JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

  Report Post
  Page 1 of 2 12 LastLast
  Results 1 to 20 of 25
  1. Maalim Jumar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th December 2010
   Location : DAR-ES-SALAAM.
   Posts : 1,312
   Rep Power : 820
   Likes Received
   69
   Likes Given
   2

   Default Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   Ndugu wapendwa wana jf!
   Kila mtu na zawadi yake kwa anaempenda au anaowapenda.
   Zawadi yangu kama mtaalam wa tasnia hii nimewafikishieni hii zawadi yangu kwa upendo wang wote!! Kwa mwaka 2011.
   Attached Thumbnails Attached Thumbnails Click image for larger version. 

Name:	MVC-092S.JPG 
Views:	1574 
Size:	44.8 KB 
ID:	19456   Click image for larger version. 

Name:	Aspen 7.7.jpg 
Views:	1486 
Size:	25.8 KB 
ID:	19457  
   Attached Files
   Spiritualist & Astrologist.


  2. PakaJimmy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th April 2009
   Posts : 16,256
   Rep Power : 16106769
   Likes Received
   8178
   Likes Given
   3665

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.


   sasa ndiyo nani huyu?
   Ni wewe?
   Mtaalamu wa tasnia gani sasa?
   "The only thing that walks back from the tomb with the mourners and refuses to be buried is the character of a man.
   What a man is, survives him... it can never be buried"
   (GENEKAI-Jamiiforums, 4th November 2010 07:32PM).
   [email protected]

  3. PakaJimmy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th April 2009
   Posts : 16,256
   Rep Power : 16106769
   Likes Received
   8178
   Likes Given
   3665

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   "The only thing that walks back from the tomb with the mourners and refuses to be buried is the character of a man.
   What a man is, survives him... it can never be buried"
   (GENEKAI-Jamiiforums, 4th November 2010 07:32PM).
   [email protected]

  4. Maalim Jumar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th December 2010
   Location : DAR-ES-SALAAM.
   Posts : 1,312
   Rep Power : 820
   Likes Received
   69
   Likes Given
   2

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   HUYU NDIE HUYO HUYO UNAESOMA MAELEZO YAKE.
   [COLOR=#0000ff]

   Tasnia ya Occult science.
   kifupi ukisha soma hiyzo makala utajua ni nini kinaongelewa.
   Happy new year 2011.
   Last edited by Maalim Jumar; 23rd January 2011 at 23:11.

  5. Rose1980's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th May 2010
   Posts : 5,709
   Rep Power : 2160
   Likes Received
   1233
   Likes Given
   1427

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   eeh jaman mbona sielew mim?naona mijipicha tu


  6. PakaJimmy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th April 2009
   Posts : 16,256
   Rep Power : 16106769
   Likes Received
   8178
   Likes Given
   3665

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   Quote By Maalim Jumar View Post
   HUYU NDIE HUYO HUYO UNAESOMA MAELEZOM YAKE.
   Genekai.
   Tasnia ya Occult science.
   kifupi ukisha soma hiyzo makala utajua ni nini kinaongelewa.
   Happy new year 2011.
   I never believe in horoscopic predictions.
   "The only thing that walks back from the tomb with the mourners and refuses to be buried is the character of a man.
   What a man is, survives him... it can never be buried"
   (GENEKAI-Jamiiforums, 4th November 2010 07:32PM).
   [email protected]

  7. Diehard's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd November 2010
   Posts : 353
   Rep Power : 632
   Likes Received
   55
   Likes Given
   103

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   Haya unayojaribu kutabiri uwe uanakuwa specific siyo eti sema wapi kutakuwa na hayo maradhi gani yataletaichachafya dunia, viongozi wepi watapata misukosuko, hali ya hewa itakuwa mbaya wapi, majanga yatatokea wapi kipindi kipi, wakimbizi toka nchi gani acha kutuibia unageneralize mambo hayo yote ni sawa kama 2010 tu, eti watu wataacha kwenye mahusianao mbona hiyo ipo sema fulani ataachana na mtu wake\,
   Wrong is wrong no matter who says it , If you don't stand for something you will fall for anything'.

