Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

    Report Post
    Page 27 of 40 FirstFirst ... 17252627282937 ... LastLast
    Results 521 to 540 of 785
    1. #1
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,526
      Rep Power : 1755
      Likes Received
      2379
      Likes Given
      166

      Default Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHIS SYKES (1924 -1968)

      Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika na Mohamed Said

      Pitio la Kitabu

      Kitabu hiki kilipochapwa kwa mara ya kwanza 1998 kwa Kiingereza nchini Uingereza na kilipoanza kuzagaa katika maktaba na maduka ya vitabu mjini London yanayouza vitabu kuhusu Afrika Watanzania wengi waliokuwa Uingereza walisisimuliwa na yale yaliyokuwa ndani ya kitabu hiki. Kubwa zaidi ilikuwa kule kufunuliwa kwa mara ya kwanza kuwa kumbe TANU chimbuko lake si Julius Nyerere bali ni marehemu Abdulwahid Sykes. Hii ilikuwa habari mpya kwa wengi hasa ikizingatiwa kuwa Nyerere mwenyewe hakuwahi kumtaja Abdulwahid Sykes kama mwenzake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hili lilikuwa la kwanza. Kitu cha pili kilichosisimua wasomaji ni kuwa mwandishi kwa kutulia kabisa alionyesha bila woga na kutafuna maneno kuwa TANU kilikuwa chama kilichojengwa katika migongo ya Waislam. Hili alilishaijisha kwa kueleza wazalendo waliokuwa bara ambao kwa umoja wao na wengi wao wakiwa Waislam walipambana na ukoloni wa Kiingereza.

      Kubwa zaidi la kusisimua ilikuwa kitabu kilieleza bila kupepesa macho au kutafuna maneno njama alizofanya Nyerere kwanza kumfuta Abdulwahid Sykes katika historia yake binafsi, TANU na katika harakati za kudai uhuru. Lakini kilichotibua sege la nyuki ni pale katika kuhitimisha kitabu mwandishi alipoweka wazi mipango ya Nyerere akishirikiana na Kanisa Katoliki baada ya uhuru kupatikana kupanga njama za kuzuia maendeleo ya Waislam. Katika kipande hiki msomaji atakutana na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mwanasiasa shupavu. Msomaji ataziona juhudi za Sheikh Hassan bin Amir katika kupambana na njama za Nyerere na Kanisa Katoliki na nini kilimfika msomi huyu maarufu wa Kiislam. Kwa wakati ule Nyerere akiwa hai ilihitaji ujasiri mkubwa kwa yeyote yule kusema au kuandika hayo.

      Nakala za kitabu zilifika Tanzania na kila aliyesoma alipatwa na mshtuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nje yake. Kitabu kiliwaudhi wapenzi wa Nyerere na wapo waliomwendea kwa kutaka afanye jambo kukomesha “uongo” wa mwandishi. Wengine hawakuamini kuwa huyo anayejiita Mohamed Said kama kweli yupo. Wengine walitaka kujua kama kweli akina Sykes na baba yao ndio waasisi wa vyama vya Waafrika katika Tanganyika katika 1929 hadi 1954 TANU ilipoasisiwa. Hii ilikuwa bahari kubwa kwa wapenzi wa Nyerere ambao wasingeweza kuogelea bila ya msaada wake Baba wa Taifa. Mawimbi ya bahari hii yalikuwa marefu na yakija kwa kasi. Juu ya haya yote Waswahili wana msemo “penye ukweli uongo hujitenga.” Nyerere asingeweza kuthubutu kukana mchango wa marehemu Abdulwahid kwake yeye binafsi na kwa TANU. Abdulwahid ndiye aliyempokoea Dar es Salaam ile ya miaka ya 1950 na akamjulisha kwa wenyeji wa mji. Wapenzi wa Nyerere hadi leo ukiwauliza Nyerere alisema nini kuhusu ukweli kuwa si yeye aliyeasisi TANU wamekuwa kimya.

