Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mashangingi yaitafuna serikali Tanzania

    Report Post
    Page 4 of 9 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 162
    1. #1
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,002
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      781
      Likes Given
      28

      Default Mashangingi yaitafuna serikali Tanzania

      Mashangingi yaitafuna serikali Tanzania

      *Yatumia Sh33bilioni kwa mwaka

      Na Ramadhan Semtawa

      WAKATI matumizi ya Serikali yakiwa yamezidi bajeti kwa Sh 900 bilioni, imebainika gharama kubwa za kuendesha magari ya kifahari maarufu kama mashangingi ni moja ya chanzo kinachochangia hali hiyo.

      Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba, mashangingi yanayotumiwa na viongozi wa serikali yapo 800 yanatumia zaidi ya Sh33 bilioni kwa mwaka ikiwa ni matumizi ya mafuta na gharama za kuyafanyia mategenezo.

      Kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana, magari hayo yanatumia wastani wa lita 300 kila moja kwa wiki, hivyo hutumia lita za mafuta 240,000 kwa kipindi hicho kwa magari yote hayo. Kwa wastani bei ya sasa ya mafuta ya diseli ni sh 1200 kwa lita hivyo magari hayo yanatumia Sh1.152 bilioni kwa mwezi. Uchunguzi umegundua kuwa gharama za kulifanyia mategenezo kwa mwezi ni Sh2 milioni kila gari hivyo gharama za kuhudumia magari hayo kwa mwezi ni Sh1.6 bilioni.

      Ukijumlisha gharama za mafuta na mategenezo kwa mwezi ni Sh 2.752 bilioni na kwa mwaka ni kiasi cha Sh33 bilioni. Kiasi hicho cha matumizi kingepungua iwapo baadhi ya viongozi ukiachia rais, waziri mkuu na makamu wa rais wangetumia magari ya kawaida.

      Kati ya magari hayo, 540 ni ya viongozi wa Serikali Kuu wakiwamo ofisi ya rais, ofisi ya waziri mkuu, makamu wa rais, mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu. Orodha hiyo ya serikali kuu imezingatia, makatibu wakuu 27, manaibu wao 27, maafisa utumishi (Ma Dap) 27, na wakurugenzi wanne kila wizara na sehemu nyingine wakurugenzi wasaidizi, huku Ikulu, ofisi ya makamu wa rais na ya waziri mkuu, kwa pamoja zikiwa na magri hayo yasiyopungua 40.

      Mengine hutumiwa na watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za serikali, wakati kwa upande wa Tamisemi ni kuanzia wakuu wa mikoa 22, makatibu tawala wa mikoa 22, makatibu tawala wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa wilaya na wakuu wa wilaya 104.

      Wakati gharama hizo zikionekana kuwa mzigo kwa walipa kodi, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, ameliambia Mwananchi: "Tena naomba uninukuu vizuri, mawaziri wataendelea kutumia magari yanayoendana na hadhi yao, waziri hawezi kutembelea Vokswagen (Bito)".

      Uchunguzi umebaini kuwa gharama hizo zimekuwa zikiongezeka maradufu katika siku za hivi karibuni kutokana mawaziri, manaibu mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala wa mikoa na wilaya kutotulia ofisini kutokana na ziara wanazofanya katika maeneo mbalimali.

      Pia imebainika kwamba, gharama za kuendesha magari hayo zimekuwa ni mzigo kwa walipa kodi kutokana na baadhi ya mawaziri kutofanya kazi vizuri huku baadhi ya magari yakionekana kuranda randa kwenye mabaa nyakati za usiku na mwisho wa wiki. Akizungumzia zaidi kuhusu magari hayo, Chenge alisema serikali haijafikia uamuzi wowote wa kupiga marufuku magari hayo ya kifahari ambayo yeye anayaita kuwa ni ya kawaida.

      "Kwanza si magari ya kifahari, wewe ndiye unayeyaita hivyo, ni kwa sababu ya umasikini wetu tu, lakini lazima waziri atembelee gari lenye hadhi yake," alisisitiza Chenge.

