Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Faida za Kufunga

    Report Post
    Results 1 to 16 of 16
    1. #1
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,859
      Rep Power : 7687
      Likes Received
      1467
      Likes Given
      0

      Default Faida za Kufunga

      WAISLAMU kwa ujumla bado wanaendelea kutimiza nguzo ya nne ya Uislamu ya Funga katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan...

      Kuna faida za mwenye kufunga kiimani na kiafya, kwa sababu wapo baadhi ya watu hufikiria kufunga ni mateso au manyanyaso kwa mfungaji.

      Faida za kufunga zipo nyingi, miongoni mwao ni kutekeleza mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu alizotuteremshia na faida ya utekelezaji huu ni kuingia peponi siku ya mwisho.

      Faida ya pili ya mfungaji wa swaumu ni kujizoesha kuwa na subira, yaani katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mtu anajifunza jinsi ya kuwa mvumilivu na kustahamili njaa, kiu na matamanio ya kimwili.

      Mtume Mohammad (SAW) anausifia mwezi huu kwa kusema, “Huo mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kusubiri na hakika subira malipo yake ni pepo.”

      Faida ya tatu kwa mfungaji ni kuwa muadilifu na kujifundisha usawa baina ya tajiri na maskini.

      Kwa hali ya kawaida tajiri ni nadra kushinda njaa, hivyo basi pindi anapokuwa katika swaumu anajua machungu ya njaa hata anapotembelewa na maskini akiombwa msaada na mtu huyo mwenye njaa aweze kumsaidia kirahisi akiwa anafahamu namna njaa inavyouma.

      Inakuwa vigumu kwa tajiri ambaye hajawahi kushinda njaa kusikia uchungu na kuwa mwepesi kumsaidia mwenye njaa kwa sababu anachukulia kama njaa ni jambo la kawaida.

      Kuhusu hilo la kufunga, lmam Ja'far Assadiq, amelizungumzia na kusema, “Hakika si jingine, Mwenyezi Mungu amefaradhisha kufunga ili tajiri na maskini wapate kulingana (katika shida ya njaa na kiu), basi akapenda viumbe vyake wawe sawa na amuonjeshe tajiri maumivu ya kushikwa na njaa ili apate kumhurumia mnyonge na apate kumsikitikia mwenye njaa.”

      Faida ya nne na ambayo ni muhimu zaidi wanayoitegemea ni kusamehewa dhambi yote ya mwaka ikiwa mwenye kufunga amefuata masharti yote na kufunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mtume Muhammad (S.A.W).
      Anasema, “Enyi watu! Hakika umewaelekeeni nyinyi Mwezi wa Ramadhani kwa baraka, rehema na msamaha, mwezi ambao ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko miezi yote, siku zake ni bora kuliko siku zote, masiku yake ni bora kuliko masiku mengine yote na saa yake ni bora na muhimu kuliko saa zote.”

      Hivyo kutokana na maneno hayo Mtume Muhammad (S.A.W), anaonyesha kufunga kwa Muislam katika mwezi huu ni bora na heri kwake.


      Kwanini swaumu ina thawabu kubwa?

      Hii inatokana na kuwa muumini anapokuwa anaswali, lazima wanadamu watakuona, ukienda kuhiji Makka lazima utaonekana na ukitoa zaka muhusika uliyempa atajua, lakini ukifunga ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayejua kama kweli utakuwa umefunga au la.

      Qur'an inasema kwamba kwa aliyefunga hastahili kujionyesha kwa vitendo vya kuonyesha unyonge, hali ya kukasirika mithili ya mtu aliyeudhiana na watu na isitoshe awe mkarimu kwa watumishi wake hadi watu wengine wa nje.

      Kitabu kinachojulikana kwa jina la ‘Wasa-ilu-sh-shia’ kinazungumzia hadithi iliyopokelewa na imamu wa sita, Imaam As-Saadiq inayosema kwamba : “Mwenye kufunga swaumu anakuwa katika ibada, hata kama atakuwa amelala, anapata thawabu ya ibada ikiwa hakumsema mtu.”

      Pia imepokelewa hadithi na Imaam As-Sadiq inayesema kwamba: “Mwenye kuificha swaumu asijitangaze kwa wengine kuwa amefunga, basi Mwenyezi Mungu atawahubiri malaika hivi “Kiumbe wangu ametakiwa alindwe na adhabu yangu, basi mlindeni na malaika watakulinda.”
      Faida ya tano ya Swaumu inahusu upande wa afya zetu, kwa kawaida chochote kifanyacho kazi sharti kipumzike kwa muda, hii inajumuisha hata kwa upande wa mitambo.

      Kwa mfano, mitambo ambayo imeundwa kwa vyuma imara tena vyenye nguvu hufika wakati ambao hulazimika kusimamishwaa kwa marekebisho ili kuiendesha kwa ubora.