      Msomi maarufu wa Chuo Kikuu cha Cambridge John Illife ambae ameandika sana historia ya Tanganyika alikasirishwa na msimamo wa mwandishi khasa pale aliposema kuwa inastaajabisha kuwa Illife ingawa alitegemea nyaraka za akina Sykes katika kuandika historia ya African Association inastaajabisha hakuona umuhimu wa kutaka kumhoji marehemu Abduwahid aliyekuwa katibu na rais wake kati ya 1951 hadi 1953. Akiandika pitio la kitabu hiki katika Cambridge Journal of African History Illife alimshambulia mwandishi katika njia ambayo haikuwa staili yake msomi mkubwa kama yeye. Illife alikuwa ameghadhibishwa kwa kuambiwa katika kitabu kuwa alimzuia mwanafunzi wake katika Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa 1969, Daisy Sykes ambae alikuwa binti ya Abdulwahid asiandike maisha ya baba yake. Daisy wakati huo msichana mdogo alikuwa amekasirishwa na jinsi TANU na magazeti yake yote, “The Nationalist” chini ya uhariri wa Benjamin Mkapa na “Uhuru” yalivyoshindwa kumwandika baba yake kwa hadhi aliyostahili. Magazeti hayo yaliripoti kifo cha Abdulwahid Sykes kwa kuwa Nyerere alikwenda mazikoni. Hapakuwa na jingine. Brendon Grimshaw ambae alikuwa Mhariri Mkuu wa “The Tanganyika Standard” na akimfahamu vyema Abdulwahid ndiye aliyendika tanzia ya maana katika “Sunday News” akasema kuwa Nyerere asingelifika pale alipofika kama si kwa msaada wa Abdulwahid Sykes na ni juhudi za ukoo wa Kleist ndiyo uliowezesha watu wa Tanganuyika kuwa na chama cha siasa. “The Standard” na “Sunday News” wakati ule lilikuwa gazeti huru halikuwa na hofu ya Nyerere. Hii ilikuwa mwaka 1968.

      Kilipotoka kitabu hiki mwaka 1998 walikuwepo watu walioona ukweli wa kuwa historia ya TANU bado haijaandikwa na kuna baadhi ya shutuma zilizoelekezwa kwake Nyerere ni muhimu yeye mwenyewe akazijibu akiwa hai kwa faida ya jamii isijesemwa kuwa kasingiziwa, walimsubiri afe ndipo wamzushie la kumzushia. Mmoja wa kundi hili la pili alikuwa marehemu Prof. Haroub Othman. Yeye alimkabili Nyerere uso kwa macho na kumuomba atoe majibu kujibu shutuma za waandishi wawili. Kwanza ajibu shutuma za Sheikh Ali Muhsin Barwani aliiyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) katika kitabu chake “Conflict and Harmony in Zanzibar” na kitabu cha Mohamed Said “The Life and Times of Abdulwahid Sykes (19241968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.” Sheikh Ali Muhsin akimtuhumu Nyerere kwa kupeleka mamluki Zanzibar kuipindua serikali ya wananchi na Mohamed Said akimtuhumu kwa chuki dhidi ya Waislam na kupotosha historia ya uhuru wa Tangnayika. Prof. Haroub alimshauri Nyerere kuwa njia nzuri ya kuiweka historia yake na uhusiano wake na Waislam sawa ni kwa yeye kuandika historia ya maisha yake. Hadi Nyerere anaingia kaburini hiili halikufanyika.

      Kitabu hiki ni muhimu kwa Waislam na wananchi wote kwa ujumla kukisoma na kuwahimiza watoto wao nao wakisome wapate kujifahamu na kufahamu changamoto za udini na chanzo chake. Ndani ya kitabu hiki mwandishi amejitahidi kukusanya mashujaa waliotupwa waliopigania uhuru wa Tanganyika hata kabla hawajasikia jina la Nyerere wala kuona sura yake, wazalendo kama Hassan Suleiman na Juma Ponda wa Dodoma. Wazalendo waliohutubia mikutano ya hadhara na kuhamasisha watu kudai uhuru hata Nyerere hawamjui kama Titi Mohamed na wengine wengi kutoka katika majimbo ya Tanganyika. Ukikianza kitabu hiki huwezi kukiweka chini hadi umefika mwisho.

      Kitabu hiki kinapatikana Ibn Hazim Bookshop Mtoro na Manyema na Tanzania Publishing House, Samora Avenue.
      Last edited by Mohamed Said; 13th March 2011 at 19:45.

    2. Miaka 50

    3. #521
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3180
      Likes Received
      426
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Mohamed Said
      Kwa faida ya ukumbi.

      Nimeandika kitabu kizima nikitumia "Sykes Papers" kama "primary source" na hizi kwa uhakika ndiyo nyaraka za TAA na TANU kwa siku za mwanzo.

      Kumbukumbu nyingi za wakati ule zilikuwa katika hifadhi Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally. Kumbuka kwa baba yao alikuwa secretary wa African Asssociation.

      Wakati ule si kama leo.

      Kiongozi alikuwa akichukua majukumu mazito ya yeye kuwa kila kitu.

