JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Toleo la Raia Mwema la leo..

  Report Post
  Results 1 to 11 of 11
  1. Mzee Mwanakijiji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Location : Kijijini
   Posts : 32,117
   Rep Power : 87995664
   Likes Received
   24670
   Likes Given
   13382

   Default Toleo la Raia Mwema la leo..   Nimeambiwa kama unaishi Dar au Kigamboni usisome Uk. 9 unaweza kuhama mji!
   [email protected]
   The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

  2. Steve Dii's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th June 2007
   Location : Kihesa - Iringa
   Posts : 6,914
   Rep Power : 49787893
   Likes Received
   1121
   Likes Given
   3323

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Swali hapo juu: Muungwana, mdhaifu au mateka?!

   Jibu: Ni muungwana aliyetekwa na wazalendo dhaifu.

  3. Dingswayo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th May 2009
   Posts : 3,969
   Rep Power : 172213110
   Likes Received
   2817
   Likes Given
   9186

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Quote By Mzee Mwanakijiji View Post

   Nimeambiwa kama unaishi Dar au Kigamboni usisome Uk. 9 unaweza kuhama mji!
   Ukurasa wa 9 unasenaje? Tupe habari.
   Batallamos hasta la victoria, siempre!

  4. #4
   Utingo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th December 2009
   Location : Lyazumbi
   Posts : 6,984
   Rep Power : 36942
   Likes Received
   1670
   Likes Given
   1087

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Quote By Dingswayo View Post
   Ukurasa wa 9 unasenaje? Tupe habari.
   unaeleza nduto za u-ali nacha za kujenga kigamboni - by Lula wa Ndali Mwananzela
   Never Underestimate the Power of Stupid People in Large Groups

  5. Safari_ni_Safari's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2007
   Location : Kibaruani
   Posts : 17,816
   Rep Power : 3277027
   Likes Received
   9582
   Likes Given
   3670

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Lula wa Ndali Mwananzela ni nani kwani? Toka jana anatajwatajwa humu.....mtujuve jamani
   "If you can't RESPECT EXISTENCE then you must EXPECT RESISTANCE!"

  6. #6
   TATE's Avatar
   Member Array
   Join Date : 11th August 2010
   Posts : 89
   Rep Power : 594
   Likes Received
   16
   Likes Given
   3

