Hivi sasa nchi yetu inashuhudia mzozo mkubwa wa kdini ambao mpaka sasa umegharimu maisha ya watu, mali, nyumba za ibada nk kinyume kabisa na mazoea yawatanzania.
Hata hivyo tatizo hili limesababishwa na mambo yafuatayo:
Kwanza, tabia ya watanzania/waumini wa dini kutikuwa na tabia ya kujisomea. Waumini wengi hususani vijana hawana utaratibu wakusoma vitabu vya dini ie quran na au biblia. Hali hii imewafanya wahuni wachache kutumia mwanya huu kufundisha na kutafsiri aya za misahafu hii kwa kupotosha ili kulenga maslahi/matakwa/hisia zao binafsi. Mathalan, Uislam (waislam) ambao hasa ndo unalalamikiwa zaidi kwa kuwa sababu ya haya matatizo (mauaji, uharibu wa mali nk) hakuna sehemu unafundisha mauaji holela ya kikatili kama haya. Isipokuwa baadhi ya mashekhe/maustaadh mfano wa HASSAN ILONGA wameamua kufundisha chuki tofauti kabisa na Uislam wa MOHAMMAD (SAW). Kiukweli uislam anaoufanya mtu kama ILONGA na ule wa mtume (SAW) ni tofauti sana.
Pili, Kutojulikana vizuri kwa historia ya nchi zetu ie Tanganyika na Zanzibar. Hii imesababishwa na vijana wengi kutokuwepo wakati wa kupigania uhuru/mapinduzi-wachache sana wamebahatika kusoma historia hizi shuleni lakini wengi zaidi hata hii historia ya kusoma hawaijui. Wengi wanalalamika kuhusu Zanzibar kujitenga na Tanganyika-hii siyo sawa. Mfano, wazanzibar tunaingizwa kwenye mtego ambao hatuujui na watu wa aina ya MAALIM SEIF S. HAMAD, SHEKHE FARID WA UAMSHO nk ambao wanadai ZANZIBAR TUSISHEREHEKEE SIKUKUU YA MAPINDUZI BADALA YAKE TUSHEREHEKEEUHURU WA '63 ALIOPEWA MWARAB.Hawa wamekuwa wakihamasisha wazanzibar kudai kujitoa kwenye muungano kwa kutumia MWAMVULI WA DINI-UISLAM ILI KUPATA KUUNGWA MKONO. Laiti wanzanzibar tungejua adma ya watu hawa ( MAALIM SEIF, FARID, UAMSHO nk ) tungekataa haraka, tunaingizwa menge kwa kutuchonganisha wa ndugu zetu watanganyika ili wapate KURUDISHA WAARAB KWA MGONGO WA UHURU WA '63 WA ZANZIBAR.
Muungano haujaleata ukristo zanzibar. ukristo umekuwapo zanzibar miaka mingi sana tu kabla ya Uhuru. Mfano kanisana Anglikan la Mkunazini limejengwa mwaka 1873, mikaka takriban 91 baadaye
ndo muungano unatokea.
Tatu, Uongozi mbovu. Viongozi wengi tuliowachagua ili kushughulikia matatizo yetu wamegeuka nafasi zao kuwa pahala pa kujipatia neema binafsi huku watanzania wengi tukiendelea kuwa masikini. Ndiyo maana vijana wameendelea kutumiwa sana kwenye vurugu hizi bila hata kufikiria kwa sababu tu wameahidiwa kitu kidogo, na wajanja wachache wamewalaghai kuwa tatizo la umaskini limesabababishwa na ukristo!!!
----------------------WAY FORWARD---------------------
1. Siku za sherehe za MAPINDUZI/MUUNGANO/UHURU wazee wangesaidia kutoa historia za nchi zetu hadharani ili kila mwanachi aijue vizuri nchi yake na malengo ya Uhuru/Mapinduzi badala ya hawa wazee kuletwa tu uwanjani tunawaona then wanaondoka bila kutuambia lolote kuhu nchi zetu.
2. Waumini wa dini tusome vitabu vyetu ili itusaidie kutopotoshwa na mashekhe/wachungaji/mapadre wahuni kwa kisingizio cha nafasi zao. Hakuna mtu mwenye hodhi(monopoly) ya elimu. Kuwa shekhe/mchungaji/padre haimaanishi wanajua kuliko sisi waumini/maamuma.
3. Viongozi wa serikali simamieni utawala bora wa sheria. Acheni visingizio. Kuna baadhi ya viongozi, majina yapo, wameshindwa kutekeleza wajibu wao badala yake wanakimbia kwenye misikiti/makanisa kujisafisa eti wanatengwa na wenzao wa dini tofauti hali ambayo huchochea chuki miongoni mwa wananchi.
Watanzania pia tuamke. Tuache kujitenga kwa dini/kabila/ukanda nk. Tukomae na viongozi hawa wababaishaji watimize wajibu wao.Tunaona jinsi elimu inavyoshuka nchini, badala tukae pamoja, tuseme pamoja, tunaanza kutengana eti oh, waislam tunafelishwa nk.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, HEKIMA, UMOJA NA AMANI ND NGAO ZETU!!!!!!!!



Follow Us Here