  8. Edward Teller's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st November 2010
   Location : Area 51
   Posts : 3,625
   Rep Power : 1290
   Likes Received
   613
   Likes Given
   692

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   Quote By maalim jumar View Post
   ndugu wapendwa wana jf!
   Kila mtu na zawadi yake kwa anaempenda au anaowapenda.
   Zawadi yangu kama mtaalam wa tasnia hii nimewafikishieni hii zawadi yangu kwa upendo wang wote!! Kwa mwaka 2011.
   alishatabir mambo gan yakatokea exactly as he said?
   “Talk slowly but think quickly”

  9. Maalim Jumar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th December 2010
   Location : DAR-ES-SALAAM.
   Posts : 1,312
   Rep Power : 820
   Likes Received
   69
   Likes Given
   2

   Default

   Quote By PakaJimmy View Post
   I never believe in horoscopic predictions.
   Kwanini usiamini utabiri?
   Ukinielezea 7bu ...huenda nikajitahidi kukufanya uweze kupenda ku-prediktiwa.

  10. Maalim Jumar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th December 2010
   Location : DAR-ES-SALAAM.
   Posts : 1,312
   Rep Power : 820
   Likes Received
   69
   Likes Given
   2

   Default

   Quote By Edward Teller View Post
   alishatabir mambo gan yakatokea exactly as he said?
   Sikuzoeshwa kusema uongo espicialy katika tasnia hii ya utabiri.
   Ila nakushauri anza kusoma hayo na ufuatilie utajua ukweli.
   Wengi wanaielewa kazi yangu na kuwasaidia....naamini ndio mara ya kwanza kukutana na makala zangu.
   Kazi kubwa si kueleza jambo moja au mawili ndani ya mwaka mzima...lakini kazi kubwa ya jujivunia ni kuelezea na kudafanua mambo ya kila siku yanayo husu jamii. Hivyo ukifaham nyota yako itakua vizuri uisome matukio yako. Wapi utaweza kuisoma kila siku za wiki ...ndani ya gazeti la mwananchi uk wa nyota.
   Pia kama upo TZ tumia simu yako ya mkononi...mtandao wowote...fanya yafuatayo: andika neno MAALIM acha nafasi MSHALE tuma kwenda 15771. Ondoa neno Mshale andika Nyota yako. Huduma hiyo utaipata kila utapotuma msg.

  11. Maalim Jumar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th December 2010
   Location : DAR-ES-SALAAM.
   Posts : 1,312
   Rep Power : 820
   Likes Received
   69
   Likes Given
   2

   Default

   Quote By Diehard View Post
   Haya unayojaribu kutabiri uwe uanakuwa specific siyo eti sema wapi kutakuwa na hayo maradhi gani yataletaichachafya dunia, viongozi wepi watapata misukosuko, hali ya hewa itakuwa mbaya wapi, majanga yatatokea wapi kipindi kipi, wakimbizi toka nchi gani acha kutuibia unageneralize mambo hayo yote ni sawa kama 2010 tu, eti watu wataacha kwenye mahusianao mbona hiyo ipo sema fulani ataachana na mtu wake\,
   Usisome kama barua!
   Jitahidi usome kama Great Thinker. Nimeeleza vizuri...siwezi kutaja kila mahali...ila nimetaja kwa vizuri...ni upande gani na hiyo itahusu dunia.
   Muhim utazamie kwa hapo ulipo sasa...utatosheka. Pia endelea kufuatilia hayo nlio yaeleza.

  12. Maalim Jumar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th December 2010
   Location : DAR-ES-SALAAM.
   Posts : 1,312
   Rep Power : 820
   Likes Received
   69
   Likes Given
   2

   Default

   Quote By Rose1980 View Post
   eeh jaman mbona sielew mim?naona mijipicha tu
   Ha ha ha!
   Umefungua picha Rose! Ulitaka uone nini hapo?
   Fungua maelezo...yalioanzia...annual year .... Utaelewa

  13. #13
   Emil's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 12th April 2010
   Posts : 6
   Rep Power : 595
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   Naona mambo hayaendi uzuri ndo maana sijaposti chochote ila nipe habari za UVCCM wanataka kutueleza nini

  14. NGULI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st March 2008
   Location : HOME
   Posts : 4,826
   Rep Power : 1436615
   Likes Received
   564
   Likes Given
   267

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   Lini mafisadi papa watakufa? Dowans ni ya nani?