      Hata hivyo, aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo kabla ya Chenge, Basil Mramba aliwahi kukaririwa na gazeti hili kuwa mashangingi ni mzigo mkubwa kwa serikali na kwamba inafanya mipango ya kusitisha ununuzi wa magari hayo.

      Alipoulizwa haoni huo umasikini wa nchi yetu ndiyo ambao ulitupasa kuacha kununua magari hayo, alijibu, " kwanza, matumizi ya serikali hayawezi kuzidi kwa ajili ya magari haya", na kuhoji:

      "Hivi siku za nyuma katika serikali zilizopita mafuta yalikuwa yakitolewa lita 50 kwa wiki, nchi yetu ilipiga hatua gani kubwa katika nyanja za maendeleo?" Chenge alipoelezwa mfano, wa serikali ya Mwalimu Nyerere kwamba iliweza kujenga viwanda na mashirika makubwa ambavyo watawala wa sasa wanayauza ovyo, alijibu tena, " wewe sikia, haya mafuta ya magari hayawezi kukuza uchumi, cha msingi watu fanyeni kazi kwa bidii, tushirikiane kutekeleza ilani ya chama na mipango ya maendeleo ya serikali."

      Hata hivyo, Chenge alisema serikali itachukua hatua kwa wale watakaobainika kutumia magari hayo katika mabaa na nyakati zisizo za kazi.

      Wakati huo huo; Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeishauri Serikali ya Tanzania kubana matumizi yake kwa kuyaelekeza fedha kwenye vipaumbele muhimu vya nchi kama afya, miundombinu, elimu na maji.

      Ushauri huo ulitolewa jana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa IMF nchini, Dk David Robinson, alipokuwa akijitambulisha kwa wanahabari jijini Dar es Salaam, katika ofisi ya shirika hilo.

      "Siwezi kulitolea maoni kwa undani kwani nahitaji muda wa kujifunza zaidi, lakini ni muhimu Serikali ikadhibiti matumizi yake ya fedha na kuzielekeza katika sekta muhimu kama afya, miundombinu, elimu na maji," alishauri Mwakilishi huyo wa IMF.

      Dk Robinson alisema hayo wakati akijibu hoja ya wanahabari juu ya ripoti ya IMF kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania, ambayo imeifagilia Serikali kuwa iko makini katika udhibiti wa fedha, wakati ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeonyesha kuwepo kwa mushkeli katika matumizi.

      Ripoti hiyo ya CAG ya hivi karibuni inaonesha kwamba Serikali imekuwa na matumizi makubwa kwa kutumia ziada ya sh900 bilioni miezi minne kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha. Taarifa ya CAG kwa mwaka 2005/06, inaonesha kuongezeka kwa matumizi ya kawaida kutoka Sh2,138,860,343,786 mwaka 2004/05 hadi Sh2,732,455,841,323 mwaka 2005/06.

      Taarifa hiyo inasema, fedha za matumizi ya miradi ya maendeleo zimepungua kutoka Sh850,533,139,955 mwaka 2004/05 hadi Sh844,103,204,420, huku deni la taifa la nje likikua hadi kutokaSh5,548,446,077 hadi Sh5,772,620,992 katika kipindi hicho na kumfanya Rais Jakaya Kikwete kuitisha mkutano na watendaji waandamizi wa serikali kuijadili katika kikao hicho kilichofanyika Dodoma, ambapo aliwatahadharisha watendaji watakaorudia makosa hayo watatimuliwa kazini.

      Takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Machi mwaka huu, zinaonesha tayari katika matumizi hayo kuna ongezeko la asilimia 5.6 ya pato la taifa, badala ya asilimia 5.1 ya pato la taifa kama ilivyokuwa imekadiriwa kwenye bajeti ya mwaka 2006/07.

      Kutokana na kuongezeka kwa matumizi hayo, taarifa ya hiyo ya BoT inaonyesha mpaka Februari mwaka huu, tayari kumekuwa na pengo la Sh978.8 bilioni.