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Quote By Utingo View Post
   unaeleza nduto za u-ali nacha za kujenga kigamboni - by Lula wa Ndali Mwananzela
   Wale wale walioboronga watawezaje kujenga mji mpya wa kisasa?
   MOJAWAPO ya mipango mikubwa ya ujenzi wa jiji la kisasa, ni ule wa ujenzi wa Kigamboni kuwa jiji jipya la kisasa uliobuniwa na ambao unatarajiwa kutekelezwa chini ya Serikali ya CCM.
   Mpango huu mkubwa una lengo la kubadilisha eneo la Kigamboni kuwa jiji la kisasa kabisa likiwa na barabara kubwa za kila aina, majengo makubwa na maeneo ya makazi ambayo yataweza kuchukua karibu watu laki tano.
   Mradi huu mkubwa umetengenezewa hadi video ya kuupigia debe kwa wafadhili; huku ukionyesha mji wa ‘njozi” ambao unatakiwa kujengwa huko Kigamboni.
   Kwa watu wanaopenda njozi, mpango wa kuijenga Kigamboni kwa kiasi hicho unavutia hisia, unaburudisha vionjo na unachochea matamanio ya ‘Paradiso ya Bongo’.
   Kwa mtu yeyote ambaye amefuatilia kile kinachoitwa “Kigamboni New City Master Plan” anaweza kuona jinsi ambavyo watawala wetu walioshindwa wamejaribu kubuni kitu ambacho masikioni mwa watu kinasikika kuwa ni kizuri na ambacho jiji la Dar linakihitaji; yaani kulihahimisha jiji la Dar lilivyoborongwa sasa na kwenda kuanza kujenga upya ng’ambo ya Kigamboni.
   Katika mipango yao wanataka kuona kuwa Kigamboni ndio panakuwa kitovu cha maisha ya kisasa. Sasa hivi Kigamboni ina wakazi wapatao zaidi kidogo ya 80,000 na mradi huu mkubwa ukikamilika Kigamboni itakuwa na watu wapatao 500,000 ikiwa ni mji unaojitegemea ukihusisha maeneo ya viwanda, maofisi, makazi na maeneo wazi. Ni mpango ambao ukiangalia kwa haraka unaweza kuamini kuwa umefikiriwa kwa kina na utakuwa ni suluhisho la tatizo la jiji la Dar la sasa.
   Ndugu zangu, lengo kubwa lisilosemwa la kujenga hilo jiji jipya la Kigamboni ni kukubali kuwa watawala wetu wa leo wameshindwa kuboresha na kujenga jiji la Dar la sasa. Ni kukubali kuwa kufanya jiji la Dar la sasa kuwa la kisasa kumewashinda sasa wanataka kujaribu eneo jipya wakiamini kuwa wataweza.
   Gharama zake kwa muda mrefu zitazidi kwa mara mia nyingi sana gharama za kuwapatia watoto wa Kitanzania elimu ya bure kuanzia msingi hadi Chuo Kikuu kwa miaka mingi ijayo! Ukiwauliza Wizara ya Ardhi na wale wenye kuupigia debe ujenzi huu watuambie gharama zake ni kiasi gani, hakuna hata mmoja anayeweza kutuambia kwa sababu ni mji wa njozi ambao hauwezi kujengwa kama kwa kutengeneza kwa kompyuta. Miji haishushwi kama Yerusalemu ya Kitabu cha Ufunuo, hujengwa kwa jasho na kwa damu!
   Watawala wetu wa sasa walioshindwa wanataka wananchi wa Kigamboni na Jiji la Dar kuanza kufikiria kuwa Kigamboni itageuka kuwa mji wa njozi miaka michache ijayo. Kama miaka hamsini iliyopita tukiwa na “master plan” ya Jiji la Dar wameweza kuiboronga na kuharibu jiji hili lililochorwa tangu zamani kwa nini tunafikiria watu wale wale wataweza kujenga jiji jipya la kisasa pembeni?
   Ati wanapita na kuomba kura wakiwashawishi wananchi kuwa Kigamboni litakuwa jiji la kisasa! Na wapo wananchi ambao wameshasahau kujenga hilo daraja la Kigamboni tu ni karibu miaka 30 sasa tangu wazo lake lianze!
   Ninachosema ni kuwa mpango huu wa Serikali ya CCM kujenga Kigamboni kuwa jiji jipya una tatizo, na si tatizo dogo bali ni kubwa. Ni tatizo la maono, falsafa na la kimtazamo.
   Kwanza, kwa sababu jiji la Dar la sasa halijashindikana kujengwa kuwa jiji la kisasa. Ninaamini kabisa Jiji la Dar likijengwa upya, miundombinu ya kisasa na mfumo mzuri wa matumizi ya ardhi bado lina uwezo wa kuhimili karibu watu milioni kumi hivi.
