Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

    Report Post
    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 92
    1. #1
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,859
      Rep Power : 7686
      Likes Received
      1467
      Likes Given
      0

      Default Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Katika zama zetu za leo kuna janga kubwa linalohatarisha uhai wa jamii ulimwenguni. Mithili ya virusi vinavyoua mwili, janga hili linasababisha msiba mkubwa wa kijamii. Janga hilo ni mmomonyoko wa maadili ambayo husaidia kustawisha jamii ya Ushoga, Ukahaba na uhusiano haramu wa kijinsia kabla ya ndoa na nje ya ndoa, Filamu za ngono, Picha za ngono, unyanyasaji wa kijinsia na ongezeko la maradhi ya zinaa, mashindano ya kukaa uchi maarufu ulimbwende, uuzaji na utumiaji wa vileo na dawa za kulevya miongoni mwa vijana ni miongoni mwa ishara kubwa za kuporomoka kwa maadili.

      Ushoga, usagaji, ubasha na ukahaba ni jambo baya na lisilokubalika kwenye jamii iliostaarabika, na karibia dini zote jambo ili linachukuliwa kuwa ni dhambi kubwa sana. Binadamu hapaswi kufuata mwendo huu ambao ni kinyume na maumbile aloumbiwa.

      Mambo haya ndiyo yamekuwa yakizishughulisha jamii. Idadi kubwa ya watu haijali hatari hii inayozidi kuwa kubwa na wanaiona kama jambo la kawaida tu. Lakini takwimu zinaonesha kuwa kila siku ipitayo kiwango cha hatari kinazidi kuongezeka. Ongezeko la maradhi ya zinaa ni kigezo kikuu cha kusaidia kuonesha ukubwa wa matatizo yanayomkabili mwanadamu.

      Kwa mujibu wa rekodi za Shirika la Afya ulimwenguni magonjwa yanayotokana na zinaa yanachukuwa sehemu kubwa ya maradhi. Ripoti zinaonesha kuwa kati ya kesi mpya za magonjwa ya zinaa zinazokadiriwa kufikia milioni 333 kila mwaka ulimwenguni kote, Ukimwi ndio tatizo kubwa zaidi.

      Kuna ongezeko la idadi ya maambukizi ya ukimwi yanayofikia watu million 2.6 kila mwaka, na vifo vya watu visivyopungua milioni 1.8 kwa mwaka.
      Takwimu za Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) zinaonesha kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi tokea pale ulipoanza imefikia watu milioni 18.8. Ripoti za shirika hilo kwa mwaka 2000 zinaielezea hivi hali ya mambo: “Ukimwi una nafasi ya kipekee katika kuleta athari mbaya za kijamii, kiuchumi na katika mipango ya sensa ya maendeleo”.

      Miongoni mwa mambo mabaya kabisa yanayozidi kushamiri ni ushoga. Katika baadhi ya nchi jambo hili limehalalishwa kama ndoa, linapewa heshima zote za ndoa na limeundiwa vyama na jumuiya. Duniani kote uovu huu unapingwa. Kushamiri kwa ushoga hivi leo kunatukumbusha hatima ya watu wa Lut waliokithiri katika uovu huu. Kama isemavyo Qur’an na Biblia, walipoukataa wito wa Lut kuiendea njia sahihi, Mwenyezi Mungu aliuangamiza mji na watu wake kwa maangamizi makubwa.

      Ushoga wa aina yoyote ule ni Haramu kwa mujibu wa Qur'an na Biblia kwa kupitia mifano ya Kaumu Lut. Aya zifuatazo zinatufahamisha wazi kuwa Ushoga kwa jinsi yake umekatazwa kwa binadamu wote.

      Na tulimtuma Lut', alipo waambia watu wake: Je, mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote kwa uchafu huo katika viumbe vyote! Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio mkwawacha wanawake? Kumbe nyinyi ni watu wafujaji!
      Q 80-81

      Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
      Leviticus 18:22

      "Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume? Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!"
      Q 26:165-166

      Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti...

      1 Corinthians 6:9

      Mwenyezi Mungu amekataza mahusiano yoyote yale kati ya Mume na Mke, nje ya ndoa au mahusiano ya jinsia moja yaani wanaume kwa wanaume au wanawake kwa wanawake.

      Mashoga wengi wakisaidiwa na wanasiasa, madaktari na wanaharakati kama vile TGNP (Tanzania Gender Networking Programme) uona ushoga kama hali ya kuzaliwa nao na ni uhuru wa mtu kuchagua aina ya maisha yake na jinsi ya kuyaendesha.

      Madaktari wenye kushabikia hali hii ya ushoga, usema kuwa wengi wao mashoga wamezaliwa wakiwa na gene za ushoga kwa hali hiyo hawapaswi kwenda kinyume na matashi na matakwa ya nafsi zao kwa kuwa wameumbwa au kuzaliwa hivyo.