      Yeye ndiye "the intelligentsia" yeye ndiye "party financier."

      Sasa ikiwa hivi hata nyumba yake ni ofisi.

      Marehemu Abdulwahid aliweka nyumba yake rehani kwa Abdulkarim Karimjee ili apate fedha za kuikimu TANU.
      Kwa jinsi ninavyo kusoma nakukulewa ni kuwa Sykes hakuwa politician.

      Vita ya ukombozi ya uhuru watu wana paricipate katika role tofauti. Sasa itakuwa ajabu mtu amabye ni financier unataka apewe sifa za politician au mtu ambaye ni politician aonekane kuwa alikuwa financer katika uhuru.

      Always politician ndo wanajulikana sio kwa tanzania tu ni dunia nzima.Hapa hakuna fitnakama unavyotaka ionekane.

      Kwa maelezo yako sykes was not a politician hata kama alikuwa ni intelijensia na Financier.
      Ni sawa kutaka General Adulrahim shimbo wa JW au mkuu wa UWT othman Rajab wajulikane na watajwe sana kuliko JK .

      Hakuna anyebishakuwa mchango wao na role yao ni kubwa but ni uwongo kusema kuna fitna
      .

      Unasema aliuza nyumba kwa ajili ya chama je unajua viwanja vingapi familiaya sykes ilipewa na kuzawadiwa na inaendelea kupendelewa baaada ya hapo. Mbona sykes kaenziwa ukiliganisha na wengine

      Unajua ni business gani watu wakiona jina sykes basi wanaliheshimu na hivyo kulipa favour.

      Sure Sykes families lost some of thier asset kama wengine wengi tu but he gained na inaendelea kugain too
      .



    4. #522
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Diehard
      Mkuu nafuatilia mtiririko wa mabandiko yako katika uzi huu naomba niseme mengi ya mabandiko yako huku yamenikwaza umekuwa ukijaribu kusema ati watu inawauma au hawataki kuukubali ukweli, mimi kama alivyosema WOS sikuwahi kujua kama kuna mpasuko wa kiasi kwamba watu wana chuki moyoni.

      Bandiko lako hili limenivutia. Wito wangu kwako na wengine yatupasa hapa tuelimishane ili nia na madhumuni ya kitabu hiki ifikiwe nayo ni ukweli kusambazwa na mwishowe Wazee wa Mohamed Said na ni wazee wetu waenziwe ipaswavyo na sio kutoa maneno ya kejeli ambayo hayatajenga na kupelekea wana JF watakaokuwa wana kwazika wasiende kuwahamasisha watu wanunue kitabu na kuwafundisha watu historia ya kweli, nilifahamu historia ya kina Sykes lakine sikuwahi msikia Mshume au Chamwenyewe nazidi kuvutiwa na Mzee Said anavyo jibu hoja na nidapodhani pana upungufu nitahoji kwa nia njema.

      By the way mi ni wa 70s so sina data nyingi kama Mzee aliyeweza hata kuwaona kina Adulawahid Sykes. Singida niliwahi hadithiwa habari hiyo ya Binti Feruzi na kuonyeshwa nyumba yake.
      Ahsante Diehard, kwa ushauri wako wa hikma na maoni niliyoyaridhia kwa roho kunjufu.

    5. #523
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Zing
      Alafu mkuu japo kwa mtazamo wangu kuna mambo umepindisha fanya uwezalo muweke huyo Abdulwahid Sykes kwenye wikipedia. Karne hii ya kizazi cha dot com .

      Maana "sisi" wakristu tumeshamuweka Nyerere kwenye wikipedia.Julius Nyerere - Wikipedia, the free encyclopedia Basi na "nyie" au wewe muweke huyo mzee wako. This is a joke lakini ina ujumbe mzito.

      Kama hutaweza mimi mkristu ukinipa electronic copy ya biography ya huyo Abdulwahid Sykes nitaiweka.
      Naamin hiyo haitadhuru supply ya kitabu chako . Na kwa kuwa lengo hasa ni waislam wajue historia ya wazee unayosema wewe ni ya ukweli basi one of the effective method ndio hiyo.
      Naomba tuelimishe ni yepi hayo (kwenye nyekundu)?