   Kwa maneno mengine, ni kuwa jiji la Dar bado lina uwezo wa kutoa nafasi kwa yote yanayopendekezwa kufanyika Kigamboni ikiwemo ujenzi wa barabara za kisasa, maeneo mapya ya viwanda na ICT, na hata maeneo mapya ya makazi ya kisasa.
   Bado jiji la Dar lilivyo sasa lina mojawapo ya matumizi mabaya kabisa ya ardhi katika nchi ya watu walio huru na wenye dalili ya kuwa na akili timamu!
   Pili, waliobuni mpango huu wameshindwa kuelewa mojawapo ya matatizo makubwa ambayo yametokea mahali popote ambapo kuna tofauti kubwa ya kimaisha na kimaendeleo. Huwezi kuwa na eneo tajiri linaloishi karibu na eneo maskini bila kuwa na mvuto wa lazima kwa maskini kujitahidi kuhamia kwenye utajiri.
   Ni kwa sababu hiyo wananchi maskini wa Mexico (iliyo Kusini mwa Marekani) wamekuwa wakijitahidi kuingia Marekani ili kutafuta maisha kwani Mexico ni maskini kulinganisha na Marekani. Lakini huwezi kuona wananchi wa Canada (iliyo Kaskazini ya Marekani) wakihangaika kuingia Marekani kwa wingi kwani Canada ina utajiri mkubwa kuweza kuhimili mvuto wa utajiri wa Marekani.
   Huwezi kuwa na jiji jipya la kisasa Kilometa chache tu kutoka Manzese, Tandale, Magomeni na Dar ya zamani! Matajiri wa sasa wa Dar wakihamia Kigamboni mpya, maskani wa sasa wa Dar nao watahamia Kigamboni mpya!
   Tatu, kutokana na mpango wa kujenga eneo la kisasa na lenye nafasi za utajiri hapo Kigamboni, tatizo lile lile lililoikuta Dar ya sasa litakuja Kigamboni na hapatakuwa na pa kukimbilia.
   Kwa miaka mingi na toka enzi na enzi wananchi kutoka sehemu zote za Tanzania hata sehemu za nchi jirani wamekuwa wakikimbilia kuja Dar kutafuta maisha. Visa vimetungwa, hadithi zimesimuliwa na filamu zimetengenezwa juu ya jambo hili la eneo lililoendelea kuvuta maskini.
   Matokeo yake tumeona kuwa jiji la Dar ambalo lilibuniwa kwa watu chini ya milioni moja likichukua karibu watu milioni nne sasa. Hiyo Kigamboni ambayo inafikiriwa itachukua watu laki tano ni kwenye makaratasi tu ifanya hivyo kwani kwanza itakomba mamilioni ya watu wa Dar (kama nilivyosema hapo juu) lakini vile vile itavuta kundi jipya la watu kutoka bara na maeneo mengine kuja “kutafuta maisha”.
   Hivyo, idadi kuwa jiji hili litakuwa ni la watu wapatao laki tano tu ni kudanganyana mchana kweupe; kwani hakuna jiji duniani lililowahi kujengwa likaweza kuwa na idadi ya watu waliokusudiwa tu. Si New York, si Tokyo na si Lagos au Kuala Lumpur. Majiji hayo yote yamejikuta yakitafuta njia na mbinu za kudhibiti msongamano wa watu.
   Kwa nini basi kabla ya kuja na njozi ya Kigamboni Mpya wasituonyeshe kuwa wanaweza kukabiliana na ongezeko la watu kwenye jiji la Dar ya zamani?
   Nne, ni kuwa huu ni mpango mbovu mno kwa sababu Kigamboni kama ilivyo Dar ni karibu na miji mikubwa mitatu ambayo bado haijajaa na inaweza kabisa kumeza idadi ya watu wa Dar na kuacha eneo la Kigamboni kuwa eneo la makazi na maeneo ya wazi ya wananchi wa jiji la Dar kupumzikia.
   Kwanza, kuna Pwani (katika miji yake yote), ipo Tanga, na upo Morogoro. Kati ya maeneo hayo matatu ni eneo moja tu ambalo ninaamini, kama nilivyodokeza wiki iliyopita, laweza kujengwa kwa haraka zaidi, na likachukua nafasi ya jiji jipya nje ya Dar na ambalo halihitaji kuanzia sifuri kama wanavyotaka CCM huko Kigamboni.
   Ninaamini ni jiji la Tanga tu ambalo lina sifa za kuweza kuwa eneo jipya la kibiashara na kiuchumi kuliko Kigamboni.
   Kwanza, kwa sababu tayari lina miundo mbinu ya kuanzia na ambayo bado inaweza kuendelezwa kwa haraka zaidi kuliko kuanzia Kigamboni. Tanga kama mnavyojua ina umeme wa kudumu kutoka kwenye Gridi ya Taifa na vile vile una miji na mitaa ambayo tayari imepimwa na ambayo ni rahisi kuboreshwa au kupanuliwa.
