JamiiSMS
    Show/Hide This

    Topic: Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

    Report Post
    Page 1 of 11 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 215
    1. Mugishagwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th April 2006
      Posts : 347
      Rep Power : 812
      Likes Received
      25
      Likes Given
      0

      Default Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

      Mengi, This Day wamjibu Mahalu

      • Wasisitiza si mwaminifu, pia alidanganya
      • Waeleza alivyoweka fedha akaunti tofauti
      • Wasema kavuliwa ubalozi, ilibainika Dar

      na Mwandishi Wetu

      MWENYEKITI Mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi, waandishi na wahariri wa Gazeti la This Day na Kulikoni, wamemjibu aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Mahalu, na kusisitiza madai dhidi yake yaliyoandikwa na magazeti hayo.

      Madai hayo ni kumhusisha Mahalu na ununuzi wa nyumba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, iliyopo 185 Via Cortina d’ Ampezzo, jijini Roma, ambapo wanaeleza kwamba, bei iliyokubaliwa awali ni tofauti na fedha zilizotolewa.

      Katika majibu yao ya maandishi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu na Wakili Deogratias Ringia mwishoni mwa wiki iliyopita, walisema kwamba makubaliano ya ununuzi wa jengo hilo yalikuwa Euro 1,032,913.80, lakini fedha zinazodaiwa kulipwa ni Euro 3,098,741.40.

      Wanaeleza kwamba, Euro 1,032,913.80 ziliwekwa katika akaunti ya Ceres SRL, kwa mujibu wa makubaliano yalivyokuwa Oktoba, 2002, wakati fedha nyingine, Euro 2,065,827.60, zilipelekwa kwenye akaunti nyingine, ya Monaco Soc Ceres SRL, asasi ambayo haikuwa mshirika katika makubaliano ya mauzo ya Oktoba mosi, 2002. Ringia alisema walalamikiwa wataegemea nyaraka hizo.

      Walalamikiwa waliosaini majibu yao, licha ya Mengi ni Furaha Thonya, Mbaraka Islam, Simon Ileta, Kiondo Mshana na Agapitus Nguma. Wameeleza kwamba, malipo ya ziada ya Euro 2,065,827.60 hayakuambatanishwa na maandishi ya makubaliano ya mauzo, kati ya Ceres SRL wala Monaco Societata a Responsabilita (Monaco Soc Ceres SRL), katika akaunti ambako fedha hizo inaelezwa zilipelekwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

      Wanaeleza kwamba, zaidi ya hapo, maagizo yanayodaiwa yalitolewa na Ceres SRL, kwamba fedha zilipwe kwenye akaunti hiyo nyingine, hayakuonyeshwa kwenye hati ya madai ya Mahalu iliyowasilishwa Mahakama Kuu.

      “Katika barua zake tofauti kwa Serikali ya Tanzania…Avvocato Pasqual Giorgio, alionya juu hatari ya kuwa na mkataba wa mauziano, unaoonyesha bei ndogo, wakati stakabadhi zinaonyesha kiasi kikubwa zaidi cha fedha, na ilishuhudiwa hivyo kwa barua yake kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje iliyoandikwa Milan Mei 5, 2004,” wanaeleza walalamikiwa hao.

      Kadhalika, wameeleza kwamba, kutokana na udanganyifu huo, ofisi ya Balozi wa Tanzania iliyopo Roma, pamoja na makazi yake, yaliingiliwa kwa nguvu na kukaguliwa na watekeleza sheria wa Italia. Kwamba suala hilo lilichunguzwa na taasisi zenye dhamana hiyo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB).

      “Japokuwa ripoti za uchunguzi huo hazijawekwa hadharani, mlalamikaji (Mahalu) alivuliwa hadhi ya kidiplomasia… na kutakiwa kurudi nyumbani Tanzania, na alipowasili, mlalamikaji hakupitia VIP… ambako kwa kawaida hutumiwa na watu mashuhuri, mabalozi wakiwamo. Nakala za picha za kuwasili kwa mlalamikaji zinaambatanishwa,” wanaendelea kueleza walalamikiwa hao.

