Wimbo ulioimbwa na mashabiki wa timu ya soka ya Ujerumani ya FC Schalke 04 inayoshiriki ligi kuu nchini humo umewakasirisha waislamu baada ya mashabiki hao kumhusisha mtume Muhammad katika nyimbo yao.
Washabiki wa FC Schalke 04 ambayo inashiriki ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga wamewakasirisha waislamu kwa kumuimba mtume Muhammad katika nyimbo yao ya kuishangilia timu yao.
Ubeti wa tatu wa wimbo huo ulikuwa na maneno "Muhammad alikuwa ni mtume ambaye alikuwa hajui chochote kuhusiana na soka".
"Lakini katika rangi zote nzuri duniani, alipenda rangi ya Bluu na Nyeupe (rangi za timu ya Schalke)".
Klabu hiyo ilitumiwa mamia ya email toka kwa waislamu wenye hasira baada ya vyombo vya habari vya Uturuki kutoa ripoti za wimbo huo.
Polisi wa mji wa Gelsenkirchen, inapotokea timu hiyo, walisema kuwa wameyapokea na wanayachunguza malalamiko ya waislamu kwa umakini zaidi.
Mkuu wa baraza la waislamu wa Ujerumani, Aiman Mazyek, alisema kuwa baraza la waisalamu halina mpango wa kuupiga marufuku wimbo hao lakini linataka maelezo zaidi kujua chanzo na sababu za kutolewa kwa wimbo huo.
Website ya shirika la habari la Ujerumani, Deutsche Welle ilisema kwamba wimbo huo unaoitwa "Bluu na nyeupe, jinsi ninavyokupenda" ulitungwa mwaka 1924 lakini haijulikani ni lini ubeti unaomzungumzia mtume uliingizwa kwenye wimbo huo.
Klabu ya FC Schalke 04 ilisema kuwa imepokea malalamiko mengi kwa njia ya email na simu na wanayafanyia kazi malalamiko hayo baada ya waislamu kutishia kuanzisha kampeni za kususia mechi za timu hiyo iwapo wimbo huo hautafutwa au ubeti huo kuondolewa katika wimbo huo.
FC Schalke 04 imewaomba wanazuoni wa kiislamu nchini humo waupitie tena wimbo huo kujua kama unaukashifu uislamu au la.

Reply With Quote

Follow Us Here