Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

    Report Post
    Page 37 of 40 FirstFirst ... 273536373839 ... LastLast
    Results 721 to 740 of 785
    1. #1
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,783
      Rep Power : 1810
      Likes Received
      2690
      Likes Given
      178

      Default Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHIS SYKES (1924 -1968)

      Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika na Mohamed Said

      Pitio la Kitabu

      Kitabu hiki kilipochapwa kwa mara ya kwanza 1998 kwa Kiingereza nchini Uingereza na kilipoanza kuzagaa katika maktaba na maduka ya vitabu mjini London yanayouza vitabu kuhusu Afrika Watanzania wengi waliokuwa Uingereza walisisimuliwa na yale yaliyokuwa ndani ya kitabu hiki. Kubwa zaidi ilikuwa kule kufunuliwa kwa mara ya kwanza kuwa kumbe TANU chimbuko lake si Julius Nyerere bali ni marehemu Abdulwahid Sykes. Hii ilikuwa habari mpya kwa wengi hasa ikizingatiwa kuwa Nyerere mwenyewe hakuwahi kumtaja Abdulwahid Sykes kama mwenzake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hili lilikuwa la kwanza. Kitu cha pili kilichosisimua wasomaji ni kuwa mwandishi kwa kutulia kabisa alionyesha bila woga na kutafuna maneno kuwa TANU kilikuwa chama kilichojengwa katika migongo ya Waislam. Hili alilishaijisha kwa kueleza wazalendo waliokuwa bara ambao kwa umoja wao na wengi wao wakiwa Waislam walipambana na ukoloni wa Kiingereza.

      Kubwa zaidi la kusisimua ilikuwa kitabu kilieleza bila kupepesa macho au kutafuna maneno njama alizofanya Nyerere kwanza kumfuta Abdulwahid Sykes katika historia yake binafsi, TANU na katika harakati za kudai uhuru. Lakini kilichotibua sege la nyuki ni pale katika kuhitimisha kitabu mwandishi alipoweka wazi mipango ya Nyerere akishirikiana na Kanisa Katoliki baada ya uhuru kupatikana kupanga njama za kuzuia maendeleo ya Waislam. Katika kipande hiki msomaji atakutana na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mwanasiasa shupavu. Msomaji ataziona juhudi za Sheikh Hassan bin Amir katika kupambana na njama za Nyerere na Kanisa Katoliki na nini kilimfika msomi huyu maarufu wa Kiislam. Kwa wakati ule Nyerere akiwa hai ilihitaji ujasiri mkubwa kwa yeyote yule kusema au kuandika hayo.

      Nakala za kitabu zilifika Tanzania na kila aliyesoma alipatwa na mshtuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nje yake. Kitabu kiliwaudhi wapenzi wa Nyerere na wapo waliomwendea kwa kutaka afanye jambo kukomesha “uongo” wa mwandishi. Wengine hawakuamini kuwa huyo anayejiita Mohamed Said kama kweli yupo. Wengine walitaka kujua kama kweli akina Sykes na baba yao ndio waasisi wa vyama vya Waafrika katika Tanganyika katika 1929 hadi 1954 TANU ilipoasisiwa. Hii ilikuwa bahari kubwa kwa wapenzi wa Nyerere ambao wasingeweza kuogelea bila ya msaada wake Baba wa Taifa. Mawimbi ya bahari hii yalikuwa marefu na yakija kwa kasi. Juu ya haya yote Waswahili wana msemo “penye ukweli uongo hujitenga.” Nyerere asingeweza kuthubutu kukana mchango wa marehemu Abdulwahid kwake yeye binafsi na kwa TANU. Abdulwahid ndiye aliyempokoea Dar es Salaam ile ya miaka ya 1950 na akamjulisha kwa wenyeji wa mji. Wapenzi wa Nyerere hadi leo ukiwauliza Nyerere alisema nini kuhusu ukweli kuwa si yeye aliyeasisi TANU wamekuwa kimya.

