Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Michango Ya Harusi

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 40
    1. #1
      Mambo Jambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2008
      Posts : 1,043
      Rep Power : 762
      Likes Received
      16
      Likes Given
      1

      Default Michango Ya Harusi

      Hii Kitu nilitaka kuipost hapa miezi kadhaa iliyopita sema nikasahau, leo kuna jamaa kanipigia anataka nimtumie dolali za mchango wa harusi ya binamu yake ambaye hata simjui wala sijawahi msikia....

      Tuendelee:-

      Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.

      Watu wanakutana kila week mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. na katika vikao vivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu...........kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo....jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much...badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye elimu na matibabu...

      MJ
      A wise man once told me, luck isn't some mystical energy that dances around the universe randomly bestowing people with safisfaction and joy..you creat your own luck.

    2. Miaka 50

    3. #2
      Chimunguru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2009
      Posts : 7,795
      Rep Power : 2149
      Likes Received
      1223
      Likes Given
      545

      Default Re: Michango Ya Harusi

      hapa nilipo nna kadi sita ambazo harusi zote zinafanyika mwezi huu mwishoni na december kila moja si chini ya alfu hamsini

    4. #3
      The Boss's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 18,175
      Rep Power : 21618
      Likes Received
      13494
      Likes Given
      17794

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Mimi kinachonishangaza ni huu utaratibu unaosema eti ukichangia elfu hamsini unakwenda na mpenzi wako,,,,lakini ukichangia elfu 25 unenda peke yako na kadi imeandikwa kabisa ni single.....

      Utasema concert....
      Wabongo bana.....

      Yaani huwezi kupata date ukaamua kwenda nae kwenye harusi
      kwa kuwa ulitoa mchango wa single.....aghhhh...

      Na bila mchango hualikwi....
      Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!

    5. #4
      AM_07's Avatar
      Member Array
      Join Date : 7th November 2009
      Posts : 76
      Rep Power : 500
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Michango Ya Harusi

      kinachokera zaidi mtu akiwa anakaribia kuoa/kulewa atakuwa karibu na wewe sana , akishapata mchango kwako ni kwaheri, i think kama tuchangie elimu na misiba tuu, anaehamua kuoa lywake
      The consultant

    6. #5
      Lyangalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th September 2009
      Location : Kintinku-Dodoma
      Posts : 613
      Rep Power : 631
      Likes Received
      61
      Likes Given
      14

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Michango ni hiari ndugu zanguni hakuna anayekulazimisha kuchanga, na kama inakukela sana weka kabisa tangazo kama professor mmoja wa UDSM alikuwa ameandika kwenye mlango wa ofisi yake "MICHANGO YA HARUSI IMESITISHWA". Sidhani kama kuna mtu anakulazimisha kuchanga. Usipende kufanya kitu kinachokuumiza na kukukosesha amani kwa sababu ya kuogopa. Kama hutaki kuchangia sema no kama unachanga changa bila kinyongo ndo faida ya kuwa mwanajamii na kusaidiana!
      A MAN'S BEST OR WORST CHOICE IN LIFE IS HIS WIFE

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Oxlade-Chamberlain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Location : dodoma
      Posts : 7,616
      Rep Power : 4422
      Likes Received
      789
      Likes Given
      750

      Default Re: Michango Ya Harusi

      mie nawashauri hii michango wanayokusanya badala ya kutumia hela zote kufanya harusi kubwa bora watumie hizi hela kuanzia maisha yao ya ndoa.ndoa nyingi nimeona harusi kubwa baada mwezi au miezi wana ndoa wanalalamika maisha magumu.Kwanini hii michango isitumiwe kwa manufaa zaidi baada ya ndoa kuliko siku ya ndoa?
      "Nobody has enough talent to live on talent alone. Even when you have talent, a life without work goes nowhere". A. Wenger

    9. #7
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,084
      Rep Power : 12251
      Likes Received
      6015
      Likes Given
      6851

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Wajameni, hakuna kitu kero kama michango ya harusi kwa sasa... imepoteza maana!! Unakuta mtu anakupangia kabisa - wewe nimekupangia laki tatu tu!!! mtu income ya kawaida halafu anataka harusi ya mil 25 na ukiuliza kachanga ngapi anakwambi milioni moja!!! Very sick tradition... na mara nyingi unakuta mtu anaoa mkewe [meaning they are already living together or have already done everything wanandoa do!!

      Sasa subiri sijui chicken party, send-off, bachelors, inner party etc. etc.

      It is not a culture to embrace especially now that we need to put all our efforts in development
      .....Ana sifa zote, nzuri na mbaya!!!

