JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Vyeti feki, digrii za kununua, na watumishi vihiyo!

  Report Post
  Page 2 of 30 FirstFirst 1234 12 ... LastLast
  Results 21 to 40 of 597
  1. Matata's Avatar
   Member Array
   Join Date : 28th March 2006
   Posts : 22
   Rep Power : 809
   Likes Received
   3
   Likes Given
   5

   Default Vyeti feki, digrii za kununua, na watumishi vihiyo!

   Jamani wanajumuiya ya Wa-Tanzania tuishio British Virgin Islands tumeshutushwa na habari kuwa kuna baadhi ya viongozi wetu serikalini wana shahada za PhD kutoka kisiwani hapa. Ukweli hapa hakuna chuo kama hicho. Hiki kisiwa ni kidogo mno kuna wakazi wapatao 23,000. Kisiwa hiki kina secondary 2 na community collage moja.

   Uchumi wa kisiwa hiki unategemea sana Utalihi na Financial services which includes offshore banking and registration of companies. Baada ya kutembelea web site ya Commonwealth Open University, Ni kweli nimegundua kuwa imekuwa registered hapa. Cha ajabu address yao ni ya hapa(box no.) lakini, Palm Chambers ambalo ni jengo halipo hapa. Kuonyesha kuwa ni fake, hawakutoa simu yao, ila wametoa fax number. Kutokana na fax number hizi number ni za USA (Florida).

   Baadae nilikwenda kwa msajiri wa makampuni nilielezwa kuwa Commonwealth Open University imekuwa registered kama kampuni lakini haina Learning Institution yoyote. Baada ya kuuliza zaidi information hizo, niliambiwa nijaze form harafu nitapewa details baada ya kulipia $ 25.

   Registry Of Corporate Affairs,
   P.O . Box 418,
   Road Town, Tortola, British Virgin Islands.
   Fax 1 284 494 6331:
   Simu 1 284 494 5491:
   E-mail [email protected] Website www.bvifsc.vg

   Sikuweza kulipia ili nipate maelezo hayo. Baada ya kujadiliana na wenzangu hapa tumejua kuna watu wajanja wachache wanatumia mwanya huu kuwaibia fedha watu na kuwapa degree baada ya kuwalipa pesa. Hicho chuo hakipo, hao jamaa ni matapeli.

   Naomba serikali, Wizara ya Elimu, UTUMISHI mjue kuwa hakuna chuo kama hicho hapa. Kama kingekuwa ni chuo basi tungeweza kuona hizo ofisi zao hapa. Kuna Mtanzania mwenzetu ambaye amekaa hapa zaidi ya miaka kumi. Hajawahi kuona ofisi hiyo (Palm Chambers).

   Tuko tayari kushirikiana na mtu yoyote ili kukomesha ununuaji wa yeti fake hasa kwa viongozi wetu.

   Shukrani.
   Last edited by Silencer; 5th August 2008 at 18:33.
   HAKUNA MATATA


  2. Mkandara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2006
   Location : T dot
   Posts : 16,573
   Rep Power : 124739545
   Likes Received
   8259
   Likes Given
   8156

   Default

   Mkira,

   Sikatai kabisa maneno yako lakini kumbuka mbunge ni mwanasiasa sio msomi. Na hii ndio hofu yangu kubwa sana kwamba wananchi wanaanza kutafsiri uwezo wa wabunge kwa vyeti vyao badala ya uwezo wao kuwakilisha wananchi wake bungeni..

   Je, kuna haja ya cheti gani kufahamu haki ya binadamu?...Umaskini wetu, Utajiri wetu na jinsi ya kupambana na maradhi!

   Mathlan - Kutembea na msichana wa miaka kumi na mbili ni - kosa! Unafikiri kwamba wenye elimu ya juu hapa ndio watakao weza kutoa jibu sahihi na lenye ukweli kuliko wabunge ambao hawakwenda shule?...Na what if record inaonyesha kwamba watoto wengi wa umri huo hutembea na wasomi kuliko watu wasiokuwa na elimu!..Na sababu kubwa imegundulika wasomi wanazo fedha za kuwarubuni watoto wadogo.

   Kwa hiyo sheria inaweza kukataza kitendo hicho lakini kwa sababu wasomi viongozi ndio wahalifu wenyewe, sheria hiyo isifanye kazi.

   Hii ndio hali halisi ya nchi zetu maskini kwa kila fani ya sheria na kiuchumi. Wasomi wetu ndio wanao- abuse sheria za nchi kiuchumi na haki za binadamu kwa kutumia elimu zao kupindisha ukweli. Mkapa alifikia kuwaita wananchi wote hawana elimu! wajinga kwa kupigia kelele swala la uwekeshaji na mikataba feki.

   Tunarudi kulekule ktk swala la kina Salim na rangi yake...

   Hao wabunge wasomi wenye vyeti halali toka Havard wameweza kutuletea nini?... mbona akina Freeman, Mtikila na Mrema ambao hawana elimu kubwa Phd huzungumza mengi ya maana kuliko wasomi wenyewe!

   Ukisoma maelezo ya Mzee Es unashindwa kabisa kuelewa kama kweli TZ kuna kiongozi msomi hata mmoja kwa hizo Scandals!

   Hata hivyo Wabunge hawakuchaguliwa kutokana na elimu zao..hii muhimu zaidi tuzingatie kwani swala hapa ni kugushi vyeti!...

   Ikiwa kuna daktari Muhimbili ambaye hana elimu ya Udaktari isipokuwa cheti chake kanunua, hii ndio maana ya kugushi. Lakini hatuwezi kumhukumu daktari Muhimbili ktk udaktari wake kwa sababu tunakisia liseni yake ya kuendesha gari sio halali. Na sababu kubwa tuliyokuwa nayo ati hakwenda shule ya kuendesha gari isipokuwa kajifunzia mtaani!

   Well, swala hili ni la traffic na ikiwa liseni yake imetolewa na taasisi husika kihalali basi hapa hakuna feki.
   Exploration of reality

  3. Sam's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th June 2006
   Posts : 586
   Rep Power : 913
   Likes Received
   61
   Likes Given
   0

   Default

   Mkandara,

   Nilikuwa sina mpango wa kujiunga na hii forum hivi karibuni. Ila hii issue is my issue I have to defend it. Mkandara, what's wrong with so called Takrima? Nadhani ukijibu swali hilo utaweza kuelewa ni kitu gani tunaongelea. Usijaribu kupoteza sura halisi ya hili jambo. Wabunge wanaofuatiliwa siyo wale ambao hawana elimu, ni wale waliotumia takrima ya elimu kujipatia madaraka. Mtu akitumia cheti feki kuwalaghai watu juu ya kiwango chake cha elimu haina maana kuwa atakuwa kiongozi mbaya hata mtu anayetumia takrima ya fedha kujipatia madaraka haina maana atakuwa kiongozi mbaya ila anawanyima watu haki ya kuchaguliwa kidemokrasia.

   Nakumbuka unakumbuka huko nyuma nilishawahi kusema viongozi wazuri hawawezi kupatikana kwa njia ya demokrasia ya kura lakini kama tukiamua kufuata mfumo huo lazima tuufanye wa haki na sawa. Kama tukiamua kuwaruhusu watu watumia takrima ya elimu basi tuwape haki na wale watu wenye hela watumia hela zao kupata madaraka.

   Ni jambo la ajabu kusikia maneno toka kwako kuwa Mrema anaongea mambo ya maana. Ngoja niishie hapa.

  4. Kyoma's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 2nd June 2006
   Location : Mfugwa Mbwa
   Posts : 124
   Rep Power : 820
   Likes Received
   53
   Likes Given
   0

   Default

   UFISADI

   Suala hapa siyo mwenye cheti au asiye nacho nani anafaa kutuongoza. Msingi wa hoja ya mjadala huu ni kuwa tunaongozwa na watu waliopata vyeti kwa njia za udanganyifu. Watu wanaoamini kuwa mafanikio yanapatikana kwa kutumia njia za mkato-overnight rewards. Raia wetu bado ni masikini na mafukara wa kupindukia. Raia wengi hawana elimu. Kazi iliyo mbele yetu ni kubwa na tunahitaji viongozi wanaoelewa hivyo. Ni bahati mbaya kuwa hawa watu bado wanaitwa waheshimiwa na hawako jela.