      Akizungumza zaidi, Dk. Robinson alieleza kwamba kwa sasa jumuiya ya nchi wahisani imekuwa ikielekeza zaidi misaada yake ya fedha kwenye bajeti kuu za Serikali ili ziwe na uhuru wa kupanga vipaumbele vyake badala ya kuamuliwa.

      Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo ya Februari mwaka huu Bodi tendaji ya IMF imeridhia kuipa Tanzanai fedha zaidi baada ya kuridhishwa na inavyotekeleza Mkakati wake wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini (MKUKUTA) katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita .

      Kwa hali hiyo Tanzania imefunzu kupewa dola za kimarekani 4.2 milioni kwa ajili ya kuendeleza jitihada hizo. Kiasi hivyo kinafanya jumla ya fedha ambazo Serikali ya Tanzania itazipata kwa ajili ya mpango huo kufikia dola za kimarekani 29.4 milioni.

      Lengo la wahisani hao ni kuona kwamba uchumi wa Tanzania unakuwa hasa katika kujenga uwezo wa matumizi bora ya fedha, kuimarisha mchango wa sekta ya fedha katika maendeleo, kuwa na sera za fedha zinazotekelezeka na mazingira bora ya biashara.

      Ripoti hiyo imeonesha kwamba katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikuwa vizuri na kufanikiwa kushusha mfumko wa bei pamoja na kujiwekea hakiba kubwa ya fedha.
      Last edited by Ole; 18th April 2007 at 23:48.
      Kennedy likes this.

    2. Study Abroad

    3. BAK
      #61
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,533
      Rep Power : 44950
      Likes Received
      8273
      Likes Given
      8280

      Default

      Quote By Bubu ataka kusema
      Waungwana imepita miezi miwili tangu habari hii itangazwe kwa wananchi je vingunge kulikoni hadi hii leo maamuzi hayo hayajatolewa?
      http://www.jamboforums.com/showthrea...ht=mashangingi
      http://www.jamboforums.com/showthrea...ia+mashangingi

      Ni mashangingi mangapi yameshanyang'anywa na yamepelekwa wapi?
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    4. #62
      Bubu Msemaovyo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th May 2007
      Location : All around the World
      Posts : 2,037
      Rep Power : 1746
      Likes Received
      719
      Likes Given
      747

      Default

      Afadhali mradi huu uanze mara moja kwani kwa taarifa nilizonazo udhibiti wa namna hii ni mzuri sana kwani car track hii itaonyesha ni kiasi gani mawaziri wetu ama maafsa wa serikali wamekuwa wakiyatumia vibaya. Hebu check waziri mzima unakwenda na gari la serikali kwa hawara kisha kwenye bar au kasino mnajirusha huko kwa gharama za wananchi. Miiko ya viongozi leo hakuna pia nina wasi wasi kama Rais wetu anauchungu na hilo kwani yuko kimya mno au hii JF haipitii? Kama kuna mmoja wetu mwana JF yuko karibu na ofisa wa ngazi ya juu ambaye yuko karibu na JK wampe website hii awe anapitia pitia ina manufaa sana ni "Online Saigon" hii isipuuzwe kabisa. Suala la matumizi mabaya ya pesa liko hapa katika kila anayeteuliwa na Rais kutaka apewe Landcruiser VX ama GX kwanini tusiwe woga kwa hili. Mwl umetuacha pabaya. Na ulisema mtanikumbuka sana. Na kweli tunakukumbuka sana.
      "If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart." Nelson Mandela