    6. #524
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,526
      Rep Power : 1755
      Likes Received
      2379
      Likes Given
      166

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Nanren
      Ndugu Diehard,
      Si wewe peke yako, ni wengi ndio tunagundua hapa JF kwamba
      kumbe watu ambao wewe umekuwa ukiishi nao bila kinyongo, wao kwenye mioyo yao wanakuona adui. Wao wanahisi wanaonewa na wakristo. Hapo juu mmoja amesema kabisa kanisa katoliki lina chuki dhidi ya uislam. Kwa dini inayohubiri upendo, nashindwa kuamini (japo mimi si mkatoliki) kuwa kanisa katoliki linaweza kuwa na chembe ya chuki kwa waislam, tena waislam wa Tanzania tu. Maana hatusikii tuhuma kama hizi nchi zingine, hata hapo kwa majirani zetu Kenya au Msumbiji.

      Inanikumbusha Afande mmoja JKT,Alikuwa ananipa adhabu au kazi nzito kila mara. Mimi nikawa naona poa tu, labda kwavile alikuwa aniona nina misuli. Lakini wakati namaliza ule mwaka mmoja ndiyo akaja kuweka wazi kuwa siku za nyuma alikuwa ananitesa kwa vile alikuwa ananishuku kutembea na "mtu" wake... Jambo ambalo halikuwahi hata kuwepo kichwani kwangu. Sasa sijui kama kanisa katoliki linajua kwamba waislam wamelistukia kuwa linawachukia.

      Kama kweli kuna kanisa lina chuki dhidi ya waislam au watu wengine wasio wakristo, basi hilo sio kanisa. Labda serikali ijifanye kanisa.
      Kanisa liulizwe nini limefanya kupitia mawakala wake Wizara ya Elimu kuwazuia vijana wa Kiislam kupata elimu.

      Kwa nini walikataa OIC isijenge Chuko Kikuu kwa Waislam Tanzania.

      Kwa nini wanapinga Tanzania kujiunga na OIC.

      Imekuwaje Kanisa linahodhi 85% ya viti katika Bunge la Tanzania.

      Kwa nini walipiga vita Darul Iman walipotaka kujenga shule ya Kiislam Kibaha.

      Kwa nini wanafanya juhudi ya kufifilisha historia iliyotukuka ya Waislam.

      Kwa nini hawaiti mkutano wa pamoja na Wasilam tukasafahiana nia.

      Kwa nini wanafanya mikutano pembeni na Waislam wanafiki ilhal viongozi
      wa kweli wa umma wapo.

      Kwa nini wanapinga Mahakama ya Kadhi.

      Nini lilikuwa kosa la marehemu Prof. Malima hata wakamwandama kiasi kile.

      Ni kule kumtaarifu Rais Mwinyi kuwa Wizara ya Elimu inadhulumu vijana wa Kiislam.

      Kwa nini wanataka wahodhi kila fursa nchini.

      Nk. nk. nk.

    7. #525
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,526
      Rep Power : 1755
      Likes Received
      2379
      Likes Given
      166

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo
      Naomba tuelimishe ni yepi hayo (kwenye nyekundu)?
      Vuta subra.

      Kuna project ya Oxford na Harvard Dictionary of African Biographies (DAB).

      Hakika wewe Mshindo Kishindo khasa.

      Kijana wa Swahili kwa Msindika Store!

      Uliliwahi duka hilo au wewe ulikuwa Swahili juu kwa marehemu Ramadhani Shabani?

      Mohamed Said ana tenda anayoichangamkia.

    8. FemaTV & Radio

    9. #526
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3180
      Likes Received
      426
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo
      Naomba tuelimishe ni yepi hayo (kwenye nyekundu)?
      jaribu kupitia japo kama page tatu au nne za mwiso utayaona. Sijakisoma hicho kitabu lakini kwa maelezo ya mwandishi kuna hoja zake

      • Anajaribu kueleza uwongo au ukweli nusu ili kulipa faraja kundi fulani la watu.

      Amejaribu kusema yeye kama muislam kakutana na vikwazo vingi. Anaamini yeye na waislam wote wanakutana na vikwazo hivi vinavyowekwa na kanisa/ nyeree juu yao. mhhhhh

      • Je watu wa dini nyingine na wasio na dini hawakutani na vikwazo katika maisha yao?
      • Kwa nini challenge anazopta mtu azihusanishe na dini na sio kabila au utamduni au falsfa ya kisiasa?
      • Je waislam kundi chache la mkoa wa kagera wanafanikiwaje kuishi na hao wakristu wengi . Mbona wapo wasomi wengi tu. Kama kweli wakristu ni kikwazo hili linaawezekanaje?

    10. #527
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,526
      Rep Power : 1755
      Likes Received
      2379
      Likes Given
      166

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo
      Ahsante Diehard, kwa ushauri wako wa hikma na maoni niliyoyaridhia kwa roho kunjufu.
      Kwa miaka mingi hili tatizo tumelizungumza.