      Msomi maarufu wa Chuo Kikuu cha Cambridge John Illife ambae ameandika sana historia ya Tanganyika alikasirishwa na msimamo wa mwandishi khasa pale aliposema kuwa inastaajabisha kuwa Illife ingawa alitegemea nyaraka za akina Sykes katika kuandika historia ya African Association inastaajabisha hakuona umuhimu wa kutaka kumhoji marehemu Abduwahid aliyekuwa katibu na rais wake kati ya 1951 hadi 1953. Akiandika pitio la kitabu hiki katika Cambridge Journal of African History Illife alimshambulia mwandishi katika njia ambayo haikuwa staili yake msomi mkubwa kama yeye. Illife alikuwa ameghadhibishwa kwa kuambiwa katika kitabu kuwa alimzuia mwanafunzi wake katika Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa 1969, Daisy Sykes ambae alikuwa binti ya Abdulwahid asiandike maisha ya baba yake. Daisy wakati huo msichana mdogo alikuwa amekasirishwa na jinsi TANU na magazeti yake yote, “The Nationalist” chini ya uhariri wa Benjamin Mkapa na “Uhuru” yalivyoshindwa kumwandika baba yake kwa hadhi aliyostahili. Magazeti hayo yaliripoti kifo cha Abdulwahid Sykes kwa kuwa Nyerere alikwenda mazikoni. Hapakuwa na jingine. Brendon Grimshaw ambae alikuwa Mhariri Mkuu wa “The Tanganyika Standard” na akimfahamu vyema Abdulwahid ndiye aliyendika tanzia ya maana katika “Sunday News” akasema kuwa Nyerere asingelifika pale alipofika kama si kwa msaada wa Abdulwahid Sykes na ni juhudi za ukoo wa Kleist ndiyo uliowezesha watu wa Tanganuyika kuwa na chama cha siasa. “The Standard” na “Sunday News” wakati ule lilikuwa gazeti huru halikuwa na hofu ya Nyerere. Hii ilikuwa mwaka 1968.

      Kilipotoka kitabu hiki mwaka 1998 walikuwepo watu walioona ukweli wa kuwa historia ya TANU bado haijaandikwa na kuna baadhi ya shutuma zilizoelekezwa kwake Nyerere ni muhimu yeye mwenyewe akazijibu akiwa hai kwa faida ya jamii isijesemwa kuwa kasingiziwa, walimsubiri afe ndipo wamzushie la kumzushia. Mmoja wa kundi hili la pili alikuwa marehemu Prof. Haroub Othman. Yeye alimkabili Nyerere uso kwa macho na kumuomba atoe majibu kujibu shutuma za waandishi wawili. Kwanza ajibu shutuma za Sheikh Ali Muhsin Barwani aliiyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) katika kitabu chake “Conflict and Harmony in Zanzibar” na kitabu cha Mohamed Said “The Life and Times of Abdulwahid Sykes (19241968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.” Sheikh Ali Muhsin akimtuhumu Nyerere kwa kupeleka mamluki Zanzibar kuipindua serikali ya wananchi na Mohamed Said akimtuhumu kwa chuki dhidi ya Waislam na kupotosha historia ya uhuru wa Tangnayika. Prof. Haroub alimshauri Nyerere kuwa njia nzuri ya kuiweka historia yake na uhusiano wake na Waislam sawa ni kwa yeye kuandika historia ya maisha yake. Hadi Nyerere anaingia kaburini hiili halikufanyika.

      Kitabu hiki ni muhimu kwa Waislam na wananchi wote kwa ujumla kukisoma na kuwahimiza watoto wao nao wakisome wapate kujifahamu na kufahamu changamoto za udini na chanzo chake. Ndani ya kitabu hiki mwandishi amejitahidi kukusanya mashujaa waliotupwa waliopigania uhuru wa Tanganyika hata kabla hawajasikia jina la Nyerere wala kuona sura yake, wazalendo kama Hassan Suleiman na Juma Ponda wa Dodoma. Wazalendo waliohutubia mikutano ya hadhara na kuhamasisha watu kudai uhuru hata Nyerere hawamjui kama Titi Mohamed na wengine wengi kutoka katika majimbo ya Tanganyika. Ukikianza kitabu hiki huwezi kukiweka chini hadi umefika mwisho.