    10. #8
      Tumain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2009
      Posts : 3,213
      Rep Power : 1146
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Budget ya Harusi siku hizi si chini ya mil.10,15, 20 ...wtf mimi naona tumezidi kuwa wapofu kula all that amount for one day tunachezea resorces...ukiangalia majirani zetu wanahitaji mtaji wa 50,000, 100,000, 200,000/- kuondokana na umaskini kwa biashara ya vitumbua, mandazi nk...
      tuna culture ya kutumia sana kwa ufahari..lol

    11. #9
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,084
      Rep Power : 12251
      Likes Received
      6015
      Likes Given
      6851

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Quote By Tumain
      Budget ya Harusi siku hizi si chini ya mil.10,15, 20 ...wtf mimi naona tumezidi kuwa wapofu kula all that amount for one day tunachezea resorces...ukiangalia majirani zetu wanahitaji mtaji wa 50,000, 100,000, 200,000/- kuondokana na umaskini kwa biashara ya vitumbua, mandazi nk...
      tuna culture ya kutumia sana kwa ufahari..lol
      Huu ndio ukoma wa jamii yetu ya sasa... tunaweka vipaumbele sehemu zisizostahili!!!

      Kuna jamaa mmoja wa nje ya afrika kuna siku alisema maneno makali kidogo lakini he was right; alisema
      You africans are so amazing, you spend fortune on funerals but nothing on birth and that is where god bless you with a life; mothers and children deaths can be prevented.

      You also spend alot on celebrating weddings but you spend less on teaching about faithful marriage

      Ilikuwa kauli nzito lakini ina ukweli!!
      .....Ana sifa zote, nzuri na mbaya!!!

    12. #10
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,084
      Rep Power : 12251
      Likes Received
      6015
      Likes Given
      6851

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Quote By AM_07
      kinachokera zaidi mtu akiwa anakaribia kuoa/kulewa atakuwa karibu na wewe sana , akishapata mchango kwako ni kwaheri, i think kama tuchangie elimu na misiba tuu, anaehamua kuoa lywake
      Mkuu umenena... ila hapo kwenye misiba mie ningependa tu-replace na kuchangia wagonjwa ili wapate huduma!!!
      .....Ana sifa zote, nzuri na mbaya!!!

    13. #11
      Tumain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2009
      Posts : 3,213
      Rep Power : 1146
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Kuna vitu siyo sahihi kwenye harusi zetu naamini tunaweza kufurahi bila kutumia hela nyingi sana mimi katika harusi item zifuatazo zinanikera..
      1. MC..yaani mchekeshaji wa masaa tu 200,000..etc sioni mantiki kabisaaa kwanini asiye rafiki tu anaongoza kwa raha halafu bure ...kama vikao vyetu infomal sehemu zingine za starehe lol
      2. Mapambo..ebwana wanakamua sijapata kuona bila sababu ya msingi
      3. Ukumbi...weka kwenye uwanja wa wazi au nyumbani kwa mzee wako finito lol

    14. #12
      Serendipity's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2009
      Location : Magogoni
      Posts : 442
      Rep Power : 614
      Likes Received
      8
      Likes Given
      1

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Mimi nadhani michango ya harusi tungebadilisha matumizi yake, badala ya kunywa na kula hizo mil 10, 15 au 20 kwa usiku mmoja, ni bora hiyo hela wakakabidhiwa bwana na bibi harusi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya makazi au iwe kama mtaji wa biashara, utakuta mtu anafanya harusi ya mil 15 au 20, lakini hana kiwanja wala nyumba.. unakuta amepanga Sinza, Kijitonyama au mbezi beach, hehe hehe.....
      We need to change our attitudes and mindset!
      If you really want something in this life, you have to work for it. <o></o>

    15. #13
      Madela Wa- Madilu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th March 2007
      Location : NORTH WEST USA
      Posts : 2,524
      Rep Power : 2441
      Likes Received
      278
      Likes Given
      286

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Hivi huu utaratibu wa sherehe za arusi na patashika zake ni utamaduni wa kabila gani Tanzania? Au ni utamaduni wetu kama watanzania? Au ni utaratibu tuliouiga kutoka utamaduni wa watu gani?

      Nchi zilizo endelea kama hapa Marekani hachangishwi mtu, sherehe zinategemea uwezo.
      Kwa sababu ni hurka yetu kukopi kila kitu kutoka dunia ya kwanza hata kama ni ugonjwa au udhaifu, nauliza tena ni utamaduni wa nchi gani unafanana na utamaduni huu wa Tanzania wa kuchangishana fedha kwa hila za kishetani?
      Labda nyie mlioa miaka ya 196.. mtuambie. baba, mama, shangazi na wajomba zenu waliwachangisha akina nani ili nyie muozwe??

