JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Zanzibar: Padre apigwa Risasi na watu wasiojulikana

  Report Post
  Page 11 of 23 FirstFirst ... 910111213 21 ... LastLast
  Results 201 to 220 of 441
  1. #1
   DSN's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd February 2011
   Location : Home Tanzania
   Posts : 2,663
   Rep Power : 4836
   Likes Received
   1498
   Likes Given
   2889

   Default Zanzibar: Padre apigwa Risasi na watu wasiojulikana

   Kwa mujibu wa Breaking News Sasa hivi toka Radio One, Padre anayejulikana kwa jina la Ambrose Mkenda amepigwa Risasi na Watu wasiofahamika kwenye gate la nyumbani kwake wakati akifunguliwa gate aingie nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar, ambako ndiko makazi yake yalipo akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha pekee yake.

   Hali yake sio nzuri kwani Risasi aliyopigwa imemdhuru maeneo ya mdomoni.

   Waliompiga Risasi Padre huyo inasemekana ni watu waliokuwa kwenye pikipiki, ambao walimvamia akisubilia afunguliwe gate kuingia nyumbani kwake.

   Kuna nini? Katika siku muhimu kwa waumini wa Kikristo kufanyika kwa tendo kama ilo kwa kiongozi wa madhehebu makubwa kama Roman Catholic.

   Wanaojua kinachojili huko Zanzibar watujuze Tafadhari kulikoni, katika siku njema kama hii ya Christmas.

   NOTE:
   Ujumbe Mkuu wa Kanisa La Roman Catholic katika Christmas ya mwaka huu 2012:
   "UPENDO NA AMANI NDIO UJUMBE MKUMBWA WA SIKUKUU HIYO"


   Picha kwa niaba ya Mwanajamii forum kwa ID ya Mchami


   TAARIFA YA LEO TAREHE 26/12/2012 KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUKIO:
   Father Ambros Mkenda wa Parokia ya Mpendae katika Kanisa Katoliki Mjini Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake majira ya saa 12 jioni wakati akitokea kanisani

   Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma Mohammed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema Father amepigwa risasi na ameumizwa sehemu ya kichwa na amekuwa akitoka damu nyingi kichwani na tayari anapatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.

   Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wahusika walifanya uhalifu huo kwa madhumuni gani kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

   “Sisi tunahesabu kuwa kitendo hiki ni kitendo cha kihalifu na tunawatafuta wahalifu waliofanya kitendo hiki kwa hivyo bado ni mapema kusema kwamba kitendo hiki kimefanywa na nani kwa kuwa bado uchunguzi wetu unaendelea na hadi sasa hakuna mtu tuliyemshika kuhusikana na tukio hili” alisema Kamanda.

   Kamanda Aziz akisimulia tukio hilo alisema walipata taarifa majira ya saa 2 na kwenda katika eneo la tukio ambapo Father alikuwa akitokea kanisani na kutaka kuelekea nyumbani kwake wakati akiwa ndani ya gari ndipo aliposhambuliwa na watu wasiojulikana na kuanguka.

   “Tumekuta mabaki ya risasi ndani ya gari yake na katika vioo vyake vya gari vimevunjika na tumekuta damu chini pale” alisema Kamanda.

   Aidha Kamanda Azizi alisema Father Ambros yeye ni mhasibu pale kanisani na hivyo mara nyingi watu wananaamini kwamba katika siku za krismass mara nyingi sadaka hukusanywa fedha nyingi na hivyo wanamini kwamba alikuwa fedha mikononi na ndipo inawezekana waliamua kumpiga risasi wakitaka kuchukua fedha hizo.

   Hata hivyo alisema uchunguzi wa awali ndio utakaoeleza ni suala gani lililopelekea kupigwa risasi lakini wanaendelea na uchunguzi huo ambapo uchunguzi ndio utakaojulikana sababu kamili ya tukio hilo.

   Akizungumzia tukio hilo, Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikan la Mkunazini amesema wamesikitishwa na wamepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo hasa kwa kuzingatia matukio kama hayo hayajawahi kutokea ya kuwahujumu viongozi wa dini.