      Kitabu hiki kinapatikana Ibn Hazim Bookshop Mtoro na Manyema na Tanzania Publishing House, Samora Avenue.
      Last edited by Mohamed Said; 13th March 2011 at 19:45.


    2. #721
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Ogah View Post
      kwa hiyo wengine tulipenya kwenye "Nyufa"? au
      Jibu lake liko kwenye kitabu tajwa, jee umesha kisoma?

    3. #722
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Ogah View Post
      samahani sana Mkuu naomba ufafanuzi kwenye hilo.........kama namba ndio zilikuwa zikitumika.........huo mfumo wa kusahihisha mitihani kw akutumia majina.....ndio upi huo?
      1) Mfumo wa mwanzo:

      Jina: Ogah
      Namba: 1732528

      2) Mfumo wa Malima:

      Namba: 1732528

    4. #723
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Coach Parcells View Post
      Naona ni jambo la ajabu utumie muda wako mwingi kulumbana na kujibu maswali humu wakati "mwandishi" wa kitabu husika yumo humuhumu lakini kabaki kimya. Halafu ukitilia maanani pia jitihada za Mohamed Said pale mwanzo za kutoa majibu zilikuwa haziridhishi kabisa, basi naanza kutilia mashaka kama Mohamed Said ndiyo mwandishi kweli wa hiki kitabu.
      Mashaka ni yako haki yako.

    5. #724
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Zing View Post
      Na je huyu Adulwahid sykes alikuwa kabila gani?.
      Kwa sisi ma trabalist tutapenda pia ili tuliweke kwenye rekodi.
      katika makabila yaliyoleta uhuru Tanganyika
      Imeelezwa kwenye kitabu tajwa.

    6. #725
      Ndjabu Da Dude's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2008
      Posts : 2,441
      Rep Power : 11665
      Likes Received
      308
      Likes Given
      138

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo View Post
      1) Mfumo wa mwanzo:

      Jina: Ogah
      Namba: 1732528

      2) Mfumo wa Malima:

      Namba: 1732528
      That's totally absurd! Kwa nini utumie jina na namba? Unaweza kutupatia vyanzo huru kuthibitisha hayo mabadiliko ya "mfumo wa Malima" unayodai? Hii ni myth mojawapo tu kati ya nyiingi ambazo Waislamu wanapenda sana ku-perpetrate.


    7. #726
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Ogah View Post
      Kitabu nimesoma........na hilo suala halijathibitika.......kwa hiyo ni sahihi kumuita Mnafik

      Kuhusu MS na maswali aliyoulizwa...........kwa kifupi hajajibu....kwa wewe kutumia maneno ya kejeli......i.e...."kutojibiwa swali lako ni jibu tosha"....nadhani unakosa adabu ya ilmu
      Halijathibitika kwako wewe, wengine wamethibitisha, kwa hiyo "mnafik" ni wewe.

      Kutojibiwa swali lako ni jibu tosha, si kejeli, ni ukweli, unauliza swali ambalo jibi lake lipo kwenye kitabu, sasa kuna sababu ipi ya kujibiwa?

      Eleza page na au quote ya sehemu inayokutatanisha kwenye kitabu, si unacho? why generalize?

      Ilm aadab, siyo adabu, adabu ni maana tofauti na aadab.

    8. #727
      Nanren's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2009
      Posts : 1,056
      Rep Power : 726
      Likes Received
      367
      Likes Given
      563

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo View Post
      Kama hujui Kanisa ni nini, mimi siwezi kukufundisha hilo.

      Kama hujuwi maana ya Kanisa utajuwaje maana ya wakala wa kanisa? Kwanza kajifunze kanisa ni nini ukishajuwa njoo uniambie umejuwa halafu tuanze kukufunda maana ya wakala wa kanisa.

      Kuhusu mengi ni mawazo yako, nawe una haki ya kuwaza upendavyo, lakini, kama umepaona palipopikwa na si pa ukweli kwenye kitabu tajwa, naomba tuoneshe hapa na utuoneshe upi ndio ukweli. Natumai tupo pamoja.
      Ninafahamu kanisa maana yake. Na nilifikiri MS naye anayeelewa, na nikafikiri na wewe unaelewa, ndio maana nikauliza mnamaanisha nini labda kwenye context ya hii thread? Je unamaanisha kanisa la kakobe au KKT, au katoliki au? Rejea alivyouliza MS. Ni vigumu kumpa majibu sahihi. Sasa nawewe kama hutaki kusema mnachomaanisha, basi, hili tuliache bila majibu.