      Swali la kuwauliza ni ili vipi wale wenye tabia ya wizi, ubakaji na uuwaji, je nao wamerithi au wamezaliwa na jene za tabia hizo za wizi na ubakaji!?
      Je wale wanao waingilia wanyama (bestiality) na wanaotembea na watoto zao wa kuwazaa (incest), vipi nao wamezaliwa hivyo!?

      Je madaktari wanatufahamisha nini kuhusianan na swala hili la kuzaliwa na gene zinazodaiwa kuwa zinasababisha ushoga?

      Madaktari wanasema nini kuhusiana na Jambo hili:

      William Byne, M.D., Ph.D., stated in his Journal of Homosexuality article "Science and Belief: Psychobiological Research on Sexual Orientation" (1995, Vol. 28, No. 3/4, pp. 303-344):
      "While some authors have speculated about the existence of 'genes for homosexuality,' genes in themselves cannot directly specify any behavior or cognitive schema. Instead, genes direct a particular pattern of RNA synthesis which in turn specifies the production of a particular protein.
      There are necessarily many intervening pathways between a gene and a specific behavior and even more intervening variables between a gene and a pattern that involves both thinking and behaving
      ."
      The term 'homosexual gene' is, therefore, without meaning, unless one proposes that a particular gene, perhaps through a hormonal mechanism, organizes the brain specifically to support a homosexual orientation.

      Psychiatrist Jeffrey Satinover, M.D., wrote in his article "The Gay Gene?" published on the Campus Crusade for Christ International website Leadership U on 7/13/02:
      "There is not any evidence that shows that homosexuality is 'genetic', and none of the research itself claims there is. Only the press and, sadly, certain researchers do-when speaking in sound bites to the public.
      Homosexuality may run in families but you get viruses from your parents, too, and some bad habits. Not everything that is familial is innate or genetic
      ."

      Simon LeVay, Ph.D., stated in a 1994 interview that appears in an article entitled "Sexual Brain" published in Discover (Vol. 5, No. 3, pp. 64-67):
      "It's important to stress what I didn't find. I did not prove that homosexuality is genetic, or find a genetic cause for being gay. I didn't show that gay men are born that way, the most common mistake people make in interpreting my work. Nor did I locate a gay center in the brain."

      George P.A. Rice, Ph.D. et al., wrote in Science (1999, Vol. 285, p. 803a):
      "We still contend that an X-linked gay gene could not exist in the population with any sizable frequency, due to the strong selection against it...
      We agree with Hamer that our results do not exclude the possibility of genetic effects underlying male homosexuality. But with the use of similar methods of family ascertainment, phenotyping, and genotyping, we were unable to confirm evidence for an Xq28-linked locus underlying male homosexuality."

      A. Dean Byrd, Ph.D., MBA, MPH et al. wrote in "The Innate-Immutable Argument Finds No Basis in Science," published in the May 27, 2001 Salt Lake City Tribune:
      "What is clear, however, is that the scientific attempts to demonstrate that homosexual attraction is biologically determined have failed. The major researchers now prominent in the scientific arena-themselves gay activists-have in fact arrived at such conclusions.
      There is no support in the scientific research for the conclusion that homosexuality is biologically determined."

      Kwa ujumla madaktari wanasisitiza kuwa, jene huwa hazionyeshi kuwa mtu anaweza kuzaliwa na tabia Fulani kama vile ushoga, yaani hakuna bibadamu anayezaliwa na jene za ushoga na tafiti hazionyeshi kuwa tabia za kishoga zipo kwenye jene, bali ushoga ni hali ambayo binadamu ujifunza kutoka kwenye jamii anayoishi na si kuzaliwa nayo.

      Maisha ya binadamu ni mitihani kila binadamu ana mtihani wake tofauti na mwenzake. kwa mfano kuna walozaliwa vipofu, kuna viziwi na vilema vya kila aina kuna walozaliwa katika familia za kimaskini na kuna walozaliwa kwenye utajiri, kuna walefu na wafupi wembamba na wanene... lakini licha ya ulemavu wao hali zao au maumbile yao kila mmoja anapaswa kuishi kulingana na sheria za Mwenyezi Mungu au zile tuliojiwekea wenyewe.

      Kuna ambao wanaishi bila kuoa au kuolewa na kuna ambao wako mbali na familia zao wote hao hawapaswi kwenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu... Wanatakiwa wazishinde hisia zao za kingono na kufuata sheria za Mwenyezi Mungu.

      Dhambi za kufanya ngono na ngono kinyume na maumbile ni moja ya mtihani mkubwa sana kuepukana nao, lakini kama utaamua kufuata matakwa na sheria za Mwenyezi Mungu kwa haki hautashindwa kuwa katika mwenendo mwema na haswa ukijikamatisha na swala/sala na dua/maombi ya kila mara basi Mwenyezi Mungu atakujaalia kushinda mitihani hiyo.

      Ushoga una athari nyingi za kiafya, ni rahisi sana kuambikizana maradhi ya ngono vile vile kwa mwanamke ambaye ni shoga kutumia kwake njia za aja kubwa kujistarehesha, ujisababishia kuregea kwa kizazi na wakati mwingine ushindwa kusukuma mtoto wakati wa kujifungua. Na hii ni hatari si kwa mtoto tu bali hata kwa mzazi mwenyewe.

