Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Akina Dada

    Report Post
    Page 1 of 3 123 LastLast
    Results 1 to 20 of 56
    1. BAK
      #1
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,539
      Rep Power : 44951
      Likes Received
      8281
      Likes Given
      8280

      Default Akina Dada

      wa wakina Kaka pia mnaweza kuchangia mjadala huu kuhusiana na hii kauli ya Kikwete,"“Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe, msifikiri kuwa maadui ni wanaume, wapo wanawake wasiopenda wenzao wapate ambapo huwafanyia hiana kwa madai kuwa watawapita kimaendeleo,” alisisitiza.

      Kwa maoni yangu adui wa mwanamke ni ujinga unaosababishwa na wanawake wengi kukosa elimu ama kwa sheria za nchi au familia zao kutoona umuhimu wa watoto wa kike kuendelea na elimu ya juu

      Je mnakubaliana na kauli hii ya Mh. kwamba adui wa mwanamke ni mwanamke!? Je kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kauli hii!?
      http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/7/28/habari4.php
      Last edited by BAK; 29th July 2007 at 19:04.

    2. Study Abroad

    3. #2
      AmazingFriend's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2007
      Posts : 74
      Rep Power : 622
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Unhappy Mfumo Dume

      Quote By Bubu ataka kusema
      wa wakina Kaka pia mnaweza kuchangia mjadala huu kuhusiana na hii kauli ya Kikwete,"“Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe, msifikiri kuwa maadui ni wanaume, wapo wanawake wasiopenda wenzao wapate ambapo huwafanyia hiana kwa madai kuwa watawapita kimaendeleo,” alisisitiza.

      Kwa maoni yangu adui wa mwanamke ni ujinga unaosababishwa na wanawake wengi kukosa elimu ama kwa sheria za nchi au familia zao kutoona umuhimu wa watoto wa kike kuendelea na elimu ya juu

      Je mnakubaliana na kauli hii ya Mh. kwamba adui wa mwanamke ni mwanamke!? Je kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kauli hii!?
      http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/7/28/habari4.php
      Kwa maoni yangu,
      Adui wa mwanamke ni mwanaume.
      Wanawake makazini wana uwezo sawa au hata kushinda
      wanaume hasa kwa umakini wa kazi zao.
      Ma-boss wengi ni wanaume, hupenda kuendeleza mfumo
      dume ambao ni mbaya sana. Kati ya managers kumi
      wa kampuni, mwanamke atakuwa mmoja au hakuna kabisa.
      Katika idara za makampuni - mfano katika benki inayomsikiliza
      mteja, idara nzima ina managers wanaume, hakuna hata mwanamke
      mmoja anaefikiriwa kupewa umeneja. Hii sio sawa, haiwezekani
      idara nzima wanaume tu ndiyo wenye uwezo, ni vizuri kuwapa
      nafasi wanawake pia.
      Kwa hali kama hizi- adui wa mwanamke ni mwanaume, hasa
      wasioamini kuwapa nafasi wanawake wajiendeleze-kila mtu
      anahitaji pesa-si wanaume tu.

      A "friend" is what the "heart" needs all the time!

    4. #3
      MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1397
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

      Default

      Du,
      Kila tatizo- basi ni mfumo dume! Hata masengenyo, wivu, umbeya je ni matokeo ya mfumo dume?
      Ila nakubali kuwa wanaume wamechangia zaidi kuharibu amani na kuleta vita duniani (angalia Iraq, Middle East N.K).
      Viongozi wengi ni wanaume- pengine wanawake wakipewa nafasi dunia itakuwa na amani zaidi????

    5. #4
      AmazingFriend's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2007
      Posts : 74
      Rep Power : 622
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Unhappy Dada/Mwanamke kiongozi

      Quote By Mzalendohalisi
      Du,
      Kila tatizo- basi ni mfumo dume! Hata masengenyo, wivu, umbeya je ni matokeo ya mfumo dume?
      Ila nakubali kuwa wanaume wamechangia zaidi kuharibu amani na kuleta vita duniani (angalia Iraq, Middle East N.K).
      Viongozi wengi ni wanaume- pengine wanawake wakipewa nafasi dunia itakuwa na amani zaidi????
      Hapana, si kila tatizo.
      Wapewe nafasi tuone wakishindwa.
      Mwanamke mwenzie asipopenda, haizuii
      yeye kupewa uongozi, huwezi kuacha kumpa
      kwa kudai mwanamke mwenzie hapendi.
      Wapewe waongoze.
      Kwa mambo mengi mabaya wafanyayo wanaume,
      ladies are not daring, mostly they think
      of their families esp. kids before doing
      the worst things!! This is very true!