   Pili, mji wa Tanga tayari una bandari na eneo zuri kwa viwanda vya kisasa ukiwa na reli ambayo imeshaunganishwa kwenda sehemu yoyote ya Tanzania. Kwa maneno mengine, hata vikianza kujengwa viwanda kwa upya au mpango ambao niliudokeza wa CHADEMA kuhusu mambo ya TEKINOHAMA Tanga bado ina uwezo hata wa kuipiku Dar kuwa jiji la kisasa zaidi.
   Tatu, Tanga ni mji ambao unaweza kufikika kiurahisi na kwa haraka kutokea Dar. Badala ya kuanza ujenzi mpya wa mabarabara ya kwenda ‘mbinguni’ huko Dar au Kigamboni, kwa sasa inahitajika ujenzi wa barabara kubwa ya kisasa kuunganisha Tanga na Dar na hivyo kufanya usafiri kutoka Dar kuja Tanga kuwa ni wa muda mfupi zaidi.
   Kwa hesabu za haraka haraka kama nilivyoonesha wiki iliyopita, treni la haraka (express) lisilotumia umeme laweza kufika Dar kutoka Tanga ndani ya saa moja na nusu. Ukijumlisha muda ambao watu wanatumia leo hii kutoka maeneo ya Dar kufika mjini utaona kuwa mtu anaweza kutoka Tanga akafika Dar mapema zaidi kuliko mtu anayetoka Mbezi ya Kimara kufika katikati ya jiji!
   Hii ina maana tukiboresha usafiri wa treni kati ya miji hii miwili mtu anaweza kuishi Tanga na kufanya kazi Dar au kinyume chake!
   Nne, wakati jiji la Dar lina ukubwa wa Kilomita za mraba 1590 (maili za mraba 614) mji wa Tanga una Kilomita za mraba zipatazo 1000 hivi (za jiji la sasa na ardhi). Idadi ya watu hata hivyo ina tofauti kubwa sana. Dar es Salaam inakaribia (au kupita kidogo) watu milioni 3 wakati mji wa Tanga una watu chini ya laki mbili na nusu.
   Hii ina maana msongamano wa watu kwenye jiji la Tanga ni karibu watu 453/Km2 wakati jiji la Dar kwa Kilometa moja ya mraba ina watu 1760. Kwa maneno mengine, hata tukiongeza idadi ya watu 500,000 (wanaopendekezwa kuhamia Kigamboni) kwenye mji wa Tanga na kufanya idadi yake ya watu iwe 750,000 bado mji wa Tanga utakuwa na wastani wa watu 750 kwa kila Kilomita ya mraba!! Bado haitakuwa imefikia msongamano wa watu ulivyo sasa kwenye jiji la Dar! Sasa kwa nini tujenge Kigamboni?
   Hapa ndipo ninapoona kuwa mpango huu wa CCM kama ulivyoanishwa katika Ilani yao 60:b(iv) una walakini - tena mkubwa. Wao wanasema wakichaguliwa mojawapo ya mpango wao ni “Kuanzisha mji wa kisasa wa Kigamboni (“Kigamboni New City)”.
   Hawatuambii watauanzisha lini, kwa gharama gani na fedha zitatoka wapi. Hawatuambii kuwa ni mpango utakaochukua miaka karibu themanini ijayo au mia moja au mitano ijayo na utawezekana vipi kama watendaji na wanasiasa ni wale wale!
   Na utafanikiwa vipi hasa kama ufisadi ambalo ndilo tatizo kubwa zaidi la maendeleo yetu utaendelea kuhofiwa hata kutajwa kwa jina kwenye kampeni zao.
   Sasa watu wa Dar wamepewa uchaguzi wa wazi. Jiji la Dar linahitaji mabadiliko tena ya haraka. Kigamboni kunahitaji kuendelezwa na kuwa ni eneo la kisasa. Ni vizuri wananchi wa Dar wawaulize wagombea wa vyama vingine kuhusu jinsi gani wataliboresha jiji la Dar na jinsi gani eneo la Kigamboni litaendelezwa.
   Natumaini mojawapo ya vyama vya upinzani vitaweza kuangalia wazo langu la kuiendeleza Tanga na kuufutilia mbali mpango wao wa mji wa njozini wa Kigamboni. Na mkumbuke nimeelezea upande wa Tanga tu sijagusa ile miji mingine ya karibu ya Morogoro na maeneo ya Pwani!
   Waliobuni na wanaoutetea mpango wa Kigamboni ni watu waliokosa fikra za utatuzi wa matatizo ya Jiji la Dar. Wanaoniudhi zaidi ni wananchi wa Jiji la Dar ambao wanapenda kugereshwa kirahisi na watasimama mistarini Oktoba 31 kuwachagua watu wale wale wenye fikra zile zile zilizoshindwa.

