Habari na Hoja mchanganyikoUna jambo umeliona kutoka chanzo chochote cha habari? Usisite, liweke hapa uwahabarishe wenzako. Hoja binafsi pia ziwekwe hapa.
Kuna jamaa yangu kaniambia kwamba kuna hiyo association inaitwa TEDET (Tanzania Eco-Development Trust), kwamba inakusanya hela za wanachama kiingilio sh. laki 5 (500.000) ambayo inajumuisha kiingilio ada ya uanachama na shamba la ukubwa wa hekari 5 huko bonde la mto RUFIJI. Kasema makubaliano ni kwamba mwanachama anapewa hilo shamba heka 5, ila anakuwa analimiwa hilo shamba heka 4 mazao ya biashara na heka moja mazao ya chakula.
Mazao ya chakula atakuwa akipewa magunia 20 ya mahindi /mpunga kwa msimu yaani misimu miwili kwa mwaka, wakati mazao ya biashara yatakuwa yakiuzwa kwa pamoja masoko ya nje na kila heka ikikadiliwa kutoa mazao ya wastani wa thamani ya milioni 1.5, lakini mkulima atakuwa akikatwa laki 2 kila heka kama garama ya uendeshaji.
Kasema hiyo Tedeti inashirikiana na KIMUDEA umoja wa wakulima wilaya ya Kinondoni, na wakazi wa Rufiji chini ya umoja wao wa RUDIDEA na kwamba wanachama wanapelekwa kuonyeshwa mashamba huko Rufiji.
Nilipo search goggle nikakuta kweli hiyo kitu ilikuwepo toka mwaka 2006, na mwenyekiti wake ni Dr. Mugishagwe. Na kuna pesa mamilioni mengi, toka kwa wafadhili zimekuwa zikiingia huko TEDET, taarifa zipo ukigoogle za upokeaji wa pesa hizo. Hakuna taarifa zaidi kuhusu huu umoja, kilimo hata hizo ada za uanachama.. Kasema ofisi zao zipo MASASI HOUSE KARIAKOO?
Kweli nikaona maelezo yake ni mazuri, lakini nikapata hofu kwamba je hii haiwezi kuwa DECI ama PUFDEA nyingine? Manake hii kusanya ya kiingilio cha laki 5 kila mwanachama, na kasema wanatakiwa wanachama elfu 10,000. Na kasema wengi sana wamejiunga. Na ahadi ni kwamba wanaanza kilimo mwaka huu.
Ndipo nikaona pengine niimwage hapa kwenye Jamvi nene labda kuna wenye datas za uhakika nisije ingia mkenge wa DECI no.2
Na kama kweli si DECI, basi wanajamvi tuchangamkie uanachama kwani maelezo yake ni mazuri.
Naona kila mmoja anaongea kwa hisia na labda nyingi sana. mimi pia ninazo habari za huu mradi na nilienda ofisini kwao kueleweshwa vizuri.
Kwa kuwa kuna maswali mengi na majibu yake mengine ni more technical kwetu sisi sote na kwa kuwa mtoa mada anatoa pia ushauri kwa wanajamii kuchangamkia hii oppotunity, nashauri yafuatayo\;
1. badala ya kuendelea na hisia, wenye nia njema waende ofisini kwao karibu na mnazi mmoja jengo ambalo kwa chini kuna duka la top shop nafikiri ni ghoropha ya tano au ya sita.
2. Kuna darasa la kuelimisha watu wote wanaotaka kujiunga, maelezo ni bure na yatahusisha juhudi ambazo zimefanyika ikiwa ni pamoja na kulipima eneo lenyewe na namna ya umwagiliaji pamoja na namna mradi utakavyendeshwa kwa muda wa miaka kumi. Kuna issue pia ya masoko yaliyopo ya ndani na nje ikiwemo serikali kununua kwa ajili ya akiba ya chakula nchini.