      Mengi na wenzake wanazidi kueleza kwamba, baada ya kuwasili kwake nchini, alitoa taarifa kwa wapelelezi, na pia kwa vyombo vya habari, alinukuliwa na hajapata kukanusha, kwamba kulikuwapo na makubaliano ya Euro 1,032,913.80 tu. Mahalu amewafungulia kesi walalamikiwa hao, kutokana na habari walizoandika na kuchapisha, zikimhusisha na kashfa ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
      Hizi ni zama za ukweli na uwazi lakini 2 + 2 = 24"Benjamin William Mkapa"


    2. Mlalahoi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st August 2006
      Location : London, UK
      Posts : 1,976
      Rep Power : 1529
      Likes Received
      261
      Likes Given
      159

      Default

      Wahenga walisema kabla hujatumbukia mtoni shurti ujue kina chake.

    3. Chifu Ihunyo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd July 2006
      Posts : 89
      Rep Power : 751
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default

      kwa kuwa mambo yameenda mahakamani na natumaini sasa kwamba Mahalu ndiyo kaamua kujimaliza na Mengi na walio andika nadhani wanajua wanafanya na amejimaliza bila ya kujua wacha tuone mchezo utakuwaje .

    4. Mafuchila's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2006
      Posts : 920
      Rep Power : 927
      Likes Received
      35
      Likes Given
      8

      Default

      Tatizo la uamuzi wa Mahalu ni kifo cha mwenye nyumba kwa kugongwa na nyoka:Kitakachofuata hapo ni msiba na matokeo kuku atachinjwa, siku ya mazishi mbuzi atachinjwa, kumaliza tatu na kuondoa matanga ndama atakwenda na maji na arobaini ikifika basi ng'ombe atakiona cha moto kisa nini eti nyoka alimgonga baba mwenye nyumba; wengi tu wataunga huo msafara, wenye masikio na wasikie.

    5. Halisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th January 2007
      Posts : 3,010
      Rep Power : 2247
      Likes Received
      494
      Likes Given
      271

      Default Balozi wa zamani wa Tanzania Italy, Prof Mahalu kizimbani kwa tuhuma za rushwa

      Balozi wa zamani wa Tanzania Italy, Prof Dr. Costa Ricky Mahalu, amefikishwa mahakamani kwa wizi, rushwa na uhujumu uchumi.

      Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB-TAKURU) ndio waliendesha mashitaka sita dhidi yake na wenzake wawili, Steward Migwano (Mhasibu) na Grace Martin (Ofisa Tawala).

      Amepata dhamana
      Last edited by Game Theory; 23rd January 2007 at 01:26.

    6. Kitila Mkumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2006
      Posts : 4,033
      Rep Power : 39468
      Likes Received
      1599
      Likes Given
      63

      Default

      Good start. Ile isije ikawa ya kutoana kafala kama alivyofanywa Ndugu Kiula yakaishia hapohapo. I hope wataendelea kote hadi IPTL, Radar, n.k.
      A Struggle Without Casualties is No Struggle-Steve Biko

    7. #7
      Wacha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2006
      Posts : 845
      Rep Power : 882
      Likes Received
      117
      Likes Given
      179

      Default

      Tunasubiri na yule aliyekwenda kufungua ubalozi malawi ambaye alikula pesa wakamuhamishia Zambia na yeye ni lazima ashitakiwe.

    8. Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 9,470
      Rep Power : 3003
      Likes Received
      1479
      Likes Given
      97

      Default

      Halisi sidhani kama kazusha ila nadhani link ni hadi kesho maana naangalia alasiri hakuna kitu . Halisi tupe hali halisi tafadhali

    9. S. S. Phares's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,021
      Rep Power : 1317
      Likes Received
      39
      Likes Given
      181

      Default

      Sasa inakuwaje Dar Leo au Alasiri hawajaandika na yeye alipelekwa mahakamani asubuhi...au ndio yale yale tena papers zetu zinaangalia waandike nini ili wauze papers tu..anyway kesho sio mbali.