   MINCING YOUR WORDS MAKES IT EASIER IF YOU HAVE TO EAT THEM LATER.

  7. #7
   Bujibuji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th February 2009
   Location : NYUMBANI PANONO
   Posts : 23,631
   Rep Power : 51528095
   Likes Received
   12921
   Likes Given
   10024

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Mwaka huu tutayasikia mengi.
   KAZI NDIO MSINGI WA MAENDELEO. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MSINGI WA FEDHA. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE- J. K. NYERERE

  8. #8
   Pasco's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd September 2008
   Posts : 17,179
   Rep Power : 400120006
   Likes Received
   16003
   Likes Given
   73180

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Quote By Safari_ni_Safari View Post
   Lula wa Ndali Mwananzela ni nani kwani? Toka jana anatajwatajwa humu.....mtujuve jamani
   Safari_ni_Safari, huyu Lula wa Ndali Mwananzela, ni mwandishi wa makala kwenye magazeti mbalimbali, sikumbuki nilianza kumsoma gazeti gani, lakini kwa sasa, huandika makala zake kwenye gazeti la Raia Mwema linalotoka kila Jumatano.

   Ushauri wa bure: tujikite zaidi kwenye uchambuzi wa anachoandika mwandishi fulani, kuliko kutaka sana kumjua mwandishi fulani ni nani.
   Kwa kutaka kumjua-ni simple mind-Discuss People.

   Kwa kununua gazeti na kulisoma au kuisoma na kusema umesoma, hiyo ni event, tukio la kusoma hivyo kuidiscus makala uliyoisoma, hiyo ni Orninary Mind-Discuss events, matukio etc.

   Kwa kuzama deep ndani ya makala, yaani baada ya kuisoma, ukaitafakari, ukaja na mawazo yako ya jinsi ulivyoielewa, hapa unakuwa una discuss ideas za makala husika hii ndio Great Mind-Discuss ideas, na hivi ndivyo JF ilivyokuwa imedhamiria iwe, theb home of Great Thinkers!

   Kwa vile huu ni ukumbi huru, ni ukumbi wa watu,
   lets all keep being together, simple mind, ordinary mind na great minds pamoja!

  9. Kicheruka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd February 2009
   Posts : 793
   Rep Power : 814
   Likes Received
   84
   Likes Given
   10