      Serikali hadi leo inajifanya hali ni shwari hakuna matatizo
      nchini kwetu.

      Hadi leo hivi ninavyoandika Waislam tunahamasishana kupiga vita
      "Mfumo Kristo."

      Makongamano yanaendelea nchi nzima.
      Serikali inajifanya hakuna kitu.

      Magazeti wala TV zote chini ya Mfumo Kristo wanatupuuza.

      Waislam tumechoka zaidi ya kuchoka kwenyewe.

      Sasa Wakristo wenye nia njema wafungue vinywa na waseme
      ingekuwaje kama sisi ndiyo tungekuwa katika nafasi ya Waislam
      tungekubali kudhulumiwa?

    11. #528
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,526
      Rep Power : 1755
      Likes Received
      2379
      Likes Given
      166

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Zing
      Kwa jinsi ninavyo kusoma nakukulewa ni kuwa Sykes hakuwa politician.

      Vita ya ukombozi ya uhuru watu wana paricipate katika role tofauti. Sasa itakuwa ajabu mtu amabye ni financier unataka apewe sifa za politician au mtu ambaye ni politician aonekane kuwa alikuwa financer katika uhuru.

      Always politician ndo wanajulikana sio kwa tanzania tu ni dunia nzima.Hapa hakuna fitnakama unavyotaka ionekane.

      Kwa maelezo yako sykes was not a politician hata kama alikuwa ni intelijensia na Financier.
      Ni sawa kutaka General Adulrahim shimbo wa JW au mkuu wa UWT othman Rajab wajulikane na watajwe sana kuliko JK .

      Hakuna anyebishakuwa mchango wao na role yao ni kubwa but ni uwongo kusema kuna fitna
      .

      Unasema aliuza nyumba kwa ajili ya chama je unajua viwanja vingapi familiaya sykes ilipewa na kuzawadiwa na inaendelea kupendelewa baaada ya hapo. Mbona sykes kaenziwa ukiliganisha na wengine

      Unajua ni business gani watu wakiona jina sykes basi wanaliheshimu na hivyo kulipa favour.

      Sure Sykes families lost some of thier asset kama wengine wengi tu but he gained na inaendelea kugain too
      .


      Kwengine sikukujibu kwa kuwa naona hakuna haja ila hili la Abdulwahid Sykes
      hakuwa mwanasiasa nitakupa fikra za watu ambao wameuliza sana kuwa kwa
      nini Abdu akipenda sana kuwapeleka watu wengine mbele na kwa nini alikuwa
      karim sana kwa TAA na TANU kiasi kuwa alipoona harakati zimepamba moto
      na mambo yametengemaa akakaa pembeni.

      Hilo hata mimi nakiri sijaweza kupata jibu.

      Ni swali kila aliyesoma kitabu na akaonana na mimi huniuliza.

      Baba yangu amepata kunambia kuwa, "Abdu angelitaka kutawala nchi hii angeliweza."

      Ila rafiki yake Abdu, Ahmed Rashad Ali anasema, "Katika umri mdogo sana Abdu alifanya
      makubwa ambayo hakuna katika kundi letu aliweza kuyafikia. Hii ndiyo sababu Abdu alikifu
      siasa mapema sana. Mimi ni Abdu ndiye aliyenijulisha kwa Jomo Kenyatta mwaka wa 1950
      pale Nairobi. Ndiyo kwa mara ya kwanza nakutana na akina Kungu Karumba, Achieng Oneko,
      Bildad Kaggia na wanasiasa wengine wa KAU."

    12. #529
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3180
      Likes Received
      426
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Mohamed Said
      Mfano wako hauingii hapa.

      Huwezi kufananisha historia ya Waislam na hiyo ya Kagera.
      Nani alikuambia historia haifananishwwi Unless hujui maana ya histry na elimu. Huwezi kuelewa na kujifunza kitu kwa kukisoma in Isolation. Kujiliza maswali mangumu kulinganisha na kuchambua ndio jibu sahii ya kufanya analysisi isioykuwa biased. Hata huko kagrea wapo wazee wako wa kiislam. Mtafute balozi Khamis kagasheki


      Hivyo ni vitu viwili tofauti zaidi ya tofauti yenyewe.
      Ni tofauti ndio maana tunataka watu wajue picha unayotoa hapa sio ya waislam wa tanzania wala sio ukweli wa tanzania nzima labda kama unaongelea dar e salaaam na pwani otheriwise useme wazi una agenda zaidi ya historia ya wzee wa kiislam