   Hivi vyuo walikopata vyeti vyao, vinaeleza kwa kinaga ubaga katika website zao kuwa utapata Phd bila kujali kiwango chako cha elimu ulichonacho. Hii inamaanisha hata kama umemaliza darasa la saba. Kibaya zaidi, vingine vinasema kuwa utapata Phd ukiwa umelala nyumbani. Viongozi wetu waliyasoma maelezo ya hivi vyuo na ndio maana wakavutiwa na kujiunga. Zamani tulikuwa na maagizo au Azimio la Musoma lililokuwa linasisitiza elimu kwa wote. Raia wetu wanahitaji kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa kwenda shule. Utahamasishwaje au utaongozwaje na watu wanaoamini kuwa unaweza kupata elimu ukiwa umelala nyumbani?

   Taifa letu linahitaji kuongozwa na wachapa kazi bila kujali viwango vyao vya elimu, lakini wawe wanatambua umuhimu wa elimu. Mfano mzuri ni wazazi wa baadhi yetu ambao hawakwenda shule lakini walikuwa ni wachapa kazi, wakulima wa Pamba, Kahawa, Majani ya Chai, Maharage na Mahindi. Wameuza mazao na kudhulumiwa na vyama vya ushirika, lakini fedha ndogo iliyopatikana ndio imetufikisha baadhi yetu hapa tulipo. Walikuwa wanatambua umuhimu wa elimu na walijitoa muhanga ili tuweze kusoma. Hawakuamini njia za mkato.

   Kuongoza ni kuonyesha njia, kushawishi na kuuza mawazo kwa wana jamii bila kutumia mabavu ili waweze kuyanunua. Hii njia ya kununua vyeti ndio wanayotuonyesha? Haya ndiyo mawazo wanayotaka tununue? Hatupashwi kutawaliwa na wahuni.

   Serikali ya Mwinyi ilisitisha msalaba wa kuwasomesha watoto wa wafanyakazi wa balozi zetu za nje kutokana na ukubwa wa gharama. Hata hivyo, serikali haikufuta mpango wa kuwasomesha watumishi wake wa ngazi za juu. Mawaziri na watumishi wenye vyeo vya juu serikalini, wamekuwa wakineemeka na msaada wa kifedha kutoka serikalini kwa ajili ya kujiendeleza kielimu.

   Fedha za Umma zinatumiwa vibaya kwa kutengenezewa mazingira ya kuhalalisha ionekane kuwa si ufisadi. Si vibaya kwa serikali kuwasomesha mawaziri wake, lakini napinga kutumia fedha za umma kununua vyeti. Mfano, waziri wetu wa mambo ya sheria mama Marry Nagu alianza masomo yake ya udaktari (Phd) katika chuo kisichosajiliwa cha Washington International University akiwa waziri wa mambo ya ustawi wa jamii na watoto katika serikali ya Mkapa. Hakuna shaka kwamba serikali imegharamia elimu ya ubabaishaji aliyoipata katika chuo hicho.

   Serikali ya Tanzania haiwezi kutoa fedha katika chuo mbacho hakitambuliki na hakijasajiliwa kwa mujibu wa sheria. Kumekuwepo na udanganyifu wa kuhalalisha matumizi ya fedha za umma katika ununuzi wa vyeti. Ama viongozi waliwasilisha makaratasi ya uongo wakati wa maombi ya fedha serikalini ili kulipia elimu yao, au aliyepashwa kuhakiki usajili wa chuo alikuwa amelala, au vyote viwili vilifanyika kwa pamoja.

   Kwa vyovyote vile, ni jukumu la viongozi kuhakikisha kuwa fedha ya serikali inatumika kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa. Nani atakubali kuongozwa na kiongozi ambaye hajuhi kama chuo anachotaka kusoma, anachosoma, au alichosoma hakijasajiliwa? Huyu ndiye tunataka aiongoze nchi katika mikataba ya mabilioni ya fedha? Nagu ni mfano tu, lakini wapo mapapa ambao ni mamia ya watumishi wa serikali wanaoshiriki katika mpango huu. Hawa viongozi hawapashwi kutuongoza.

   Mwaka 1994/1995 CCM iliweka sharti la mgombea wake wa kiti cha uraisi kuwa na kiwango cha juu cha elimu. Pamoja na ukweli kuwa sharti hili limepunguza haki ya msingi ya raia ya kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba yetu, pia ndio chanzo cha kuongezeka kwa idadi kubwa isiyo na kifani ya wabunge, mawaziri, na wasomi ambao wana vyeti vya kununua. Wanafanya hivyo kujizatiti ili kukabiliana na masharti mengine ya viwango vya elimu katika nafasi nyingine za uongozi kama yatajitokeza siku za usoni.

   Ikumbukwe kuwa wasomi wengi wa Tanzania wanajiandaa, ama wengine wamekwisha ingia kwenye duru la siasa. Hii inatokana na ukweli kwamba siasa ndio sekta pekee inayotoa ajira ya uhakika kuliko sekta nyingine yoyote nchini kwetu (Job security-Ilimradi ujue kula na vipofu). Anayebisha akamuulize Kingunge Ngombale Mwiru au Sir George Kahama aliyekuwa waziri katika baraza la kwanza la mawaziri tulipopata uhuru na alikuwemo katika baraza la mawaziri la Mkapa lililovunjwa, yaani miaka zaidi ya arobaini baada ya uhuru.

  5. Luka's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 6th June 2006
   Posts : 3
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default

   Hivi niambieni ni nani katika hao waliforge hivyo vyeti waliotia mikataba ya uongo yenye kuwadhalilisha wananchi? Hao wenye Diploma hizo fake wala sio hata mmoja wao ana kashfa. Jamani tuache kuwaonea watu ambao hawana makosa. Vyuo vimewapa vyeti, kama ni vya chini hilo si suala. Hivi Institute of Sales Promotion ile ya Kurasini na kile Chuo cha Uhasibu cha kurasini vilikuwa sawa? Vyote vilitoa Diploma. Tutafute mtu ambaye katumia vibaya diploma yake kama Chenge na Mama Ndosi ambao walipitisha hiyo mikataba, hao resume zao maybe ndiyo mnaona ni za kweli. Hawa wana diploma zinazofahamika, lakini walipitisha mikataba ya ajabu. Angalieni sasa NSSF wamefanya nini!

   Nitamjaji muajiriwa wangu kama atanipa resume nzuri na kunifanyia kazi mbovu. Tuanze kuwajudge hawa waliotumia elimu zao vibaya kwanza. Hawa wengine hatuna ushahidi nao.

  6. Field Marshall ES's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th April 2006
   Posts : 13,876
   Rep Power : 196824
   Likes Received
   722
   Likes Given
   225

   Default

   Kutoheshimu sheria yaani THE RULE OF LAW ndio hasa tatizo letu bongo, na siku tutakapo amuka na kuelewa hili na kulishughulikia ipasavyo itatutalia mataizo yote tuliyonayo kisiasa na kiuchumi as a nation,

   viongozi wenye vyeti vya uongo, meaning kwamba hawakusoma kufikia viwango vya elimu ya vyeti walivyovitumia kupata madaraka ya kisiasa ni lazima watafutwe na wafungwe jela bila huruma! Yes wamevitumia hivyo vyeti kuwafanya wengine wenye elimu ya kweli kushindwa kura za maoni au hata kuenguliwa na vyama vyao vya siasa kwa kutokuwa na elimu ya kutosha wakati hawa wenye vyeti vya wizi wameonekana wana uwezo mkubwa kielimu,

   Kwa mfano, CCM wanataka mgombea urais awe na angalau Degree moja, sasa ina maana kuna walioondolewa kwa kutokuwa nazo na waliopitishwa kwa kuwa na za uongo, na hata kwenye ubunge na sehemu zingine, ninasema serikali ifuatilie hawa viongozi, tena hata huko bungeni ni aibu kubwa kuwa na hawa wapumbavu ambao wanajulikana hata bila ya kuwafuatilia,

   Guys ngaja niwaambieni, kule bungeni kuna wabunge wapumbavu ambao wakati kikao cha bunge la taifa kinaendelea wao wanatafuta picha za porno au za uchi kwenye internet wanazi-print na kuzisambaza ndani ya bunge! Tena mmoja wa hao mabingwa sasa ni waziri! Now look, serikali inatumia hela za kodi ya wananchi kulipia ile internent, kumlipa mbunge posho ya kila siku, kumpa gari lenye thamani ya dola $ 40,000, kumpa dola $ 32,000 baada ya miaka mitano ili awawakilishe wananchi bungeni, halafu wajamaa wanakuja kutafuta picha za uchi na kuzigawa ndani ya bunge tukufu la wananchi, hawa ndio wenye vyeti vya wizi hawa! Na mmoja wao sasa ni waziri hana hata aibu!