      Ili ndoa iitike ni lazima sherehe zake ziwe za kukata kwa Nyengo?

      Masikini ni yule atumiaye kipato asichokuwa nacho.

      Pendekezo langu kwenu nyie ambao hamjaoa ni hili.

      Achaneni na ununda huu wa kudhani sherehe kubwa ndo fahari ya ndoa.
      Acheni kuchangia harusi za watu wengine kwa mtindo huu usiojulikana asili yake.
      Jiandaeni kufunga harusi Private ambazo zitahusisha ndugu wa karibu tu na bajeti ndogo kabisa ya uwezo wa mfuko wako.

      Kuna harusi hapa Marekani jumla ya watu wote katika harusi ni 40 tu. ukitoa wanandoa. Pamoja na ukweli kwamba wana ndugu jamaa na marafiki debe zima.
      Kupanga ni kuchagua, hakuna mwenyenia ya wazi ya kuchagua kitu kibaya lakini tuliowengi sikuzote hushindwa kupanga, na hivyo kushindwa kuchagua.

      Sasa hawa wenye mifedha ya nguvu wanaandaa sherehe ndogo, sisi tuytemeao makalio nusu wazi tunaandaa sherehe kama wana wa Wafalme.

      Kama kuna nchi moja ilojaaa majuha waotao mchana si nyingine ni nchi yetu tukufu Tanzania.


      Nahisi Utamaduni wetu wa kuandaa sherehe zilizo zidi uwezo wetu na hamu yetu unatokana na ukweli kwamba, vipato vingi Tanzania si halali. Kwani viapatao vingi kwa namna moja au nyingine vina uhusiano na wizi udanganyifu na uuaji.
      Fedha haramu siku zote hutumika katika namna iliyo haramu. Kibaya zaidi fedha haramu hujenga utamaduni haramu katika jamii bila kujali mipaka.
      Watu wenye vipato halali nchini Tanzania ghafla wameshitukia wakijitumbukiza katika utamaduni haramu ambao asili yake ni ibilisi kwa kudhani kwamba wana enzi asili yao.

      Kila mtu angependa kunya mavi mengi na makubwa kwa mpigo vile afanyavyo Tembo. Je Kuna mwenye makalio makubwa ya kuwa na ngebe ya kumwiga Tembo huko msalani?
      Huu utaratibu wa kuazima makalio ya wengine yakusaidie huko msalani ni utamaduni gani??
      Last edited by Madela Wa- Madilu; 13th November 2009 at 02:51.
      MYPEOPLE PERISH FOR LACK OF KNOWLEDGE. HOSEA 4:6

    16. #14
      Ustaadh's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th October 2009
      Posts : 408
      Rep Power : 572
      Likes Received
      7
      Likes Given
      1

      Unhappy Re: Michango Ya Harusi

      Itisha michango kuwa umepata nafasi ya masomo nje ya nchi unaomba uchangiwe ili upate nauli ....wachache sana watakuchangia....

    17. #15
      Ruge Opinion's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd March 2006
      Location : DAR ES SALAAM
      Posts : 1,058
      Rep Power : 890
      Likes Received
      149
      Likes Given
      79

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Mimi nimeishafanya uamuzi wa kutochangia harusi hovyo. Ni watu wachache tu walio karibu sana na mimi ndio ninaowachangia. Hata hivyo viwango vya kuchangia wanvyoviweka havinipi shida kwa sababu harusi za watu nisiowajua siendi hata nikipewa kadi. Kwa hiyo mimi najiamulia ni nani nimchangie na kiasi gani. Lakini uamuzi huo umenifanya nichukiwe na watu. Mimi sijali. Niko tayari kuchangia mtoto wa jirani aliyekosa au kupungukiwa karo, au mgonjwa aliye hospitalini, au mtu aliyefiwa. The paradox is mgonjwa anakaa hospitali miezi watu hawaendi kumjulia hali au wanaokwenda hawaendi na msaada wowote. Lakini akifariki hao hao wanalala kwenye msiba siku tatu au hata nne na michango wanatoa kwa mbwembwe kwa kuwa watu wanakuwa wanashuhudia. Lengo hapa ni kujitangaza na sikusaidia. It is completely irational.
      Loosing is a starting point to success

    18. GP
      #16
      GP's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2009
      Location : every where
      Posts : 1,951
      Rep Power : 919
      Likes Received
      76
      Likes Given
      96