  15. Nyangomboli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th November 2010
   Location : Mwisenge
   Posts : 1,360
   Rep Power : 834
   Likes Received
   271
   Likes Given
   14

   Default

   Quote By Nguli Jabali View Post
   Lini mafisadi papa watakufa? Dowans ni ya nani?
   hii ndo yenyewe. pia maalim atufanyie mahesabu tumjue anaemiliki dowans.

  16. Maalim Jumar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th December 2010
   Location : DAR-ES-SALAAM.
   Posts : 1,312
   Rep Power : 820
   Likes Received
   69
   Likes Given
   2

   Default

   Quote By Emil View Post
   Naona mambo hayaendi uzuri ndo maana sijaposti chochote ila nipe habari za UVCCM wanataka kutueleza nini
   Angalia kwenye matukio ya mwaka mpya nime-attach as annual Prediction.

  17. Maalim Jumar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th December 2010
   Location : DAR-ES-SALAAM.
   Posts : 1,312
   Rep Power : 820
   Likes Received
   69
   Likes Given
   2

   Default

   Quote By Nyangomboli View Post
   hii ndo yenyewe. pia maalim atufanyie mahesabu tumjue anaemiliki dowans.
   Labda unataka kujua kama nami nawajua....
   haihitaji tena namba.
   Last edited by Maalim Jumar; 23rd January 2011 at 23:00.

  18. Husninyo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th October 2010
   Posts : 23,292
   Rep Power : 344358669
   Likes Received
   8325
   Likes Given
   5194

   Default

   Quote By Nyangomboli View Post
   hii ndo yenyewe. pia maalim atufanyie mahesabu tumjue anaemiliki dowans.
   tena atufanyie hayo mahesabu mmiliki awe anatudai maelf badala ya mabilioni.

  19. kilimasera's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Posts : 3,073
   Rep Power : 1236
   Likes Received
   212
   Likes Given
   261

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   Quote By Rose1980 View Post
   eeh jaman mbona sielew mim?naona mijipicha tu
   haieleweki hii

  20. kilimasera's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Posts : 3,073
   Rep Power : 1236
   Likes Received
   212
   Likes Given
   261

   Default Re: Yajue matukio ya mwaka 2011...pia matukio ya nyota yako kwa undani.

   PREDICTION OF ANNUAN YEAR 2011.
   MTABIRI: MAALIM ABALHASAN JUMAR.