Mimi sijapata hiyo laki tano lakini ikitimia tu nawahi mapema kwa kuwa nilielimika na nikapewa pia makabrasha yanayousiana na huo mradi. Naamini mradi huu usipoingizwa siasa unaweza kabisha kuliondoa taifa hili kwenye njaa inayojirudia mara kwa mara.
Asante sana mkuu, hizi ndo data tunazitaka ili tujue ni kweli ama deci?
Sasa labda mkuu ulifanikiwa kujua kama mradi umeanza tayari? je uhai wa wanachama, wana vikao wanavyofanya kujua mwenendo mzima wa project? samahani mkuu in case unajua zaidi, lakini hata hivo naamini JF jamvi nene data zaidi zitakuja!
Na kwa kusaidiana hivi tukijuvyana wasio jua wanachangamkia, lakini kama ni kanyaboya, basi inapunguza wengine wasiuingie mkenge!
Naona kila mmoja anaongea kwa hisia na labda nyingi sana. mimi pia ninazo habari za huu mradi na nilienda ofisini kwao kueleweshwa vizuri.
Kwa kuwa kuna maswali mengi na majibu yake mengine ni more technical kwetu sisi sote na kwa kuwa mtoa mada anatoa pia ushauri kwa wanajamii kuchangamkia hii oppotunity, nashauri yafuatayo\;
1. badala ya kuendelea na hisia, wenye nia njema waende ofisini kwao karibu na mnazi mmoja jengo ambalo kwa chini kuna duka la top shop nafikiri ni ghoropha ya tano au ya sita.
2. Kuna darasa la kuelimisha watu wote wanaotaka kujiunga, maelezo ni bure na yatahusisha juhudi ambazo zimefanyika ikiwa ni pamoja na kulipima eneo lenyewe na namna ya umwagiliaji pamoja na namna mradi utakavyendeshwa kwa muda wa miaka kumi. Kuna issue pia ya masoko yaliyopo ya ndani na nje ikiwemo serikali kununua kwa ajili ya akiba ya chakula nchini.
Mimi sijapata hiyo laki tano lakini ikitimia tu nawahi mapema kwa kuwa nilielimika na nikapewa pia makabrasha yanayousiana na huo mradi. Naamini mradi huu usipoingizwa siasa unaweza kabisha kuliondoa taifa hili kwenye njaa inayojirudia mara kwa mara.
Mkuu,
Heshima kwako. Kwa sababu ulihudhuria darasa...naomba utupatie yale yaliyojiri huko japo kwa juu.
1. Mradi umeshaanza au unatazamiwa kuanza lini?
2. Mpaka sasa wana wanachama wangapi?
3. Nikilipa laki 5 na kuwa mwanachama, namilikishwa hiyo hekari 5 au nakuwa nimeikodi kwa kipindi cha mradi tu?
4. Ni gharama gani nyingine nitalazimika kuingia zaidi ya hiyo laki 5?
5. Uongozi mzima wa mradi ni wakina nani?
Ni hayo tu kutoka kwangu, tafadhali tuelimishe kwa jinsi ulivyuelewa wewe.
Ahsante
__________________ "Our cherished rights of liberty and equality depend on the active participation of an awakened electorate.", Barack H. Obama. Presidential Announcement Speech, Springfield, Ill, Feb 10, 2007.
Kama una nguvu za kuwekeza ktk kilimo,basi bora ujitafutie shamba mwenyewe,haya mashamba ya kutafutiana/kupeana/kuitana yanaweza kuja leta shida huko mbele. Ardhi nzuri ipo kama unataka kulima tafuta au kama wewe ni mshirika mzuri jiunge na mwenzio muingie shambani.