      Na kwa upande wa wanaume pia kuna athari nyingi zikiwemo kuziba mirija yake ya kiume kupungua kwa nguvu zake za kiume, na maambukizo rahisi ya maradhi.

      Kwa hakika Mwenyezi Mungu hakuumba mashoga na wasagaji. Hii ni hali ya tamaa ya kibinadamu, tabia hii anaipata aidha kwa kushawishiwa au kuiga kutokana na mazingira aliyokulia.

      Na ujikuta baada ya mazoea ya kipindi kilefu maumbile yake na tabia zake zimebadilika na kushabihiana za upande wa pili. Athari unazozipata kwa kujifanya mke au mume yaani kuwa kinyume na maumbile yake ya asri, tabia hizo zinakupelekea kuharibika kwa mfumo wako wa kigene... Haya yanatokea baada ya kipindi kirefu cha kujifanya shoga...!

      Hakujawahi kutokea mtoto alozaliwa leo akapimwa gene zake na matokeo yakasema kuwa kijana au msichana huyu atakuja kuwa na tabia za ushoga, usagaji, wizi au ubakaji...!!

      Haya ni maisha ambayo binadamu anajitengenezea au kutengenezewa na wale walomtangulia au alowatangulia... Ushoga upo ndani ya uwezo wetu hiki si kilema cha kuzaliwa nacho...

      Inafahamika kuwa kila binadamu ana sehemu mbili ndani ya nafsi yake yaani hasi na chanya (Positive & negative) wema na uovu. Hali hizi siku zote ushindana... Hapo ni juu yako kuamua ni kipi cha kukifuata kile ambacho unahisi kinakupendeza sasa na kikakuangamiza kesho au kile ambacho unahisi hakikupendezi leo lakini kikakuokoa kesho...

      Leo hii nchi zilizoendelea kama Uingereza zimepitisha mitaala ya kufundishia mashuleni kuanzia shule za chekechea, mitaala hii ni ile ya kuwafundisha watoto wao kuwa suwala la ushoga ni jambo la kawaida tu, na kila mtu ana haki ya kuchaguwa jinsia aipendayo anapofika umri wa miaka 16.

      Vitabu na vijarida vingi vimeandikwa katika kadhia hii ya kushabikia ushoga. Kuna vitabu vya watoto vyenye hekaya za kushawishi na kufundisha, kuwa kuishi na wazazi wa jinsia moja (homosexual) ni jambo jema na si jambo baya au la ajabu, kinachozingatiwa tu wewe mtoto anyanyaswi na wazazi hao wa kishoga.

      Ni ngumu kidogo kuiwacha hii tabia, lakini ni jambo lililo ndani ya uwezo watu wa kuamua. Kuna masimulizi mengi ya watu ambayo walisha wahi kuwa mashoga kwenye jinsia zote mbili. Na wengi wao wamefanikiwa kuondokana na hali hii ya ushoga na wamewacha kabisa na wengi wao wameamua kuwemo kwenye ndoa za halali (ndoa ya mke na mume) na maisha yao ni ya furaha... haya hayaji tu kwa kusema mungu akipenda bali kwa kufanya jitihada za kweli na kumuomba Mwenyezi Mungu akupe wasaa na nguvu za kutotamani kurudi kwenye maangamizi...!

      You were not born with homosexual preference. Nobody is...!
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)

    2. FemaTV & Radio

    3. #21
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,859
      Rep Power : 7686
      Likes Received
      1467
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Quote By Nehondo
      Nakupinga jambo moja la TGNP kusupport mashoga sio kweli. Mi nilikuwepo kwenye matukio yote ya gender festival ambayo yanatumika kama platform ya watu kuongea kuhusiana na theme zinazowekwa. Na TGNP walijibu kuwa wao wanatambua jinsia mbili tu ya mwanamke na mwanaume...na sio mashoga au wasagaji.

      Na kuhusu maadili ni kweli yanamong'onyoka kwa sababu ya utandawazi. Media inapositive na negative side...na negative side ndo hiyo so serikali inabidi iwe makini na media
      Mkuu, kwa habari za kuaminika ni kwamba hao mashoga siku ile ya tamasha walialikwa rasmi na TGNP, na si kualikwa tu, walilipwa mpaka posho za maudhurio.

      Hii hapa chini ni mmoja wa waandishi Dada Gloria Tesha. Mwandishi wa habari kutoka gazeti la habari leo

      Na hii ndio sehemu ya ripoti yake.

      Quote By Gloria Tesha
      SIKUWEZA kujizuia kutokwa machozi pale nilipomuona mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 14 hadi 16 akitembea kwa kutingisha makalio, na kuzungumza huku akicheka kama mtoto wa kike katika Tamasha la 10 la Jinsia jijini Dar es Salaam lililofanyika wiki iliyopita.