    5. #63
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 811
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Bubu Msemaovyo
      Afadhali mradi huu uanze mara moja kwani kwa taarifa nilizonazo udhibiti wa namna hii ni mzuri sana kwani car track hii itaonyesha ni kiasi gani mawaziri wetu ama maafsa wa serikali wamekuwa wakiyatumia vibaya. Hebu check waziri mzima unakwenda na gari la serikali kwa hawara kisha kwenye bar au kasino mnajirusha huko kwa gharama za wananchi. Miiko ya viongozi leo hakuna pia nina wasi wasi kama Rais wetu anauchungu na hilo kwani yuko kimya mno au hii JF haipitii? Kama kuna mmoja wetu mwana JF yuko karibu na ofisa wa ngazi ya juu ambaye yuko karibu na JK wampe website hii awe anapitia pitia ina manufaa sana ni "Online Saigon" hii isipuuzwe kabisa. Suala la matumizi mabaya ya pesa liko hapa katika kila anayeteuliwa na Rais kutaka apewe Landcruiser VX ama GX kwanini tusiwe woga kwa hili. Mwl umetuacha pabaya. Na ulisema mtanikumbuka sana. Na kweli tunakukumbuka sana.
      Idea ya kusimamia haya magari ni nzuri. Tatizo ni kuwa mradi huu ni viable au kuna watu wanaandaa ulaji wao? Nadhani watu wanakumbuka issue ya speed Gavana ilikuwa hivi hivi kumbe ni mradi wa mtu au kunamtu kashakula 10% wenyewe wanarema MKUKUBI (Mkakati wa kukuza kukuza umasikini na kukuza uchumi Binafsi) Wasiwasi wangu ni kuwa mradi huu unaweza kuongeza gharama za matumizi kuliko ilivyo sasa.

      Swa la kujiuliza je kweli tunahitajia magari mengi kiasi hicho? ni mtumishi wa ngazi gani anatakiwa kuwa na gari ya serikali? Mfano mkurugenzi au mkurugenzi msaidizi anakaa Masaki Dereva anakaa Kibaha na analala huko na gari hivi kweli hapa masaki tunahitaji 4WD CC 4,000? Kwanza mimi na shangaa hawa hawa ndio wanapewa exemption ya kodi.

      Nadhani wafanye kama Kagame alivyouza magari hii ndio njia rahisi na nyepesi. Watangaze public Auction na watu binafsi wanunue na TAKURU wahakikishe hayauzwi kama nyumba za serikali zilivyouzwa.
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE

    6. #64
      Bro,Jay4's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th August 2007
      Posts : 385
      Rep Power : 676
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Mie nauliza kitu kimoja,huku mamtoni ni nadra kuona mtu ana dereva,wengi wao kila mtu anapiga kirungu mwenyewe,labda tu viongozi wakubwa kama senators na magavana,lakini bongo hadi DC ana dereva,na serikali inamlipia kila kitu,huu umaskini ni wa kujitakia tu.
      SOMENI ALAMA ZA NYAKATI, CCM KABURI LIMECHIMBWA KILICHOBAKI NI KUWAFUKIA

    7. #65
      Koba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2007
      Location : Pasadena California
      Posts : 4,006
      Rep Power : 1408
      Likes Received
      177
      Likes Given
      103

      Default

      Quote By Bro,Jay4
      Mie nauliza kitu kimoja,huku mamtoni ni nadra kuona mtu ana dereva,wengi wao kila mtu anapiga kirungu mwenyewe,labda tu viongozi wakubwa kama senators na magavana,lakini bongo hadi DC ana dereva,na serikali inamlipia kila kitu,huu umaskini ni wa kujitakia tu.
      ...hata hao Senators wanaendesha magari yao na ni magari yao na wala sio ya serikali,kweli jamani 11000 cruisers na mafuta tunazihudumia huo ni upuuzi wa hali ya juu,kila mtu anunue gari lake mbona walimu na wengineo wananunua ya kwao...magari yabaki machache tuu au maofisa wakubwa sana sio mpaka deputies na directors nao wanunuliwe gari na serikali...kwa kweli kama kuna kitu kinaweza kuipunguzia serikali matumizi basi ni hayo magari lakini sijui muungwana hata kama anafikiria...itabidi tuanzishe kampeni ili waache huu upuuzi,its time now!