   Twamshukuru mwenyezi mungu kwa kwa kutujaalia afya njema.Waliopo kwenye maradhi na matatizo mbali mbali twawaombea kwa mwenyezi mungu shifaa na kuepukana na dhiki walizo nazo.
   Mwaka huu wa 2011 utaanzia siku ya jumamosi miongoni mwa siku saba (7) za wiki . Siku hii kitaalamu inatawaliwa na sayari iitwayo zuhali (Saturn) miongoni mwa siri iliyonayo sayari hii ni kutofanikisha mambo mazuri … ni sayari nyepesi kufanikisha mambo yanayohusu uharibifu wowote. Kuonekana kwa sayari hii huashiria ugumu ambao hudumu kwa muda mrefu kwenye matatizo mbali mbali. Imeitwa kitaalamu (nahsatul akbar) au (great misfortune) au mkosi mkubwa.
   Inamaanisha iwapo itakuandama kwenye mambo yako ya kimaisha au jingine itakua ugumu kupata faraja kutoka kwenye jambo hilo.Utapohitaji kutoka kwenye balaa hilo itahitaji subra na jitihada za ziada bila kukata tamaa. Utakuta kati yetu imewakumba na wamekosa utatuzi ulio muafaka mara nyingi wameishia kukata tama… jambo ambalo kitaalamu ni makosa…hakika nyota hii ya zuhali inayo maelezo marefu.
   Sayari hii inayo maangalizi ya aina mbili takriban kama zilivyo sayari zingine ambazo ni chanya (positive) au hasi (negative).
   Mwaka huu utatawaliwa na nyota inayoitwa simba( Leo) nyota hii imeingia kwenye utawala wa sayari iliopo ndani ya siku ya jumamosi. Nyota ya simba inahukumiwa na nyota iitwayo jua (sun) nyota hii ya simba huonekana upande wa mashariki wa dunia. Upande huo zinapatikana nyota tatu(3) ambazo ni (i) Kondoo (ii) Simba (iii) Mshale. Nyota hizo zote zinazo nguvu zake za asili ambayo ni moto kitaalamu twaziita (muthalathat nariyyat) au (Triangle fierry).
   Ukiangalia kwa mwaka huu 2011 au tangu mwaka 2009 – 2010- ilikua ni bakht (fortune) ambayo imetokea duniani kwa kua hizi nguvu za asili ya moto huashiria mabadiliko ya ajabu japo yanapokosekana huashiria huzuni ya ajabu.
   Pia waliozawa tarehe hizi kwa kila mwezi, mwaka huu wa 2011 mafanikio kwao yamechukua nafasi kubwa iwapo hawatozingirwa kwa mabalaa (mikosi) nazo ni 8-17-26 na hizi tarehe huashiria nguvu kubwa kwenye mipango yenu.
   Mwaka huu utatuashira haya yafuatayo:
   VURUGU:Mwaka huu si vyema kuanzisha ugomvi aina yeyote iwe majumbani,kazini,mitaani,majim boni hata watawala wa nchi mbali mbali…kwa kua kuanzisha huko hakutaleta natija(faida) pia kutakua na kudumu kwa visasi visivyo mafanikio kwa muanzishiwa au mwanzishaji. Mambo haya yatatokea mwaka huu mara kwa mara zaidi itakua kuanzia mwezi pili(Feb) na mwezi sita (June) na mwezi wakumi (Oct).
   MIGOGORO:Mizozo na kutengwa /kutenga hili litahusisha kuachwa/kuacha kwenye mahusiano. Kufukuzwa kazi na kukosa jambo muhimu haya zaidi yatatokea mwanzo wa mwaka huu 2011 na mwisho wa mwaka huu 2011.
   WAKIMBIZI: Duniani wakimbizi watjitokeza kuwa ni wengi hasa waliopo upande wa mashariki wa dunia. Hali hii itatokea zaidi.
   MARADHI: Watu watasumbuka kwa maradhi ya mgongo na kichwa na tumbo, Haya yatasumbua walimwengu hasa zaidi mwanzo wa mwaka 2011 na mwisho wa mwaka 2011.
   HALI YA HEWA:Dunia itakua si shwari na hivyo hivyo itanyesha mvua kubwa itayosababisha uharibifu mkubwa.
   VIFO: Hali za huzuni hadi kusababisha vifo kwa vikongwe wengi duniani na wenye heshima zao na hivyo hivyo vifo vya kuhuzunisha vitajitokeza zaidi mwezi wa kwanza (Jan) na mwezi wa nane (Aug) na mwezi wa kumi na moja (Nov) itakua ni ajili ya maradhi ya mlipuko.
   KUKAMATWA: jua hili litatokea mwanzo wa mwezi wa kwanza (04.Jan.2011) itaonekana zaidi mashariki ya kati Afghanistani,China na maeneo mengineyo hapo. ( 01.June.2011.01.July.2011). Mwezi utakamatwa 15.June.2011)
   MAUAJI: ya kinyama yatajitokeza ambayo yatahuzunisha ulimwengu kama ajali za ndege,meli,treni,magari vyombo vitavyotumia moto zaidi. Hali hiyo itayotokea mwezi wa tano na mwezi wa saba.
   SAFARI: nyingi hazitokua salama ispokua kwa kuanzishwa kwa maombi maalumu.
   VIONGOZI: Duniani watakumbwa na taabu nyingi katika utawala wao hali hiyo itaanzia mwanzo wa mwezi wa nne(April) na kuendelea.
   HITIMISHO: Yanaweza kuepukwa hayo kwa kuzidisha maombi(Du3’a) mara kwa mara. Kunaweza valiwa vito ambavyo vitasaidia kuweka mambo shwari. Vito hivyo vinaitwa (RUBBY) au ( BLUE SUPPHIRE) vito hivyo vivaliwe kwa kufuata utaratibu maalumu.
   MWENYEZI MUNGU IBARIKI TANZANIA,BARA LA AFRIKA NA DUNIA YOOTE! AAMIIN.