      Swali hapa linakuja, kwa nini sisi ambao tumeumbwa dhaifu tusivipumzishe viungo vyetu, hasa tumbo ambalo huendelea na kazi mfululizo kwa miezi 11? Hapo utauona ulazima wa kupumzisha matumbo yetu ili kuhifadhi afya zetu.

      Kuhusu hilo la kusaidia kiafya hata madaktari wakubwa duniani wamewahi kulizungumzia hilo la kufunga.

      Baadhi ya madaktari wakuu ulimwenguni, wamekaririwa wakithibitisha kuwa kufunga kuna faida kwa mfungaji na hata Mtume Mohammad (S.A.W.) anathibitisha hilo pale anaposema, “Fungeni ili mpate afya nzuri.”

      Naye Imam Ja'far (A.S) anasema, “Kila kitu kina utakaso, kitakaso cha mwili ni kufunga (Swaumu).”

      Kwa mujibu wa daktari mmoja mkubwa kutoka Marekani, Dk. Car, amewahi kusema, “Ni wajibu juu ya kila mgonjwa ajizuie kula japokuwa kwa muda wa siku moja katika kila mwaka.”

      Dk. Car katika maelezo yake aliongeza, “Vijidudu viambukizavyo maradhi huendelea na kunawiri pale mwenye mwili anapoendelea kula na kuvilisha, hivyo basi vitaendelea kukua.’’

      Baadhi ya madaktari Waislamu na wasio Waislamu wameafiki shauri hili.

      Naye Dk. Abdul Aziz bin Ismail anadai kwamba kufunga siku moja ni kinga ya maradhi kwa mwaka.

      Isitoshe kwa siku za hivi karibuni, kuna hospitali mbalimbali zinazohimiza na kusisitiza umuhimu huu, kadhalika mara nyingi tunashuhudia wagonjwa wengi ambao huzuiwa kula kwa manufaa ya afya zao.

      Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Cairo, Dk. Muhammad Dhawahir, anasema: “Ugonjwa wa kuzidi maji mwilini, unene, moyo, ini, pafu na mengineyo huzuiwa kwa mtu kufunga Swaumu.”
      MziziMkavu likes this.
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)


    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,178
      Rep Power : 19208
      Likes Received
      8121
      Likes Given
      26593

      Default Re: Faida za Kufunga

      Kufunga kuna Faida nyingi sana kwa afya ya Binadamu haswa kwa hao wanaofunga huu mwezi wa Ramadhani.

      185. Na siku hizi ni za mwezi wa Ramadhani (1) mwezi wenye daraja tukufu kwa Mwenyezi Mungu ndipo ilipo teremshwa Qur'ani ili kuwaongoa watu wote kwa hoja zake zilizo wazi zinazo fikishia kheri, na zenye kutenga baina ya Haki na baat'ili kwa nyakati zote na vizazi vyote. Basi mwenye kuuwahi mwezi huu naye ni mzima, si mgonjwa, yupo mjini si msafiri, yampasa afunge Saumu. Na aliye mgonjwa anaye dhurika kwa kufunga au alioko safarini anaweza kula, na juu yake kuzilipa zile siku alizo kula kwa kufunga utapo ondoka udhuru. Kwani Mwenyezi Mungu hataki kuwapatisha watu mashaka na taklifa bali Yeye anapenda kuwafanyia watu sahala. Na Mwenyezi Mungu amekubainishieni Mwezi wa Saumu, na amekuongoeni ili mpate kutimiza siku za kufunga, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa uwongofu alio kuongoeni, na akakupeni tawfiki njema.
      (1) Imethibiti kwa matibabu ya kisasa kuwa Saumu kwa namna ya Qur'ani ina faida nyingi, katika hizo ni kuwa inasaidia katika kutibu maradhi ya sukari, inatengeneza matumbo, inapunguza maumivu ya viungo, na maradhi ya moyo, inapumzisha nyama za mwili, na inasafisha uchafu mwingi wenye madhara, na pia inakuwa ni kinga kwa maradhi mengi mengineyo. Je, vipi kwa mtu asiye jua kusoma na kuandika ayajue yote haya?
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    4. #3
      BabaDesi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2007
      Posts : 2,378
      Rep Power : 1083
      Likes Received
      250
      Likes Given
      1387

      Default Re: Faida za Kufunga

      ...Huku kufunga kwa upande wa kidini sina neno nako. lakini kwa upande wa kiafya ninatatizika na pale tumbo linapokuwa halina kitu siku nzima halafu jioni unakula mchanganyiko wa sukari, pilipili, chumvi, mafuta, vyakula laini na vigumu at once. halafu usiku wa manane tena. Hii imekaaje? Haina athari kwa kile ulichotegemea kupata kiafya kwa kufunga?