      Kupika information mlianza kwanza kwa "ku-speculate" kwamba muslims walikuwa wengi kuliko non muslims, Out of this mkajaribu kujihakikishia na sensa ya mwaka 1967 mkaona haiwa-support, mkaamua ku-speculate kwamba The Census was doctored. Mkaamua kwa makusudi kuchambua majina ya kiislam na kuonyesha kuwa waislam ndio walipigania uhuru wa nchi hii, as if wengine wote hawakushiriki and as if uhuru ulikuwa unapiganiwa kwa misingi ya dini badala ya utaifa. Mkaangalia ndani ya waajiriwa serikalini na wanafunzi elimu ya juu mkasema kuna njama hapa maana majina ya kiislam ni machache, mkaanza tena ku-speculate kwamba wanahujumiwa na kanisa na mawakala wa kanisa. Ndipo kila mara mnajaribu kuja na ushahidi (manufactured evidence) usio na mashiko kuonyesha kuwa mnachoongea ni kweli. Mengine juu ya kupika/ku-doctor, angalia post ya Joka kuu kwenye post #749 kuhusu "padre". Na pia angalia post #647 ya bwana LGFumbuka.

      Look here my brother, I have so many muslim friends and even some relatives, and I like them. Karibu wote hawaungi mkono madai yenu nyie, sasa you may decide kuwaita wao ni mawakala, but at the end of the day, Tanzania as a country itabaki na sisi wote (wakristo, wapagan, wahindu,mabohora, pamoja na waislam-hata kama wewe hutawatambua kwamba ni waislam). Nyie acheni kupika data kwa lengo la kutaka kutugawa.
      Last edited by Nanren; 13th March 2011 at 17:19.

    9. #728
      Ndjabu Da Dude's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2008
      Posts : 2,441
      Rep Power : 11665
      Likes Received
      308
      Likes Given
      138

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo View Post
      Mashaka ni yako haki yako.
      Si useme tu wewe ndiye mwandishi kweli wa hicho kitabu?

    10. #729
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Zing View Post
      • Je kanzu ni vazi la kiislam au ni vazi la kitamaduni?
      • Je jina selemani. Michael ni jina la kiiislam au ni majina la watu wa utamaduni fulani?
      • Je mabush men sahara kule wasiovaa nguo hawawezi kupelekwa uislam au itabidi wote kwanza wavalishwe nguo kabla ya kukubaliwa na Allah ?


      Kuna vitu wewe unfanya kwenye imani yako ya usilam sio vya imani bali ni vya kitamduni ya kiarabau hivyo hivyo hata mimi mkristu kuna baadhi ya vitu ninafanya sio vya imani ya kikiristu bali ni utamaduni wa a kimagharibi. Bila kujua na kukubali haya utabaki gizani .

      Sometime penda kujichallnge hata kile unachoamini
      1) Sijui, kawaulize ma Padri, mbona wao wanavaa kanzu.

      2) Tuitane kwa majina mazuri, ndio mafundisho ya kiIslaam.

      3) Sina elimu ya Sahara kuwa na ma-bushman rejea vitabu vyako ulivyosoma, kama umekosea rudi tena ukiwa umesharekebisha swali.

      Hakuna kitu nnachokifanya chenye utamaduni wa ki Arabu ambacho kinvunja mila za kiIslaam, hali kadhalika hufanya hata utamaduni usio wa kiArabu ili mradi hauvunji mila za kiIslaam. Uislaam ni mfumo wa maisha unaoamrisha mema na kukataza mabaya.

    11. #730
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Coach Parcells View Post
      That's totally absurd! Kwa nini utumie jina na namba? Unaweza kutupatia vyanzo huru kuthibitisha hayo mabadiliko ya "mfumo wa Malima" unayodai? Hii ni myth mojawapo tu kati ya nyiingi ambazo Waislamu wanapenda sana ku-perpetrate.
      Wewe katafute vyanzo huru, sisi tumekuwekea hivyo. Mengine ni yako.