   MAWASILIANO KWA MTABIRI:
   MOB PHONE: 0713-351781.
   E-mail : [email protected]
   Facebook: maalim.jumar
   03.01

   MATUKIO YA KILA NYOTA 2011.
   MTABIRI: MAALIM ABALHASAN JUMAR.


   1-Kondoo(Aries) Machi 21-Aprili 20.
   Mwaka huu ni mzuri hasa kwenye mambo yanayohusu ilmu.Utapata nafasi ya kuongeza ujuzi ulionao.Mipango ya safari za mbali ni muda muwafaka.Namba yao ya bahati mwaka huu ni (10).
   KIPATO: Jitahidi uongeze ufanisi wako au ujuzi wako ili uimarishe kipato chako. Ajira utayoipata itakuongezea mafanikio makubwa sasa katika maisha yako. Hili iwapo huna mikosi(mabalaa).
   MAPENZI: Utadumu kwenye upendo wako au utapata ushirikiano hasa ukishirikishaa ndugu zako. Salaam mara kwa mara zitakuongezea upendo kwa umpendae. Fikra zako binafsi ndio zitanusuru uhusiano uliopo.
   AFYA:Utasumbuliwa zaidi meno,kichwa itasababishwa ajili ya kipato au ajira uliyo nayo.
   UADUI: Utaibiwa mara kwa mara hali hiyo itakuongezea hofu nyingi.Pia taarifa nyingi zitakutia hofu.

   2-Ng’ombe(Taurus) Aprili 21-Mei 21.
   Mwaka huu ni muda muafaka kuongeza ujuzi au kwenda kupata ujuzi zaidi.Utaandamwa kwa maneno/kesi zaidi.Kazi zitakunyanyua katika maisha yako.Namba yako ya bahati ni (11).
   KIPATO:Utapata kupitia rafiki zako.Mialiko mingi itakuongezea kipato chako.Taarifa nyingi ndio zitahatarisha kipato chako.Utatuzi wahitajika zaidi.
   MAPENZI: Zingatia ushauri wa wazazi wako kwenye mahusiano yako.Siri nyingi zitakuharibia matarajio yako kwenye mahusiano.Matatizo yataanzia hapo hapo ulipo.
   AFYA: Maradhi ya wasi wasi yatakuandama. Hutosikia vizuri,sauti kukwaruza mara kwa mara.
   UADUI:Utaharibiwa mipango yako au kuandamwa zaidi ajili ya mbinu zako katika maendeleo .

   3-Mapacha(Gemini) Mei 22- Juni 21.
   Mwaka huu utajazwa swifa nyingi za ukweli/uongo pia utasaidiwa. Hali hiyo itakuongezea raha.Muda muwafaka kupata hifadhi kwa kila kitu chako. Walio karibu nawe watasafiri mbali nawe!.Namba yako ya bahati ni 21.
   KIPATO: Subira yahitajika kwenye kipato chako.Utadanganywa hali ambayo itakuharibia mambo yako.Utafanyiwa kila hila(ujanja) ili uharibikiwe.
   MAPENZI: Utaempata ndie anae kufaa maishani . Hali itayojitokeza ni vizuri uwe mwenye subira ili usizae nje ya ndoa!.Utapoanzisha uchumba haraka utakubalika.Shida zahitajika utatuzi.
   AFYA: Maradhi yatakua chanzo kwa kutofanikisha mipango yako ya makazi.Utasumbuliwa zaidi kupumua/mikononi maumivu/kuwashwa.
   UADUI: Migogoro itaanzia kwenye kazi /biashara zako.Hali hii itaendelea hata kukuingiza kwenye mashauri yasio makini.