    5. #4
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,859
      Rep Power : 7687
      Likes Received
      1467
      Likes Given
      0

      Default Re: Faida za Kufunga

      Quote By BabaDesi
      ...Huku kufunga kwa upande wa kidini sina neno nako. lakini kwa upande wa kiafya ninatatizika na pale tumbo linapokuwa halina kitu siku nzima halafu jioni unakula mchanganyiko wa sukari, pilipili, chumvi, mafuta, vyakula laini na vigumu at once. halafu usiku wa manane tena. Hii imekaaje? Haina athari kwa kile ulichotegemea kupata kiafya kwa kufunga?
      Unapaswa uangalie chakula unacho kula na pia uligawe tumbo lako sehemu tatu, sehemu ya chakula, pili sehemu ya maji, na tatu sehemu ya hewa, na si kupapia mavyakula kama vile kesho hakuna kula tena.
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)


    6. #5
      bona's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th November 2009
      Location : tanzania
      Posts : 982
      Rep Power : 681
      Likes Received
      85
      Likes Given
      235

      Default Re: Faida za Kufunga

      binafsi si mwislam napenda zaidi niongelee ktk upande usio wa kiimani yaani realistic coz kiiman vitu vingi si realistic, kufunga 30days to be honest ina shape vizuri mwili wako kiafya, kama kila mwaka unaweza funga kwa siku 30 nadhan unanafasi ya mwili wako kua ktk hali nzuri throughout the yr! hongereni waislam kwa hili mnaweka miili yenu vizuri!
      MziziMkavu likes this.
      ... if it is a Miracle, any sort of evidence will answer, but if it is a Fact, proof is necessary.

    7. Miaka 50

    8. #6
      SILENT WHISPER's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 2,046
      Rep Power : 917
      Likes Received
      572
      Likes Given
      159

      Default Re: Faida za Kufunga

      waislam hawafungi siku nzima...! wanakula usiku. wanafunga mchana.

      semeni ukweli..! kufunga alifunga Yesu tu.!
      POLITICIAN, ONE WHO SHAKES YOUR HAND BEFORE ELECTION AND YOUR CONFIDENCE LATER

    9. #7
      Mshirazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th December 2009
      Posts : 428
      Rep Power : 566
      Likes Received
      31
      Likes Given
      45

      Default Re: Faida za Kufunga

      Quote By SILENT WHISPER
      waislam hawafungi siku nzima...! wanakula usiku. wanafunga mchana.

      semeni ukweli..! kufunga alifunga Yesu tu.!
      Umenena yaliyokweli,,Waislamu hatufungi siku nzima, tunafunga linapochomoza jua asubuhi hadi linapozama,, hivyo ndivyo tulivyoambiwa.
      Bila shaka ISSA (AS) nae alielekezwa kufunga hivyo alivyofunga. kikubwa hapa ni kuonesha UTIIFU (kufuata maamrisho)

    10. #8
      Majala Kimolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2007
      Posts : 316
      Rep Power : 666
      Likes Received
      26
      Likes Given
      31

      Default Re: Faida za Kufunga

      Quote By SILENT WHISPER
      waislam hawafungi siku nzima...! wanakula usiku. wanafunga mchana.

      semeni ukweli..! kufunga alifunga Yesu tu.!
      Ndio kufunga huko kwa maana na uelewa. Hapa inategemea utaratibu wa utekelezaji. Kwaresma (nikosoe kama nimekosea silabi) ina utaratibu wake na huitwa funga. Kufunga maana yake ni kujizuia na si lazima iwe kula na kunywa, hata kuongea pia yaweza kuwa funga. Muda na kitu cha kujizuia ndio kinachotofautisha wafungaji.
      Ili kutofautisha hayo unatakiwa kujua utaratibu unaotumika
      Upo hapo mkuu?

    11. #9
      Ndibalema's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th April 2008
      Location : Mbagala
      Posts : 6,595
      Rep Power : 2000
      Likes Received
      1628
      Likes Given
      1610

      Default Re: Faida za Kufunga

      Quote By SILENT WHISPER
      waislam hawafungi siku nzima...! wanakula usiku. wanafunga mchana.

      semeni ukweli..! kufunga alifunga Yesu tu.!
      Mbona hueleweki ndugu yangu!!
      mara hawafungi, mara wanafunga mchana.
      Tukuelewe lipi??
      "Makalio ya sufuria hayaogopi moto"

    12. #10
      Kabonde's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th August 2008
      Posts : 417
      Rep Power : 633
      Likes Received
      18
      Likes Given
      66