      A "friend" is what the "heart" needs all the time!

    6. #5
      AmazingFriend's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2007
      Posts : 74
      Rep Power : 622
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Mzalendo Halisi,
      Kuwa mzalendo kweli, kwa kumpa mwanamke
      nafasi aongoze. Ok?

      A "friend" is what the "heart" needs all the time!

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1397
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

      Default

      Amazingfriend,
      Yes- mimi sina neno kutoa nafasi dada/mama zetu waongoze! Ikiwa pia lakina akina mama wenzao watawapa kura!
      Ila kweli mwananke akipata pesa hufikiria watoto, familia na maendeleo- sisi wanaume tukipata za ziada mara zingine tunasahau wake na familia- tunakuwa kwenye pombe zaidi, na mambo ya mabibi n.k
      Ila kweli wanawake wakipewa nafasi- ni wazuri tu sana- mara nyingi kuliko wanaume. Sema pia wanawake wengine hupata hizo nafasi kwa njia za mkato kupitia wanaume- hii huwavunjia heshima!

    9. #7
      AmazingFriend's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2007
      Posts : 74
      Rep Power : 622
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default very very true!! hapo umepatia kabisa!

      Quote By Mzalendohalisi
      Amazingfriend,
      Sema pia wanawake wengine hupata hizo nafasi kwa njia za mkato kupitia wanaume- hii huwavunjia heshima!

      100% true!!!
      Kutokana na kutopewa hizo nafasi, huamua kuzipata
      kwa style hiyo!! What a shame!!
      AF.

      A "friend" is what the "heart" needs all the time!

    10. #8
      mashoo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th July 2007
      Location : USA
      Posts : 100
      Rep Power : 624
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Red face Mfumo Dume Ufeeeeeeee

      Adui wa mwanamke ni mfumo DUME period! hayo mengine ni blah blah tu.Kuwe na haki sawa kwa wanawake na wanaume ktk nafasi za kazi na masomo ili tuprove hili!Nimependa wazo la viti maalum kutolewa bungeni I hope litapita ili wanawake waingine bungeni kwa nguvu zao na sio kubebwa au vinginevyo including 'technology know who'tunalingojea hilo kwa hamu sana na hiyo itapunguza kupasha viti bungeni badala yake kutakuwa na kuchangia mada kama JK alivyosema.
      Nadhani pia UWT itapitisha hilo wazo la watoto wa kike kuendelea na masomo baada ya kujifungua, hii itawasaidia kuwa na future pamoja na mtoto atakayezaliwa kwasababu mkimkatisha masomo nini hatima yake? si umaskini uliokithiri?? Napinga wazo la JK kuwa hiyo itasababisha watoto wengi kubeba mimba.
      Lets think progressive here...I wish U all the best.

    11. #9
      MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1397
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

      Default

      Quote By AmazingFriend

      100% true!!!
      Kutokana na kutopewa hizo nafasi, huamua kuzipata
      kwa style hiyo!! What a shame!!
      AF.
      Amazingfriend,
      Je inabidi nafasi wazipiganie au wapewe? Hizo za kupewa ndo hapo wanajivunjia heshima! Ila tatizo la Bongo kazi nyingi na hata nafasi za juu ni mlango wa nyuma! Na rushwa zipo za aina nyinyi- zote ni rushwa tu! Hata kupanda cheo unakuta rushwa! sasa tufanyeje?