    8. Miaka 50

    9. HAM
      #66
      HAM's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th September 2007
      Posts : 67
      Rep Power : 608
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Mimi kwa muono wangu ni kuwa ni lazima tufanye Tathmini kabla ya mradi kuanza.Unaweza ukapata gharama kubwa ya kusimamia Magari ya serikali kuliko hali ilivyokuwa kabla yake.
      Tukifanya Tathmini na kuona usimamizi utaleta value for money kwa maana kupunguza gharama ni dhahili kuwa mradi ufanyike.
      Wasiwasi mkubwa unakuja kwa uzoefu wa kampuni kutoka nje ya Tanzania kufanya kazi hizo,nadhani gharama yake itakuwa kubwa kuliko gharama ya sasa.
      Sio kama nakataa,napenda mchakato lakini si mchakato tu bali ni ule wenye maslahi na Taifa.Babu Ataka Kusema yeye haoni sababu ya kuhitaji kampuni toka South Afrika,pengine kuchukuliwa kwa Kampuni hiyo kumetegemea uwezo wa Kitechnologia ukilinganisha na kampuni za nyumbani.

      Nawasilisha.

    10. #67
      Joel's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st September 2007
      Location : Dar es salaam
      Posts : 299
      Rep Power : 658
      Likes Received
      33
      Likes Given
      26

      Default

      kusema ukweli swala la magari ya serikali linaumiza mno watanzania, maana kama member mmoja alivyosema hata deputy director naye ana shangingi.
      defender moja mpya inauzwa 30m halafu ni gari imara ajabu ambayo hata service yake haina gharama sasa sijui kwa nini wasitumie hayo tena kwa wale ambao kazi yao inawafanya wasafii mikoani mara kwa mara.wengine waliopo mijini watumie mabasi ya idara zao

    11. #68
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 811
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default

      Hii iumganishwe na ile nyingine ya mashangingi. By the way Mchambuzi siku hizi kazamia wapi?
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE

    12. #69
      Mr. Zero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2007
      Posts : 4,066
      Rep Power : 1433
      Likes Received
      478
      Likes Given
      72

      Default

      Quote By Mtoto wa mkulima
      Hii iumganishwe na ile nyingine ya mashangingi. By the way Mchambuzi siku hizi kazamia wapi?
      Kazi aliyotumwa na EL ameimaliza! Unaona sasa mambo kimya hakun anayemfuatilia EL!!!
      "The Only Necessary for the Triumph of Evil is for Good Men to do Nothing" Edmund Burke (1729 - 97)

    13. #70
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 811
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mr. Zero
      Kazi aliyotumwa na EL ameimaliza! Unaona sasa mambo kimya hakun anayemfuatilia EL!!!
      yeah na mimi nilijua tuu nitapata jibu mkuu. lakini naamini bado huwa anachungulia humu na kuona EL hashambuliwi kwa hiyo anapiga kimya. watu hapa walishabikia apewe U JF expert hehehehehehheheheh ila wengi walijiuliza atadumu hapa baada ya kumaliza kazi yake? Ila mshikaji yupo makini kiaina namkubali hasa inapokuja issue ya EL !!!!
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE

    14. BAK
      #71
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,533
      Rep Power : 44950
      Likes Received
      8273
      Likes Given
      8280

      Default

      Quote By Mtoto wa mkulima
      Hii iumganishwe na ile nyingine ya mashangingi. By the way Mchambuzi siku hizi kazamia wapi?
      Hakuna haja ya kuiunganisha hii. Hii ni update kutafuta habari kama kuna utekelezaji wowote uliofanyika tangu tamko la sirikali.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    15. #72
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 811
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Bubu ataka kusema
      Hakuna haja ya kuiunganisha hii. Hii ni update kutafuta habari kama kuna utekelezaji wowote uliofanyika tangu tamko la sirikali.
      Sawa mkuu nashukuru kwa kunielewesha na ni kweli maana kuna issue nyingi huwa tunajadili hapa na zinaishia hewani naona juzi Mkjj alikuja na update zake hapa na hii ndio inatakiwa mwana kama ni kula tunakula hadi mkia mfano issue ya Ditto inaishia kiaina etc. I agree is good idea.
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE

    16. BAK
      #73
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,533
      Rep Power : 44950
      Likes Received
      8273
      Likes Given
      8280

      Default Vigogo wadaiwa kukwamisha mpango wa mashangingi

      Hivi Rais akiamua jambo kwa manufaa ya nchi Mawaziri wanaweza kumpinga kweli!?

