Jamani jamani tusitake kutibuana akili hapa, mie kila leo napata kizunguzungu juu ya kazi halisi ya mheshimiwa PM wetu na hadi bado kwa kweli sijajua. Ebu oneni hapa sasa, amekuwa kama kiranja wa chekechea.
Lowassa kuwauliza wakuu watatu wa mikoa kwanini timu za mikao yao hazikuhudhuria mashindao ya raidha.
By Saidi Nguba | Published 06/29/2007 | Habari Mpya | Unrated
WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amesema atawauliza Wakuu wa Mikoa ya Kigoma, Lindi na Mtwara kwa nini timu za mikoa yao hazikufika kwenye mashindano ya kitaifa ya riadha aliyoyafungua mjini Dodoma leo (Ijumaa Juni 29, 2007).
“Nakutana nao Jumatatu saa 7.30 mchana na nitawauliza kwa nini timu za mikoa yao hazikuja Dodoma,” alisema Lowassa alipokuwa akiyafungua mashindano hayo ya 46 ya siku mbili, kwenye uwanja wa Jamhuri.
Aliongeza: “Nimeamua kuja hapa kwa sababu michezo ya riadha imekuwa ikiendelea vizuri sana miaka ya nyuma, lakini sasa imezorota…nataka tusaidiane tuifufue.”
Wakuu wa mikoa 21 ya Tanzania Bara wako Dodoma kusikiliza kikao cha Bunge, hasa wakati huu wa makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inajumuisha Tawala za Mikoa na Serikalia za Mitaa.
Jumatatu mchana watakutana na Waziri Mkuu kujadili namna ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2007/2008.
Waziri Mkuu Lowassa alisema kuwa Tanzania ina vipaji vingi vya riadha na akawataja wanariadha mashuhuri duniani waliotokea hapa nchini ambao ni pamoja na Philbert Bayi, Suleiman Nyambui, Juma Ikangaa, Francis Naali na John Yuda.
Wengine ambao ni wanawake aliowataja kuwa walifanya vizuri ni pamoja na Mwinga Mwanjala, Nzael Kyomo na Restituta John.
“Wote hawa ni uthibitisho kuwa tuna vipaji vya kuosha kutupatia sifa katika nchi yetu…ni jukumu la vyama vya michezo kushirikiana na Serikali kukuza vipaji mbalimbali vilivyoko nchini,” aliongeza.
Katika ufunguzi huo, wanariadha walishindana mbio za mita 400 wanawake na mita 5000 wanaume na mita 200 kwa walemavu ambazo Waziri Mkuu alizishuhudia.
Alitoa medali kwa Luiza John aliyeshinda mita 400 wanawake; Dickson Marwa, mita 5000 na Wilbrod Constantine, mita 200 walemavu.
Waziri Mkuu pia alimwelekeza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Margareth Sitta ambaye alikuwepo uwanjani, kueleza, ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, lini mashindano ya michezo ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu yatarejeshwa baada ya kusitishwa mwaka 2003.
Mapema risala ya Shirikisho la Riadha Tanzania ilieleza kuwa ushiriki wa mikoa katika Mashindano ya Riadha ya Taifa haujawa mzuri tangu kusitishwa kwa mashindano ya shule.
suala la msingi, je nini outcome ya hayo aliyosema ? jibu, NOTHING.

Reply With Quote


Follow Us Here