    12. #10
      MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1397
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

      Default

      Quote By mashoo
      Adui wa mwanamke ni mfumo DUME period! hayo mengine ni blah blah tu.Kuwe na haki sawa kwa wanawake na wanaume ktk nafasi za kazi na masomo ili tuprove hili!Nimependa wazo la viti maalum kutolewa bungeni I hope litapita ili wanawake waingine bungeni kwa nguvu zao na sio kubebwa au vinginevyo including 'technology know who'tunalingojea hilo kwa hamu sana na hiyo itapunguza kupasha viti bungeni badala yake kutakuwa na kuchangia mada kama JK alivyosema.
      Nadhani pia UWT itapitisha hilo wazo la watoto wa kike kuendelea na masomo baada ya kujifungua, hii itawasaidia kuwa na future pamoja na mtoto atakayezaliwa kwasababu mkimkatisha masomo nini hatima yake? si umaskini uliokithiri?? Napinga wazo la JK kuwa hiyo itasababisha watoto wengi kubeba mimba.
      Lets think progressive here...I wish U all the best.
      Mashoo,
      Acha kutafuta mchawi- Mfumo dume kila kitu! Wanawake pia wana tamaa ya kushindana, ktk new fashion n.k sasa hii inawweka ktk vishawishi!

    13. #11
      AmazingFriend's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th June 2007
      Posts : 74
      Rep Power : 622
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mzalendohalisi
      Amazingfriend,
      Je inabidi nafasi wazipiganie au wapewe? Hizo za kupewa ndo hapo wanajivunjia heshima! Ila tatizo la Bongo kazi nyingi na hata nafasi za juu ni mlango wa nyuma! Na rushwa zipo za aina nyinyi- zote ni rushwa tu! Hata kupanda cheo unakuta rushwa! sasa tufanyeje?
      Ni vizuri kuzipigania kwa qualifications na presentations,
      ila kama wanavyoteuliwa wanaume, wanawake pia iwe hivyo.
      Usawa kwa mambo yote. Kumbuka si kila nafasi wanaume
      mmegombea! True? Guess that will be fair enough.
      Ladies are capable.

      A "friend" is what the "heart" needs all the time!

    14. #12
      mashoo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th July 2007
      Location : USA
      Posts : 100
      Rep Power : 624
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Sijakataa wanawake wanashindana, wanchukiana na wanaoneana wivu nk. lakini huwezi kusema hicho ndio kinawashinda kuendelea au kupata vyeo kazini.Namini kama m'mke amepata nafasi ya kupata elimu nzuri akapata proffessional yake nzuri, kama kuna nafasi ya kazi na ana right qualification ataipata, trust me hata kama kuna mwanamke around ambaye hampendi! upo hapo? that's my point! wanawake wapewe nafasi sawa kielimu na kijamii,na hii ianzie ktk malezi nyumbani mtreat mtoto wa kike sawa na wa kiume,na tuachane na mila potofu kuwa mwanaume ndio bora zaidi na mengine yataenda sambamba!

    15. BAK
      #13
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,539
      Rep Power : 44951
      Likes Received
      8281
      Likes Given
      8280

      Default

      Mimi nina maoni tofauti kuhusiana na viti maalum vya wanawake. Hata katika nchi nyingi za magharibi sasa hivi wanatafuta namna ya kuongeza idadi ya wanawake katika mabunge yao baada ya kuona kwamba mabunge yao miaka nenda miaka rudi bado idadi ya wabunge wanawake ni ndogo sana. Sijui wataamua nini ili kuongeza idadi ya wanawake katika mabunge yao maana kuna upinzani mkubwa hasa kutoka kwa baadhi ya wanaume kwamba hakuna yeyote anayestahili kupata upendeleo wa aina fulani ili kuingia bungeni.

      Kuhusu bunge letu mimi naona kuna haja ya kundeleza upendeleo maalum kwa wanawake ili mradi tu wanawake watakaochaguliwa ni wasomi na wapo makini katika mambo mengi yanayoendelea Tanzania na ulimwengu kwa ujumla. Nawafahamu wanawake mbali mbali kwenye makampuni au mawizara ambao kwa maoni yangu wanastahili kabisa kuwa wabunge, lakini wakisimama na wanaume wengi hawataambulia chochote hivyo wapewe upendeleo maalum, vinginevyo asilimia 99 ya Bunge itakuwa ni wanaume.

      Kwa kumalizia matatizo ya wanawake kwa maoni yangu ni wengi wao kutokupata elimu ya juu ama kutokana na mfumo uliokuwepo au wazazi kutoona umuhimu wa watoto wa kike kuendelea na elimu ya juu na mfumo dume ambao unawanyima madaraka wanawake wasomi katika nyanja mbali mbali walizosomea. Hili la adui wa maendeleo ya mwanamke ni mwanamke mimi silioni.