   Hivi Watanzania tulimkosea nini Mungu? Hivi wazee mnajua kuwa ile siku rais wetu alipokuwa anatangaza baraza la mawaziri alikuja pale akiwa na list isiyokwisha kuna majina aliyaongeza pale pale, na mengine aliyatoa pale pale mbele ya waandishi wa habari? Sasa mnashangaa kuwa tuna viongozi wasiokuwa na vyeti vya ukweli? WHY? Si viongozi wa ngazi za uwaziri wanatakiwa wapekuliwe kisayansi na kinadharia na Secret Service kabla ya kupewa uwaziri? Sasa kwa mantiki hii ya kuongezwa dakika ya mwisho tutategemea nini?

   Mungu Aibaraki Bongo!


  7. Mkandara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2006
   Location : T dot
   Posts : 16,573
   Rep Power : 124739545
   Likes Received
   8259
   Likes Given
   8156

   Default

   Sam,

   nakumbuka sana ndugu yangu na mimi siku zote nimekuwa mkweli ktk swala hili.

   Kwanza nakumbuka EN tulimjadili wakati wa uchaguzi kwa diploma yake ya Mzumbe. Kuna kila maneno yaliyosemwa lakini hakuna mwananchi yeyote Songea alimchagua EN kwa sababu ya digrii yake ya Mzumbe. Na kama Elimu na uzoefu ndiyo unaomfanya mbunge ashinde nadhani Ghama alikuwa na kila sifa kuliko EN - Hilo moja.

   Pili, kumbuka mimi ninayo kumbukum,bu kubwa sana! ni mara tu baada ya uchaguzi pale bunge walipoweka washindi wake kwenye tovuti yao ndipo tulipovumbua hilo swala la digrii ya Commonworth. Nikawauliza kuna mtu kati yen anayo hakika kwamba jamaa huyu hakusoma kupitia mtandao? maanake wengi walifikiri kwamba elimu yake ni sawa na ile ya Mrema...Baada ya uchunguzi wangu niligundua kwamba unaweza kupata digrii kupitia mtandao kwa muda wa mfupi sana na kwa gharama ndogo. tatizo ni nini hapa! fedha au muda!

   Je, hii elimu inaweza kweli kuheshimika?...Well, kama ni fedha kuna watu wamesoma Urusi na Bulgaria kwa kiasi hichohicho cha fedha hali marekani, Uingereza na Canada huwezi kusoma hata semister moja. Je elimu ya Urusi na Bulgaria haina thamani kwa sababu ni cheap!

   Pili ikiwa ni muda, mshikaji, Marekani na Canada watoto wao wa darasa la saba ni sasa kabisa na mtoto wa darasa na tano Bongo miaka yetu. Kuna graduates wa GDE hawafahamu hata kuandika hali wametumia miaka mingi kuliko mwanafunzi wa Bongo. Trust me watoto wengi waliosoma shule ya mzingi Africa huwashangaza watu wa hapa inapofikia habari ya kitabu. Taabu kubwa tu kwa watoto wetu huwa lugha na ile exposure ya western world basi.

   Mzee Es,
   Ndugu yangu nakubaliana na wewe kabisa kwamba watu hao wasakwe na kwa bahati mbaya wabunge wote uliowasema (watazama Pono) ni wasomi wetu waliosoma Havard, UDSM na huko Uingereza. mshikaji ukikaa na hawa jamaa huwezi kuamini elimu zao, bora Mtikila mwenye staha na mwoga wa Mungu wake kuliko hao wenye madigrii.

   Uchafu wote unaotokea nchini umeletwa na hao wasomi kwa sababu wasomi hawahawa ndio wamegeuka kuwa wataalam.

   Je, unakumbuka ile hesabu niliyoitoa awali?... hesabu ile ilikuwa kuwaonyesheni tofauti kati ya elimu ya darasa against hekima na busara. Bahati mbaya sana sikuweza kuona kama kuna mtu aliweza kulibu swali lile maana kesho yake tu Bcstimes ilitutoka kifo kibaya!... naweza kurudia hapa tena na nakuhakikishia wasomi wengi watashindwa ikiwa hawakutumia hekima na busara. Na mzee wetu Simba wa nyika (Kawawa)hapo alipo anaweza kabisa kukupa jibu la swali hili kiulainiiiii!
   Exploration of reality

  8. Kyoma's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 2nd June 2006
   Location : Mfugwa Mbwa
   Posts : 124
   Rep Power : 820
   Likes Received
   53
   Likes Given
   0

   Default

   Mkandara

   Suala la msingi hapa sio muda au fedha unazotumia kumaliza shule. Vyuo unavyo viongelea vya Urusi, Bulgaria, Uingereza, Canada, na Marekani vimesajiliwa. Fedha na muda vinaweza kutofautiana kutokana na nchi kilichopo hicho chuo na mfumo wa elimu unaotumika katika nchi husika, lakini viwango vyao vya ufundishaji vimehakikiwa na vinakubalika. Vyuo vingi vimeanzisha mpango wa kutoa elimu kwa baadhi ya fani katika internet. Haviuzi vyeti ila vinatoa elimu kwa njia ya mtandao kama ilivyokuwa njia ya posta.

   Vyuo kama Pacific University, Washington International University, na vingine katika mkumbo huo havitambuliki. Ni vyuo vya kitapeli, na vingine havina hata majengo. Vinaendeshwa kwenye mikoba kama zile kampuni za zamani za Clearing and Forwarding za Samora avenue hapa Dar. Tofautisha kati ya kusoma na kununua cheti. Lugha zinazotumiwa katika mitandao ya hivi vyuo zinaonyesha bayana kuwa unauziwa cheti. Unapoambiwa kuwa bei ya Phd ni $..na hawajali kiwango chako cha elimu ulichonacho, alafu unaulizwa kama unataka cheti kionyeshe kuwa ulisoma kwa muda fulani hata kama hukusoma huo muda watafanya hivyo, ni udanganyifu. Vingine vinasema ukisha tuma fedha watakutumia cheti hata kama “thesis” yako utaituma baadae.

   Wasomi wetu wa kweli wameamua kutuibia, lakini wanaonunua vyeti hawapashwi kuchukuwa nafasi ya wasomi wa kweli. Wote ni wahalifu na hawatakiwi kuwa viongozi wetu. There are certain standards that we should uphold. Pacific University na Washington International University vimekwisha vikishwa mahakamani na vimepigwa marufuku katika majimbo mengi ya huko Marekani. Nina wasiwasi na mtu anayeamini upatikanaji wa elimu kwa njia za udanganyifu kuwaongoza watu ili wajikwamue na wimbi la ujinga. La muhimu zaidi ni ufisadi wa kuhalalisha matumizi ya fedha za umma katika ununuzi wa vyeti. Mimi naheshimu sana haki za raia wetu kama zilivyoidhinishwa na katiba ya nchi yetu, hivyo sipingi kuongozwa na watu waliosoma au ambao hawajasoma. Ninachopinga ni kuongozwa na wasomi wezi au watu ambao hawajasoma lakini wananunua vyeti.