    12. #731
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Coach Parcells View Post
      Si useme tu wewe ndiye mwandishi kweli wa hicho kitabu?
      Si mimi mwandishi wa hicho kitabu, wala sijawahi kuandika kitabu lakini MS kanipa motisha kubwa kupitia mjadala huu, naomba nijaaliwe na mimi niweze kuandika kitabu (angalau kimoja) chenye manufaa kama vya MS kabla ya umauti haujanifika. Amiin.

      Napenda uelewe, wengi wa wazee wanaotajwa kwenye kitabu, ni wazee wangu pia, mimi nimezaliwa.na nimekulia Kariakoo, nyumba ambayo inatajwa sana iliyo new street, kwa sasa Lumumba ambayo ndipo ilipoanzia TANU (Lumumba na Kariakoo) nyumba ya tatu yake ni kwa shangazi langu (Lumumba na Udoe), katikati ya hii nyumba na hiyo ofisi ya TANU ndio jengo jipya la ghorofa la CCM, kwa sasa hata hii nyumba ya shangazi yangu linajengwa ghorofa. Kwa hayo, nadhani utaelewa mnasaba wa hiki kitabu na mimi.

    13. #732
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3185
      Likes Received
      428
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By JokaKuu View Post
      Mdondoaji,

      ..kwa experience yangu ya kufanya mitihani nchini, sikuwahi kuona suprises zozote zile ktk matokeo ya mitihani ya kitaifa. ninachomaanisha ni kwamba matokeo ya mitihani ya kitaifa yalikuwa reflective ya performance ya mwanafunzi ktk kipindi chake akiwa shuleni.
      Unajua haya mambo ya elimu kama ni kutolea mfano 1ja kuelezea elimu basi mfanoo mimi nina mfano halisi wa kelezea elimu ya tanzania kwa upana wake. Na siyo hiyo

      Kuhusu hili la Elimu mimi nimekaa mtaa filani hapa dar . Mtaa huo kuna wanafuzi wa kike fulani wawili na ni marafiki. Tatizo la wanafunzi ni kujihusha na mapenzi tena na mijibaba ambao ina wake.

      Mbaya zaidi na inasikitisha katika hawa wanafunzi kuna mmoja mzazi wake yeye kwake sio isssue kwa hilo jibaba kwenda kwao. Huyu mtoto mwingine wazazi wake ni wakali .


      Sokwa simple probability unaweza kujua kati ya hao ni yupi japo anaweza kupata a DIV III na yupi atapata DIV IV.

      Tatizo lingine inakuja shule wanayosoma.Kwa nidhamu na makuzi ya watoto hawa wawili ni wazi hawana self discipline na ni wao, wazazi wao na shule wa kulaumiwa..........

      Japo shule wanayosmyosma kuna watoto wachache wanafanya vizuri tena wa dini zote, tatizo la hawa watoto wawili linaonyesha tatizo la elimu si tu kwa muislam bali kwa watu wote.
      Shule zote zinahitaji wanafunzi wenye self discipline. Na wote tumesoma tumepita hukooooo

      • Ni wachache walibarikiwa kuwa na self discpline by themsselves na ndio wale walikuwa nafanya vizuri zaidi awe ni Abdalah, Issa au john .Wengine tulihitaji control kidogo kutoka kwa wazazi, walimu tution,kutafutiwa shule fulani,jamii, etc


      Education is About Student, Parent ,school, teachers na Wizara inakuja ya mwisho kabisa.
      Unless waislam waseme mambo ya kupima perfomance ya wanafunzi yanawadhulumu wanafuzi wa kiislam

      Sasa kuanza kutacle tatizo la elimu ya waislama kwakulaumu wizara ni kupotea njia. utashangaa unaweza kuweka midirector wote waislam na wasahihishaji wote waislam bado matokeo yasibadilike. Sasa sijui hao wasahihishaji wataiwa wanafiki

    14. #733
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,864
      Rep Power : 7692
      Likes Received
      1479
      Likes Given
      0

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Nguruvi3 View Post
      Mohamed Said,
      Baada ya changamoto nyingi nikuhabarishe kuwa watu wengi wamezama katika kurasa zako na wanazisoma. Tofauti na wasomaji makasuku hawa wanatafakari kwa kina na weledi. Wapo waliokwama kufungua kurasa zinazofuata kwasababu hawajaelewa sura iliyotangulia.