      Posted Date::12/19/2007
      Vigogo wadaiwa kukwamisha mpango wa mashangingi
      Na Ramadhan Semtawa
      Mwananchi

      WAKATI kukiwa na kilio cha wadau mbalimbali, likiwemo Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kutaka serikali ipunguze ununuzi na uendeshaji magari ya kifahari na badala yake kuboresha maslahi ya wafanyakazi, sasa mpango unadaiwa kwamishwa na baadhi ya watendaji wajuu serikalini.

      Mpango wa kupunguza magari hayo ulitolewa kama agizo kutoka Ikulu, lakini hadi sasa utekelezaji wake nunasuasua kutokana na kukumbana na upinzani kutoka kwa baadhi ya mawaziri na watendaji serikalini.

      Habari zilizopatikana kutoka serikalini zinaeleza kwamba wanaohujumu mpango huo ni wale wanaomiliki magari hayo kwa kujiuzia kwa njia ya mkopo, hivyo kunufaika na utaratibu wa serikali wa kuendelea kuyanunua.

      Kiutaratibu magari ya serikali baada ya kupita muda wa miaka karibu mitano hukopeshwa kwa watumishi wake au mengine kuuzwa kwenye minada. katika orodha ya watumishi wanaonunua wamo makatibu wakuu na hata mawaziri.

      Taarifa hizo zinaeleza kuwa tayari utekelezaji wa kuhakiki magari hayo ulibaini kuwepo magari ya kifahari aina ya Toyota Landcruiser VX na GX takribani 2,000, ambayo yamenunuliwa katika vipindi tofauti.

      Idadi hiyo haihusu magari aina nyingine ya serikali, ambayo yakichanganywa yanafikia zaidi ya 10,000, ambayo baada ya uhakiki na utaratibu wa kawaida baadhi yao yalipaswa kuuzwa.

      Kununua gari moja aina ya VX hadi kukamilisha taratibu zake za kuliingiza nchini ni zaidi ya sh 110 milioni, ambazo zinaweza kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya 10 kwa gharama ya Sh7 milioni kwa kila chumba.

      Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo alilisema mwishoni mwa wiki kwamba mpango huo uko katika hatua za utekelezaji.

      Chambo ambaye alizungumza mbele ya Waziri wake, Andrew Chenge, alisema; " Hilo si suala la waziri, ni letu sisi watendaji. Kwa sasa suala hilo linaendelea kushughulikiwa na wakati ukifika likikamilika mtaambiwa".

      Hata hivyo, Chambo hakufafanua wala kujibu swali aliloulizwa kwamba wapo baadhi ya watendaji na mawaziri wanapinga mpango huo.

      Wakati Chambo akitoa jibu hilo, taarifa zaidi zinaonyesha suala hilo lilipaswa kufikishwa katika Baraza la Mawaziri kwa maamuzi, lakini hadi sasa haijafanyika kutokana na kukwama katika ngazi ya kisera.

      Vyanzo hivyo vinabainisha zaidi kwamba, wapo baadhi ya mawaziri hunufaika na magari hayo kutokana na kuyamiliki baada ya muda kwa kuyatumia katika shughuli binafsi za nyumbani mara baada ya kununuliwa mapya.

      Kwa mujibu wa taarifa hizo, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), inaongoza kwa kuwa na magari mengi mchanganyiko, ikifuatiwa na wizara ya afya kisha miundombinu yenyewe.

      Hivi karibuni serikali ilitangaza mpango wa kupunguza idadi ya viongozi wanaotumia magari hayo ambao kwa VX wangepaswa kuwa mawaziri na manaibu wao huku makatibu wakuu na manaibu watapata GX.

      Wakurugenzi wa Idara, Taasisi, Mamlaka na Mashirika ya Serikali watakuwa wakitumia magari ya kawaida ambayo yana thamani tofauti na VX na GX.

      Tayari uhakiki wa magari hayo ambayo ulianzia Ikulu na kisha Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), umekwisha kamilika katika wizara zote.