   Natofautiana na wewe pia katika suala la watoto wa Majuu na wale wa kibongo kuwa na uelewa tofauti kutokana na uwiano wa madarasa waliomo. Sidhani kama kuna uhusiano wa moja kwa moja na hili sakata la waheshimiwa. Lazima uzingatie utofauti wa mfumo wa elimu wa Marekani na Tanzania. Hakuna physical instrument (muzani) ambao unaweza kupima ubora wa mfumo wa elimu wa nchi moja kulinganisha na nchi nyingine. Urahisi au ugumu wa masomo hauwezi kuwa kigezo cha kipimo cha mfumo wa elimu wa nchi husika. Watoto wetu kwenda Marekani na wakafaulu vizuri mitihani kuzidi hata wamarekani wenyewe, haimaanishi mfumo wetu wa elimu ni mzuri. Kipimo pekee cha mfumo wa elimu wowote duniani, ni jinsi hiyo elimu wanayoipata watu wa hiyo nchi inavyowawezesha kuyabadili mazingira yao. Kama mfumo wa elimu hauwawezeshi watu kuyabadili mazingira yao haufai.

   Hatuwezi kutamba kuwa watoto wetu wanawazidi watoto wa kimarekani wakati karibu vitabu vyote wanavyosoma watoto wetu mashuleni kwetu vinatungwa na hao wamarekani. Hakuna kitu tunachoweza kutengeneza sisi wenyewe. Watoto wa kimarekani wanatengeneza alafu sisi tunanunua. Hapa naongelea hata ile mifano ya nyoka (toys) wanayouziwa watoto wetu hapa Tanzania inatengenezwa Marekani na kwingineko hata kama sisi tuna nyoka halisi walio jaa tele. Mfumo wa marekani unawasaidia wamarekani kuyabadili mazingira yao, wakati mfumo wetu hautusaidii kuyabadili mazingira yetu. Tunapofanya comparison, lazima tuweke upenzi wan chi pembeni.

  9. Mkandara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2006
   Location : T dot
   Posts : 16,573
   Rep Power : 124739545
   Likes Received
   8259
   Likes Given
   8156

   Default

   Kyoma,

   Nakubaliana na wewe moja kwa moja ikiwa mtaweza kutupa vigezo kama hivyo ulivyotaja hapo juu.

   1. Walionunua vyeti kwa fedha -Hawa ni wabunge ambao hawakupata elimu kama vyeti vyao vinavyoonyesha...hawa ni akina nani?

   Pia kama sheria hii ipo basi, tuwatafute madaktari, walimu, wataalm wote ambao inawezekana wamenunua vyeti hivi. Tukianza na wabunge, kisha hata wafanya biashara wote ambao wamefungua biashara zinazohitaji Utaalam. Huwezi kfungua hospital ikiwa wewe huna elimu ya Udaktari klwa sababu kuna safty mesures kibao ambazo unatakiwa kuzifahamu.

   2. Kuna fungu lan hao waliosoma hizo shule za Mtandao ambazo hazitambuliiki nchini humo.

   Kyoma hapa nina Utata mkubwa kwa sababu shule kama Pacific University na Washington International University hazitambuliki kwao Marekani kwa sababu ambazo wewe na mimi hatuzifahamu, lakini sio swala la kutokuwa na majengo ya shule. Kumbuka hizi ni shule zinzzotoa elimu kimataifa kwa njia ya Mtandao. Yawezekana kabisa Vyuo hivyo havukukamilisha masharti ya usajili wa shule za mtandao nchini humo.

   Kuna shule nyingi za elimu kwa njia ya mtandao ambazo zimesajiliwa na hazina majengo - hizi zipo ktk list ya kutambulika lakini pia hazitambuliwi na baadhi ya vyuo vikuu nchini humo. Na kuna baadhi ya viongozi Mareakani wamesoma vyuo hivi kujiendeleza. Na kuna watu wengine wamesomeshwa majumbani mwao na walimu maalum kutokana na fedha zao bila kwenda shule na wamehitimu masomo yao. Je, hawa pia tuwatoe nje?

   Commonwealth kinatambulika huko kiliposajiliwa lakini hii isiwe sababu ama kigezo kwetu kuitambua shule hiyo. Pia kwa sababu Washington University haitambuliki Marekani kama chuo haina maana hata sisi tusikubali cheti cha msomi huyo.

   Kwanza tuwe na Utaratibu wetu kuhusu Elimu na viwango vyake. Tuwe na masharti ya Elimu hiyo kama ilivyo ktk UHASIBU. Kisha baada ya kuweka viwango ndipo tunaweza kutazama ni vyuo vipi vinavyo-tosheleza elimu tunayoitaka..

   Kuhusu watoto nitarudi baadaye!
   Exploration of reality

  10. Kyoma's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 2nd June 2006
   Location : Mfugwa Mbwa
   Posts : 124
   Rep Power : 820
   Likes Received
   53
   Likes Given
   0

   Default

   Mzee Mkandara

   Nadhani utaratibu wetu kuhusu Elimu na viwango vyake tunao. Kinachotakiwa ni sisi wenyewe kuupitia. Masharti ya Elimu yapo na wala sio katika Uhasibu peke yake kama ulivyoandika. Kipo chombo cha kuwasajili madaktari wanaomaliza Muhimbili na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi. Vipo vyombo vya kusajili Wanasheria na Wahandisi. Hata Waalimu wana madaraja kutokana na viwango vyao vya elimu. Vyuo vyetu nchini lazima viwe accredited na National Accreditation Council. Hata katika ngazi za chini, vyeti vyote vinavyotolewa na National Examinations Council vinatambuliwa na hiki chombo. Kwa sababu Tanzania sio kisiwa, vyeti vinavyotambuliwa na hiki chombo, ndivyo vinavyotambuliwa na vyombo vya nchi nyingine.

   USA has a bunch of approved accrediting bodies. Anayetoa approval kwa hivi vyombo ni U.S Department of Education. Kama US Department of Education inakitambua chuo, basi, nchi yetu inakitambua pia and vise versa. Kuna Accrediting bodies katika USA ambazo haziko approved na US Department of Education. Mfano, “World online Education Accrediting Commission, Board of online Universities Accreditation, Distance Graduation Accrediting Association and so forth”. Kuwepo kwa neno “Accreditation” ni mtego na haimaanishi kuwa chombo hicho kinatambuliwa na US Department of Education.

   Hata wewe Mzee Mkandara unaweza kuanzisha Chuo Kikuu ambacho kina ofisi katika nyumba ya Babu yako katika kisiwa cha Ukerewe, lakini unachapisha vyeti na kuwatumia watu ukiwa Columbus Ohio. Kwenye website yako unaweza kuandika kuwa kiko Accredited na “Internal Learning Accreditation Association” na ukatengeneza website ya hiyo Association. Taratibu za kuhakiki vyeti katika nchi zote duniani ikiwepo Tanzania zipo na lazima zifuatwe.

   Nakubaliana na wewe kuwa kuna vyuo ambavyo vinaendeshwa nchini Marekani, lakini bado havijatimiza masharti ya usajili. Vingine vimetuma maombi wakati huo vinaendelea kutoa elimu kwa walengwa na hata kama havijasajiliwa. Lakini vyuo tunavyoviongelea hapa, havijawahi kuomba usajili katika mamlaka husika kwa sababu vinajihusisha na uuzaji wa vyeti na wala sio kutoa elimu. Mfano, Washington International University ilikuwa ikiendesha biashara yake katika majimbo ya Hawaii na Oregon. Ilipogundulika ikapigwa marufuku kwenye hayo majimbo na wakahamishia anwani yao kwenye visiwa vya Caribbean. Columbia Commonwealth University walipigwa marufuku California wakahamia Montana nako wakapigwa marufuku, wakahamia Wyoming. Baadae wakaandika kwenye website yao kuwa wamepata usajiri nchini Malawi katika Serikali ya Kamuzu Banda. Hata hivyo, Mfanyakazi wa Ubalozi wa Malawi nchini Marekani, aliwahi kutoa maelezo kwenye mtandao wa watu kutoka Malawi kuwa hiki chuo hakijasajiliwa kihalali nchini Malawi.