Hiyo title deed ya shamba hilo ina jina la nani? Mnaweza mkawa mnaitwa ili mkalisafishe shamba,liksha kuwa safi basi hamna chenu.
mimi hawa jammaa nishawahi kuwasililiza good idea tatizo huyu msimamiz mkuu au mwenyekiti wazere wa mjini nilipowatajia hapo hapoa wakaniambia nymaza na ishia huyu mzee ni soo sasa kivipi kuniambia huyu mzee mwenzani ni soo sijui mwenyekiti wa teted ni haji muji shangwe sasa sjui wadau faili lake la uko nyuma likoje fukueni?
Kuna jamaa yangu kaniambia kwamba kuna hiyo association inaitwa TEDET (Tanzania Eco-Development Trust), kwamba inakusanya hela za wanachama kiingilio sh. laki 5 (500.000) ambayo inajumuisha kiingilio ada ya uanachama na shamba la ukubwa wa hekari 5 huko bonde la mto RUFIJI. Kasema makubaliano ni kwamba mwanachama anapewa hilo shamba heka 5, ila anakuwa analimiwa hilo shamba heka 4 mazao ya biashara na heka moja mazao ya chakula.
Mazao ya chakula atakuwa akipewa magunia 20 ya mahindi /mpunga kwa msimu yaani misimu miwili kwa mwaka, wakati mazao ya biashara yatakuwa yakiuzwa kwa pamoja masoko ya nje na kila heka ikikadiliwa kutoa mazao ya wastani wa thamani ya milioni 1.5, lakini mkulima atakuwa akikatwa laki 2 kila heka kama garama ya uendeshaji.
Kasema hiyo Tedeti inashirikiana na KIMUDEA umoja wa wakulima wilaya ya Kinondoni, na wakazi wa Rufiji chini ya umoja wao wa RUDIDEA na kwamba wanachama wanapelekwa kuonyeshwa mashamba huko Rufiji.
Nilipo search goggle nikakuta kweli hiyo kitu ilikuwepo toka mwaka 2006, na mwenyekiti wake ni Dr. Mugishagwe. Na kuna pesa mamilioni mengi, toka kwa wafadhili zimekuwa zikiingia huko TEDET, taarifa zipo ukigoogle za upokeaji wa pesa hizo. Hakuna taarifa zaidi kuhusu huu umoja, kilimo hata hizo ada za uanachama.. Kasema ofisi zao zipo MASASI HOUSE KARIAKOO?
Kweli nikaona maelezo yake ni mazuri, lakini nikapata hofu kwamba je hii haiwezi kuwa DECI ama PUFDEA nyingine? Manake hii kusanya ya kiingilio cha laki 5 kila mwanachama, na kasema wanatakiwa wanachama elfu 10,000. Na kasema wengi sana wamejiunga. Na ahadi ni kwamba wanaanza kilimo mwaka huu.
Ndipo nikaona pengine niimwage hapa kwenye Jamvi nene labda kuna wenye datas za uhakika nisije ingia mkenge wa DECI no.2
Na kama kweli si DECI, basi wanajamvi tuchangamkie uanachama kwani maelezo yake ni mazuri.
Asante wakuu.
Mod. tafadhali iacheni kwa muda hapa tupate datas
Mimi mashaka yangu ni hilo jina la mwenyekiti Dr. MUGISHAGWE linatia shaka
__________________ KAMA KESI YA MBUZI HAKIMU ATAKUWA FISI................
Mimi hii kitu nimeisikia kwa ndugu zangu walioingia huko. Nilikwenda Rufiji kwa shughuli binafsi nikaambiwa hiyo TEDET haimiliki hayo mashamba ambayo watu wanaonyeshwa. Wakazi wa Wilaya si wanajua wamililki wote wa ardhi an miradi ya maendeleo iliyopo kwenye eneo lao lakini huu hata wakazi wa Rufiji wenyewe hawajui.
Nadhani hawa jamaa wanatumia style ya Deci ya kutoa matumaini ya faida nono. Wizara ya ardhi na kilimo zitoe tamko, uongozi wa wilaya nao utoe tamko.