      Hata hivyo niligundua kuwa hayupo peke yake baada ya kuona kundi la vijana kama yeye wanaojulikana kama mashoga likipitia huku na kule katika tamasha hilo na wakati mwingine kujitambulisha kama wanawake.

      Nilianza kuwaonea huruma wazazi wao na pia kuwalaumu lakini pia nikailaumu jamii na hata serikali kwa kuwa nilijua nguvu za taasisi hizo zingeweza kuwanusuru watoto na vijana hao kuwa mashoga kwa kuwa niliamini kibaiolojia zipo tiba na kisaikolojia pia.

      Kilichonisukuma kuandika wazo hili pamoja na uchungu kwa hali ya vijana wale na pia baada ya kuona wanaharakati wakigawanyika kutokana na ushiriki wa mashoga hao katika Tamasha hilo huku wengi wakiilaumu TGNP kuwaalika mashoga hao katika tamasha hilo wakidai tabia na mambo wanayoyafanya vijana na wanaume hao si maadili ya Kitanzania na inahamasisha jamii iamini kuwa ni kitu cha kawaida.

      Pamoja na malalamiko hayo, TGNP haikuwa wazi kueleza kuwa imewaalika au la baada ya kudai kuwa tamasha ni huru kwa kila mtu, halikubagua mtu kwa jinsia, kabila, dini au rangi.

      Hata hivyo baadaye ilifahamika kuwa waliwaalika kwa kuwa waliwalipa posho ya ushiriki wao. Nami kwa sehemu nakubaliana na wanaharakati hao kuwa tamasha lilikuwa huru kwa kila mtu.

      Hakuna aliyekasirika ushiriki wa yeyote, lakini kwa mashoga hawa, lawama zilikuwa nyingi kutokana na namna walivyojitambulisha kuwa ni wanawake wakati ni wazi ni wanaume na kutaka Katiba Mpya iwatambue huku baadhi ya wanaharakati wakionekana kuwatetea kuhusu suala hilo la Katiba.

      Binafsi naona huu si utetezi wa haki za binadamu bali ni ukatili wa jinsia, najua nitawaudhi wengi katika hili, lakini nani asiyefahamu kuwa nchi hii inaongozwa na sheria na kanuni na iko wazi kuwa kumuingilia mtu kinyume cha maumbile ni kosa la jinai?

      source: HabariLeo
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)

    4. #22
      Papa Mopao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th October 2009
      Posts : 1,740
      Rep Power : 837
      Likes Received
      248
      Likes Given
      344

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      [QUOTE=afrodenzi;2591317]Hivi kumbeee

      Quote By IGWE

      . i meant what i said...

      kwani we una shida nao??
      na Je wamekufanya nini??
      Tuangalie usalama wa vizazi vijavyo kiroho na kimwili, Mungu atawaweka wapi watoto wako, wajukuu zako kwa haya madhambi?

    5. #23
      Losemo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th March 2010
      Posts : 175
      Rep Power : 499
      Likes Received
      26
      Likes Given
      8

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Wako wapi kina Mzee wa upako, kakobe. Lwakatare, Mwingira and the like waombee pepo hili liondoka na sio kujidai wanaondoa mapepo kumbe wanadanganya watu. ningwaelewa wangeshughulikia mambo ya msingi kama haya na sio kujidai utapata gari la mzee wa upako

    6. #24
      KIBONGOMKUTI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 666
      Rep Power : 565
      Likes Received
      160
      Likes Given
      222

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Duh nawaheshimu sana TGNP wanaharakati wa ukweli na wenye mafanikio makubwa, lakini kama ni kweli wameanza kushadadia mashoga nahisi hii itakuwa inasababishwa na mambo mengi baadhi yaake yakiwa ni
      (a) TGNP kutegemea wafadhili ili kuendesha shughuli zake na hatimae kulazimika kumeza matapishi ya wahisani wao kwa kukiuka mila na desturi zetu nzuri na kuleta mabadiliko ambayo hata hao walioendelea wanajutia yalipowafikisha.
      (b) Baadhi ya Wanaharakati wa TGNP watakuwa wameshajiunga na hao mashoga na wanataka kusambaza sumu ya ushenzi kwa kuuvikakofia ya unaharakati.
      (c) TGNP wameanza kulewa sifa kama tulivyo wanadamu wengi sasa wanaanza kudandia Treni kwa mbele.
      Maundumula likes this.

    7. #25
      Kabengwe's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th October 2009
      Location : Kusadikika
      Posts : 221
      Rep Power : 531
      Likes Received
      11
      Likes Given
      12

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      We are polluted by the media.

      Media inafanya tuone ushoga, kuvaa robo tatu uchi, mauaji, fujo etc ni mambo ya kawaida.
      Kizazi kinachokuja kuja kitakuwa polluted even more. Bora hata kizazi chetu kimekuwepo wakati media haijachafuka kiasi ilichofikia.

      Ushoga kwa watu walioishi nje ya nchii ni jambo la kawaida coz wameshahalibiwa na media movement towards publicizing social evils

      Ni vita ngumu sana. Na sehemu sahihi kurekebisha haya mambo ni familia which is also spoiled.
      Maundumula likes this.