      Ahsanteni

      Nguruvi
      Mkuu mbona unanichanganya mimi na mtoa mada...? Kulikoni!?
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)


    15. #734
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Nanren View Post
      Ninafahamu kanisa maana yake. Na nilifikiri MS naye anayeelewa, na nikafikiri na wewe unaelewa, ndio maana nikauliza mnamaanisha nini labda kwenye context ya hii thread? Je unamaanisha kanisa la kakobe au KKT, au katoliki au? Rejea alivyouliza MS. Ni vigumu kumpa majibu sahihi. Sasa nawewe kama hutaki kusema mnachomaanisha, basi, hili tuliache bila majibu.

      Kupika information mlianza kwanza kwa "ku-speculate" kwamba muslims walikuwa wengi kuliko non muslims, Out of this mkajaribu kujihakikishia na sensa ya mwaka 1967 mkaona haiwa-support, mkaamua ku-speculate kwamba The Census was doctored. Mkaamua kwa makusudi kuchambua majina ya kiislam na kuonyesha kuwa waislam ndio walipigania uhuru wa nchi hii, as if wengine wote hawakushiriki and as if uhuru ulikuwa unapiganiwa kwa misingi ya dini badala ya utaifa. Mkaangalia ndani ya waajiriwa serikalini na wanafunzi elimu ya juu mkasema kuna njama hapa maana majina ya kiislam ni machache, mkaanza tena ku-speculate kwamba wanahujumiwa na kanisa na mawakala wa kanisa. Ndipo kila mara mnajaribu kuja na ushahidi (manufactured evidence) usio na mashiko kuonyesha kuwa mnachoongea ni kweli. Mengine juu ya kupika/ku-doctor, angalia post ya Joka kuu hapo chini kuhusu "padre". Na pia angalia post #647 ya bwana LGFumbuka.

      Look here my brother, I have so many muslim friends and even some relatives, and I like them. Karibu wote hawaungi mkono madai yenu nyie, sasa you may decide kuwaita wao ni mawakala, but at the end of the day, Tanzania as a country itabaki na sisi wote (wakristo, wapagan, wahindu,mabohora, pamoja na waislam-hata kama wewe hutawatambua kwamba ni waislam). Nyie acheni kupika data kwa lengo la kutaka kutugawa.
      Leta ushahidi wa unayoyasema kama umesoma kitabu, MS kataja majina ya waliokuwepo, sasa kama wewe unaona yapo zaidi ya hayo si uyalete. unaficha nini? mbona MS hajaficha? sasa nani anae "speculate" alyeandika kitabu na majina na vielelezo au wewe unaesema bila majina, bila vielelezo?

      Mradi Kanisa umelijuwa nimefurahi sana. Sasa rejea kwenye hayo makanisa uliyoyataja, Jee yalikuwepo wakati huo? kama hayakuwepo basi utabaki na lililo kuwepo. Ndio hilo hilo au kwa kukurahisishia tafuta nyerere alikuwa anatumika kanisa lipi? ukilipata, ndio hilo hilo, wala usihangaike sana.

    16. #735
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3185
      Likes Received
      428
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo View Post

      Hakuna kitu nnachokifanya chenye utamaduni wa ki Arabu ambacho kinvunja mila za kiIslaam, hali kadhalika hufanya hata utamaduni usio wa kiArabu ili mradi hauvunji mila za kiIslaam. Uislaam ni mfumo wa maisha unaoamrisha mema na kukataza mabaya.
      Kuwa mkweli ndugu

      • je kwa muislam muhaya au mpare ni rahisi kwake kuoa mtoto wa mjomba wake
      • Je kwa muislam wa Qatar kuna ugumu gani kuoa mtoto wa mjomba wake?