   Alisema tukio hilo ni miongoni mwa matukio ya kushtusha na yanaashiria hali mbaya ya kiusalama na kuwaomba viongozi wa serikali kuchukua hatua za tahadhari kubwa kwani matukio kama hayo yameanza kutokea kwa viongozi wa dini ambapo mwanzo ilianzia kwa Sheikh Soraga na baadae kutokea kwa Father Ambros.

   “ Hii ni hali ya hatari katika nchi yetu na haipendezi lakini serikali lazima ijue sisi hatuwezi kujua wala hatuwezi kujilinda lakini serikali inapaswa kutulinda sisi ndio wananchi wake” alisema Askofu Hafidh.

   Askofu Hafidh alisema hivi karibuni kumekuwepo vipeperushi vilivyosambazwa na watu vikiwatisha watu wenye imani ya kikristo ambapo alisema miongoni mwao walikuwa na khofu juu ya kusambazwa kwa vipeperushi hivyo na kuiomba serikali iongeze ulinzi.

   “Tumeona hivi vipeperushi na kwa kweli tulikuwa na khofu juu ya vipeperushi hivi lakini ndio tunasema tunaelekea wapi katika maisha haya” alisema Akofu Hafidh.

   “Sisi hatuamini kwamba kuna kisasi kwa viongozi wa dini lakini tunachukulia hilo ni tukio la kihalifu na pia hatuna vipeperushi vya aina yoyote vinavyoelezea kuwatisha viongozi wa dini kwa hivyo tunachukulia hayo ni matukio ya kihalifu na wala hatuamini kwamba matukio haya ni ya dini fulani” alisema Kamanda Azizi.

   Akielezea kuhusiana na hilo Kamanda Aziz alisema jeshi la polisi limejipanga na kuzidisha ulinzi katika maeneo yote ya makanisa ambapo kumesambazwa polisi wa kutosha kwa kuwa wanajua wakati wa sherehe mambo ya kihalifu hujitokeza.

   “Sisi kawaida huwa tunaweka ulinzi siku za sherehe zozote lakini kwanza makanisa yote yamewekwa ulinzi wa kutosha kabisa lakini wahalifu wanapotaka kufanya uhalifu huwezi kujua watatumia mbinu gani na saa ngapi na watafanya uhalifu huo wapi, lakini ulinzi upo wa kutosha” alisisitiza Kamanda Aziz.
   Last edited by DSN; 26th December 2012 at 11:08.


  2. hodogo's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 11th March 2012
   Posts : 239
   Rep Power : 541
   Likes Received
   91
   Likes Given
   60

   Default Re: Zanzibar: Padre adaiwa kupigwa Risasi

   Quote By Mdondoaji View Post
   Kim ,

   Shida watu wanaumwa bado na propaganda za udini. Ila wakristo ndugu zanguni ni vema mtafakari hili swala la mfumo kristo nchini. Ubaguzi unaondelea unajenga chuki na matabaka na mwishoe kila jambo linatfsiriwa kwa udini na chuki.

   Nilikuwapo

   Falsafa ya mfumo kristo ni falsafa mufilisi inayobebwa na watu waliofilisika kifikra, ambao wanajitahidi "kuibaka" historia kwa kutoa hata takwim bila tathmini ya kitaalamu.

   Kwa mtazamo wako Mdonoaji, kujaribu kuturejesha kwenye mada hii wakati tukitafakari vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani nchini, inatia shaka, inawezekana wewe ni msemaji wa hiki kikundi na unajaribu kupima joto la jamvi!

  3. kelao's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2012
   Posts : 3,241
   Rep Power : 40163
   Likes Received
   610
   Likes Given
   800

   Default Re: Zanzibar: Padre adaiwa kupigwa Risasi

   So sad!lakini kama ni uchokozi dhidi ya kanisa Catholic wajue watapata matatizo makubwa.tunamwombea huyo padre apone haraka.hao watu wanaosukuma hayo mambo ya kidini Mungu atawashushia mkono wake wenye nguvu.