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Quote By TATE View Post
   Wale wale walioboronga watawezaje kujenga mji mpya wa kisasa?
   MOJAWAPO ya mipango mikubwa ya ujenzi wa jiji la kisasa, ni ule wa ujenzi wa Kigamboni kuwa jiji jipya la kisasa uliobuniwa na ambao unatarajiwa kutekelezwa chini ya Serikali ya CCM.
   Mpango huu mkubwa una lengo la kubadilisha eneo la Kigamboni kuwa jiji la kisasa kabisa likiwa na barabara kubwa za kila aina, majengo makubwa na maeneo ya makazi ambayo yataweza kuchukua karibu watu laki tano.
   Mradi huu mkubwa umetengenezewa hadi video ya kuupigia debe kwa wafadhili; huku ukionyesha mji wa ‘njozi” ambao unatakiwa kujengwa huko Kigamboni.
   Kwa watu wanaopenda njozi, mpango wa kuijenga Kigamboni kwa kiasi hicho unavutia hisia, unaburudisha vionjo na unachochea matamanio ya ‘Paradiso ya Bongo’.
   Kwa mtu yeyote ambaye amefuatilia kile kinachoitwa “Kigamboni New City Master Plan” anaweza kuona jinsi ambavyo watawala wetu walioshindwa wamejaribu kubuni kitu ambacho masikioni mwa watu kinasikika kuwa ni kizuri na ambacho jiji la Dar linakihitaji; yaani kulihahimisha jiji la Dar lilivyoborongwa sasa na kwenda kuanza kujenga upya ng’ambo ya Kigamboni.
   Katika mipango yao wanataka kuona kuwa Kigamboni ndio panakuwa kitovu cha maisha ya kisasa. Sasa hivi Kigamboni ina wakazi wapatao zaidi kidogo ya 80,000 na mradi huu mkubwa ukikamilika Kigamboni itakuwa na watu wapatao 500,000 ikiwa ni mji unaojitegemea ukihusisha maeneo ya viwanda, maofisi, makazi na maeneo wazi. Ni mpango ambao ukiangalia kwa haraka unaweza kuamini kuwa umefikiriwa kwa kina na utakuwa ni suluhisho la tatizo la jiji la Dar la sasa.
   Ndugu zangu, lengo kubwa lisilosemwa la kujenga hilo jiji jipya la Kigamboni ni kukubali kuwa watawala wetu wa leo wameshindwa kuboresha na kujenga jiji la Dar la sasa. Ni kukubali kuwa kufanya jiji la Dar la sasa kuwa la kisasa kumewashinda sasa wanataka kujaribu eneo jipya wakiamini kuwa wataweza.
   Gharama zake kwa muda mrefu zitazidi kwa mara mia nyingi sana gharama za kuwapatia watoto wa Kitanzania elimu ya bure kuanzia msingi hadi Chuo Kikuu kwa miaka mingi ijayo! Ukiwauliza Wizara ya Ardhi na wale wenye kuupigia debe ujenzi huu watuambie gharama zake ni kiasi gani, hakuna hata mmoja anayeweza kutuambia kwa sababu ni mji wa njozi ambao hauwezi kujengwa kama kwa kutengeneza kwa kompyuta. Miji haishushwi kama Yerusalemu ya Kitabu cha Ufunuo, hujengwa kwa jasho na kwa damu!
   Watawala wetu wa sasa walioshindwa wanataka wananchi wa Kigamboni na Jiji la Dar kuanza kufikiria kuwa Kigamboni itageuka kuwa mji wa njozi miaka michache ijayo. Kama miaka hamsini iliyopita tukiwa na “master plan” ya Jiji la Dar wameweza kuiboronga na kuharibu jiji hili lililochorwa tangu zamani kwa nini tunafikiria watu wale wale wataweza kujenga jiji jipya la kisasa pembeni?
   Ati wanapita na kuomba kura wakiwashawishi wananchi kuwa Kigamboni litakuwa jiji la kisasa! Na wapo wananchi ambao wameshasahau kujenga hilo daraja la Kigamboni tu ni karibu miaka 30 sasa tangu wazo lake lianze!
   Ninachosema ni kuwa mpango huu wa Serikali ya CCM kujenga Kigamboni kuwa jiji jipya una tatizo, na si tatizo dogo bali ni kubwa. Ni tatizo la maono, falsafa na la kimtazamo.
   Kwanza, kwa sababu jiji la Dar la sasa halijashindikana kujengwa kuwa jiji la kisasa. Ninaamini kabisa Jiji la Dar likijengwa upya, miundombinu ya kisasa na mfumo mzuri wa matumizi ya ardhi bado lina uwezo wa kuhimili karibu watu milioni kumi hivi.
   Kwa maneno mengine, ni kuwa jiji la Dar bado lina uwezo wa kutoa nafasi kwa yote yanayopendekezwa kufanyika Kigamboni ikiwemo ujenzi wa barabara za kisasa, maeneo mapya ya viwanda na ICT, na hata maeneo mapya ya makazi ya kisasa.
   Bado jiji la Dar lilivyo sasa lina mojawapo ya matumizi mabaya kabisa ya ardhi katika nchi ya watu walio huru na wenye dalili ya kuwa na akili timamu!
   Pili, waliobuni mpango huu wameshindwa kuelewa mojawapo ya matatizo makubwa ambayo yametokea mahali popote ambapo kuna tofauti kubwa ya kimaisha na kimaendeleo. Huwezi kuwa na eneo tajiri linaloishi karibu na eneo maskini bila kuwa na mvuto wa lazima kwa maskini kujitahidi kuhamia kwenye utajiri.
   Ni kwa sababu hiyo wananchi maskini wa Mexico (iliyo Kusini mwa Marekani) wamekuwa wakijitahidi kuingia Marekani ili kutafuta maisha kwani Mexico ni maskini kulinganisha na Marekani. Lakini huwezi kuona wananchi wa Canada (iliyo Kaskazini ya Marekani) wakihangaika kuingia Marekani kwa wingi kwani Canada ina utajiri mkubwa kuweza kuhimili mvuto wa utajiri wa Marekani.
   Huwezi kuwa na jiji jipya la kisasa Kilometa chache tu kutoka Manzese, Tandale, Magomeni na Dar ya zamani! Matajiri wa sasa wa Dar wakihamia Kigamboni mpya, maskani wa sasa wa Dar nao watahamia Kigamboni mpya!
   Tatu, kutokana na mpango wa kujenga eneo la kisasa na lenye nafasi za utajiri hapo Kigamboni, tatizo lile lile lililoikuta Dar ya sasa litakuja Kigamboni na hapatakuwa na pa kukimbilia.
   Kwa miaka mingi na toka enzi na enzi wananchi kutoka sehemu zote za Tanzania hata sehemu za nchi jirani wamekuwa wakikimbilia kuja Dar kutafuta maisha. Visa vimetungwa, hadithi zimesimuliwa na filamu zimetengenezwa juu ya jambo hili la eneo lililoendelea kuvuta maskini.
