| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 327
|
||||||||||||
|
#2
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
hata wakati wa kukusanya maoni ya vyama vingi 80% ya watanzania walikuwa hawataki vyama vingi..same thing here na FEDERATION itakuja tuu na kitu kizuri sana,dunia ya leo hatutaki kubanwabanwa acha tupanue nchi na uhuru wa kwenda popote na kufanya chochote as long as unaheshimu sheria na ujinga kama watu wa BOT na Richmond nakuhakikishia hautatokea
|
|
#3
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Date::10/23/2008
Shirikisho A. Mashariki lapigwa mwereka Na Ramadhan Semtawa Mwananchi UAMUZI wa wakuu wa nchi 26 za Afrika kuunganisha soko la pamoja katika nchi hizo, umeondoa ndoto ya kuanzisha shirikisho la kisiasa la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hatua hiyo inatokana na mpango wa wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Soko la Pamoja kwa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (Comesa), kuanzisha mchakato huo ambao utameza mambo ya jumuiya hizo. Shirikisho la Afrika Mashariki linahusisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi na Rwanda na tayari nchi hizo zilishapiga hatua kubwa kuelekea kuwa kitu kimoja, huku mabilioni ya fedha yakiwa yametumika katika mchakato huo, ambao pia ulihusisha kutafuta maoni kwa wananchi. Baadhi ya taasisi za Shirikisho la Afrika Mashariki zilishaanza kufanya kazi, ikiwemo sekretarieti inayoratibu shughuli zote za shirikisho hilo, bunge, mahakama huku mamilioni mengine yakitumika kujenga ofisi za makao makuu mjini Arusha, lakini uamuzi uliofanywa juzi unaweza kuwa mwanzo za kuzorota kwa harakati hizo. Akijibu swali kutoka gazeti hili kuhusu uamuzi huo wakuu wa nchi 26 uliofanywa nchini Uganda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe alisema ni dhahiri hapo baadaye kama mchakato utakwenda kama ulivyo, shirikisho hilo halitakuwepo. "Dah..., ndiyo, halitakuwepo, kadri tunavyokwenda katika mpango huu wa kuunganisha soko la nchi zetu hizo za jumuiya tatu, ni dhahiri kuna mambo yatabidi yajiondoe," alisema. Membe alifafanua kuwa mpango huo wa kuunganisha jumuiya tatu unalenga kuwezesha kuwepo soko kubwa la pamoja la watu 527 milioni na mfumo wa forodha. Hata hivyo, alisema mchakato wa kuelekea soko la pamoja kwa EAC bado unaendelea na kwamba, kama ni kusitishwa, basi hiyo itakuja kufahamika baadaye baada ya mchakato wa jumuiya hizo tatu. "Lakini mchakato ndani ya EAC ambao tumefikia sasa kuhusu Common Market (soko la pamoja), bado unaendelea, huku taratibu za soko jipya nazo zikiendelea,"alifafanua. Membe alisema katika mchakato huo wa jumuiya tatu, wakuu hao wameunda timu ya kuangalia taratibu za kisheria kwa ajili ya kutafuta uhalali wa jambo hilo. "Sasa, katika kufanikisha mpango huo wa kuanzisha soko kubwa kwa kuunganisha Comesa, Sadc na EAC, wakuu wameamua kuunda timu ya wataalamu ambayo itafuta uhalali kisheria," alisisitiza. Kwa ufafanuzi, Membe alisema timu hiyo itafanya kazi kwa kipindi cha miezi sita kuona njia bora za kuweza kufanikisha ndoto hiyo. Alisema kuanzishwa kwa soko kubwa la pamoja katika ukanda huo kwa kuunganisha ukanda wa Kusini, Kati na Mashariki ya Afrika hadi Misri, kutakuwa na faida kubwa kwa maendeleo ya ukanda huu. "Kwa hiyo, kuanzisha Free Trade Area, kuna manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kuweza kukaribiana na matatizo mbalimbali kama misuko misuko ya kuanguka kwa taasisi za kifedha katika mataifa makubwa," alisisitiza. Membe alisema eneo hilo lina wakazi hao 527 milioni kati ya idadi jumla ya wakazi wa Afrika ambao ni 940 milioni, ambao wanachukua sehemu kubwa ya bara hilo. Waziri Membe alitetea kuwa China imekuwa ikipata maendeleo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu hivyo biashara inayofanyika nayo pia huwa kubwa. Katika Shirikisho la Afrika Mashariki inatarajiwa kuwapo maingiliano makubwa zaidi ya kiuchumi na biashara, pia kuondolewa vikwazo vya kufanya kazi baina ya mataifa hayo pamoja na masuala muhimu ya uwekezaji katika ardhi suala ambalo limezua utata miongoni mwa mataifa hayo, huku mengine yakipinga hatua hiyo. Katika hatua nyingine, Membe alisema wakuu hao wamejadili kwa kina mambo yanayoendelea katika nchi za Somalia, Burundi na Mauritania. Alisema kwa upande wa Burundi msuluhishi wa mgogoro huo ambaye ni Waziri wa Usalama wa Afrika Kusini, Charles Nqakula, alitoa utekelezaji wa mpango wa amani nchini humo. Hata hivyo, alisema hadi sasa mpango huo umekwama kutokana na kundi la FNL Palipehutu lilanalongozwa na Agathon Rwasa, kukaata kubadili jina la kundi hilo ili kuondoa dhana ya ukabila ambayo inapingana na katiba. Kuhusu kuingizwa katika serikali, alisema kundi hilo linadai kuwa na jeshi kubwa msituni ambalo ni takriban askari 21,000 lakini linashindwa kuthibitisha huku likidai fedha nyingi kwa ajili ya kuwalipa.
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 06:33 AM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||