   4-Kaa (Cancer) Juni 22- Julai 23.
   Mwaka huu maradhi yatazidi kukuandama.Utazidi kua mnyonge…utasengenywa(kutetwa). utakua kwenye wakti wa kujikatia tamaa.unahitaji kupewa ushauri na kupatiwa utatuzi zaidi.Namba yako ya bahati mwaka huu ni 22.
   KIPATO:Utakachokianzisha kitaleta faida/kuendelea japo kiduchu.Ndugu/marafiki zako watakua ni wenye msaada kwako.Uheshimu zaidi mawazo yao.
   MAPENZI:Uhusiano wako utakumbwa na migogoro/mizozo ya mara kwa mara. Hali hiyo itadumu na itakua tatizo endelevu.Unaweza kujitahidi na uwe mwanye ustahamilivu ili kutengana kusitokee.Kwa hili utatuzi wahitajika haraka.
   AFYA:Usiendekeze starehe zaidi kwa kua humo itakuharibia swiha yako.Mazingatio ya swiha ndio itakuwekw hali iwe vzuri au mbaya.Akina mama mtasumbuliwa maeneo ya uzazi. Maumivu ya kifua ni wanaume na wanawake.
   UADUI: Misaada utayoipokea ndio itakua chanzo kukuharibia mipangilio yako.Uwe karibu yao marafiki zako hata ukigundua mabaya yao..wewe usiwaoneshe chuki. Tahadhari zako ziwe za rohoni(usiri).

   5-Simba (Leo) Julai 24-Agosti 23.
   Mwaka huu ni mwafaka kujihudumia kwenye afya au kujichunguza hali ya mwili wako/akili(mawazo)yako.unayo nafasi kuanzisha biashara/uchumba/kujenga…yatatimia ukiwa huna mikosi(mabalaa).Namba yako ya bahati mwaka huu ni 23.
   MAPENZI:Mahusiano yataendelea.Ulienae atazidisha migogoro/magomvi.Wanaotafuta mahusiano utaekutana nae anafaa zaidi.Ajili ya mahusiano yako vitu vingi vitapotea!.
   KIPATO:Muda muafaka kuifuatilia ajira .Waliopo kwenye vyanzo vya mapato yao ni muda muafaka kutekeleza yote yalio muhimu ili kuepuka majuto.Epuka matumiziyasio muhimu(starehe).
   AFYA: Utasumbuliwa zaidi maradhi ya manjano(Jaundice) moyo(Bp) hali hiyo itakukosesha utulivu. Pia utaongeza ukorofi…jitahidi upate utatuzi wa hayo.
   UADUI: Maneno mengi utayosikia au kuambiwa vizuri ufanye subira ili usifikwe na matatizo makubwa.Hali hii itakua inajirudia mara kwa mara.

   6-Mashuke (Virgo) Agosti 24- Sept 23.
   Mwaka huu huzuni zilizopita ujitahidi na unaweza kujiandaa kujiweka vizuri..hali hii itafanikisha iwapo huna mikosi.Mipango ya mali/kipato itaimarika. Yote uliohitaji kununua ni vyema ukatekeleza haraka. Ubakhili wako si vzuri /si suluhisho.Namba yako ya bahati mwaka huu ni 3,6,9.
   KIPATO: Endelea kufuatilia mikataba yako au ahadi zako hasa za kuongeza kipato.Yote hayo vizuriuwe mwangalifu.Kudanganywa au kuzidiwa kutajitokeza.Mipango na utimilifu wa ahadi iwapo huna mikosi.
   MAPENZI: Utadanganywa katika mahusiano yako na hali hiyo itajitokeza zaidi.Hofu zitaongezeka hali hiyo itamshitua mkeo/mumeo/umpendae.Ukweli ni kidogo kwenye mahusiano ni vizuri uwe mwenye subiri.
   AFYA: Umpendae vizuri umchunguze tabia(Afya) yaake.Mizozo iepuke ili ugonjwa wa shinikizo la damu lisikusumbue!.
   Mawazo yatakusumbua vidonda vya tumbo(Ulcer).
   UADUI: Uchijunge mwenyewe hizo misifa (Majigambo) ndio itakua sababu ya kuandamwa na kufanyiwa vitimbi.