    17. #736
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3185
      Likes Received
      428
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Ogah View Post
      Kitabu nimesoma........na hilo suala halijathibitika.......kwa hiyo ni sahihi kumuita Mnafik

      Kuhusu MS na maswali aliyoulizwa...........kwa kifupi hajajibu....kwa wewe kutumia maneno ya kejeli......i.e...."kutojibiwa swali lako ni jibu tosha"....nadhani unakosa adabu ya ilmu
      Oga au yeyote aliyekisoma kitabu embu nisaidie kwenye kitabu mzee wetu wa Adulwahid Sykes anatajwa kama kabila gani ?

    18. #737
      Nanren's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2009
      Posts : 1,056
      Rep Power : 726
      Likes Received
      367
      Likes Given
      563

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo View Post
      Leta ushahidi wa unayoyasema kama umesoma kitabu, MS kataja majina ya waliokuwepo, sasa kama wewe unaona yapo zaidi ya hayo si uyalete. unaficha nini? mbona MS hajaficha? sasa nani anae "speculate" alyeandika kitabu na majina na vielelezo au wewe unaesema bila majina, bila vielelezo?

      Mradi Kanisa umelijuwa nimefurahi sana. Sasa rejea kwenye hayo makanisa uliyoyataja, Jee yalikuwepo wakati huo? kama hayakuwepo basi utabaki na lililo kuwepo. Ndio hilo hilo au kwa kukurahisishia tafuta nyerere alikuwa anatumika kanisa lipi? ukilipata, ndio hilo hilo, wala usihangaike sana.
      Tatizo ni kwamba MS kaingia mitini, sasa hapa hoja zimekuzidi, na wewe mshirika unajitahidi ujibu zote (japo unashindwa) unaishia kujibu kijuu juu sana (doesnt befit you) , matokeo yake majibu yako yanazua tena maswali tuliyouliza mwanzoni. Ngoja nikupe break. I'll be back after 3 days kuona kama wewe au MS mmekuja na convincing answers.

      For now I just leave you with this:

      YOU CAN STILL REMAIN A GOOD MUSLIM TO YOUR GOD WHILE CO-EXISTING WITH NON-MUSLIMS IN TANZANIA WHILE WE ALL KEEP TRUSTING AND RESPECTING ONE ANOTHER AS TANZANIANS!

      All the best in your search for convincing answers!

    19. #738
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3185
      Likes Received
      428
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Nanren View Post

      Kupika information mlianza kwanza kwa "ku-speculate" kwamba muslims walikuwa wengi kuliko non muslims, Out of this mkajaribu kujihakikishia na sensa ya mwaka 1967 mkaona haiwa-support, mkaamua ku-speculate kwamba The Census was doctored. .
      Sasa kwa wale ukiendeleza logic baadae

      • Anasema wabunge wa tanzania 85% ni wa kanisa
      • Inawezeka na pia hata 85% ya wapiga kura wote ni wa kanisa kama wamo wasilam na wa dini nyingine basi ni wale wanafiki tu ndo wanapiga kura ndio maana wanawachagua wa kanisa

      Kweli katika kuajaribu kuunganisha unganisha mambo ili kukidhi kiu yake ya kidini kwa hili nilibaki nacheka. Hoja kama hizi ndio maana hata anasema kina kilaini wanamuogopa eti hawataki kukutana naye yeye muislam na kiongizi wa wasilam wa kweli na sio wa Bakwata. Haya mambo unaweza kuongea na Mtikila sio thetype of Kilainis



    20. #739
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,915
      Rep Power : 2990
      Likes Received
      2548
      Likes Given
      3634

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Zing

      Unajua haya mambo ya elimu kama ni kutolea mfano 1ja kuelezea elimu basi mfanoo mimi nina mfano halisi wa kelezea elimu ya


      tanzania kwa upana wake. Na siyo hiyo

      Kuhusu hili la Elimu mimi nimekaa mtaa filani hapa dar . Mtaa huo kuna wanafuzi wa kike fulani wawili na ni marafiki. Tatizo la wanafunzi ni kujihusha na mapenzi tena na mijibaba ambao ina wake.

      Mbaya zaidi na inasikitisha katika hawa wanafunzi kuna mmoja mzazi wake yeye kwake sio isssue kwa hilo jibaba kwenda kwao. Huyu mtoto mwingine wazazi wake ni wakali .