   Mara nyingi CNN wamekuwa wakifanya investigative reporting kuhusu utapeli unaofanywa na hivi vyuo. Siku moja walikwenda kukifuatilia hiki chuo cha Washington International University huko katika visiwa vya Caribbean lakini waliambulia jengo moja la zamani ambalo halikuonekana kama kuna mtu anaishi. Hawakufanikiwa kuongea na mtu yeyote anayehusiana na hicho chuo, lakini wakituma barua zinajibiwa. Piece nyingine waliyoitoa ilikuwa ni ya Chuo kilichokuwa na anwani nchini Marekani lakini walipofika kwenye hiyo anwani, wakakuta ni jengo liloharibika na hakuna anayeishi, hata mmiliki wa hilo jengo hajuhi kinachoendelea. Walitumia waandishi wao kutoka uarabuni na wakaagiza vyeti kutoka katika hicho chuo kwa kutumia majina ya wanaowaita “terrorists” na vyeti vyote vikafika baada ya kutuma fedha kwa njia ya e-bay. Unaweza kuwasiliana na CNN moja kwa moja wakakutumia hizo pieces.

   Tofautisha kati ya vyuo vinavyofundisha lakini havijapata usajili na vile vinavyojihushisha na utapeli wa kuuza vyeti. Kwa vyovyote vile, Serikali yetu ya Tanzania haitambui vyeti vinavyopatikana kutoka katika vyuo ambavyo havijasajiliwa na taasisi yenye mamlaka ndani ya nchi husika. Utaratibu huo tunao na watu wanalipwa kufanya kazi hiyo.

   Mzee Mkandara, hakuna chuo kilichosajiliwa ma mamlaka husika alafu kisitambuliwe na chuo kingine. Kwa mfano nchini Marekani, sheria inavilazimisha vyuo vyote vilivyosajiliwa na mamlaka husika kuvitambua vyeti vya vyuo vyote vinavyotolewa na vyuo vyote vilivyosajiliwa na mamlaka husika. Huu ndiyo utaratibu unaofuatwa Tanzania, Uingereza na kwingineko.

   Well, kuhusu watu waliosoma majumbani kwao hakuna mtu anasema watolewe nje. Kila nchi inautaratibu wake. Mfano; nchini Marekani, Department of Civil Service ndio wanahusika na educational requirements kutokana na job specifications. Mtu kama Brandy ni mwanamuziki wa kike aliyepata elimu nyumbani toka utotoni. Siku akiamua kutafuta kazi, (ingawa hawezi kwasababu ya fedha), ndipo tatizo linakuja. Kuna kazi ambazo hazitakiwi kuwa na Elimu. Lakini kuna nyingine zinataka uwe na High School Diploma. Kama alipata home Schooling, inampasa akafanye mtihani wa GED. Akifaulu, atapata hiyo kazi. Akitaka kujiunga na Ohio State University, lazima akafanye SAT. Hata Tanzania tuna utaratibu wake, ukitaka kuingia chuo kikuu, kuna kitu wanaita Mature Entry Exams, kama hutaki hiyo basi kuna mtihani wa kidato cha sita ambapo utafanya kama Private Candidate. Ukifaulu, unaingia chuo kikuu bila kujali umepata home- schooling au la!

   Lakini kumbuka katika nchi yoyote, at a professional level, Huwezi kusema mimi nimesomea nyumbani hivyo naomba kazi ya Udaktari, Uhandisi, Ualimu, Ujaji, Uanasheria n.k. Lazima uwe na cheti. Sheria za nchi zote hizi zinasema wazi kuwa lazima uwe umepata cheti kutoka katika taasisi inayotambulika au chuo kilichosajiliwa na mamlaka husika ndani ya hiyo nchi. Mawaziri na wabunge waliopata vyeti kutoka katika hivyo vyuo wanajulikana na unaweza kuwaona katika mtandao wao wa Bunge. Viongozi hawa wamepata hivi vyeti kwa njia za udanganyifu na baadhi yao, wametumia fedha za serikali.

   Tunajenga utamaduni mbovu, badala ya serikali kutumia chombo chake yaani national Accreditation Council ili kuhakiki vyeti vya wabunge na mawaziri. Kama wakikuta vimepatikana kutoka katika vyuo visivyosajiliwa kama ilivyo sasa, waendeleze upekuzi wa kujua kama fedha ya umma ilitumika kugharamia hiyo elimu na kuhakikisha wahusika wanashitakiwa. Serikali yetu inafanya kinyume kwa kuwageukia raia wa kawaida na kuwambia walete ushahidi. Gazeti la leo la Daily News limeandika report kutoka kwa Mkaguzi mkuu wa Serikali inayosema kuwa Serikali imepoteza shilingi billioni 140 kwa mwaka wa fedha 2004/2005 ambapo mojawapo ya sababu ni kutokana na matumizi ya fedha yaliyofanywa na baadhi ya wizara bila kujali taratibu zilizowekwa na serikali. Badala ya kuwauliza wale waliopewa fedha wamezitumia je? Ziko wapi? Kwanini zilitumika bila kufuata taratibu? Wananchi ndiyo wanageuziwa kibao kuwa walete vigezo na ushahidi.

  11. Spiderman's Avatar
   JF Admin Array
   Join Date : 1st January 1970
   Posts : 486
   Rep Power : 100000
   Likes Received
   235
   Likes Given
   6

   Default

   MBUNGE ANAYEDAIWA KUONGOPA ELIMU YAKE:
   Jalada lafika ofisini kwa DPP


   • Ilikuwa wakati wa kampeni za uchaguzi
   • DCI asema tayari upelelezi umekamilika


   Na Esther Mvungi

   MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) amepokea jalada la mbunge anayedaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu elimu yake wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.

   Akizungumzia suala hilo ofisini kwake, Mkurugenzi wa Mashitaka, Geoffrey Shaidi, alithibitisha ofisi yake kupokea jalada hilo.
   “Jalada limefika leo mezani kwangu… limepokewa ofisini Juni 6,” Shaidi alisema jana.

   DPP ambaye hakuzungumzia undani wa jalada hilo, alisema ofisi yake italishughulikia na hakutaka kutaja jina la mbunge kwa wakati huu.


   Awali, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, akizungumza na Uhuru alisema ofisi yake imekamilisha upelelezi kuhusu mbunge huyo na kuwasilisha jalada kwa DPP.

   Manumba alisema ofisi yake ilipata taarifa za malalamiko kuhusu mbunge huyo na si kweli kwamba inawahoji wengine kadhaa.

   Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuwa wabunge kadhaa wamehojiwa na polisi kwa kughushi vyeti vikiwemo vya elimu.

  12. Spiderman's Avatar
   JF Admin Array
   Join Date : 1st January 1970
   Posts : 486
   Rep Power : 100000
   Likes Received
   235
   Likes Given
   6

   Default

   Wabunge walioghushi elimu Moro kushitakiwa kwa pamoja

   Na Mkombe Zanda, Morogoro

   WAKATI kazi ya kuhoji wabunge wanaodaiwa kufanya udanganyifu kuhusu viwango vya elimu zao kwenye uchaguzi uliopita likiendelea chini ya usimamizi wa Jeshi la Polisi nchini, mashitaka ya pamoja yanaandaliwa dhidi ya wabunge na madiwani wote wanaotuhumiwa kuhusika na udanganyifu huo mkoani hapa.

   Mashitaka hayo yanaandaliwa na wananchi zaidi ya 200 ambao wameungana kwa pamoja mkoani hapa na kuunda kundi lenye wafuasi wa vyama mbalimbali vya kisias kwa nia ya kuwafikisha mahakamani wabunge na madiwani ambao wanatuhumiwa kufanya udanganyifu huo.

   Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini kwa kuwa bado taratibu husika hazijakamilika kuhusiana na mpango huo, baadhi ya wafuasi wa kundi hilo walidai kuwa wanaandaa mashitaka dhidi ya wabunge na madiwani ili kukomesha udanganyifu huo.

   Wafuasi hao walisema kimsingi hawakutendewa haki na wahusika kwa maelezo kuwa walilazimishwa kupiga kura kwa ushawishi usiokuwa sahihi, jambo ambalo liliwanyima nafasi ya kuchagua viongozi wenye sifa zinazofaa kuiongoza jamii.

   Walisema tayari wameshaorodhesha majina ya watuhumiwa wote kwenye kesi hiyo inayotarajiwa kufunguliwa mahakamani hivi karibuni, ili kuhakikisha watuhumiwa hao wanaadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

   Lakini hata hivyo, wafuasi wa kundi hilo hawakuwa tayari kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa maelezo kuwa bado ni mapema.