   7-Mizani (Libra) sept 24-Okt 23.
   Mwaka huu misaada itahitajika kwa ndugu zako au watoto wao. Ni vizuri uwasaidie haraka watapohitaji. Upendo utaongezeka juu yako. Ndoto nyingi zitakusumbua mawazo yako.Mikataba ifuatilie kwa umakini zaidi.Namba ya bahati mwaka huu ni 7.
   KIPATO: Miradi yako au makampuni yako yataendelea vizuri. Mambo mengi yataendelea vzuri iwapo huna mikosi(mabalaa).Yote uliokuwa wayasubiri utayafahamu.
   MAPENZI: Mpenzi wako atakua mbali nawe! Vizuri uwafuate na kuzidisha mawasiliano nae.Utayohisi kwenye mahusiano mara nyingi yatakua yenye usahihi.Mahusiano yasasa ni chanzo cha mafanikio yako.Hili nalo iwapo huna mikosi.
   AFYA: Utasumbuliwa zaidi viungo au kichwa au mgongo hali hii itakuzidishia wasi wasinkwako. Jitahidi kutafuta tiba .
   UADUI: Utazidi kuandamwa kwa sababu ya kipato chako ili uharibikiwe.Unaweza kutafuta utatuzi pia!.

   8-Nge (Scorpio) Okt 24-Nov 22.
   Mwaka huu siri zako nyingi zitafichuka.Mambo muhimu kwako uyatekeleze ni kujenga/kununua kiwanja au shamba ikiwa unao uwezo.Hifadhi akiba zako.Ulilokua hujalifaham khatma yake sasa utalijua.Namba yako ya bahati mwaka huu ni 17.
   KIPATO: Kitaendelea kua chenye furaha.Matanuzi yako au starehe zako ni muda muwafaka. Vizuri upunguze hayo matumizi yako.Kipato chako kitakuinua zaidi mwaka huu.Wasaidie rafiki zako shida zao!.
   MAPENZI: Utafanikisha mahusiano mengi kupitia cheo ulicho nacho au nafasi utayokua nayo.Kutajitokeza mashauri ambayo yatakusumbua.Utatuzi wahitajika!.
   AFYA: Jitahidi ufuate utatuzi tatizo ulilo nalo Jitahidi uombewe du’aa kwa ajili ya afya yako ya kiakili.Ugonjwa wa haja ndogo na viungo vya uzazi vitasumbua.
   UADUI: Utaandamwa kwa ajili ya ukaribu uliopo.Hata hizo safariutazozifanikiwa itakua sababu ya kuhasidiwa.

   9-Mshale (Sagittarius) Nov 23-Des 21.
   Mwaka huu ni muda mwafaka kuwazidishia furaha watoto wako hasa kwenye majukumu uliyo nayo.Pia kwa watoto wa ndugu zako na jamaa zako.Starehe ni nyigi ambazo zitakuvutia hata utajisahau kwenye mambo muhimu.Mazoezi ya mwili ni muhimu kwa afya yako yafanyike mara kwa mara.Namba za bahati mwaka huu ni 3,6,9.
   KIPATO: Kitatetereka zaidi ajili ya afya yako au matatizo yatayokufika.KItu muhimu utakikosa pia itakuharibia mambo yako kwenye kipato.Muda mwafaka kutafuta kazi au shughuli bora zaidi.
   MAPENZI: Yataendelea kwa upendo.Misaada mingi itapatikana kutoka kwa mpenzi wako.Pia marafiki zako watakusaidia kudumisha haya mahusiano yako.Vizuri kujua kama huna mikosi …kama mikosi unayo hayo hayatotimia.
   AFYA: Inshaallah! Kwa sasa utawezeshwa kupata tiba sahihi katika haya maradhi yako.Maradhi yatayokusumbua zaidi ni mapaja,makalio.
   UADUI: Makazi au maeneo unayoishi itakua chanzo cha matatizo.Vizuri uwe mwenye subira na kujitahidi kutatua hali hiyo kwa uangalifu na umakini.

   10-Mbuzi (Capricorn) Des 22-Jan 20.
   Mwaka huu maradhi yatakusumbua mara kwa mara. Maradhi ya kuwashwa,majipuna maumivu ya mgongo.Mambo mengi hayatokuwa sawa.Utatelekezwa au kususiwa hata kufukuzwa kwenye mambo muhimu.Utatuzi muhimu wahitajika.Namba ya bahati kwako mwaka huu ni moja.
   KIPATO:Utadhulumiwa na kupoteza.Mizozo itajitokeza mara kwa mara kwenye kipato.Utafanyiwa vimbwanga ili uharibikiwe.HIli linahitaji utatuzi haraka.
   MAPENZI: Katika uhusiano huu hakuna ukweli kabisa!.Vizuri uwe mwenye subira kwa yote utayoyaona au kusikia …japo kwakoitakua ugumu wa kuamini…ni vizuri utilize hasira zako.
   AFYA: Magonjwa yatayokusumbua zaidi ni (gout) maumivu makali ya mgongoni.
   UADUI: Mipango yako ambayo itayokuletea mizozo ni ile utayojishughulisha kuhusu maisha yakosaidia kuliko kuleta ushindani. Ukiendekeza ushindani utaharibikiwa mambo yako muhimu.

