Katika siku chache zilizopita TANAPA (Tanzania National Parks) wameibuka kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa wao si wala rushwa, wala kuajiri kwa kujuana. Kama kuna secta chafu Tz zinazonuka rushwa na kujuana basi TANAPA ni namba moja. Kuna idadi kubwa ya wafanyakazi ndani ya TANAPA ambao ni wa ukoo mmoja, pia kuna wafanyakazi wengi ambao ni ndugu wa vigogo walioko makao makuu ya TANAPA Arusha. Kama huna kigogo ndugu yako pale TANAPA makao makuu Arusha uwezi pata kazi hata kama ungekuwa umefaulu kwa kiwango gani. Hawa jamaa uwaingiza gharama za kujiandaa kwa usaili watoto wa Watanzania wenzao huku wakijua kuwa kuna walioandaliwa kupata nafasi hizo. Kuna wafanyakazi wengine ambao hata hawakusoma maswala ya uhifadhi lakini wameajiriwa TANAPA
Napenda kutumia nafasi hii kuwatahadharisha TANAPA kuwa waache mara moja propaganda zao za kujisafisha mbele ya Watanzania kuwa eti wao wako open katika kuajili. IWAPO HAWATAACHA HIZO PROPAGANDA TUTAANZA KUWATAJA VIGOGO WA TANAPA AMBAO WAMEINGIZA NDUGU ZAO NDANI YA TANAPA, MMOJA WA KIGOGO NI YULE ALIESTAAFU UHIFADHI MKUU KWENYE HIFADHI FULANI HUKO ARUSHA KISHA AKAPEWA MKATABA MAKAO MAKUU YA TANAPA NA AKAFANIKISHA KUAJILIWA KWA MWANAE MWAKA JANA

Reply With Quote



Follow Us Here