  4. dkirenga's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 21st December 2012
   Posts : 192
   Rep Power : 492
   Likes Received
   22
   Likes Given
   1

   Default Re: Zanzibar: Padre adaiwa kupigwa Risasi

   Asalaa wana JF kweli inaumiza sana kuwadhuru viongozi wa dini tupate wapi Amani ndugu zangu

  5. kwamwewe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th July 2010
   Posts : 1,117
   Rep Power : 5589
   Likes Received
   138
   Likes Given
   162

   Default Re: Zanzibar: Padre adaiwa kupigwa Risasi

   Quote By Buntungwa View Post
   Tumechoshwa na kauli za kijinga namna hii.
   kauli nyengine za kijinga ni kama hizi, hasa watu wanapokuwa hawataki kuoa na kupenda kuchukua vya watu

   yaweza kutokea hata haya

   KARIBU MLIMA SAYUNI...UWANJA WA UWAZI NA UKWELI KUHUSU MASUALA YOTE YA KIBIBLIA NA UKRISTO: Mchungaji Auwawa kwa baada ya kufumaniwa


   kauli nyengine za kijinga ni hizi http://www.bongo5.com/padri-atiwa-mb...-kifo-05-2007/

  6. kelao's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2012
   Posts : 3,241
   Rep Power : 40163
   Likes Received
   610
   Likes Given
   800

   Default

   Quote By Bilal Yussuf View Post
   please msikimbilie kujenga hoja au kuhusisha jambo hili na udini mana inawezekana padri ana visasi na kundi ama mtu fulani nje au ndani ya kanisa.
   naomba tuliachie jeshi la polisi lifanye kazi yake kisha tusubiri ripoti yao itakavyo sema.
   jeshi la police lipi ndugu yangu? Hili hili la CCM au lingine!


  7. hodogo's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 11th March 2012
   Posts : 239
   Rep Power : 541
   Likes Received
   91
   Likes Given
   60

   Default Re: Zanzibar: Padre adaiwa kupigwa Risasi

   Quote By abdul 28 View Post
   uthaifu wa watanganyika jamii forums
   1) kushindwa kufikiria nini chanzo matatizo ni nini
   kulisukuma au kulihusisha tatizo hili na uamsho
   kushabikia udini
   vipi mtu haija thibitishwa hata na serekali ukurupuke na kusema uamsho hao
   jiulize kwa nini uamsho haijafutwa kisheria


   CHANZO CHA MATATIZO CCM NA SEREKALI YAKE KUTUMIA SERA YA DINI KUFICHA UHALISIA HILI HALITA WASAIDIA
   utamsikia kesho kutwa Benard Member atawambia umoja wa EU na jumuiya za kimataifa ya kuwa uwamsho wameuwa Padri zanzibar waisilamu wanawaonea waikristo zanzibar
   hii ni kuificha dhana ya wazanzibar kudai nchi yao juu ya jumuiya za kimataiofa

   zanzibar matokeo ya kuuliwa viongozi wa dini sio mageni askari wa FFU walimpiga shekhe wa msikiti wa mtendeni risasi ndani ya msikiti na ziko kesi nyingi ila hawa askari ubaya ubaya huzizima kutiwa tindi kwa shekhe suraga

   sasa wana jamii fikirieni kwa makini hasa watanganyika
   ccm na serekali yake wasipindishe mnadai ya uamsho uamsho wanataka nchi yao sio chengine huu ni udhaifu wa ccm na raisi wao usalama wa taifa na polisi
   Wewe ni msemaji wa uamsho? Hujashuhudia serikali ikionekana kama inafumbia macho baadhi ya matukio katika jamii kutokana na mgongano wa masilahi kwa watendaji hao serikalini?

   Ndio maaana marehemu Baba wa Taifa alipokua anasisitiza dhamira Za kauli za kisiasa kuendana na matendo katika maisha halisi ya wanasiasa, alitumia kauli kama "KUIMBA KIJAMAA NA KUCHEZA KIBEPARI!" Ishi unachokihubiri na kukiamini! Ndo maana siku hizi wanasiasa wanadai kupiga vita ufisadi ili hali wenyewe ni mafisadi wakubwa!!

  8. Otorong'ong'o's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th August 2011
   Location : Uvunguni
   Posts : 20,084
   Rep Power : 241984751
   Likes Received
   4857
   Likes Given
   2380

   Default Re: Zanzibar: Padre adaiwa kupigwa Risasi

   Ohhh my God....nini tena jamani..sasa nakumbuka ule uzi wa Mzee Mwanakijiji.

  9. Zuwely salufu's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 7th October 2012
   Posts : 107
   Rep Power : 485
   Likes Received
   18
   Likes Given
   0

   Default Re: Zanzibar: Padre apigwa Risasi na watu wasiojulikana

   Amani itawale znz kwa nini znz?