    8. Miaka 50

    9. #26
      Roulette's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 15th December 2010
      Posts : 5,472
      Rep Power : 35628
      Likes Received
      5024
      Likes Given
      5750

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Kwa kweli, Qur'an inasema (Suratul Tin, 95) : Alahi Salah bi Ahkamil Hakimil (Isn't God the greater of all the juges?)
      Na Bibilia inasema (Matayo 7: 1-5): Do not judge, or you too will be judged.
      Nauliza, hivi kuna big sinners and small sinners? If we are all sinners, who gives you the right to condemn the sins commited by other persons? huyajui maisha yao, na hujui ni wema gani wanafanya. we mwenyewe ulipo huja kamilika.
      Naomba tuwe waelewa na kabla ya kuhukumu tuanze kwa ushahuri.
      Asanteni.
      Gaijin and Azimio Jipya like this.
      Information is not knowledge

      Albert Einstein

    10. #27
      bwaxxlo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th October 2009
      Posts : 145
      Rep Power : 1343
      Likes Received
      100
      Likes Given
      15

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Kusema ukweli, nimefanya kazi na mashoga kadhaa katika nchi mbalimbali. Nachotaka kueleza ni kwamba, hawa watu wako katika kila sehemu. Sitashangaa kama humu ndani baadhi yenu ni 'closeted'. Kwanza naomba uelewe jambo moja: Binadamu sio wanyama pekee wanaotabia ya kupendelea kufanya mapenzi na wanyama wa jinsia moja. Kwa listi kamili ya wanyama wote wenye tabia hii, gonga kwenye link hii: List of animals displaying homosexual behavior - Wikipedia, the free encyclopedia.

      Wengi hapa mnatumia kitu tofauti kujielezea pointi zenu. Ni sawa sawa na mtu kutumia kijiko kulima halafu aseme baadae kuwa kulima shamba ni impossible kwa sababu kijiko hakiwezi kutumika. Kutumia kitabu cha dini ambayo tayari inapinga tabia fulani basi unakuwa biased. Cha pili, tuache double standards. Nina hakika baadhi yenu hapa mnafahamu wanaume/wanawake mitaani kwenu ambao kwa namna moja au nyingine anavutiwa zaidi na watu wa jinsia yake. Nakumbuka shule ya sekondari kuwa watu walikuwa wanamtamani mwanaume mwenzao walale naye. Hiyo tayari ni tabia ya homosexual. Tatu, tabia ya binadamu katika kutamani binadamu wenzake sio black & white kama mnavyotaka kuiweka. Fikiria tabia ya binadamu katika kutamaniana ni curved. Kwa kitaalamu inaitwa Kinsley scale. Katika ironic twist, sio kwamba watu wanatamani 100% watu wa jinsia tofauti bali ni huwa wanatamani watu wa jinsia zote mbili ila ni society ndio inawasukuma watamani jinsia moja zaidi kuliko nyingine. Kama ukichukua jamii ambayo haina idea ya homophobia, basi utaona kuwa sexuality inajionyesha kwa pande zote. Shida ni kwamba watu wengi mkifikiria mashoga, jambo la kwanza mnawaza kufirana. Hapo ndio unapokosea. Halafu, ukiangalia nchi nyingi ambazo tabia ya ushoga iko huru utagundua kuwa asilimia ya mashoga ni chini ya 1% ya adults wote. Kwa hiyo argument ya kuwa hakuna kuzaliana watoto haishiki maji. Mimi mwenyewe sidhani kuwa kuruhusu mashoga waoane ni idea nzuri Tanzania ila sioni sababu ya kuwapiga mawe. Kama watu wawili wamekuwabiliana, waache wafanye watakavyo ila mradi hakuna anayedhuriwa au kulazimishwa.

      A lot more damage is done by people panicking than with the actual situation they panic over.
      Roulette likes this.

    11. #28
      Gaijin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2007
      Posts : 11,319
      Rep Power : 12953
      Likes Received
      4591
      Likes Given
      2499

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Quote By RussianRoulette
      Kwa kweli, Qur'an inasema (Suratul Tin, 95) : Alahi Salah bi Ahkamil Hakimil (Isn't God the greater of all the juges?)
      Na Bibilia inasema (Matayo 7: 1-5): Do not judge, or you too will be judged.
      Nauliza, hivi kuna big sinners and small sinners? If we are all sinners, who gives you the right to condemn the sins commited by other persons? huyajui maisha yao, na hujui ni wema gani wanafanya. we mwenyewe ulipo huja kamilika.
      Naomba tuwe waelewa na kabla ya kuhukumu tuanze kwa ushahuri.
      Asanteni.
      Kwanza nadhani Waislam hawana mfumo wa dhambi zote ni sawa. Wao dhambi zina daraja, na hukumu za dhambi hizo ziko wazi (watu wanatakiwa wachukuwe hizo hukumu)

      Pili, ikiwa tusihukumu, tusingepeleka wengine rumande kwa makosa ya kuiba na mengineyo kwa sababu hatujui wema gani wanafanya (maybe they are like Robinhood). Kwa hiyo kukaa tukasema tusihukumu hilo halipo, kama vitabu vimeandika matendo fulani ni dhambi, sisi kuyasema hayo matendo ni dhambi hatujahukumu, Mungu ndiye aliyehukumu kwa kutuambia kuwa hayo ni dhambi.