      Default Re: Michango Ya Harusi

      sichangii mtu na wala sitahitaji mchango wa mtu!.
      M4C

    19. #17
      Gudboy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th August 2009
      Location : DSM
      Posts : 805
      Rep Power : 658
      Likes Received
      9
      Likes Given
      10

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Huwa nasema siku zote bora hata harusi za waislam ambazo hazina complication nyingi, watu wakipiga mpunga na ndizi kazi kwisha. Utakuta mtu anabudget ya harusi ya milioni 20, halafu yeye ana milioni 1, sasa huu umekua mradi au? sasa hiyo pesa akipata yote anapeleka kwenye harusi then ikiisha wanarudi kuwa maskini. Watu kama wanaomba michango basi iwe kwa ajili ya maisha na sio kwa ajili ya kula siku moja then kwisha. Mimi Mungu akisaidia nikawa na mipango ya harusi sitawachangisha watu, na kila aliyekaribu nami nitamwalika. Hapo hapo mtu akiambiwa achangie yatima au wagonjwa wnakua wagumu sana kufanya hivyo
      Kuwa na Mashori wengi si kipimo cha Urijali, kama mwanaume wa kweli, nyumbani wapate Ugali

    20. #18
      Sinkala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2008
      Location : Your office's next door
      Posts : 1,346
      Rep Power : 800
      Likes Received
      163
      Likes Given
      45

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Quote By MTM
      Mkuu umenena... ila hapo kwenye misiba mie ningependa tu-replace na kuchangia wagonjwa ili wapate huduma!!!
      Tatizo ni kwamba mtu akiwa anaumwa huwa haitangazwi sana, lakini akiaga dunia ndo habari inasambazwa kwa kasi. Unaweza ukawa na moyo wa kusaidia mgonjwa lakini usipate taarifa na ghafla tu unakuja kujulishwa habari ya msiba.
      Annuntio vobis gaudium magnum; habemus Papam: Eminentissimum ac Reverendissimum Dominum, Dominum Georgium Marium Sanctae Romanae Ecclesiae Cardinalem Bergoglio qui sibi nomen imposuit Franciscum

    21. #19
      Mambo Jambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2008
      Posts : 1,043
      Rep Power : 762
      Likes Received
      16
      Likes Given
      1

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Kuna kitu kwenye kikao za harusi zinaitwa "UCHAKAVU" ina maanisha michango ya kula na kunywa pale kwenye kiao cha harusi, watu wanapiga beer na nyama choma kwenda mbele....usishangae ukatoa uchakavu 50,000 wakati umekunya beer mbili na kipande cha kuku..........hizi tuache jamani
      A wise man once told me, luck isn't some mystical energy that dances around the universe randomly bestowing people with safisfaction and joy..you creat your own luck.

    22. GP
      #20
      GP's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2009
      Location : every where
      Posts : 1,951
      Rep Power : 919
      Likes Received
      76
      Likes Given
      96

      Default Re: Michango Ya Harusi

      Quote By Mambo Jambo
      Kuna kitu kwenye kikao za harusi zinaitwa "UCHAKAVU" ina maanisha michango ya kula na kunywa pale kwenye kiao cha harusi, watu wanapiga beer na nyama choma kwenda mbele....usishangae ukatoa uchakavu 50,000 wakati umekunya beer mbili na kipande cha kuku..........hizi tuache jamani
      heeeeeeeee, yani hapo mkuu umelenga!.
      ebwana kuna kikao kimoja nilihudhuria, mshkaji alikunywa bia 4, kumbe watu wanamuangalia tu spidi yake, kufika kwenye uchakavu si akatoa 1000/=, acha akunjwe shati alipie,. hakuna usawa mie ninywe maji ya 300 mwingine anywe bia 5 halafu tutoe sawa uchakavu, Lol.
      M4C

    Page 1 of 2 12 LastLast

    Similar Topics

    1. Michango ya harusi Tanzania imezidi!
      By Luluka in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 75
      Last Post: 18th January 2012, 15:53
    2. Michango ya harusi
      By SMART1 in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 15
      Last Post: 8th November 2011, 16:32
    3. michango ya harusi
      By maimuna in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 1
      Last Post: 13th September 2011, 11:20
    4. Michango ya harusi inavyonitesa
      By Kiranja Mkuu in forum JF Chit-Chat
      Replies: 64
      Last Post: 27th June 2011, 11:54
    5. Michango ya harusi
      By pmwasyoke in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 39
      Last Post: 5th August 2010, 16:26

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...