    10. Kichuguu's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 7,548
      Rep Power : 9270151
      Likes Received
      2129
      Likes Given
      1393

      Default

      I worked with this guy at UDSM when he was Dean of the Faculty of Law. I never knew that he can be so corrupt. It is very hard to tell who are the corrupt elements in the society just by their faces, that is why it is necessary to overhaul our constitution and introduce strong mechanisms of check and balance, which currently are non-existent.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    11. Wacha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2006
      Posts : 845
      Rep Power : 882
      Likes Received
      117
      Likes Given
      179

      Default

      Muonja asali ..........................

    12. Tabasamu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 275
      Rep Power : 768
      Likes Received
      5
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By kichuguu View Post
      I worked with this guy at UDSM when he was Dean of the Faculty of Law. I never knew that he can be so corrupt. It is very hard to tell who are the corrupt elements in the society just by their faces, that is why it is necessary to overhaul our constitution and introduce strong mechanisms of check and balance, which currently are non-existent.
      Kichuguu,
      Mind you he is a friend and worked with the Father of all Corruption Mkapa Ben.
      Francis Jr likes this.

    13. Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 30,750
      Rep Power : 21949230
      Likes Received
      20325
      Likes Given
      10300

      Default

      Je aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje anaweza kuitwa kutoa ushahidi mahakamani (for the prosecution or defence)? Hii kesi naweza kuona itakavyoisha.. itakuwa ni null prosequi na DPP!
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    14. S. S. Phares's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,021
      Rep Power : 1317
      Likes Received
      39
      Likes Given
      181

      Default

      Kwa system ya mahakama ya Tanzania na kwa rekodi waliyonayo hasa kwenye kesi za vigogo...Iwapo huyu bwana atakutwa na hatia ya kuiba hizo euro mil 3 basi nitamuona zumbukuku.

    15. Mwawado's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 2nd November 2006
      Location : Tulsa, Oklahoma/MFA-TZ
      Posts : 1,271
      Rep Power : 974
      Likes Received
      136
      Likes Given
      271

      Default

      Haya mambo makubwa,Prof.Mahalu kwa kauli yake mwenyewe aliomba kesi hiyo ipelekwe Mahakamani.Kwa kuzingatia uhuru wa Mahakama,kila kitu kitakuwa wazi,kwa imani yangu kila aliyehusika kwa namna yoyote ataitwa kutoa ushahidi!sina uhakika kama Mtukufu Rais akiwa madarakani anaweza kutoa Ushahidi Mahakamani (wenye kujua sheria tunaomba mtufahamishe),kuna uhakika wa wazi kuwa Rais akiwa Foreign ministers alipitisha baadhi ya manunuzi ya nyumba za Balozi zetu!,

      Naona hii ni drama nyingine ktk utawala wa JK,lakini yetu macho,inaweza kuwa ndio namna ya ufanyaji kazi kwa kasi mpya na nguvu mpya kwani kila kukicha kunakuja jipya.Tulianza na Richmond lakini mungu bariki,mvua zimeficha ukweli wa $172millioni,tukaja na sakata la nyumba za serikali,lakini nalo liliisha nguvu pale Ditopile alipompiga Mbonde risasi!.Juzi juzi tu kulikuwa na sakata kubwa na serikali ya Bwana Blair kuhusu ununuzi wa Rada kutoka BAE,naona nalo linapindwa na kesi hii ya Mahalu.Hivi ndivyo tulivyo,sasa tungoje jingine ambalo litatuondoa kwenye kesi hii.Huwezi kusikia jambo zuri na la manufaa kwa wananchi wa kawaida kila kuchapo ni drama kila pande ya nchi.

      Nipo Quebec na baridi imekolea mno,lakini niliposikia hili la Mahalu nimetafuta computer iko wapi nami niseme kidogo,Wana Forum fuatilieni kwa ukaribu sakata hili kuna mengi mtayapata kutoka kwa Prof.Mahalu ambaye alikuwa karibu mno na Rais wa awamu ya Tatu,na ni wazi kabisa kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu kiongozi (Mr Luhanjo) ataitwa Mahakamani kutoa ushahidi na Balozi Ibrahim Nkya pia ataitwa kutoa ushahidi kwani ndiye alikuwa mnunuzi wa nyumba kwenye Balozi mbalimbali.Wenye habari za kina tunaomba mzimwage hapa.