      Ama kwa kuchukua hatua za kuwanyanyasa sio sawa, lakini kupigia kelele na kusema kuwa ni uovu hakuna ubaya.
      Azimio Jipya and Maundumula like this.

    12. #29
      Apollo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2011
      Location : Dar Es Salaam, Tanzania. ZION.
      Posts : 3,397
      Rep Power : 1083
      Likes Received
      658
      Likes Given
      1301

      Default

      Quote By Gaijin

      mkuu, tupe mistari na sio kusema tu. Mbona mwenzio ametoa mistari kutoka kwenye quran.

    13. #30
      Apollo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2011
      Location : Dar Es Salaam, Tanzania. ZION.
      Posts : 3,397
      Rep Power : 1083
      Likes Received
      658
      Likes Given
      1301

      Default

      Quote By bwaxxlo
      Fikiria tabia ya binadamu katika kutamaniana ni curved. Kwa kitaalamu inaitwa Kinsley scale. Katika ironic twist, sio kwamba watu wanatamani 100% watu wa jinsia tofauti bali ni huwa wanatamani watu wa jinsia zote mbili ila ni society ndio inawasukuma watamani jinsia moja zaidi kuliko nyingine. Kama ukichukua jamii ambayo haina idea ya homophobia, basi utaona kuwa sexuality inajionyesha kwa pande zote. Shida ni kwamba watu wengi mkifikiria mashoga, jambo la kwanza mnawaza kufirana. Hapo ndio unapokosea. Halafu, ukiangalia nchi nyingi ambazo tabia ya ushoga iko huru utagundua kuwa asilimia ya mashoga ni chini ya 1% ya adults wote. Kwa hiyo argument ya kuwa hakuna kuzaliana watoto haishiki maji. Mimi mwenyewe sidhani kuwa kuruhusu mashoga waoane ni idea nzuri Tanzania ila sioni sababu ya kuwapiga mawe. Kama watu wawili wamekuwabiliana, waache wafanye watakavyo ila mradi hakuna anayedhuriwa au kulazimishwa.

      A lot more damage is done by people panicking than with the actual situation they panic over.
      hapo umeongea ukweli.

    14. #31
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,291
      Rep Power : 1195
      Likes Received
      1179
      Likes Given
      1551

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Mimi nikaishakutana na mtu mwenye falsa ya kwamba dini zote zinamuabudu Mungu mmoja
      huwa naachana naye hapo hapo. hivyo nimeishia kwenye kipengele hiki na karibia dini zote jambo ili linachukuliwa kuwa ni dhambi kubwa sana.
      mwanzoni kabisa. nitaimiss hii makala

    15. #32
      Gaijin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2007
      Posts : 11,319
      Rep Power : 12953
      Likes Received
      4591
      Likes Given
      2499

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Quote By Apollo
      mkuu, tupe mistari na sio kusema tu. Mbona mwenzio ametoa mistari kutoka kwenye quran.
      Huyo niliemwambia keshaelewa .......au kama bado atasema afahamishwe, naamini X-paster atampa mistari yakumtosha tu
      Roulette likes this.

    16. #33
      Roulette's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 15th December 2010
      Posts : 5,472
      Rep Power : 35628
      Likes Received
      5024
      Likes Given
      5750

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Quote By Gaijin
      Kwanza nadhani Waislam hawana mfumo wa dhambi zote ni sawa. Wao dhambi zina daraja, na hukumu za dhambi hizo ziko wazi (watu wanatakiwa wachukuwe hizo hukumu)

      Pili, ikiwa tusihukumu, tusingepeleka wengine rumande kwa makosa ya kuiba na mengineyo kwa sababu hatujui wema gani wanafanya (maybe they are like Robinhood). Kwa hiyo kukaa tukasema tusihukumu hilo halipo, kama vitabu vimeandika matendo fulani ni dhambi, sisi kuyasema hayo matendo ni dhambi hatujahukumu, Mungu ndiye aliyehukumu kwa kutuambia kuwa hayo ni dhambi.

