kikwete analiona hilo, na analifunikiza chini ya mkeka kwa kukenyuakenyua meno tu. Kwa hilo analijua kwani Tanzania yaweza kushika namba ya pili duniani kwa kuwa na Rais Mtabasamu - kazi je?
      Lipo swala lingine lililoguswa na huyo Mdau wa Kanada (Michuzi 14/08/12) kuhusu ajali, na hasa pendekezo lake kwa Serikani kwamba kwa kupitia Sumatra wabuni mbinu za kulikabili! Waaapi? Sumatra wako Arusha wanapambana na wamiliki wa Noah. Badala ya kuwapa moyo hao wawekezaji wadogo, ambao walau wanawaajiri vijana wachachewache, wanawazushia majanga, mara - eti wao ndio waleta ajali, eti magari hayakutengenezwa kwa ajili ya abiria, eti.....?
      Mbona bajaji zinabeba abiria? Mbona baiskeli zinabeba abiria? Mbona Pikipiki zina leseni za kubeba abiria?
      Kama hii ndiyo kazi ya hiyo SUMATRA, watapata wapi na lini hiyo nafasi ya kubuni mbinu za kuthibiti mwendo wa mabasi na malori - kwa kifupi, kusimamia nidhamu ya utumiaji wa barabara kwa vyombo vyote?
      Maoni na onyo langu kwa wabiringisha mashangingi ni moja tu - Siku ya arobaini itafika kama ilivyofika kwa Gadafi na Mubaraka - jibu la Je, tuyafanyeje haya majuha matatu litapatikana. Kwani sasa hivi Gadafi na Mubaraka wanabiringisha nini? Huo upole, uvumilivu, ukimya na kujifunga mkanda kwa Mtanzania wa kawaida kutafika mwisho siku moja, na ninawahakikishia kwamba hata hao wajukuu na vitukuu vyenu ambao mnawalimbikizia mali ya dhuluma, haitawafaa kitu. Ndugu zangu, muda wa kujikomboa ni huu! Muda wa kujirudi na kujua kwamba hiyo Tanzania ni ya wote ni huu! Mwenye cheo, apaswa kujua kwamba ni mtumishi, na kile kidogo alicho nacho akitumie kwa akili na busara kwa manufaa ya watanzania wote. Huo ndio mwito na wosia wa baba wa taifa ambaye alijinyenyekesha na kujinyima sana kwa manufaa ya mwafrika, hadi mauti yalipomkumba!
      Hivi kweli, Rais mzima unacheka tu tangu asubuhi hadi jioni na unajua fika kwamba hakuna madawa hospitalini - watu waliokupa madaraka uwatetee wanakufa, lakini kuna watu kwenye wizara ya afya wanabiringishabiringisha magari yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni Mia moja kila moja just to go for lunch!!!!!!!!!!!!!!!! Shetani ni muovu lakini hata yeye halielewi hilo. Wanaolielewa ni ninyi mafidhuli, mabwenyenye, mabepari, wahujumu, walarushwa, walanguzi na majangili ambao mama yenu ni Chukua Chako Mapema (CCM)!
      Aibuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!
      Nyasirori likes this.

    4. #162
      Tumbomoto's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 2nd August 2012
      Posts : 5
      Rep Power : 344
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Mashangingi yaitafuna serikali Tanzania

      ITAFUTIWE BEI ILI TUNUNUE MTAMBO WA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA GESI YA SONGOSONGO!
      Kwana hata hiyo ndege ya Rais ni ya kuuza! Hata baba mtakatifu hana ndege. Siku akihitaji ndege hukodeshwa kutoka kwenye kampuni ya ndege (Alitalia)! Sisi ni masikini, sisi ni walala hoi! Tunachohitaji ni maji safi, Dawa na madaktari kwenye hosipitali, shule, barabara, na umeme wa kuaminika na siyo ndege ya Rais! We don't need that! We don't need that! We don't need it!

      NA HATA HIYO IKULU YENYEWE INATAKIWA IBOMOLEWE AU IUZWE KWANI KAMA BABA WA TAIFA ALIVYOAGUA, SIKU HIZI LIMEKUWA PANGO LA WEZI NA SIYO ALAMA YA HESHIMA NA HADHI YA MTANZANIA!

    5. Miaka 50
    Page 9 of 9 FirstFirst ... 789

    Similar Topics

    1. Replies: 21
      Last Post: 5th May 2011, 15:22
    2. Replies: 3
      Last Post: 4th April 2011, 12:34
    3. Confirmed - Serikali kununua Mashangingi zaidi ya 100
      By Superman in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 31
      Last Post: 10th January 2009, 12:27
    4. Replies: 58
      Last Post: 30th December 2008, 13:16
    5. Serikali yashtukia uzito wa mzigo wa mashangingi ya viongozi
      By BAK in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 30
      Last Post: 24th December 2008, 05:58

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...