      Historia ya wazee wangu na Nyerere sasa ni "classic" ikisomeshwa mwanafunzi hasinzii.
      Kwa heshima ya hao wazee tundelee kuwaita wazee wetu na sio wako. Au ndio unachukua haki miliki ya wazee wote wa kiislam tena wa dar tu ? Na hawa wazee wetu wapo wengi. Sasa hii ya mwanafunzi kusinzia maana yake ni nini??? Kuna wanafuzi hawasinzii kwenye hesabu na physics na bado hawafanyi vizuri na unaweza kusinzia kwenye history na bado mtihani ukafanya vizuri tu........

      Fanya juhudi uulize wanaoisomesha wakwambie. Kijana mmoja kafundisha historia rasmi akamaliza katika moja ya vyuo
      vikuu vyetu. Kisha akawaambia wanafunzi wake kuwa kwa kumaliza somo lile angependa
      kuwasomesha kitabu cha Abdulwahid Sykes... Kanipigia simu anasema darasa utadhani limemwagiwa maji.
      Wanamdai kitabu...
      Nomba utofautishe marekkting ya kitabu na hoja za kitabu. Naona unachanganya mambo mawili. Ndio hivi hivi vitabu tulifundiswa nakusoma na kukariri kuwa Ukoloni na utumwa ndio chanzo maedeleo yetu duni. Leo hii mimi sio mwanafunzi naelewa zaidi ya yale niliyofundishwa.

      Sasa kwa wanafuzi hicho kitabu kinaweza kuwa SUMU. Hasakama hawana mwalimu mzuri wa kuwaleza kilichoandikwa humo sio ukweli wote na labda sio uwongo. wakitoka kwenye uanafunzi wao baadae watajua ukweli kama hivi leo navyojua zaidi ya utumwa na ukoloni basi utawala bora ni chanzo cha sisi kutoendelea


      Kumbuka pia neno mwanafunzi lina maana yake.

      Huyu ndiye yule kijana aliyeonywa na profesa wake asikinukuu kitabu changu.

      Hii ndio ile nasema tofautisha marketting ya kitabu na Hoja za kitabu. Umesema Oxford wamesema kinfaa kwa kufundisha tanzania . kwa style hiyo haao oxford hawakawii kukumwbia kinfaa kufundisha hata wanafunzi wa sayari Mars. Oxoford na cariccurlum ya tanzania wapi na wapi. Oxford hao hawana say hata juu y kitabu gani kinafaa na kipi hakifai kufundisha UK ije kuwa tanzania

    13. #530
      shadhuly's Avatar
      Member Array
      Join Date : 8th January 2011
      Posts : 95
      Rep Power : 443
      Likes Received
      10
      Likes Given
      6

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      kwa kweli khabari kubwa mjadala umenoga.nimependezwa na busara na hekima za watu wanavyozionesha.kitabu bado nakisoma insh nikimaliza nitarudi ukumbini kutoa kile nilichokiona na kukifahamu.muhimu kukisoma kitabu ili uwe ktk safe side.

    14. #531
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3180
      Likes Received
      426
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Mohamed Said
      Kwengine sikukujibu kwa kuwa naona hakuna haja ila hili la Abdulwahid Sykes
      hakuwa mwanasiasa nitakupa fikra za watu ambao wameuliza sana kuwa kwa
      nini Abdu akipenda sana kuwapeleka watu wengine mbele na kwa nini alikuwa
      karim sana kwa TAA na TANU kiasi kuwa alipoona harakati zimepamba moto
      na mambo yametengemaa akakaa pembeni.

      Hilo hata mimi nakiri sijaweza kupata jibu.
      Jibu ndo hilo diffence betwen Skykes na Nyerere ni kuwa

      • Sykes was not a poltician na Nyerere was
      • Nyerere was chosen to be a Leader

      Ni policts na politican ndo wanakuwa front page kwenye news na maandiko wakati behind the scene wanaowezesha mambo ndio hao kina sykes. na hiyo siyo fitna ukweli ndo huo.Kusema kwamba kuna fitna alifanya nyerere na kanisa ndo hapo nakataa

      Roho ya serikali ya UK ni wizara ya fedha lakini Sio chanceleor wala secretary a wa exchequer anajulikana duniani kuliko David Cameron ambaye ni PM . Kwa nini simply bcs David cameroon amechaguliwa kuwa Leader

      Btn
      Nakushauri weka maelezo machache ya huyo mzee wetu sykes wikipedia

    15. #532
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3180
      Likes Received
      426
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Mohamed Said
      Kwa miaka mingi hili tatizo tumelizungumza.