   Matokeo yake tumeona kuwa jiji la Dar ambalo lilibuniwa kwa watu chini ya milioni moja likichukua karibu watu milioni nne sasa. Hiyo Kigamboni ambayo inafikiriwa itachukua watu laki tano ni kwenye makaratasi tu ifanya hivyo kwani kwanza itakomba mamilioni ya watu wa Dar (kama nilivyosema hapo juu) lakini vile vile itavuta kundi jipya la watu kutoka bara na maeneo mengine kuja “kutafuta maisha”.
   Hivyo, idadi kuwa jiji hili litakuwa ni la watu wapatao laki tano tu ni kudanganyana mchana kweupe; kwani hakuna jiji duniani lililowahi kujengwa likaweza kuwa na idadi ya watu waliokusudiwa tu. Si New York, si Tokyo na si Lagos au Kuala Lumpur. Majiji hayo yote yamejikuta yakitafuta njia na mbinu za kudhibiti msongamano wa watu.
   Kwa nini basi kabla ya kuja na njozi ya Kigamboni Mpya wasituonyeshe kuwa wanaweza kukabiliana na ongezeko la watu kwenye jiji la Dar ya zamani?
   Nne, ni kuwa huu ni mpango mbovu mno kwa sababu Kigamboni kama ilivyo Dar ni karibu na miji mikubwa mitatu ambayo bado haijajaa na inaweza kabisa kumeza idadi ya watu wa Dar na kuacha eneo la Kigamboni kuwa eneo la makazi na maeneo ya wazi ya wananchi wa jiji la Dar kupumzikia.
   Kwanza, kuna Pwani (katika miji yake yote), ipo Tanga, na upo Morogoro. Kati ya maeneo hayo matatu ni eneo moja tu ambalo ninaamini, kama nilivyodokeza wiki iliyopita, laweza kujengwa kwa haraka zaidi, na likachukua nafasi ya jiji jipya nje ya Dar na ambalo halihitaji kuanzia sifuri kama wanavyotaka CCM huko Kigamboni.
   Ninaamini ni jiji la Tanga tu ambalo lina sifa za kuweza kuwa eneo jipya la kibiashara na kiuchumi kuliko Kigamboni.
   Kwanza, kwa sababu tayari lina miundo mbinu ya kuanzia na ambayo bado inaweza kuendelezwa kwa haraka zaidi kuliko kuanzia Kigamboni. Tanga kama mnavyojua ina umeme wa kudumu kutoka kwenye Gridi ya Taifa na vile vile una miji na mitaa ambayo tayari imepimwa na ambayo ni rahisi kuboreshwa au kupanuliwa.
   Pili, mji wa Tanga tayari una bandari na eneo zuri kwa viwanda vya kisasa ukiwa na reli ambayo imeshaunganishwa kwenda sehemu yoyote ya Tanzania. Kwa maneno mengine, hata vikianza kujengwa viwanda kwa upya au mpango ambao niliudokeza wa CHADEMA kuhusu mambo ya TEKINOHAMA Tanga bado ina uwezo hata wa kuipiku Dar kuwa jiji la kisasa zaidi.
   Tatu, Tanga ni mji ambao unaweza kufikika kiurahisi na kwa haraka kutokea Dar. Badala ya kuanza ujenzi mpya wa mabarabara ya kwenda ‘mbinguni’ huko Dar au Kigamboni, kwa sasa inahitajika ujenzi wa barabara kubwa ya kisasa kuunganisha Tanga na Dar na hivyo kufanya usafiri kutoka Dar kuja Tanga kuwa ni wa muda mfupi zaidi.
   Kwa hesabu za haraka haraka kama nilivyoonesha wiki iliyopita, treni la haraka (express) lisilotumia umeme laweza kufika Dar kutoka Tanga ndani ya saa moja na nusu. Ukijumlisha muda ambao watu wanatumia leo hii kutoka maeneo ya Dar kufika mjini utaona kuwa mtu anaweza kutoka Tanga akafika Dar mapema zaidi kuliko mtu anayetoka Mbezi ya Kimara kufika katikati ya jiji!
   Hii ina maana tukiboresha usafiri wa treni kati ya miji hii miwili mtu anaweza kuishi Tanga na kufanya kazi Dar au kinyume chake!
   Nne, wakati jiji la Dar lina ukubwa wa Kilomita za mraba 1590 (maili za mraba 614) mji wa Tanga una Kilomita za mraba zipatazo 1000 hivi (za jiji la sasa na ardhi). Idadi ya watu hata hivyo ina tofauti kubwa sana. Dar es Salaam inakaribia (au kupita kidogo) watu milioni 3 wakati mji wa Tanga una watu chini ya laki mbili na nusu.
   Hii ina maana msongamano wa watu kwenye jiji la Tanga ni karibu watu 453/Km2 wakati jiji la Dar kwa Kilometa moja ya mraba ina watu 1760. Kwa maneno mengine, hata tukiongeza idadi ya watu 500,000 (wanaopendekezwa kuhamia Kigamboni) kwenye mji wa Tanga na kufanya idadi yake ya watu iwe 750,000 bado mji wa Tanga utakuwa na wastani wa watu 750 kwa kila Kilomita ya mraba!! Bado haitakuwa imefikia msongamano wa watu ulivyo sasa kwenye jiji la Dar! Sasa kwa nini tujenge Kigamboni?
   Hapa ndipo ninapoona kuwa mpango huu wa CCM kama ulivyoanishwa katika Ilani yao 60:b(iv) una walakini - tena mkubwa. Wao wanasema wakichaguliwa mojawapo ya mpango wao ni “Kuanzisha mji wa kisasa wa Kigamboni (“Kigamboni New City)”.
   Hawatuambii watauanzisha lini, kwa gharama gani na fedha zitatoka wapi. Hawatuambii kuwa ni mpango utakaochukua miaka karibu themanini ijayo au mia moja au mitano ijayo na utawezekana vipi kama watendaji na wanasiasa ni wale wale!
   Na utafanikiwa vipi hasa kama ufisadi ambalo ndilo tatizo kubwa zaidi la maendeleo yetu utaendelea kuhofiwa hata kutajwa kwa jina kwenye kampeni zao.
   Sasa watu wa Dar wamepewa uchaguzi wa wazi. Jiji la Dar linahitaji mabadiliko tena ya haraka. Kigamboni kunahitaji kuendelezwa na kuwa ni eneo la kisasa. Ni vizuri wananchi wa Dar wawaulize wagombea wa vyama vingine kuhusu jinsi gani wataliboresha jiji la Dar na jinsi gani eneo la Kigamboni litaendelezwa.
   Natumaini mojawapo ya vyama vya upinzani vitaweza kuangalia wazo langu la kuiendeleza Tanga na kuufutilia mbali mpango wao wa mji wa njozini wa Kigamboni. Na mkumbuke nimeelezea upande wa Tanga tu sijagusa ile miji mingine ya karibu ya Morogoro na maeneo ya Pwani!
   Waliobuni na wanaoutetea mpango wa Kigamboni ni watu waliokosa fikra za utatuzi wa matatizo ya Jiji la Dar. Wanaoniudhi zaidi ni wananchi wa Jiji la Dar ambao wanapenda kugereshwa kirahisi na watasimama mistarini Oktoba 31 kuwachagua watu wale wale wenye fikra zile zile zilizoshindwa.