  10. Elizabeth Dominic's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 7th December 2007
   Posts : 4,560
   Rep Power : 429498058
   Likes Received
   3561
   Likes Given
   3974

   Default Re: Zanzibar: Padre apigwa Risasi na watu wasiojulikana

   Nakuombea upone Pd. Sad indeed.........Kikwete and co mmeifanyia nini nchi yetu sasa?
   Enyi mnaoumiza binadamu wenzenu kwa udini na unafiki mwengine SHAME be upon you, hakika mtalipwa stahiki zenu

  11. Kapwila Matulu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th March 2009
   Location : Lumo Kigilagila
   Posts : 7,485
   Rep Power : 6459
   Likes Received
   2633
   Likes Given
   710

   Default Re: Zanzibar: Padre adaiwa kupigwa Risasi

   Quote By abdul 28 View Post
   utamsikia kesho kutwa Benard Member atawambia umoja wa EU na jumuiya za kimataifa ya kuwa uwamsho wameuwa Padri zanzibar waisilamu wanawaonea waikristo zanzibar
   hii ni kuificha dhana ya wazanzibar kudai nchi yao juu ya jumuiya za kimataiofa
   Sasa kudai nchi ya Zanzibar ndio Padri apigwe risasi? Wazanzibari waisilamu hawana akili kabisa

  12. Kapwila Matulu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th March 2009
   Location : Lumo Kigilagila
   Posts : 7,485
   Rep Power : 6459
   Likes Received
   2633
   Likes Given
   710

   Default Re: Zanzibar: Padre apigwa Risasi na watu wasiojulikana

   Quote By Mdondoaji View Post
   ... Ila wakristo ndugu zanguni ni vema mtafakari hili swala la mfumo kristo nchini.
   Zanzibar nako mnadai kuna mfumo Kristo? Huu wimbo wajinga wachache wamewakaririsha wajinga wengi, kila kitu mfumo Kristo!

  13. Mponjori's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st February 2011
   Location : ukarawa
   Posts : 2,213
   Rep Power : 1057
   Likes Received
   530
   Likes Given
   21

   Default

   Quote By Kitimoto View Post
   Leo alikuja kijana amevaa kanzu nyumbani kwangu akiomba msaada wa fedha kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto yatima, kwa kifupi nilimwambia sina pesa. Ni mara ya nne kuja, siku za nyuma walikuwa wawili, walishakuja wakiomba mchango kwa ajili ya ujenzi wa icho kituo nikawapatia. Wakaja tena wakiomba kwa ajili ya ujenzi wa Madrasa nikawapatia, wakaja kwa ajili ya watoto yatima nikawapatia.

   Baada ya haya majanga wanayoyafanya kwa sisi Wakristo nimesitisha michango na najuta kuwapa michango siku za nyuma. Kwa hii habari ya leo akija/wakija nitamwambia/nitawaambia wazi aende/waende kutafuta michamgo kwa waislamu wenzao.
   mkuu nakushauri uendelee mungu atakulipa. Onyesha tofauti

  14. MUNDALI WA ILEJE's Avatar
   Member Array
   Join Date : 27th September 2012
   Posts : 32
   Rep Power : 472
   Likes Received
   9
   Likes Given
   0

   Default Re: Zanzibar: Padre apigwa Risasi na watu wasiojulikana

   Da sasa wanatupeleka kubaya ndugu zangu wameanza na viongoz wa dini

  15. mchemsho's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th June 2011
   Location : MotherLand
   Posts : 2,967
   Rep Power : 1313
   Likes Received
   563
   Likes Given
   267

   Default Re: Zanzibar: Padre apigwa Risasi na watu wasiojulikana

   get well soon catholic Father....aliyepigwa risasi ni binadamu mwenye nyama anaumia pia, hayo ya utumishi polisi ndio watatithibitishia kwamba alipigwa risasi sababu ya utumishi wake au la! again , get well soon!

  16. mpemba mbishi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th November 2011
   Posts : 1,131
   Rep Power : 0
   Likes Received
   177
   Likes Given
   0

   Default Re: Zanzibar: Padre apigwa Risasi na watu wasiojulikana

   Sheikh Farid= Alijiteka mwenyewe

   Sheikh Soraga= Alijimwagia mwenyewe

   Padri Mkenda= Kajipiga mwenyewe.