      Ama kwa kuchukua hatua za kuwanyanyasa sio sawa, lakini kupigia kelele na kusema kuwa ni uovu hakuna ubaya.
      Kuyaongelea sio kosa Gaijin, ila kama kweli tunaongea kwa maana ya kuleta mabadiliko tunatakiwa kusema ka ushahuri, sio kusema kwe kuhukumu. Mfano, nikiwa na rafiki yangu malaya malaya, siwezi kumwambia: on a mimi sio malaya, wewe ni malaya, unakosea. Hapo haiji kabisa.
      Ila nikimwambia: umalaya ni mbaya kwa sababu hizi (kidini, kimaadili (awe na yeye anaikubali hiyo dini na hayo maadili), kiafya, kwa image yako in general etc)
      Mwisho kabisa, dhambi katika uislam zina tofauti, ni kweli, ila hawajasema dhambi hii inarank wapi ukilinganisha na kuzini, kutembea nje ya ndoa, umalaya etc. Kwa hiyo mimi hadi sasa naichukulia at the level of dhambi zingine za ngono.
      Information is not knowledge

      Albert Einstein

    17. #34
      Gaijin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2007
      Posts : 11,319
      Rep Power : 12953
      Likes Received
      4591
      Likes Given
      2499

      Default Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Quote By RussianRoulette
      Kuyaongelea sio kosa Gaijin, ila kama kweli tunaongea kwa maana ya kuleta mabadiliko tunatakiwa kusema ka ushahuri, sio kusema kwe kuhukumu. Mfano, nikiwa na rafiki yangu malaya malaya, siwezi kumwambia: on a mimi sio malaya, wewe ni malaya, unakosea. Hapo haiji kabisa.
      Ila nikimwambia: umalaya ni mbaya kwa sababu hizi (kidini, kimaadili (awe na yeye anaikubali hiyo dini na hayo maadili), kiafya, kwa image yako in general etc)
      Mwisho kabisa, dhambi katika uislam zina tofauti, ni kweli, ila hawajasema dhambi hii inarank wapi ukilinganisha na kuzini, kutembea nje ya ndoa, umalaya etc. Kwa hiyo mimi hadi sasa naichukulia at the level of dhambi zingine za ngono.
      Kwanza dhambi hizo ulizozitaja zina rank kwenye uislam

      Ushoga na usagaji uko juu (ndo maana jamii nzima iligharikishwa na hakuna jamii ilogharikishwa kwa adultry)

      Mbili kwenye rank inakuja anaefanya zinaa Hali yupo kwenye ndoa ( ndo maana adhabu yake ipo kubwa zaidi kuliko mzinifu aliye single)

      Tatu ndo anakuja mzinifu asiye katika ndoa.

      Na hata mtu awe na maisha mema kiasi gani akifanya dhambi ya zinaa anatakiwa ahukumiwe kwa dhambi hiyo bila ya kuangalia maisha yake sehemu nyengine ( na hiyo ndo hukumu ya Kiislam)

      So kuwa kila mmoja wetu ana dhambi kwa hiyo asizungumze kuhusu hukumu zikizoainishwa tayari na Mungu ni makosa

      Ni sawa na kumuona mwizi ukasema tusimhukumu (kidini) kwa vile ni mwema wakati mwengine.

      Dini zinaruhusu mtu kuhukumiwa kwa Yale ambayo Mungu ameshayatolea hukumu

    18. #35
      simplemind's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2009
      Posts : 2,844
      Rep Power : 1154
      Likes Received
      508
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Kufanya ngono kinyume na maumbile siyo homosexuals tu hadi heterosexual couples,and it would appear the practice is spreading even among married couples.
      Roulette likes this.

    19. #36
      Nkwesa Makambo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 26th August 2011
      Posts : 1,029
      Rep Power : 0
      Likes Received
      163
      Likes Given
      153

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Quote By bwaxxlo
      Kusema ukweli, nimefanya kazi na mashoga kadhaa katika nchi mbalimbali. Nachotaka kueleza ni kwamba, hawa watu wako katika kila sehemu. Sitashangaa kama humu ndani baadhi yenu ni 'closeted'. Kwanza naomba uelewe jambo moja: Binadamu sio wanyama pekee wanaotabia ya kupendelea kufanya mapenzi na wanyama wa jinsia moja. Kwa listi kamili ya wanyama wote wenye tabia hii, gonga kwenye link hii: List of animals displaying homosexual behavior - Wikipedia, the free encyclopedia.

      Wengi hapa mnatumia kitu tofauti kujielezea pointi zenu. Ni sawa sawa na mtu kutumia kijiko kulima halafu aseme baadae kuwa kulima shamba ni impossible kwa sababu kijiko hakiwezi kutumika. Kutumia kitabu cha dini ambayo tayari inapinga tabia fulani basi unakuwa biased. Cha pili, tuache double standards. Nina hakika baadhi yenu hapa mnafahamu wanaume/wanawake mitaani kwenu ambao kwa namna moja au nyingine anavutiwa zaidi na watu wa jinsia yake. Nakumbuka shule ya sekondari kuwa watu walikuwa wanamtamani mwanaume mwenzao walale naye. Hiyo tayari ni tabia ya homosexual. Tatu, tabia ya binadamu katika kutamani binadamu wenzake sio black & white kama mnavyotaka kuiweka. Fikiria tabia ya binadamu katika kutamaniana ni curved. Kwa kitaalamu inaitwa Kinsley scale. Katika ironic twist, sio kwamba watu wanatamani 100% watu wa jinsia tofauti bali ni huwa wanatamani watu wa jinsia zote mbili ila ni society ndio inawasukuma watamani jinsia moja zaidi kuliko nyingine. Kama ukichukua jamii ambayo haina idea ya homophobia, basi utaona kuwa sexuality inajionyesha kwa pande zote. Shida ni kwamba watu wengi mkifikiria mashoga, jambo la kwanza mnawaza kufirana. Hapo ndio unapokosea. Halafu, ukiangalia nchi nyingi ambazo tabia ya ushoga iko huru utagundua kuwa asilimia ya mashoga ni chini ya 1% ya adults wote. Kwa hiyo argument ya kuwa hakuna kuzaliana watoto haishiki maji. Mimi mwenyewe sidhani kuwa kuruhusu mashoga waoane ni idea nzuri Tanzania ila sioni sababu ya kuwapiga mawe. Kama watu wawili wamekuwabiliana, waache wafanye watakavyo ila mradi hakuna anayedhuriwa au kulazimishwa.