   Makala ni nzuri sana na imechambuliwa kiitaalamu. Najiuliza kama serikali imeshindwa kujenga na kuhamia makao makuu Dodoma, Je Kigamboni itaweza? Kweli hizi ni njozi

  10. #10
   TATE's Avatar
   Member Array
   Join Date : 11th August 2010
   Posts : 89
   Rep Power : 594
   Likes Received
   16
   Likes Given
   3

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Ilo wazo la kuendeleza mji wa Tanga kwa kweli limenitamanisha.
   MINCING YOUR WORDS MAKES IT EASIER IF YOU HAVE TO EAT THEM LATER.

  11. pat john's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 31st March 2009
   Posts : 245
   Rep Power : 697
   Likes Received
   37
   Likes Given
   9

   Default Re: Toleo la Raia Mwema la leo..

   Wakazi wa Kigamboni walitoa ujumbe kwa JK, kwamba njozi zake azipeleke kwao Bagamoyo. Inashangaza kwa kweli kuona badala ya kutumia rasilmali nyingi kujenga mahitaji ya wananchi tunaibuka na njozi za miji ya kisasa, wakati iliyopo sasa hivi inatushinda. Kumbuka hata hiyo msasani na upanga ilitarajiwa kuwa miji ya kisasa lakini tumeambulia patupu. Tuanze kwa kuheshimu mipango bora ya ardhi ndipo tuote habari ya miji ya kisasa.

  Similar Topics

  1. Mwandishi 'Msomaji raia' wa Raia Mwema
   By The Boss in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 21
   Last Post: 5th December 2012, 16:16
  2. Toleo la Raia Mwema la Kesho leo..
   By Mzee Mwanakijiji in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 6
   Last Post: 23rd October 2011, 01:12
  3. Msomaji raia wa raia mwema analipwa na slaa?
   By kakadeo in forum Uchaguzi Tanzania
   Replies: 21
   Last Post: 7th October 2010, 12:13
  4. Na Raia Mwema nalo....
   By Mzee Mwanakijiji in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 49
   Last Post: 6th June 2008, 00:54

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...