   Hapo sioni kama kuna tatizo tusikuze Mada au vyenginevyo tuwalaumu wenyewe na au tuwaulize kwanini hua wanafanya hivi?

  17. Mmwaminifu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th October 2010
   Posts : 988
   Rep Power : 872
   Likes Received
   165
   Likes Given
   96

   Default

   Quote By mpemba mbishi View Post
   Huyo Padri kajipiga mwenyewe ili achafue mazingira! Kuna tabia ya VIONGOZI WA DINI wa Zanzibar kujifanyia matukio wenyewe au mumeshaanza kusahau wajameni!!
   mh! Hapa unamaanisha ana akili sawa na yule aliyejiteka.

  18. #217
   Tewe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th January 2008
   Posts : 609
   Rep Power : 833
   Likes Received
   92
   Likes Given
   12

   Default

   Vita vyetu si juu ya damu na nyama ila ni juu ya falme na mamlaka

  19. Mmwaminifu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th October 2010
   Posts : 988
   Rep Power : 872
   Likes Received
   165
   Likes Given
   96

   Default

   Quote By mpemba mbishi View Post
   Sheikh Farid= Alijiteka mwenyewe

   Sheikh Soraga= Alijimwagia mwenyewe

   Padri Mkenda= Kajipiga mwenyewe.

   Hapo sioni kama kuna tatizo tusikuze Mada au vyenginevyo tuwalaumu wenyewe na au tuwaulize kwanini hua wanafanya hivi?
   Mkuu. Hii analysis yako unataka kumaanisha nini?

  20. Kapwila Matulu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th March 2009
   Location : Lumo Kigilagila
   Posts : 7,485
   Rep Power : 6459
   Likes Received
   2633
   Likes Given
   710

   Default Re: Zanzibar: Padre adaiwa kupigwa Risasi

   Quote By dudus View Post
   Naona hatuelewani, labda niulize kivingine: Nitajie nyumba za ibada, viongozi, na waumini wa dini ambao ni walengwa "maalumu" wa Kony kwenye mashambulizi yake. Huko Zanzibar tumeshuhudia dini fulani tu ikilengwa kwenye mashambulizi; kwa ufananisho huo, nitajie upande wa Kony.
   Huyo KIM KARDASH hawezi kukuelewa mkuu, si unajua elimu zao!

  21. Queen Kyusa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th April 2011
   Posts : 631
   Rep Power : 666
   Likes Received
   136
   Likes Given
   166

   Default

   Quote By abdul 28 View Post
   uthaifu wa watanganyika jamii forums
   1) kushindwa kufikiria nini chanzo matatizo ni nini
   kulisukuma au kulihusisha tatizo hili na uamsho
   kushabikia udini
   vipi mtu haija thibitishwa hata na serekali ukurupuke na kusema uamsho hao
   jiulize kwa nini uamsho haijafutwa kisheria


   CHANZO CHA MATATIZO CCM NA SEREKALI YAKE KUTUMIA SERA YA DINI KUFICHA UHALISIA HILI HALITA WASAIDIA
   utamsikia kesho kutwa Benard Member atawambia umoja wa EU na jumuiya za kimataifa ya kuwa uwamsho wameuwa Padri zanzibar waisilamu wanawaonea waikristo zanzibar
   hii ni kuificha dhana ya wazanzibar kudai nchi yao juu ya jumuiya za kimataiofa

   zanzibar matokeo ya kuuliwa viongozi wa dini sio mageni askari wa FFU walimpiga shekhe wa msikiti wa mtendeni risasi ndani ya msikiti na ziko kesi nyingi ila hawa askari ubaya ubaya huzizima kutiwa tindi kwa shekhe suraga

   sasa wana jamii fikirieni kwa makini hasa watanganyika
   ccm na serekali yake wasipindishe mnadai ya uamsho uamsho wanataka nchi yao sio chengine huu ni udhaifu wa ccm na raisi wao usalama wa taifa na polisi
   Sasa mkuu kama wanadai nchi yao ndo washambulie wakristo hao ndo wameshika nchi yao! Hata kama mnasema tz ina mfumo kristo mbona znz imejaa waislamu huo mfumo kristo upo wapi


  Page 11 of 23 FirstFirst ... 910111213 21 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...