      Default Re: Faida za Kufunga

      Waislamu hawafungi wanachofanya ni kugeuza usiku kuwa mchana na mchana kuwa usiku.Mijitu inaamka sanane za usiku inabugia mivyakula utadhani wanaachana na kula maisha hamna kitu waache kudanganya watu.Hakuna mtu aliwahi kufunga hapa dunia zaidi ya Yesu mwana wa Mungu wengine wanajaribu kidogo sana lakini waislamu hawafungu na hawajawihi kufunga hata siku moja.Kwanza ukifunga hutakiwi kumtangazia mtu lauka kama ukimtangazia mtu tayari umeshapata thawabu zako kwa mtu uliye mtangazia.Waislamu wanapoutangazia ulimwengu wameanzakufunga wanakuwa wamekiuka kanuni muhimu ya ufungaji

    13. #11
      Gaijin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2007
      Posts : 11,319
      Rep Power : 12954
      Likes Received
      4591
      Likes Given
      2499

      Default Re: Faida za Kufunga

      kanuni muhimu ya kufunga aliyoiweka nani?
      MziziMkavu likes this.

    14. #12
      MIGNON's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2009
      Posts : 561
      Rep Power : 656
      Likes Received
      171
      Likes Given
      128

      Default Re: Faida za Kufunga

      KABONDE,naona unapoteza maana ya habari ya mwanzo.Pili unapotumia maneno kama "MIJITU" una maana gani?
      Ni vizuri tujifunze kuitumia nafasi hii vizuri katika kuelimishana na kupeana habari.Kama huna la kuchangia nyamaza na fanya mambo mengine.
      Naipenda sana forum ya technology hamna upuuzi kama unaoonekana katika forums nyingine.
      Tujitahidi kuwa wastaarabu kwani habari hizi zinasomwa na watu wengi mpaka vijana wa shule.
      MziziMkavu likes this.

    15. #13
      Majala Kimolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2007
      Posts : 316
      Rep Power : 666
      Likes Received
      26
      Likes Given
      31

      Default Re: Faida za Kufunga

      Quote By Kabonde
      Waislamu hawafungi wanachofanya ni kugeuza usiku kuwa mchana na mchana kuwa usiku.Mijitu inaamka sanane za usiku inabugia mivyakula utadhani wanaachana na kula maisha hamna kitu waache kudanganya watu.Hakuna mtu aliwahi kufunga hapa dunia zaidi ya Yesu mwana wa Mungu wengine wanajaribu kidogo sana lakini waislamu hawafungu na hawajawihi kufunga hata siku moja.Kwanza ukifunga hutakiwi kumtangazia mtu lauka kama ukimtangazia mtu tayari umeshapata thawabu zako kwa mtu uliye mtangazia.Waislamu wanapoutangazia ulimwengu wameanzakufunga wanakuwa wamekiuka kanuni muhimu ya ufungaji
      Mwaisa kanuni ipi na ya nani?
      Yaonekana wewe ni kobe hata kwenye kwaresma Duh! badilika kidogo, dunia yaisha hii unakoelekea ni uzeeni, vuta kabusara kidoooogo ka kumjua Mungu na kufanya Ibada
      MziziMkavu likes this.

    16. #14
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,859
      Rep Power : 7687
      Likes Received
      1467
      Likes Given
      0

      Default Re: Faida za Kufunga

      Tabia ya mtu uonekana kwenye maneno yake.
      MziziMkavu likes this.
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)


    17. #15
      Ngalikihinja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st September 2009
      Posts : 4,441
      Rep Power : 1451
      Likes Received
      1007
      Likes Given
      96

      Default Re: Faida za Kufunga

      Quote By Ndibalema
      Mbona hueleweki ndugu yangu!!
      mara hawafungi, mara wanafunga mchana.
      Tukuelewe lipi??
      Uelewe kuwa wanafunga masaa 12 tu na siyo siku nzima.................maana siku nzima ina masaa 24

    18. #16
      elimumali's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 13th January 2010
      Posts : 138
      Rep Power : 502
      Likes Received
      3
      Likes Given
      11

      Default Re: KUFUNGA BILA KUSALI

      Miaka mingi imepita sikujaaliwa kufunga kutokana na vidonda vya tumbo. Namshukuru Mwenyezi Mungu mwaka huu nina nafuu kubwa, nimeamua kufunga nami nipate thawabu za mwezi huu mtukufu.
      Kitu kimoja kinanitatiza, Waislamu naombeni mnipe maelekezo na matumaini. Pamoja na kwamba nafunga kwa moyo mkumjufu, na nimenuia hasa, lakini NAKOSA MUDA WA KUSWALI, ofisini niko busy, natoka usiku na nafuturu saa mbili usiku. JE, NI KWELI KWAMBA KUFUNGA BILA KUSALI NI SAWA NA KUWA NASHINDA NA NJAA BURE?

    Similar Topics

    1. Replies: 4
      Last Post: 4th August 2011, 08:44

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...