Re: Askofu Malasusa msemaji wa familia ya Lowasa

By
Pasco
Wajemeni, Maaskofu ni Wachungaji, kazi ya wachungaji ni kuwachunga kondoo wa Bwana wasipotee, Masiya alikuja kwa waliopotea na wale walio elemewa na mizigo ili wapumzishwe.
EL amepotea na ameelemewa na mizigo ya tuhuma, shutuma na kila aina ya bezo, dhihaka, kejeli, matukano, ya kila aina mpaka chuki binafsi mumo humo, kwa watu wa Mungu, huu ndio wakati wa kukaa karibu kabisa na EL na sio kumtenga, bali kumkumbatia mpaka aguswe na roho wa Bwana, atakuja mbele ya kadamnasi ya watu, atatubu, atasamehewa, atatakaswa na atangara kama mbalamwezi tayari kwa 2015!.
Amini nawaambieni, 'jiwe walikolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni'. Kwake Yeye, wa kwanza atakuwa wa mwisho, na wamwisho atakuwa wa kwanza.
Acha Maaskofu watimize mapenzi ya Bwana, ya kuwarudisha kundini kondoo waliopotea.
Mbona huo mchakato ameshaunza mara baada ya kugundua kosa. EL siyo mchezo! Hajapoteza vision yake. Anailinda kama mboni ya jicho. Kwaufundi mkubwa anarekebisha yaliyopita na kuweka sawa pale palipo pinda. Sijui issues za integrity yake zitakuwaje ili 2015 ndoto yake itimie ila namuona ameamua kupigana kufa na kupona!!
We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
Ralph Waldo Emerson
Follow Us Here