   Aidha taarifa zilizopatikana katika uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na mpango huo, ilibainika kuwa tayari kuna zaidi ya wanachama 200 kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa mkoani hapa, ambao walijitokeza katika kujaza fomu ya udhamini wa mpango huo, ambao wapo tayari kusimama mahakamani kwa lengo la kutoa ushahidi dhidi ya watuhumiwa hao.

   Wafuasi hao walisema lengo la kufungua mashitaka hayo kuionesha jamii kuwa hawakufurahishwa na hadaa waliyofanyiwa na baadhi ya wagombea kwenye uchaguzi mkuu uliopita na hivyo kuchagua viongozi wasiokuwa na sifa stahiki.

   “Watu tulishawishika kuwapigia kura kwa sababu ya kuvutiwa na viwango vyao vya kielimu, kumbe tulidanganywa hawana hata hizo elimu walizokuwa wakitutangazia kwenye majukwaa ya kampeni, huku ni kutudharau,” alisema kiongozi wa mpango huo.

   Kuanzishwa mpango huo kunatokana na vuguvugu la kisiasa mkoani hapa hasa mjini mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliopita ambapo CCM iliibuka na ushindi mkubwa huku CUF ikiendelea kudai kuwepo kwa ubadhirifu wa kura na udanganyifu wa kielimu kwa baadhi ya wagombea wa CCM.

   Hata hivyo, uongozi wa CUF mjini hapa ambako ndiko yalipo maskani ya shughuli zote muhimu za kundi hilo linalotaka kuwafungulia kesi ya pamoja wabunge na madiwani hao, ulikanusha kuhusika na harakati hizo na kubainisha kuwa wao wanahusika moja kwa moja na kesi inayoendelea mahakamani hivi sasa, dhidi ya Mbunge wa Morogoro Mjini, Bw. Omar Nibuka kuhusu utata wa elimu yake.

   Mwenyekiti wa CUF mjini hapa, Bw. Habib Mlapakolo, alisema ingawa wapo tayari kutoa ushirikiano kama watahitajika kufanya hivyo kwa sababu wanataka haki itendeke, lakini kwa sasa hawafahamu lolote kuhusu mpango huo.

   Lakini hata hivyo, CUF mjini hapa imeitaka Polisi na mamlaka nyingine zinazohusika katika kuhoji wabunge wanaodaiwa kufanya udanganyifu kuhusu elimu zao, kuishirikisha pamoja na wananchi wengine wa kawaida ili kutoa fursa kwa Watanzania wanaoufahamu ukweli kuhusu tuhuma za wabunge hao, kutoa ushahidi wao.

   Bw. Mlapakolo alisema ili kazi hiyo ionekane kuwa yenye na inayozingatia haki na uadilifu ni lazima iwepo fursa ya kupokea ushahidi kutoka kwa watu wengine.

  13. Kyoma's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 2nd June 2006
   Location : Mfugwa Mbwa
   Posts : 124
   Rep Power : 820
   Likes Received
   53
   Likes Given
   0

   Default

   Admin,

   Suala la wananchi 200 wa Morogoro kuwashikia kidedea viongozi waliochaguliwa kwa kutumia vigezo vya elimu wasiokuwa nayo linatia moyo. Cha kushangaza ni kuwa viongozi haohao labda wangechaguliwa hata kama wasingeongopa kuhusu viwango vyao vya elimu. Ushauri wangu ni kuwa hili suala la wananchi kuchukuwa jukumu la kuwafikisha Mahakamani hawa waheshimiwa lisiwe la kisiasa kwani litakufa kabla halijaanza.

   Raia wa Morogoro wanahitaji ushirikiano kutoka kwa wasomi wa kujitolea waliobobea katika masuala ya sheria na hata ushirikiano kutoka serikalini. Hili ni jambo linalohusu muafaka wa kitaifa. Inabidi tuwashe Mwenge na tuupitishe sio tu kwenye siasa, bali hata katika fani zote kama alivyosema Mzee Mkandara.

   Rejea maneno aliyoyasema na Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msolla alipozungumza kwa mara ya kwanza na wafanyakazi wa wizara yake kwenye makao makuu ya wizara hiyo mjini Dar es Salaam. Nanukuu;
   "Kughushi vyeti kwa vijana wanaojiunga na elimu ya juu kumesababishwa na kuimarika kwa teknolojia ya mawasiliano lakini hatua zaidi lazima zichukuliwe kwani kuwaondoa tu chuoni haitoshi, hatua nyingine zitakazochukuliwa ni kuwasaka na kuwagundua watu waliopata vyeti kwa kununua digrii kutoka mataifa ya nje ambako Marekani inaongoza kwa biashara hiyo. "Kuna hili suala la mtu kuwa na fedha na kuuziwa digrii...anatakiwa kusema anahitaji cheti cha aina gani na kwa daraja gani kisha akiwasilisha hundi anatumiwa digrii yake. Watu wa aina hii lazima hatua zichukuliwe ili kuwabaini na tuwachukulie hatua," Mwisho wa kunukuu.

   Baada ya tamko la Waziri Msolla, niliwahi kuandika mahala kuwa imefikia wakati wa kuwauliza viongozi wetu kutoa matamko yanayoambatana na ushahidi. Haiwezekani Waziri akasoma kwenye gazeti habari za kununua digrii nchini Marekani, alafu akahisi kwamba, watanzania wamekwisha zinunua. Sidhani kama hisia zinatengeneza mikakati na ajenda za kuiongoza Wizara. Itabidi tuwe tunawabana viongozi wetu palepale wanapotoa matamko. Profesa Msolla alikuwa na ushahidi gani kuwa watanzania wananunua digrii? Tena Marekani? Au ni ile ya waswahili wa pwani ujuana kwa vilemba? Mimi naamini alikuwa anajua kwa undani alichokuwa anasema. Imekuwa kitambo toka atoe tamko hilo, lakini sasa hivi tunaona wananchi ndio wanalivalia njuga hili suala.

   Wakati wa kampeni za Uraisi huko majimboni, Kikwete alikuwa anawasihi na kuwahimiza wananchi kumsaidia kwa kuwachagua wasomi kwenye majimbo ambayo wagombea wa CCM walikuwa wanasema wanaelimu kadha wa kadha. “Nawahitaji hawa wasomi, wachagueni jamani” alinukuliwa na vyombo vya habari wakati akiwauza wabunge hao.

   Hata alipochagua baraza lake la mawaziri, ingawa alikana kuwa hakuwachagua mawaziri kwa sababu ya usomi wao, lakini vyombo vyake vya propaganda kama IPP media, vimeandika kuwa wananchi wamelisifia baraza la Mawaziri la Kikwete kuwa lina jumla ya Madaktari na maprofesa kumi na kitu. Huu ni upotoshaji wa hali ya juu. Niliwahi kuandika mahala pia kuwa hakuna anayekwenda ndani na kuchunguza uhalali wa udaktari wa viongozi wetu. Tunachotajiwa ni idadi ya wasomi tu. Si ajabu kukuta udaktari wa kiongozi fulani ni wa vitunguri “gourd” uliopatikana kutokana na “home schooling” karibu na Mlima Kolelo au Kaole Bagamoyo, na wala sio wa mifupa kama tunavyodhani. Au Uprofesa wa kiongozi fulani ni wa kutajirisha watu kama ule wa Profesa Majimarefu na wala sio wa daraja la ufundishaji vyuoni kama tunavyoamini. Au ile inayoitwa “diploma ya mazingira” iliyopatikana Bulgaria, ni “Certificate of attendance” tena ya warsha ya mazingira ya siku moja.

   Viongozi wote wanaonunua vyeti, wanaweza kuchaguliwa katika hali ya kawaida bila hata kuongopa juu ya viwango vyao vya elimu. Ikumbukwe kuwa wengine walishakuwa mawaziri kabla ya kuanza huu ulaghai. Wasiwasi wangu ni kuwa, kama wameweza kutuongopea katika suala la elimu, ni kitu gani kingine wametuongopea? Baadhi yao wametuweka kwenye mikataba ya ulaghai wakishirikiana na wasomi wa kweli. Rai yangu ni kuwa hawa wote hawapashwi kuwa viongozi wetu. Hili suala siyo la kuwaachia wenyewe wajiamulie hatima yao. Ni suala la sisi raia wote kuwapigia makelele mpaka wakaachia ngazi.