      Hivi karibuni TUCTA katika moja ya maazimio yake kutaka nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi, ni kuitaka serikali ipunguze matumizi ya anasa kwa kuacha kununua magari hayo ya kifahari.

      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    17. #74
      MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1396
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

      Default Re: Vigogo wadaiwa kuwamisha mpango wa mashangingi

      Mashangingi watu wachache- wakati wananchi wengi maskini -wala hawana mlo- je huu ni uungwana???? Nyumba mbavu za mba- wakati kiongozi unaenda na gari la 100m kuwahamasisha waondokane umaskini- hii inawezekana kweli??

      Pesa ni hiyo2 ya mlipa kodi na misaada!
      Uadilifu Kiwe Kigezo Muhimu Zaidi Kuwa Kiongozi Tanzania Kwa Sasa!

    18. #75
      Koba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2007
      Location : Pasadena California
      Posts : 4,006
      Rep Power : 1408
      Likes Received
      177
      Likes Given
      103

      Default Re: Vigogo wadaiwa kuwamisha mpango wa mashangingi

      kwa magari 10000 na bei ya 100m kila moja ni

      10000 x 100000000 = 1000000000000 ( billion 1000 au trilion 1) ukiongeza na posho za mafuta,matengenezo na madereva(nasikia mabosi wanapewa madereva),usisahau posho za safari..

    19. #76
      MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1396
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

      Default Re: Vigogo wadaiwa kuwamisha mpango wa mashangingi

      Tanzania sii maskini!

      We dont know how we prioritize the spending of our meagre resouces- ningekuwa JK ningepunguza sana matumizi ya haya magari ya bei mbaya natafuta Kampuni ya kutupa magari ya serikali- at 30m Max. ningepata tu toka China au India. Savings ningejenga shule za sekondari 1000 na Chuo Kikuu kingine zaidi ya Dodoma!

      I dont think kweli kuna mpango wa kuondoa umaskini- hii ni nadharia tuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!

      Yet JK kimyaa!!!!!!!!!! yupo US wala hayaongelie haya!
      Uadilifu Kiwe Kigezo Muhimu Zaidi Kuwa Kiongozi Tanzania Kwa Sasa!

    20. #77
      Mnhenwa Ndege's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th December 2007
      Posts : 247
      Rep Power : 634
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Vigogo wadaiwa kuwamisha mpango wa mashangingi

      it is very sad to know that other people in Bongo leave comfortably at the expense of the tax payers money, our money, our sweat, our votes. come the next election tutawapigia kura and they will continue doing the same.

      sasa nani wajanja sisi au wao? Abraham Lincon said; "you can fool some people some time but you cannot fool all the people all the time."time will tell

    21. #78
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,648
      Rep Power : 13618
      Likes Received
      834
      Likes Given
      318

      Default Re: Vigogo wadaiwa kuwamisha mpango wa mashangingi

      Nakubaliana na Koba kwa mikokotoo yake!
      Kwa utafiti wangu mwenyewe (kwani nishawahi kutumia shangingi), ni kwamba Toyota VX mpya (CC 4200) inatumia lita moja kwa kilometa 5.6 katika lami kama unaendesha kwa spidi isiyozidi kilometa 80 kwa saa, na idadi hiyo inapungua kama unaenda spidi zaidi ya hiyo! Na kwa kawaida injini za magari haya huanzia ujazo wa CC 3000 mpaka CC 5700, sasa kwa kiwango hiki cha injini na unywaji wa mafuta lazima gharama za uendeshaji ziwe juu. Chukulia umbali wa kutoka Dar Es Salaam mpaka Arusha, kilometa 768 (lami tupu), ina maana shangingi hili (tuchukulie mfano wa lile la cc 4200 ambayo ndio mengi sana waliyopewa wakuu wa wilaya na wakurugenzi) litatumia lita 137, kwa mwendo wa kilometa 80 kwa saa. Na kwa sasa lita moja ya dizeli ni kama shilingi 1400/-, kwa hiyo gari litatumia shilingi 1,075,200/-(milioni moja na elfu sabini na tano, kutoka Dar kwenda Arusha! Bado hujapiga mahesabu ya kurudi, hujamlipa dereva!

