Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Rais wa zamani wa Malawi Anyang'anywa Pasipoti Yake

    Report Post
    Results 1 to 2 of 2
    1. #1
      TANMO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Tanzagiza
      Posts : 5,045
      Rep Power : 7769
      Likes Received
      1806
      Likes Given
      3439

      Arrow Rais wa zamani wa Malawi Anyang'anywa Pasipoti Yake

      Watanzania tunaweza kujifunza kutokana na hii habari ninayoweza kuiita njema....

      Rais wa zamani wa Malawi Bakili Muluzi amenyang'anywa pasipoti yake na tiketi yake ya ndege wakati akijiandaa kuelekea Uingereza kwaajili ya matibabu kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili nchini humo.

      Bakili Muluzi, alikuwa akijiandaa kusafiri kuelekea Uingereza kwaajili ya uchunguzi wa afya yake wakati maafisa wa kupambana na rushwa walipoamua kumnyang'anya pasipoti yake na tiketi yake ya ndege.

      "Tumeishikilia pasipoti ya Muluzi ili kumfanyia uchunguzi wa mambo mbali mbali" alisema Alex Nampota, mkuu wa kitengo cha kupambana na rushwa nchini Malawi (ACB).

      Muluzi alikuwa asafiri jana jumapili kuelekea Uingereza ambako amekuwa akienda mara kwa mara kwaajili ya uchunguzi wa afya yake.

      Mkuu huyo wa kitengo cha rushwa alifanikiwa kupata kibali toka mahakama kuu cha kushikilia nyaraka za kusafiria za Bakili Muluzi.

      Muluzi aliyeiongoza Malawi toka mwaka 1994 hadi 2004 anakabiliwa pia na tuhuma za kuiba dola milioni 12 toka kwenye mfuko wa misaada.

      Nampota alisema pia kwamba amefanikiwa kupata kibali cha kuchukua mali za Muluzi na kuzipiga mnada ili kuzirudisha pesa hizo iwapo Muluzi atashindwa katika kesi yake hiyo inayomkabili ambayo bado haijaanza kusikilizwa.

      Muluzi ndiye kiongozi wa ngazi ya juu sana kuchukuliwa hatua katika harakati za rais wa Malawi wa sasa Bingu wa Mutharika ambaye amedhamiria kutokomeza rushwa nchini humo.

      Muluzi kwa upande wake alisema kuwa ameshangazwa na hatua hiyo ya kumzuia kwenda hospitali kufanyiwa upasuaji ambao hauwezi kufanyika nchini Malawi.

      "Sidhani kama nchi hii ingewafanyia marais wake waliopita vitu kama hivi" alisema Bakili Muluzi.

      Wakili wa Muluzi, ndugu Jai Banda alisema kuwa wataipinga hatua hiyo ya ACB jumatatu.



      Huyo mnafki tu.. Kama huo ugonjwa angekuwa nao raia wa kawaida ambaye hana pesa za kwenda kufanyiwa upasuaji Uingereza ni haki yake kufa siyo?
      Kwa nini alivyokuwa rais asingefungua hosiptali hapo malawi ambayo ingekuwa na uwezo wa kumtibu yeye ili na wananchi nao wanufaike nayo?
      Do Something......

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4015
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Rais wa zamani wa Malawi Anyang'anywa Pasipoti Yake

      Bingu anaonyesha wasomi wanatakiwa kufanya nini kwenye siasa. Mambo yamebadilika sana baada ya yeye kuiongoza Malawi.

    4. Miaka 50

    Similar Topics

    1. Mtoto wa Rais wa Guinea anyang'anywa utajiri wake na US, France
      By KIM KARDASH in forum International Forum
      Replies: 20
      Last Post: 27th October 2011, 15:17
    2. Anyang’anywa silaha kwa kukutwa kalala kwenye gari
      By kilimasera in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 3
      Last Post: 11th January 2011, 18:43
    3. Anyang'anywa Uraia Baada ya Kuoa Mke wa Pili
      By MziziMkavu in forum Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
      Replies: 10
      Last Post: 30th May 2010, 02:36
    4. Mugabe anyang'anywa Knighthood yake. Hatambuliki tena na ukoo wa kifalme!
      By Richard in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 0
      Last Post: 25th June 2008, 20:03
    5. Replies: 125
      Last Post: 23rd January 2008, 01:22

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...