    16. #14
      Mwendapole Old's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th December 2006
      Posts : 655
      Rep Power : 768
      Likes Received
      7

      BAK,
      Kuendelea kuwapa nafasi za upendeleo wanawake bungeni kwa mtizamo wangu kutaendelea kuwaweka daraja la chini. lazima ifike mahali wanawake wapate nafasi kwa kuzishindia (on merit) sio kwa favor. Ikiwa tutaendeleza mtindo wa nafasi za upendeleo tutasahau kuwa wanatakiwa wawe kwenye equal footing na wanaume
      kama kweli wananwake wanataka kuwa na nafasi sawa na wanaume katika ngazi mbalimbali ni lazime wawe na courage ya kuzipigania, kuchagua wanawake wenzao, na kuacha kile kinachoitwa PHD(Pull Her Down) Ukweli ni kwamba anayemshusha mwanamke ni mwanamke mwenzie...stereotyping iko kwenye akili za mwanamke sio mwanaume..tukubali ukweli tuanzie hapo; wanaume wanachukulia pale wanawake walipoachia..yaani, mwanamke anajidharau, au anamdharau mwanamke mwenzie, ndipo mwanamume anapata courage ya kumkandamiza/kumdharau mwanamke husika
      Vikao vya wanaume kumzungumzia mwanamke vinahusiana na mambo kadhaa ya tabia au mahusiano yake na wanaume; lakini vya wanawake dhidi ya wanawake wenzao ni vya mauaji (character assasination)ya hali ya juu ya sifa za mwanamke husika tena kwa sababu za kizushi/wivu/binafsi/ na mambo kama hayo

      sorry dadas, you gotta start with yourselves

    17. #15
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 4,032
      Rep Power : 1416
      Likes Received
      609
      Likes Given
      44

      Default

      Ni mjadala mkali, lakini kama kuna mtu atakayetoa excuse ya mfumo dume, basi asiache kusema mwanamke nadiye anayetake part ya kuunda huo mfumo dume. Nadhani wanaume wengi vidume dunia hiyo walizaliwa na kina mama9 Mbali na waliozaliwa kwa chupa) na kulelewa zaidi na kina mama. Kwa kina mama wanapart kubwa ya lawama kuhusu huo mfumo.

    18. #16
      Mama Lao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th January 2007
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 355
      Rep Power : 702
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default

      Tunachotakiwa kinadada ni KUJIAMINI. Hizi special favours ndio zinatufanya tuonekane "wanyonge". What a man can do we can also do.
      Shida ni pale tunapotaka kutumia "uanamke" ku win over men or over other females.
      Msimamo wangu ni kwamba apart from getting education...take us to school. We do not need any favours!
      Mjenga nchi, ni mwananchi!

    19. #17
      Mwendapole Old's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th December 2006
      Posts : 655
      Rep Power : 768
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default

      Mama lao,
      suala ni
      -Kujiamini
      -Kujiheshimu
      -Elimu
      -Exposure (nina maana huwezi kugombea uongozi ikiwa hujui A,B,C zake..na wala hujui pa kuanzia...)
      -Support (from family/husband/fellow women
      ..mengine yafuate

    20. #18
      Maxence Melo's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 20th March 2006
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 3,043
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      1343
      Likes Given
      1432

      Default

      Quote By Mama Lao
      We do not need any favours!
      Aminia Mama Lao!

      Wow!

      Sasa najaribu kupiga picha najikuta ni flash tu zinatokea na picha zinaungua tu. You know why? Pingeni WAZIWAZI hii kitu ya viti vya upendeleo Bungeni. Hapo nitakupeni credit kuwa sasa wanawake wameamua!

      Pingeni bila kuchoka! Pingeni pia suala la mahari kutolewa na mwanaume mkitoa mbadala wa hayo. Bado mna safari ndefu sana mama zanguni. Napenda kukuungeni mkono lakini elewa katika wanawake 100 ni 5 tu ambao wako imara karibia na wanaume katika mambo mengi.