   11-Ndoo (Aquarius) Jan 21-Feb 19.
   Mwaka ni mzuri kwenu hasa wenye kuhitaji wapenzi wa uhakika na wakweli.Mliopo kweye mahusiano mizozo itakua ni mingi…pia yahitaji uvumilivu ili kudumisha mahusiano yenu ya upendo.Mwaka huu jitahada ni nyingi kwenye hili(Growing spiritual).Namba yako ya bahati ni (11).
   KIPATO: Uhakika si mkubwa kwa kua wasiwasi nimwingi.Vizuri kuyalipa madeni yako bila kuhofia kipato chako ukifanya hivi itakuongezea bahati zaidi au baraka.Utapoteza sana kwenye mali zako au vitu vyako.Utatuzi wahitajika.
   MAPENZI: Unao wahitaji wengi waondio utaokutana nao.Vizuri utoe maamuzi kwa haraka kutekeleza azma yako.Mapenzi yatakua yenye faraja katika maisha yako ya sasa.Vizuri kuangalia afya zenu kabla ya kulianzisha penzi.Au ni vzuri kuangalia chochote kitacho husu yeye.
   AFYA: Macho yako hayatoona vizuri.Moyo utakua unashituka mara kwa mara.Yatayokua yanakusumbua jitahidi uyapuuze na upumzike zaidi.
   UADUI: Utatishwa zaidi na kususiwa kwenye mambo yako yatayokuletea faida.Hali hiyo itakuongezea unyonge.Si vizuri kuwaonesha au kuwadhihirishia chuki wote walio karibu yako.( Almighty Allah saves you).

   12-Samaki (Pisces) Feb 20-Machi 20.
   Mwaka huu mashaka ni mengi kwenye mipango yako.Ahadi nyingi hazitotimia.Mipango mingi haitotekelezwa.Utaibiwa na kupeteza zaidi.Unaoshirikiana nao kwenye shughuli zako nao watakuongezea mashaka zaidi.Namba yako ya bahati ni 30.
   KIPATO: Utayoyapangilia yatakuletea faida na kukuzidishia bahati. Safari ndefu au za mbali ndio zitakua chanzo kukuongezea mali.
   MAPENZI:Unao pendana nao ni chanzo cha kuzidi huu upendo.Mizozo itahusu mali(kipato). au cheo chako.Hali yeyote itayo jitokeza inahitajika uwe mvumilivu.Utatuzi wahitajika!.
   AFYA: Mafua yatkusumbua zaidi pia shinikizola damu. Na huo mgongo . Haya maradhi yatakua chanzo cha maumivu mengi mwilini.Maeneo ya kifua na magotini yatasumbua.
   UADUI: Mizozo kwenye uhusiano ndio sababu kubwa itayokuongezea huzuni.Lipa madeni yako ili uepuka uadui na unyonge.   Mawasilano na mtabiri: MAALIM ABALHASAN JUMAR.
   Phone; 0713-351781.
   e-mail: [email protected]
   Facebook: maalim.jumar


  Page 1 of 2 12 LastLast

  Similar Topics

  1. JF jikumbusheni matukio yenu mwaka huu wa 2011!!.
   By Maalim Jumar in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 3
   Last Post: 7th June 2011, 14:00
  2. Matukio Haya 7 Bomba Wikiendi hii – 27 May 2011
   By vusile in forum Entertainment
   Replies: 0
   Last Post: 26th May 2011, 11:45
  3. Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio
   By Edson in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 204
   Last Post: 20th May 2011, 17:39
  4. Matukio yatakayofanya tuukumbuke 2011
   By mzambia in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 1
   Last Post: 1st January 2011, 11:50
  5. Matukio ya kukumbukwa katika mwaka 2008
   By Balantanda in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 14
   Last Post: 2nd January 2009, 00:24

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...