      Serikali hadi leo inajifanya hali ni shwari hakuna matatizo
      nchini kwetu.

      Hadi leo hivi ninavyoandika Waislam tunahamasishana kupiga vita
      "Mfumo Kristo." ...............
      Mfumo kristo ni mfumo gani huo ebu tufafanulie au toa mfano mmoj au miwili MS.
      kwama ni kweli upo basi inabidi turdi kwenye mfumo pagani maana sio sahii kuwa na mfumo kristu wala mfumo islam teh teh teh

    16. #533
      Mpevu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2010
      Location : Anonymous
      Posts : 1,586
      Rep Power : 747
      Likes Received
      76
      Likes Given
      103

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Zing
      Mfumo kristo ni mfumo gani huo ebu tufafanulie au toa mfano mmoj au miwili MS.
      kwama ni kweli upo basi inabidi turdi kwenye mfumo pagani maana sio sahii kuwa na mfumo kristu wala mfumo islam teh teh teh
      Hapo kwenye red naona kama 'panakereketa' vileee.
      I'LL BE WEARING A SMILE ON MY FACE.... but firm on issues,, JK's 1st address to the national assembly in Dodoma-2006.

    17. #534
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3180
      Likes Received
      426
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Mpevu
      Hapo kwenye red naona kama 'panakereketa' vileee.

      yah japo ni nje ya mada labda itatusaidia kuelewa kama mfumo kristu ni

      • Jumalipili na jumamosi kuwa siku za mapunziko . So dawa iwe itauwa kazi seven days a week.
      • Uchaguzi wa wanafunzi kufaulu mashuleni na vyuoni .Utaratibu wa utumia kigezo cha maksi "unawadhulumu" dini fulani so dawa sijui itakuwa kuangalia majina dini ili uchaguzi ufanyike sawa kwa dini "yao" "yetu" "ile" na wale wasio na dini
      • Ajira na interview sharti la usawa wa kidini lizingatiwe zaidi kuliko taaluma na uwezo.
      • Teuzi za vyeo. hivyo hivyo kama hapo juu.

      baaadaye tutahamasiahana kwenye move ya ukabila juu ya mfumo "uchaga" ""unyakyusa" na "uhaya"

      teh teh teh . Hii ndo itakuza Tanzania ya karne ya 21 very fast Development but going backwards

    18. #535
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,668
      Rep Power : 21814
      Likes Received
      735
      Likes Given
      3189

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Majimshindo
      Umekisoma kitabu tajwa? Au upo katika jamii ya wakurupukaji na kutafuta "loopholes" ili upate tu cha kubishia?
      Kumbe unajua kuwa kuna "loopholes".............sa sa hizi loopholes zinarekebishwa vipi?

      Quote By Majimshindo
      Tatizo kubwa ni kuwa hujakisoma kitabu tajwa, hizo unazo "quote" ni "excerpts" tu. Ungesoma kitabu ungepata majibu ya mengi ya maswali yako, pengine ungekuja hapa na maswali mengine kabisa, hapo ndio pangekuwa patamu. Unakuja na maswali kupiti "excerpts", huoni kuwa humtendei haki muandishi?
      Ndugu yangu............Kitabu nilikinunua mwenyewe na nimekisoma...............ndio kinachowekwa hapa ni "excerpts"........kwani hizo excerpts zimetokea wapi?.......kumtendea haki muandishi ni pamoja na kuhoji loopholes ili arekebishe na ili ukweli ujulikane.............hiyo ndio azma.....au nakosea

    19. #536
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,668
      Rep Power : 21814
      Likes Received
      735
      Likes Given
      3189

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Mohamed Said
      Nyerere alikuwa akiamini hakuna mwingine awezae kufikiri ila yeye tu.

      Lakini woga wake mkubwa ilikuwa Waislam.


      Waliokuwa karibu nae wanasema hakuna kitu alichokuwa hataki kukisikia kama
      Uislam.
      ....................
      Hizi tunaziita Chuki Binafsi................wako wengine hapa wamefanya kazi na Mwl.........na hilo ulisemalo si kweli.......kwani alishauriwa na alikuwa msikivu na akashaurika...............
      ............inawezekana ilimtokea mtu specific........lakin si kwa ajili ya dini ya Uislam........