      Well, si wanaume wote wanawa-beat wanawake. Hilo liko wazi; Mwenyezi Mungu hakukosea kuwawekeni kuwa wasaidizi wetu ati... Ninyi ni kila kitu kwa mwanaume. Bila ninyi hatujiwezi; watapinga wengi hili lakini ukweli ndio huo! Mwanamke ni nuru ya mwanaume na mabavu ya mwanaume huisha kwa mwanamke... Labda awe nunda tu!

      Lakini...
      Haiba ya mwanamke si kuwa hajiwezi; utaiona kazi na uwezo wake kwa mwanaume aliyeoana nae au mwenzake wa ndoa. Never feel down; wale wanaowabeza au kuwafikiria vinginevyo wana mifumo dume vichwani mwao lakini ukweli wa mambo u ndani ya vichwa vyao.

      Ni mawazo tu
      Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' |Click HERE for Details

    21. BAK
      #19
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,539
      Rep Power : 44951
      Likes Received
      8281
      Likes Given
      8280

      Default

      Quote By Mwendapole
      BAK,
      Kuendelea kuwapa nafasi za upendeleo wanawake bungeni kwa mtizamo wangu kutaendelea kuwaweka daraja la chini. lazima ifike mahali wanawake wapate nafasi kwa kuzishindia (on merit) sio kwa favor. Ikiwa tutaendeleza mtindo wa nafasi za upendeleo tutasahau kuwa wanatakiwa wawe kwenye equal footing na wanaume
      kama kweli wananwake wanataka kuwa na nafasi sawa na wanaume katika ngazi mbalimbali ni lazime wawe na courage ya kuzipigania, kuchagua wanawake wenzao, na kuacha kile kinachoitwa PHD(Pull Her Down) Ukweli ni kwamba anayemshusha mwanamke ni mwanamke mwenzie...stereotyping iko kwenye akili za mwanamke sio mwanaume..tukubali ukweli tuanzie hapo; wanaume wanachukulia pale wanawake walipoachia..yaani, mwanamke anajidharau, au anamdharau mwanamke mwenzie, ndipo mwanamume anapata courage ya kumkandamiza/kumdharau mwanamke husika
      Vikao vya wanaume kumzungumzia mwanamke vinahusiana na mambo kadhaa ya tabia au mahusiano yake na wanaume; lakini vya wanawake dhidi ya wanawake wenzao ni vya mauaji (character assasination)ya hali ya juu ya sifa za mwanamke husika tena kwa sababu za kizushi/wivu/binafsi/ na mambo kama hayo

      sorry dadas, you gotta start with yourselves
      Kama tunataka Bunge letu lionyeshe hali halisi ya nchi yetu kwamba ina wanawake na wanaume ili kufanikisha hili basi upendeleo wa viti maalum vya akina mama inabidi uendelee ili mradi tu watakaoteuliwa ni wasomi na wana uwezo sio tu wakuwa wabunge bali pia mawaziri.

      Kutaka wanawake wagombee na wanaume basi bunge litajaa wanaume na kwa maoni yangu hili si jambo jema kwa maendeleo ya nchi yetu.

      Kwanza wagombea wanaume ndio watoa takrima (RUSHWA)wazuri wakati wa kampeni kwa kuangusha mapilau dhidi ya wafuasi na hata wasio wafuasi, kuwapeleka bar wanywe mpaka wawe chakarii na hata kuwapa pesa pia.

      Pili kuna wapiga kura ambao hata kama mwanamke ana qualifications zaidi ya mwanaume basi watakuwa radhi kumpigia kura mwanaume(mfumo dume) badala ya mwanamke.

      Marekani ambayo imepata uhuru wake mwaka 1776, miaka 231 iliyopita mpaka leo kuna watu wanasema "America is not ready for a Woman president." hili mimi linanishangaza sana. Kwenye senate yao ya watu 100 wanawake hawafiki hata 20!! kwenye Congress ya watu 450 wanawake kama sikosei hawafiki hata 100.

      Wanawake wameshaonyesha kama wanauwezo kama wanaume. Wanarusha ndege, wanafuzu Phd, Masters katika fields mbali mbali masters na wakipewa nafasi ya kuongoza pia wanafanya vizuri tu, lakini kizingiti chao kikubwa ni mifumo dume katika nchi mbali mbali duniani.