      Sokwa simple probability unaweza kujua kati ya hao ni yupi japo anaweza kupata a DIV III na yupi atapata DIV IV.

      Tatizo lingine inakuja shule wanayosoma.Kwa nidhamu na makuzi ya watoto hawa wawili ni wazi hawana self discipline na ni wao, wazazi wao na shule wa kulaumiwa..........

      Japo shule wanayosmyosma kuna watoto wachache wanafanya vizuri tena wa dini zote, tatizo la hawa watoto wawili linaonyesha tatizo la elimu si tu kwa muislam bali kwa watu wote. Shule zote zinahitaji wanafunzi wenye self discipline. Na wote tumesoma tumepita hukooooo
      Ni wachache walibarikiwa kuwa na self discpline by themsselves na ndio wale walikuwa nafanya vizuri zaidi awe ni Abdalah, Issa au john .Wengine tulihitaji control kidogo kutoka kwa wazazi, walimu tution,kutafutiwa shule fulani,jamii, etc

      Education is About Student, Parent ,school, teachers na Wizara inakuja ya mwisho kabisa. Unless waislam waseme mambo ya kupima perfomance ya wanafunzi yanawadhulumu wanafuzi wa kiislam

      Sasa kuanza kutacle tatizo la elimu ya waislama kwakulaumu wizara ni kupotea njia. utashangaa unaweza kuweka midirector wote waislam na wasahihishaji wote waislam bado matokeo yasibadilike. Sasa sijui hao wasahihishaji wataiwa wanafiki
      Zing,

      ..I am with you 100%.

      ..kwa experience yangu tulipokuwa shuleni tulikuwa tunajuana kabisa nani mwenye uwezo na nani alikuwa anaburuzwa. you could tell hata nani ataongoza ktk mtihani wa kitaifa iwe form 4 au 6. hata primary wanafunzi mnakuwa pamoja miaka 7 na mnajuana nani ana nafasi ya kufaulu na nani anasubiri miujiza.

      ..kwa mtizamo wangu hata suala la kuvuja mitihani halina athari kubwa ikiwa usimamizi wakati wa kufanya mtihani utakuwa mkali. kuna madogo walikuwa nyuma yangu shuleni mitihani yao yote ilivuja. kitu cha ajabu matokeo yalipotoka bado yalikuwa reflective ya performance yao ya miaka 4 shuleni.

      ..masuala ya elimu siyo ya kufikiria kirahisi-rahisi kama anavyoyasimulia Sheikh Mohamed. hata watoto wa baba na mama mmoja mara nyingine hutokea wakafaulu kwa viwango tofauti na kufikia ngazi tofauti za elimu. nidhamu ya mwanafunzi, mchago wa wazazi, waalimu, jamii inayowazunguka, mazingira ya shule, vyote hivyo vinachangia ktk end product ambayo ni, matokeo mitihani na ubora wa kitaaluma wa mwanafunzi. hiyo namba ya mtahiniwa unaitumia mara 3 ktk miaka 13 ya masomo tangu primary mpaka a-level.

    21. #740
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3185
      Likes Received
      428
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo View Post
      Mradi Kanisa umelijuwa nimefurahi sana. Sasa rejea kwenye hayo makanisa uliyoyataja, Jee yalikuwepo wakati huo? kama hayakuwepo basi utabaki na lililo kuwepo. Ndio hilo hilo au kwa kukurahisishia tafuta nyerere alikuwa anatumika kanisa lipi? ukilipata, ndio hilo hilo, wala usihangaike sana.
      Ok nyerere alikuwa anatumika kanisa katoliki. Je huyu Adbdulwahid sykes na wazee wa dar Es Saalaaam walikuwa wanatumika ka Islam gani ( Sunni au Shia au ....)

      Maana hatutaishia hapa Usije ukataka kuandika kitabu cha Adbulwahid sykes kama Musilm . kumbe akaja shikeh XXX mwingine akasema ukweli uliofichwa kuhusu kuhusika kwa waislam waislam wa kishia au sunni Tanzania. Inawezekana MS kazi ya ukweli wake bado kabisa hata 10%.

    Page 37 of 40 FirstFirst ... 273536373839 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...