   Nakumbuka Mzindakaya alikuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma mwaka 1991/1992 na akapata ziara ya siku mbili nchini Ireland kwa mwaliko wa rafiki zake wa kizungu aliojuana nao huko Kigoma. Haikuwa safari ya kiserikali. Cha kushangaza, kwenye mtandao wa wabunge ameweka kuwa ana cheti kilichopatikana huko Ireland. Hivi wanao hakiki vyeti wapo? Labda akiwa ziarani alipata kozi ya siku mbili.

   Jenerali Ulimwengu aliwahi kutoa makala katika gazeti la Rai, yenye kichwa cha habari “Simwogopi Nsanzugwanko”. Ulimwengu alibainisha wazi kwamba, Mheshimiwa Nsanzugwanko anajipachika digrii ambazo hana, yaani hakuzipata kwa njia halali ya kwenda shule. Haya maneno siyo ya Kyoma, Mzee Sam, au Mzee ES manake inaweza ikaonekana ni porojo. Ni maneno ya mtu aliyewahi kushika kushirikiana na hawa waheshimiwa katika ngazi za uongozi wa kitaifa. Ni mtu wa karibu nao na anawajua vizuri. Sijawahi kusikia kauli au maelezo ya Mheshimiwa Nsanzugwanko ya kukana maandishi ya Ulimwengu kwa watanzania, au kutetea digrii alizokuwa anaziongelea Ulimwengu. Wote tunajua nyazifa mbalimbali alizoshika huyu Mheshimiwa katika historia ya nchi yetu.

   “Jalada la Mbunge mmoja lafika ofisini kwa DPP, DCI asema tayari upelelezi umekamilika”. Well, labda tuvute subira tukiwa na imani kuwa utawala wa Raisi Kikwete utajenga utamaduni mpya tofauti na ule tuliouzoea. Lakini lazima tukumbushane kuwa imekuwa ni kawaida kwa serikali kutoa kafara kwa mtu mmoja awe kiongozi au mtumishi wa kawaida ili kutuliza hasira za raia juu ya masuala ya msingi yanayohusu nchi yetu.

   Pamoja na ufisadi wa kiwango cha juu uliokuwa unaendelea chini, na hata kazi yote aliyoifanya Warioba, ni kiongozi mmoja tu wa ngazi za juu aliyefikishwa mahakamani bila hata kutiwa hatiani. Tuliona tukio lililotokea uwanja wa ndege wa Dar wakati Waziri wa mambo ya ndani kwa wakati ule Ndugu Mrema alipowakamata waliokuwa wanatorosha madini nje ya nchi. Tulichoambulia ni msamiati wa neno “vigogo”.

   Tumeshuhudia mikataba ya wendawazimu ya kuiuza nchi yetu ambayo inaonyesha bayana kuwa yalikuwepo mazingira ya rushwa. Raia wa kawaida wakihoji, viongozi wanasema walete ushahidi. Raia wa kawaida atapata wapi ushahidi wa mikataba inayofanyika sirini? Ili kuwapoza raia wa kawaida, wasiendelee kuhoji, tunapewa habari kuwa mtendaji wa kijiji afikishwa mahakamani kwa kutoa rushwa katika kesi ya wizi wa kuku.

   Tumeendeleza pia utamaduni wa kihuni toka enzi za Kambarage. Mtu akifuja mali za shirika fulani, anahamishiwa shirika lingine. Hawa watu hawapashwi kuchaguliwa, kuhamishwa, au kuteuliwa kwa nafasi yoyote ya uongozi. Tukifanya hivyo, tunakuwa tunawachanganya. Ni sawa na mtoto mdogo anapofanya kosa unampa zawadi, na anapofanya kitu cha maana unampa adhabu. Ataendelea kufanya makosa akitegemea kuzawadiwa.

   Ripoti ya gazeti la leo linalomilikiwa na Serikali “Daily News” ambayo imetolewa na Mkaguzi mkuu wa Serikali, inaonyesha kuwa shilingi bilioni 2.2 ni mojawapo ya fedha zilizopotea ndani ya wizara moja ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa katika mwaka wa fedha wa 2004/2005. Fedha hizo hazijarudishwa hazina hivyo, hazijulikani zilipo. Pamoja na kuwa tulikuwa hatujuhi hizo habari, na wala hatuna utaratibu wa kujua habari kama hizo kabla ya kuwachagua viongozi wetu, kiongozi wa wizara hiyo kwa mwaka huo wa fedha tumemzawadia na kumpandisha cheo kuwa Raisi wa nchi yetu. Sidhani kama kuna mtu anaweza thubutu kumuuliza swali.

   Mambo tunayoyafanya mara kwa mara, na kwa muda mrefu mpaka yakazoeleka na mwishowe yakakubalika katika jamii yetu yanaitwa utamaduni. Inakuwa ni sehemu muhimu ya maisha yetu na ndiyo hasa tunawaridhisha watoto, wajukuu, na vitukuu vyetu. Watanzania hatutambuliki nje na ndani ya nchi kwa sababu ya rangi yetu, bali kwa sababu ya historia, maisha, na utamaduni wetu. Hatuwezi kujikomboa na balaa la ujinga na umasikini, na tukajenga nchi inayotambulika duniani kwa utamaduni wa wanataaluma na wanasiasa wetu kuwa na vyeti vya kununua.

  14. Mkira's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th May 2006
   Posts : 470
   Rep Power : 1283
   Likes Received
   105
   Likes Given
   7

   Default

   Kyoma maelezo yako ni sahihi kabisa!

   hili suala ni baya lakini cha ajabu watu wengine wanaonekana kuliunga mkono. Labda nao wana vyeti vya aina hiyo!

   Ninakubalina na wewe kuwa hao wangeliweza tu kuchaguliwa hata bila kununa hizo elimu feki. Kama mtu anasema ana phD na wakati ni amepata cheti na elimu ya juu mtu wa aina hiyo anachaguliwa kuwa waziri na inapotokea anakwenda kwenye argument na maziri wenzanke wkenye intenationa argument, he/she will always flop.
   Prof Msolla aleisema lakini kuanzia hapo yuko kimya!

   kundelea kubishana na anayetetea hili suala la vyeti ni kupoteza muda kama naye ana cheti cha aina hiyo!!

  15. Matata's Avatar
   Member Array
   Join Date : 28th March 2006
   Posts : 22
   Rep Power : 809
   Likes Received
   3
   Likes Given
   5

   Default

   Nchi yetu iwezi kuendelezwa na viongozi wanao forge vyeti au kuuziwa vyeti, Kwanza ni serious crime. Ndio hao hao viongozi waliokuwa wanawauzia watanzania nafasi za masomo ya elimu ya juu pale wizarani. Kama ulivyosema Ndg. Mkira, anayewatetea watu hao naye labda ni mhusika mkuu.

   Napenda pia kumuunga mkono Ndg. Kyoma kwa maelezo mazuri juu ya swala hili. Hapo nyuma nilitoa maelezo kuhusu the so called “ Commonwealth Open University” (http://www.commopu.org) nikawaeleza kuwa hapa British Virgi Islands hakuna Commonwealth University bali ni matapeli wanafanya biashara ya kuuza vyeti, kama kawaida nilipata upinzani mkubwa kutoka kwa watu hao hao wanaosupport hivyo vyeti vya kununua, mwishowe topic ikafa na mimi ni kakaa kimya.

   Ukifungua hiyo website yao utaona kuwa wana maproffessor, hiyo yote ni danganya toto. Wanaorodheshwa ni watu wale wale waliowapatia hivyo vyeti, na mmoja wao na mfahamu mimi binafsi ni kiongozi kwenye serikali ya Gambia( West Africa). Mimi kama mkazi wa British Virgin Islands ambako wanasema chuo kipo nilishindwa kuona hizo ofisi zao, hiyo biashara ni ya watu wawili au watatu wanafanyia shughuli zao majumbani ofisini hawana igawa wagekuwa registered kwenye ofisi ya Registreer of companies. Nilijaribu kuwasiliana nao ilinijiunge nao kimasomo, baada ya kugundua kuwa ni mkazi wa hapa hawakujibu barua zangu. Kwa wasomaji wapya, tembelea tovoti yao mtagundua kuwa kinachotakiwa tu ni fedha wala si elimu. Kwa kuwa nyie mko mbali jaribu kuwasiliana nao watawajibu, baada ya hapo ndipo mtajua ukweli wa hii Open University.