    16. Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 30,750
      Rep Power : 21949230
      Likes Received
      20325
      Likes Given
      10300

      Default

      Hivi kwanini unaenda kupeleka kesi mahakamani kama upepelezi haujakamilika?
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    17. Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2006
      Posts : 1,752
      Rep Power : 1100
      Likes Received
      82
      Likes Given
      7

      Default

      Ni haki ya sheria kuchukua mkondo lakini bado nachelea kusema si hao watatu tu kwenye hili, wapo wengi na ndiyo maana swala la toka 2002 limejitokeza 2006 .Vile vile inawezekana maslahi binafsi ya likiukwa sasa imefikia muda wa kuwadabisha wakiukaji yaani Mahalu et al.

    18. Nyangumi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th January 2007
      Posts : 597
      Rep Power : 826
      Likes Received
      14
      Likes Given
      6

      Default

      Ndugu yangu Kichuguu.
      Kuna bwana mmoja amezungumzia kuwa CCM ni gari bovu limekwisha haribika.One spare part won't make any diffence, we need to overhaul the whole car.Mtandao wa CCM haurekebishiki zaidi ya kumuambukiza mtu mpya anayeingia.Dawa pekee ni kuutupilia mbali wote.Usisahau pia kuwa ukitaka kunywa chai nzuri ya sturungi usitumie kikombe kilichokuwa na chai ya maziwa bila ya kukiosha.

    19. Phillemon Mikael's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 5,692
      Rep Power : 1862
      Likes Received
      1598
      Likes Given
      31

      Default

      tunataka hizo euro milioni 2 walizo top zirudi,,sio maneno matupu....kesi sawa vema but isije ikawa wameamua kumtoa kafara ili kurejesha imani ya wananchi kwa serikali ambayo hivi karibuni imeshuka mno...

      nimetoka kuangalia sasa hivi maj gen antori kamazima alikuwa anaagwa leo ,kwenye speech yake hosea akasema "general ametufikisha hapo alipotufikisha leo...",kamazima kwenye hotuba kasema"...nilipokuwa jeshini,nidhamu ndio jambo la muhimu,psb maneno ninayowaachia ni UADILIFU,UWAZI,UAMINIFU..."

      Sasa notation ninayoipata hapa ni kuwa utendaji kazi wa hawa watu ni tofauti na huenda hosea alikuwa hamkubali ANATORI kiutendaji,,,na inaelekea hosea atakuja na aproach ya kuonekana zaidi...na atapewa nguvu kama sheria mpya ya rushwa itapita.

    20. Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2006
      Posts : 1,752
      Rep Power : 1100
      Likes Received
      82
      Likes Given
      7

      Default

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      Je aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje anaweza kuitwa kutoa ushahidi mahakamani (for the prosecution or defence)? Hii kesi naweza kuona itakavyoisha.. itakuwa ni null prosequi na DPP!
      Mzee MKJ,

      Nafikiri Hakuna sheria Tata juu ya hilo,Inawezekana kabisa kama anaushahidi hata kama si kuitwa Physically lakini anaweza akautoa ushahidi wake kimaandishi na kuwakilisha,Lakini hili litategemea na mwendesha mashitaka kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo, Ila tu kwa hulka yetu ya Kitanzania na tunavyoendesha mambo hata kama ni muhimu kuitwa anaweza asiitwe kwa kuogopa tu kufanya hivyo kwasababu ni Rais, Lakini si kwasababu kwamba sheria hairuhusu.

      Sheria inampa kinga Rais kushitakiwa akiwa madarakani Lakini haimpi kinga ya kuwa shahidi.


    Page 1 of 11 123 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Replies: 71
      Last Post: 21st January 2012, 19:45
    2. Hakimu ajitoa kesi ya Mahalu
      By Rutashubanyuma in forum Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
      Replies: 5
      Last Post: 5th August 2011, 20:27
    3. Tetesi: Kesi ya Prof. Mahalu – Zengwe jipya jikoni
      By WhoToldU in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 15
      Last Post: 27th May 2011, 22:40

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...