Kwa ufupi: Dar es Salaam. Serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh17.7 trilion katika Mwaka wa fedha 2013/2014, huku ikiweka kipaumbele katika upatikanaji wa nishati ya umeme.
Tofauti na miaka iliyopita, bajeti hiyo inatarajiwa kusomwa Juni 16 mwaka huu kwenye mkutano wa 11 mjini Dodoma na itatanguliwa na bajeti za wizara za Serikali.
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusu mwelekeo wa bajeti hiyo ya Serikali alisema mapato ya Serikali yanatarajiwa kukusanywa kiasi cha:
- Sh10.6trilioni Serikali Kuu
- Sh9.9trilioni Mapato TRA
- Sh741bilioni yasiyo ya kodi
- Sh372bilioni Halmashauri
- Sh3.8trilioni Kutoka nje.
Kwa mujibu wa Dk Mgimwa, kipaumbele cha pili ni kuboresha miundombinu ya Bandari za Tanga, Dar es Salaam, Mtwara na ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo.
Vipaumbele vingine ni:
- Reli
- Maji
- Elimu
- Bila kusahau sekta za afya, ujasiriamali na kilimo’ aliogeza Dk Mgimwa.
Ni mwelekeo wa makadirio ya matumizi ya Serikali katika Mwaka wa fedha 2013/2014 yanayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni Juni 16, Mwaka huu na Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa.
CHANZO: Mwananchi, Jumanne, Machi 26, 2013