Re: Is Pres. Kagame behind General Imran Kombe's assasination?
Tatizo letu tunajua sana kuongea,utekelezaji ni sifuri.Hainiingii akilini kuwa Kagame alihusika na mauaji ya Kombe hata kama habari hiyo itakuwa imetoka CIA.Iliwezekana vipi kwa yeye kupenyeza majasusi wake mpaka wakapanga njama na kutekeleza mauaji hayo bila ya sisi wenyewe kugundua njama hizo.Na kama aliweza kutekeleza yote hayo bila ya watu wetu wa usalama kugundua basi kuna haja tena ya haraka kuunda upya mfumo wetu wa usalama wa Taifa ili tuepukane na mabaya yanayoweza kuja kujitokeza nchini mwetu zaidi ya suala la kifo cha Imran.Kwa mtazamo wangu ninaona kuwa haya yote yanatokana na maadui wa Kagame ambao bado wako katika zama zao za uhutu na utusi na wameshindwa kumkabili huyu jamaa na hivyo kutafuta njia mbadala ya kumchonganisha na jirani zake ili wasaidiwe katika kumkabili na hivyo kumuondoa madarakani ili kuendeleza sera zao za kibaguzi.Ni nani ambaye hajui na haoni kasi ya maendeleo iliyopo nchini Rwanda kwa sasa hivi?Mwacheni ajenge nchi yake sababu kwa hali ilipokuwa imefikia nchini Rwanda kama si kwa yeye kujitokeza ninaamini kabisa hali ingekuwa mbaya zaidi ya yale tuliyoshuhudia.Na kila siku iendayo kwa Mungu huwa ninaomba atujaalie Makagame japo wawili tu,mmoja aende Somalia na wa pili aje Tanzania ili kumaliza porojo za mitaani na kurudisha watu katika utekelezaji wa majukumu ya ujenzi wa nchi na kuondoa uzembe usio na maana unaorudisha nyuma maendeleo kwa kisingizio cha demokrasia(Tanzania) na huyu sio wa ukoo wangu(Somalia)Mchawi wetu tunaye wenyewe,tusijaribu kufuata mambo ya nchi jirani kuficha matatizo yetu.I stand to be challenged.
UKICHOKA KUFANYA SIRI,FUMANIWA TU YAISHE . By Simon Kitururu.
Follow Us Here