      Hiyo habari inasema serikali ina mashangingi kama 10,000 hivi! Sasa kama haya yote yanaenda Ngurdoto (ambako sijui umbali wake kutoka Arusha mjini) ina maana ni lita nyingi sana za dizeli zitatumika. Mfano, mkuu wa wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya ambaye yuko umbali wa kilometa 1610 kutoka mjini Arusha (iliko Ngurdoto)atatumia shilingi 2,254,000/- (milioni mbili na laki mbili na nusu) kwenda tu! Bado hajarudi. Nimechukulia wilaya hii kama mfano kwa sababu ina barabara ya lami tupu toka Kyela hadi Arusha, hapa hujaongelea safari ya mkuu wa wilaya ya Nkansi kule Rukwa ama yule wa Tunduru kule Ruvuma ambako hawajui hata lami inafananaje!
      Sasa mtu anaposema kuwa Tanzania ni maskini wakati kiongozi wa nchi hii hii inayodai ni maskini anatumia gari la milioni 110 kwa safari zisizo na ulazima inakuwa kama mzaha fulani vile!
      Nadhani hata Wajapani wanatushangaa sana tukiagiza na kutumia magari ya namna hiyo huku wakitupatia misaada ya kuendesha sirikali zetu!
      Kwa hiyo basi, sisi walipa kodi tunapopiga kelele kuhusu matumizi haya mabaya ya kodi zetu tunakuwa na mantiki! Kuna magari mengi tu ya bei rahisi na yenye "Four Wheel Drive" ambayo yana bei karibu robo ya ile ya shangingi, sijajua kwa nini hawa watawala wanakuwa na vichwa vigumu kuelewa somo hili.
      Hizi pesa za kuendeshea mashangingi zingebanwa na kutumika kutengeneza barabara zetu kwa kiwango cha lami, ili tuweze kutumia magari madogo (sedan/salon) kusafiria na kupunguza gharama.

      Naona niishie hapa, najisikia kupiga mtu!
      Last edited by Idimi; 22nd December 2011 at 12:38. Reason: picha
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    22. #79
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,648
      Rep Power : 13618
      Likes Received
      834
      Likes Given
      318

      Default Re: Vigogo wadaiwa kuwamisha mpango wa mashangingi

      Mjadala huu umeishia wapi?
      Mwageni mada hapa mahali jamani.
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    23. #80
      MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1396
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

      Default Re: Vigogo wadaiwa kuwamisha mpango wa mashangingi

      Tuna la kuongea IDIMI?

      Nchi ina watu wanakula kilaini..na JK yuko majuu anaomba misaada!

      Tz if and only if.. we revisit our spending priorities... hatuna haja ya misaaada!! Hatuhitaji hata shilingi moja ya wazungu!

      Tukusanye kodi, tuzibe kapu ninalovuja, na kupunguza matumizi kama haya ya mashangii.. period!

      Hii dhana ya Uvasko Da Gama na bakuli kuomba omba huwa nalichukia kama ukoma!

      Ukinifanya raisi leo.. in 5 to 10 years lazima nitaifanya budgeti isiwe tegemezi... and this is possible!
      Uadilifu Kiwe Kigezo Muhimu Zaidi Kuwa Kiongozi Tanzania Kwa Sasa!

    24. FemaTV & Radio
    Page 4 of 9 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Replies: 21
      Last Post: 5th May 2011, 15:22
    2. Replies: 3
      Last Post: 4th April 2011, 12:34
    3. Confirmed - Serikali kununua Mashangingi zaidi ya 100
      By Superman in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 31
      Last Post: 10th January 2009, 12:27
    4. Replies: 58
      Last Post: 30th December 2008, 13:16
    5. Serikali yashtukia uzito wa mzigo wa mashangingi ya viongozi
      By BAK in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 30
      Last Post: 24th December 2008, 05:58

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...