      A lot more damage is done by people panicking than with the actual situation they panic over.
      hiyo ni juhudi za binadamu ambao ni'advanced wanyama pori' kuhalalisha ushenzi wao kwa kutafuta matendo yao kati ya wanyama pori. KWA HIYO BASI BINADAM MKAMILIFU HAWEZI KUKUBALIANA NA MAHUSIANO YA JINSIA MOJA ETI KWA VILE MBWA NAO WANAMAHUSIANO YA AINA HIYO. ni mtazamo unaotokana na matatizo ambayo sisi wenye busara ni budi tukae chini tutafiti tujue chanzo chake na namna ya kuwasaidia watu hawa.

    20. #37
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,859
      Rep Power : 7686
      Likes Received
      1467
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Muda si mrefu tutasikia vilio vya uongo kutoka kwa mashoga kuwa wananyanyaswa ili kupata sapoti ya David Cameron.
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)

    21. #38
      Roulette's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 15th December 2010
      Posts : 5,472
      Rep Power : 35628
      Likes Received
      5024
      Likes Given
      5750

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Quote By Gaijin
      Kwanza dhambi hizo ulizozitaja zina rank kwenye uislam
      Ushoga na usagaji uko juu (ndo maana jamii nzima iligharikishwa na hakuna jamii ilogharikishwa kwa adultry)
      Mbili kwenye rank inakuja anaefanya zinaa Hali yupo kwenye ndoa ( ndo maana adhabu yake ipo kubwa zaidi kuliko mzinifu aliye single)
      Tatu ndo anakuja mzinifu asiye katika ndoa.
      Na hata mtu awe na maisha mema kiasi gani akifanya dhambi ya zinaa anatakiwa ahukumiwe kwa dhambi hiyo bila ya kuangalia maisha yake sehemu nyengine ( na hiyo ndo hukumu ya Kiislam)
      So kuwa kila mmoja wetu ana dhambi kwa hiyo asizungumze kuhusu hukumu zikizoainishwa tayari na Mungu ni makosa
      Ni sawa na kumuona mwizi ukasema tusimhukumu (kidini) kwa vile ni mwema wakati mwengine.
      Dini zinaruhusu mtu kuhukumiwa kwa Yale ambayo Mungu ameshayatolea hukumu
      Kwa kweli sina utaalam mkubwa katika ufafanuzi wa dini ya kiislam ila leo ndio kuskia hiyo ranking. Itakua imefanyiwa baada ya Kur'an kuteremshwa (Bidaa)...
      Information is not knowledge

      Albert Einstein

    22. #39
      Gaijin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2007
      Posts : 11,319
      Rep Power : 12953
      Likes Received
      4591
      Likes Given
      2499

      Default Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Quote By RussianRoulette
      Kwa kweli sina utaalam mkubwa katika ufafanuzi wa dini ya kiislam ila leo ndio kuskia hiyo ranking. Itakua imefanyiwa baada ya Kur'an kuteremshwa (Bidaa)...
      Huna utaalamu kisha unakata "fatwa" kuwa ni bidaa...unanchekesha

    23. Ame
      #40
      Ame's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Location : Global Citizen
      Posts : 1,513
      Rep Power : 1184
      Likes Received
      650
      Likes Given
      2615

      Default Re: Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

      Even discussing ushoga kwangu ni evil....Kwani evil communication corrupts intents! Walaaniwe mashoga wote na washabiki wao maana wanaidhalilisha kazi njema ya uumbaji wa Mungu ambaye ametupa utashi na dhamira njema!

    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Chanzo cha kuzidi kuporomoka maadili
      By mdau wetu in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 2
      Last Post: 19th October 2011, 20:02
    2. Replies: 0
      Last Post: 6th July 2011, 10:49
    3. SIKUKUU YA IDD:Biashara ya KITI MOTO YAANZA KUSHAMIRI
      By Pdidy in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 9
      Last Post: 21st September 2009, 14:45
    4. kuporomoka maadili Vs maisha ya ndoa.
      By Mbu in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 36
      Last Post: 15th August 2009, 11:15
    5. Replies: 10
      Last Post: 13th February 2009, 22:44

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...