Tangu huu mgogoro wa kiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda ukiwahusisha hasa viongozi wa nchi hizi uanze kumekuwepo na maoni tofauti kutoka kwa wananchi wa hizi nchi mbili. Kinachonishangaza ni jinsi vyombo vyetu (Tanzania) vya habari hasahasa magazeti yanavyochagiza huu mgogoro kwa kuibuka na vichwa vikubwa vikubwa vya habari vinavyoihusu Rwanda na raisi wake. Nahisi magazeti yanafanya hivyo ili kuuza, hivyo wananufaika na huu mgogoro lakini kwa upande mwingine wanachochea moto katika huu mgogoro badala ya kuupoza.