Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Celtel yamdhamini Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro

    Report Post
    Results 1 to 3 of 3
    1. #1
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,874
      Rep Power : 19447
      Likes Received
      8655
      Likes Given
      28272

      Default Celtel yamdhamini Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro

      Ni katika harakati za kupambana na UKIMWI
      Na Mwandishi Wetu
      KAMPUNI ya simu za mkononi ya Celtel Tanzania, imetoa sh. milioni 40 kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo ili ashiriki kupanda Mlima Kilimanjaro.....



      Meneja Uhusiano wa Celtel Tanzania, Beatrice Mallya alisema Dar es Salaam jana kuwa Alhaj Mwinyi alikabidhiwa fedha hizo juzi mjini Moshi ikiwa ni mchango wa Celtel kumwezesha kushiriki Geita Kiliclimb Challenge kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya maradhi ya UKIMWI nchini Tanzania.

      Alisema Celtel kwa kushirikiana na kampuni ya mgodi wa madini ya dhahabu ya Geita, wamemwezesha Alhaj Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro ili kutekeleza dhamira yake ya kupambana na UKIMWI. Alhaj Mwinyi alianza kupanda mlima huo juzi (Jumamosi).

      Beatrice alisema Celtel ilianza kudhamini wapandaji Mlima Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka minne iliyopita na itaendelea kudhamini kwa vile inaamini nguvu na juhudi zinazotumika kupanda mlima huo, zinaleta matumaini ya kupambana na UKIMWI.

      "Tumefurahi zaidi kwamba mwaka huu Rais mstaafu, Alhaj Mwinyi anapanda Mlima Kilimanjaro kwa udhamini wa Celtel," alisema Beatrice na kubainisha kwamba kampuni hiyo pia mwaka huu inawakilishwa na Meneja wa Kitengo cha Fedha wa Celtel, Prisca Tembo kupanda mlima huo.

      Akizungumza baada ya kukabidhiwa kitita hicho cha fedha, Alhaj Mwinyi mwenye umri wa miaka 83, alisema amepata msukumo wa kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuendeleza juhudi zake katika mapambano dhidi ya UKIMWI, ikiwa ni njia mojawapo ya kuisaidia Tanzania na kutekeleza kauli mbiu ya Serikali kwamba Tanzania inawezekana bila UKIMWI.

      "Lengo letu ni kuhakikisha jamii inaishi katika maisha salama bila kupata maambukizi ya UKIMWI kama tunavyoshauriwa na wataalamu, kuzingatia muongozo uliopo," alisema Alhaj Mwinyi.

      Alisema alijisikia furaha na kuona fahari baada ya Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Celtel Afrika Mashariki, Bw. Bashar Arafeh kumweleza dhamira ya kampuni hiyo kumdhamini ili apande Mlima Kilimanjaro.

      "Niliona ufahari! Nilikuwa na shauku ya kupanda Mlima Kilimanjaro mwaka huu, lakini ahadi kutoka kwa Bw. Bashar iliniongezea matumaini na morali ya kupanda Mlima Kilimanjaro, kwa lengo lile lile la kupambana na maambukizi ya UKIMWI kwa watu wetu na taifa letu," alisema Alhaj Mwinyi.

      Alhaj Mwinyi aliishukuru Celtel kwa kumdhamini na mchango mkubwa ambao kampuni hiyo inatoa kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali hasa elimu.

      Global Publishers - Tanzania Newspapers


    2. #2
      Rikab Mikail's Avatar
      Member Array
      Join Date : 7th June 2009
      Posts : 16
      Rep Power : 514
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Celtel yamdhamini Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro

      Hiyo ya mwaka gani? Celtel nafikiri imekufa siku nyingi... je hii ni baada au kabla ya *~*?

    3. #3
      MpigaFilimbi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th April 2008
      Location : Uvunguni
      Posts : 1,089
      Rep Power : 786
      Likes Received
      127
      Likes Given
      76

      Default Re: Celtel yamdhamini Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro

      hawa naona wana agenda na huyu mzee kwa miaka hiyo 83 tusijekuambiwa sijui nini arrest!! wana uhakika ana mazoezi ya kutosha ya kupanda mlima mrefu kuliko yote Afrika?
      "If you are going through HELL, keep going..."-W.Churchill

    Similar Topics

    1. Ni muda gani mwanaume unatakiwa kumaliza kupanda mlima?
      By AZIMIO in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 34
      Last Post: 16th June 2011, 10:18
    2. Jamani nataka kupanda Mlima Kilimanjaro, naombeni msaada
      By sekulu in forum Business & Economic Forum
      Replies: 9
      Last Post: 6th June 2011, 10:17
    3. Walemavu kupanda mlima kilimanjaro
      By Steven Sambali in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 2
      Last Post: 1st October 2008, 01:35
    4. Mlima Kilimanjaro wazua mzozo
      By X-PASTER in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 9
      Last Post: 27th September 2008, 03:22
    5. Replies: 5
      Last Post: 15th June 2008, 23:54

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...