   Kama kuna institution yoyote hapo nyumbani inayochunguza hizi case za kununua madegree watembelee hii tovoti. Tuendelea kupiga vita na kuwafichua wanunuzi wa haya ma-degree fake.
   HAKUNA MATATA

  16. Field Marshall ES's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th April 2006
   Posts : 13,876
   Rep Power : 196824
   Likes Received
   722
   Likes Given
   225

   Default

   Wazee Mkira, Kyoma, na Matata,

   Maneno mazito, na salam zinafika kwani kila mbunge ana mtandao na huwa hizi habari zinasomwa kila siku na huwa zinazungumzwa, hii forum sio wengi wanaoishitukia lakini pole pole wanaingia kwa hiyo hatuongei na ukuta hapa na ni lazima tuendelee kupiga kelele kwa kuheshimu mazingara tuliyonayo ambayo ni ya kuingia humu kwa majina bandia na kumwaga vitu,

   Serikali ikiwa right tuseme na ikikosea tuseme zaidi na kupiga kelele kwani in a million time tunawasemea wasioweza kusema, yaani wanyonge na vitabu vyote vya dini yoyote ile vinasema it is ok with the Gods!

  17. Gagnija's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th April 2006
   Posts : 5,340
   Rep Power : 85902917
   Likes Received
   2011
   Likes Given
   1701

   Default

   Kyoma,
   Niliwahi kuuliza huko nyuma bcstimes kama inaweza kuwa kweli mtu mwenye
   ordinary diploma ya CBE kusoma MBA ,nikajibiwa kuwa hilo halina tatizo.

  18. mzeewabusara's Avatar
   Member Array
   Join Date : 7th June 2006
   Posts : 11
   Rep Power : 797
   Likes Received
   19
   Likes Given
   0

   Default

   Waandishi wa habari mbona hamtaki kuwataja hao ambao tayari wamekwishashtakiwa na majalada yao yako kwa DPP?. Tafadhali waandishi wa kitanzania jitahidini kufanya intensive investigative journalism ili watu wapate habari za uhakika.
   Mfano suala la NSSF sijaona kama kuna mwandishi yeyote ambaye amefanya investigative journalism na kutupa ukweli wa mambo.

  19. Field Marshall ES's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th April 2006
   Posts : 13,876
   Rep Power : 196824
   Likes Received
   722
   Likes Given
   225

   Default

   Hawa waandishi uchwara, wote sasa hivi wako kwenye mkao wa kula kutoka "Mtandao", sasa wamepewa kazi mbili nazo ni kumfunika Mkapa na kuwatangaza viongozi wawili JK na EL, tena bila hata ya aibu hata kama inabidi waseme uongo, kwa mfano

   (1). JK alipokwenda US, hakuonana rasmi na mzee Bush lakini tukaambiwa maneno mengi ya uongo kumbe ukweli ni kwamba alionana na Chenney na baadaye Bush alipita tu na kumsalimia basi!!!!!!

   (2). Tunaambiwa kwamba JK ni rais wa kwanza mu-Afrika, kuongea kwenye CNBC na Bloomberg TV network, tena wanasema bila ya aibu! Kwamba JK ndiye rais wa kwazna kwenda NASDAQ na kufungua ile kengele ya biashara, what a uongo!

   Mandela ndiye anayeshikilia record ya kila sifa huko ma-US, ndiye rais wa kwanza mu-Afrika kufanyiwa kila maajabu, ikiwa ni pamoja na kupokewa na Mayors wa NY kuanzia Dinkins, Giuliani, mpaka Bloomberg na mpaka leo akiwa mstaafu mambo yake huko US bado ni yale yale, huko NASDAQ marais kibao kina Obasanjo, Kofuor, Mubarak, Mbeki, mpaka mzee wa damu Kagame amefika na kufungua, kuacha wanamichezo hasa wakimbiaji Marathon wa Kenya na Ethiopia, huenda huko kila siku kwa hiyo nyie Mtandao na waandishi uchwara acheni kamba zenu,

   Andikeni mambo muhimu ya taifa, kama ni serikali ya awamu ya nne iachieni ifanye vitu vionekane watasifiwa sio kupiga ngomaa tu na wakati matendo hayaonekani, kampeni zilishaisha tena mzee JK mwenyewe aliomba wapambe wavunje vikundi vya siasa ndani ya CCM, sasa nyinyi vipi mbona bado tu hamuachi? Wananchi wanaanza kuchoka na misifa tuuu wakati ndio kwanza tunaanza upya kugawana umeme!

   Mzee wa Busara Bravo!

  20. The Invincible's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th May 2006
   Location : Online
   Posts : 3,216
   Rep Power : 1443
   Likes Received
   487
   Likes Given
   1

   Default

   Wajameni
   Suala la media za Bongo, hata mimi zimeniacha hoi. I guess they struggle to survive. Strategy waliyotumia ili kuendelea katika biashara ndio kununuliwa na wana mtandao wa JK.

   Nimesoma matoleo mengi ya Rai kwa mfano. Kikwete anasifiwa kwa namna ambayo malaya tu wanaweza kuamini. Bila shaka ni backlash ya BM na JU wa Rai juu ya kuvuliwa uraia wake. Mapato ya uandishi wa ovyo ovyo namna hii ni kutupotosha sisi wananchi. Ama kweli wapiganapo fahari wawili, ziumiazo....... Na vijigazeti vingine vyote ni uharo mtupu. Havielewi hata umuhimu wao kama media katika jamii.

   Samahani nimetoka kidogo nje ya mada ya vyeti feki.
   Jiunge na timu ya kuondoa CCM madarakani

  21. Kyoma's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 2nd June 2006
   Location : Mfugwa Mbwa
   Posts : 124
   Rep Power : 820
   Likes Received
   53
   Likes Given
   0

   Default

   Mzee ES,

   Wahenga walituasa kuwa "Kizuri cha jiuza, kibaya cha jitembeza"

   By the way, magazeti yakiandika habari zisizo saihi kuhusu serikali na ambazo haziwafurahishi viongozi wetu, yanakanywa na mengine yaliwahi kufungiwa chini ya kivuli cha kutokufuata maadili ya uandishi wa habari. Lakini wanapoandika habari za uongo uleule lakini wa kuwasifia viongozi, hakuna maadali yaliyokiukwa. IPP Media ni taasisi kubwa sana ya habari nchini kwetu. Inawafikia wananchi waliowengi kuzidi vyombo vingi vya habari. You should be ashamed of yourself!

   Hivi nani kasema kuwa nchi yetu haina kazi? Rai yangu ni kwamba watu wengi wamepata kazi katika taasisi ya habari, lakini kazi zenyewe hazijapata watu. Tangu lini Fundi Cherehani akawa Mhariri wa habari zinazo husu siasa? Umewahi kuona wapi a primary school drop out aliyenunua cheti cha Uandishi wa habari anapewa jukumu la kuandika habari za viongozi wenye Phd za kununua?


  Page 2 of 30 FirstFirst 123412 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Tume ya kuhakiki vyeti vya watumishi serikalini lini/ tcu mko wapi
   By mbasamwoga in forum Nafasi za Kazi na Tenda
   Replies: 4
   Last Post: 7th September 2011, 12:19
  2. Vyeti feki vyuo vya uganda changamoto serikali mpya ya sudan
   By BASIASI in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 0
   Last Post: 18th August 2011, 23:17
  3. kwanini viongozi wenye vyeti feki bado wapo madarakani?
   By Papa Diana in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 1
   Last Post: 1st March 2011, 17:37
  4. Replies: 1
   Last Post: 8th June 2009, 15:26
  5. Watani wa Jadi(Wakenya), Ajira Bongo na vyeti feki
   By MpigaFilimbi in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 9
   Last Post: 11th February 2009, 11:58

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...