      Mwl Nyerere hakuogopa Uislam.......alishirikiana nao vizuri tu............ushahid upo mwingi sana

    20. #537
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,668
      Rep Power : 21814
      Likes Received
      735
      Likes Given
      3189

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Mohamed Said
      .
      1.Imekuwaje Kanisa linahodhi 85% ya viti katika Bunge la Tanzania.

      2.Kwa nini wanafanya mikutano pembeni na Waislam wanafiki ilhal viongozi
      wa kweli wa umma wapo.

      ..
      Ngoja nianze na tafakuri ya hayo maswali mawili hapo juu
      1. Hivi kweli mtafiti/mwanazuoni na mwandishi makini anaweza kuuliza swali vague namna hiyo

      2. Unaweza kutuambia ni Wa-Islam wepi hao wana/likutana na Wakatoliki na wapi..............na ili tuujue unafiki wao. Mikutano iko mingi sana imefanyika

    21. #538
      JF-BAN1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 10,447
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3753
      Likes Given
      2889

      Default

      Quote By Mohamed Said
      Vuta subra.

      Kuna project ya Oxford na Harvard Dictionary of African Biographies (DAB).

      Hakika wewe Mshindo Kishindo khasa.

      Kijana wa Swahili kwa Msindika Store!

      Uliliwahi duka hilo au wewe ulikuwa Swahili juu kwa marehemu Ramadhani Shabani?

      Mohamed Said ana tenda anayoichangamkia.
      Mimi nilikuwa karibu na kwa kina Marehem Ramadhan Shaaban nyumbani kwetu ni kona ya Udoe na Swahili.

    22. #539
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,668
      Rep Power : 21814
      Likes Received
      735
      Likes Given
      3189

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Zing
      yah japo ni nje ya mada labda itatusaidia kuelewa kama mfumo kristu ni

      • Jumalipili na jumamosi kuwa siku za mapunziko . So dawa iwe itauwa kazi seven days a week.
      • Uchaguzi wa wanafunzi kufaulu mashuleni na vyuoni .Utaratibu wa utumia kigezo cha maksi "unawadhulumu" dini fulani so dawa sijui itakuwa kuangalia majina dini ili uchaguzi ufanyike sawa kwa dini "yao" "yetu" "ile" na wale wasio na dini
      • Ajira na interview sharti la usawa wa kidini lizingatiwe zaidi kuliko taaluma na uwezo.
      • Teuzi za vyeo. hivyo hivyo kama hapo juu.
      baaadaye tutahamasiahana kwenye move ya ukabila juu ya mfumo "uchaga" ""unyakyusa" na "uhaya"

      teh teh teh . Hii ndo itakuza Tanzania ya karne ya 21 very fast Development but going backwards
      Kuna mtu hapa alizungumzia kuhusu utafiti uliofanywa kutafuta Dawa ya Malaria...........na wataalamu walivyochangia kuhusu utafiti ule.......

      Tukaambiwa kuwa Prof Shaba aliuliza swali............hiyo dawa itauzwa bei gani?............hili swali lina maana kubwa/pana sana

    23. #540
      Zing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Posts : 1,780
      Rep Power : 3180
      Likes Received
      426
      Likes Given
      552

      Default Re: Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

      Quote By Mohamed Said
      Kanisa liulizwe nini limefanya kupitia mawakala wake Wizara ya Elimu kuwazuia vijana wa Kiislam kupata elimu.

      Kwa nini walikataa OIC isijenge Chuko Kikuu kwa Waislam Tanzania.

      Kwa nini wanapinga Tanzania kujiunga na OIC.

      Imekuwaje Kanisa linahodhi 85% ya viti katika Bunge la Tanzania.

      .......................
      Nk. nk. nk.

      Kwenye kitabu chako hujaeleza haya ila nyuma ya pazia na dhima na dhumuni la kitabu chako imejikita zaidi hoja si tu za za kidini bali za kujenga chuki. Hapa ndo nakuelewa vizuri.



      ....Imekuwaje Kanisa linahodhi 85% ya viti katika Bunge la Tanzania.
      Mkuu Inabidi uone aibu japo kidogo katika hoja zako.mbona nyingine hazionyeshi reasoning. sasa ubunge asilimia kubwa si wanachaguliwa na sio kuteuliwa. kama ni kweli kanisa lina hodhi 85% basi tu conclude kuwa

      • 85% ya watanzania na wapiga kura ni wa "kanisa. " na wanaanya fitna hawachagui wengine
      • Au 85% ya wanaopigia kura waislam na wakristu wanaridhishwa na watu wa bunge wa "kanisa" kuliko wengine teh tehteh

    Page 27 of 40 FirstFirst ... 17252627282937 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...