      Kwa hiyo bado Tanzania tuna haja ya kuendeleza upendeleo maalum kwa viti vya wanawake, kama tunataka Bunge la wanaume watupu basi tuufute huu upendeleo na matokeo yake tutayaona.

    22. #20
      MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1397
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

      Default

      Quote By Bubu ataka kusema
      Kama tunataka Bunge letu lionyeshe hali halisi ya nchi yetu kwamba ina wanawake na wanaume ili kufanikisha hili basi upendeleo wa viti maalum vya akina mama inabidi uendelee ili mradi tu watakaoteuliwa ni wasomi na wana uwezo sio tu wakuwa wabunge bali pia mawaziri.

      Kutaka wanawake wagombee na wanaume basi bunge litajaa wanaume na kwa maoni yangu hili si jambo jema kwa maendeleo ya nchi yetu.

      Kwanza wagombea wanaume ndio watoa takrima (RUSHWA)wazuri wakati wa kampeni kwa kuangusha mapilau dhidi ya wafuasi na hata wasio wafuasi, kuwapeleka bar wanywe mpaka wawe chakarii na hata kuwapa pesa pia.

      Pili kuna wapiga kura ambao hata kama mwanamke ana qualifications zaidi ya mwanaume basi watakuwa radhi kumpigia kura mwanaume(mfumo dume) badala ya mwanamke.

      Marekani ambayo imepata uhuru wake mwaka 1776, miaka 231 iliyopita mpaka leo kuna watu wanasema "America is not ready for a Woman president." hili mimi linanishangaza sana. Kwenye senate yao ya watu 100 wanawake hawafiki hata 20!! kwenye Congress ya watu 450 wanawake kama sikosei hawafiki hata 100.

      Wanawake wameshaonyesha kama wanauwezo kama wanaume. Wanarusha ndege, wanafuzu Phd, Masters katika fields mbali mbali masters na wakipewa nafasi ya kuongoza pia wanafanya vizuri tu, lakini kizingiti chao kikubwa ni mifumo dume katika nchi mbali mbali duniani.

      Kwa hiyo bado Tanzania tuna haja ya kuendeleza upendeleo maalum kwa viti vya wanawake, kama tunataka Bunge la wanaume watupu basi tuufute huu upendeleo na matokeo yake tutayaona.
      Bubu,
      Napenda your reaction- as a realist! Ni vema wanawake wapewe nafasi za upendeleo kwa sasa- hadi hapo wengi watakapokuwa na elimu na kuanza kupambana na mfumo dume kwa kura. Huu mfumo dome umekuwepo miaka maelfu- inashangaza leo eti JK anasema haungi mkono Viti maalumu! Tuna uhuru miaka 40 tu- hizi sababu za kihistoria zitachukua mda kusahihisha- sii leo au miaka 10 pengine miaka 50 ijayo!
      Licha ya Marekani angalia hapa Afrika out of 53 states kuna raisi mmoja tu Mwanamke! Middle East Hakuna!
      Kwa hiyo wakati wanawake ndo wanasoma kwa wingi sasa wanasoma viti maalumu muhimu. Otherwise basi CCM waamue baadhi ya majimbo wagombee akina mama tu (say 40% of majimbo)- ila hii itakuwa ni ukiukaji wa haki za wanaume who are capable! Angalia hata waliojitokeza kugombea CCM- 85% ni wanaume!
      Rome was not built in one day!
      Halafu Bubu angalia hata hapa JF wengi ya wanawake wanaongea tu- pamoja huwa ni wasomi wazuri- ukiwaambia wagombee- wapi?

    23. Miaka 50
    Page 1 of 3 123 LastLast

    Similar Topics

    1. Kwa akina dada na hii mnasingiziwa?
      By Judgement in forum Jokes/Utani + Udaku/Gossips
      Replies: 24
      Last Post: 28th November 2011, 12:38
    2. swali kwa akina dada tu!
      By Jakubumba in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 36
      Last Post: 27th October 2011, 18:42
    3. Akina dada hii imekaaje?
      By KakaKiiza in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 12
      Last Post: 20th September 2011, 13:46
    4. Replies: 47
      Last Post: 11th February 2011, 12:35
    5. Avatar za akina dada
      By Quinine in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 64
      Last Post: 7th February 2011, 13:51

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...