Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Pamoja na magari ya thamani; tanzania haina maabara ya kupimia ebola: Aibu ya nani?

    Report Post
    Results 1 to 6 of 6
    1. #1
      MAKOLE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2012
      Posts : 426
      Rep Power : 454
      Likes Received
      112
      Likes Given
      107

      Default Pamoja na magari ya thamani; tanzania haina maabara ya kupimia ebola: Aibu ya nani?

      Serikali inathamini kununua magari yenye thamani kubwa wakati haina hata maabara ya kupimia ugonjwa wa Ebola. Fuatilia sakata hili kutoka gazetii la mwananchi:



      ‘Serikali haina maabara ya kupima Ebola’
      Send to a friend

      Thursday, 16 August 2012 21:29


      Geofrey Nyang'oro na Zaina Malongo

      SERIKALI imeweka wazi kuwa hadi sasa hakuna majibu sahihi yanayoweza kuthibitisha kuwapo kwa ugonjwa wa
      Ebola kwa kuwa hakuna maabara ya kupima ugonjwa huo.

      Aidha hali hiyo imesababisha vimelea vya mtu aliyedaiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo kupelekwa Uganda ambako kuna mabara zinazofanya kazi ya uchunguzi na kutambua ugonjwa huo.

      Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hussein Mwinyi alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua hatua ilipofikia kuhusu ugonjwa wa Ebola.

      Agost 5 mwaka huu maofisa wa afya walifika Hosptali Teule ya Wilaya ya Karagwe ya Nyakahanga na kumuona mgonjwa akiwa na baadhi ya dalili zinazofanana na ugonjwa wa Ebola na kuzipeleka Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.

      Akifafanua hilo Dk Mwinyi alisema hadi sasa hakuna majibu ya vipimo hivyo kwa kuwa vilipelekwa Uganda ambao wana maabara zinazothibitisha tatizo hilo.

      Alifafanua kuwa hadi sasa bado majibu ya vipimo hivyo vya ugonjwa huo wa mlipuko havijarejea nchini lakini akawatoa hofu watanzania akisema hadi sasa hakuna kesi nyingine iliyoripotiwa.
      “Nikweli hatujapata majibu ya vipimo vile,lakini hakuna sababu kwa watanzania kuwa na hofu kwani hakuna kesi nyingine ya mgonjwa iliyopatikana hadi sasa”alisema Dk Mwinyi.

      Mwinyi alifafanua kuwa serikali kupitia wizara hiyo ya Afya inaendelea na mchakato wa kuelimisha jamii juu ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huo ambao hauna dawa.

      “Ugonjwa huu unaambukizwa na kirusi aina ya fangasi, vimelea hivyo vipo vingi na vinatofuatiana na ndio sababu tumepeleka Uganda kupima, lakini kwa kuwa tatizo hilo limekuwa likijirudia nchini tunaona haja ya sisi kuwa na kipimo hicho”alisema Mwinyi.

      Wakati mtu mmoja akigundulika kuwa na dalili za ugonjwa huo wa Ebola, nchi jirani ya Uganda ulishatokea na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100.Mwinyi alisisitiza kuwa serikali bado inafuatilia majibu hayo na kwamba pindi yatakapopatikana itayatoa kwa umma.

    2. Miaka 50

    3. #2
      idawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,685
      Rep Power : 3352
      Likes Received
      1248
      Likes Given
      474

      Default Re: Pamoja na magari ya thamani; tanzania haina maabara ya kupimia ebola: Aibu ya nani?

      hii ni aibu kwa taifa,kuna hatari huyo mgonjwa akapandikiziwa ebola hata kama alienda na ugonjwa wa kawaida.

    4. #3
      Sometimes's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th December 2010
      Posts : 1,372
      Rep Power : 761
      Likes Received
      233
      Likes Given
      39

      Default Re: Pamoja na magari ya thamani; tanzania haina maabara ya kupimia ebola: Aibu ya nani?

      Usishangae kukosekana kwa Maabara peke yake. Jiulize tuna CT Scan ngapi Tanzania!

    5. #4
      Cape city's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th October 2011
      Location : CAPE TOWN
      Posts : 96
      Rep Power : 405
      Likes Received
      23
      Likes Given
      1

      Default Re: Pamoja na magari ya thamani; tanzania haina maabara ya kupimia ebola: Aibu ya nani?

      Kipi cha kushangaza hapo?? Hiyo ndio nchi yenu isiyojua vipaumbele muhimu wa wananchi wake!!wakati Dr's tunagoma tupate vifaa tiba mahospitalini tulionekana wauaji..shiit!

    6. #5
      Jackbauer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : CTU
      Posts : 4,876
      Rep Power : 1692
      Likes Received
      1348
      Likes Given
      277

      Default Re: Pamoja na magari ya thamani; tanzania haina maabara ya kupimia ebola: Aibu ya nani?

      kinachomshangaza mwandishi ni kipi?


    7. #6
      bitimkongwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2009
      Posts : 1,655
      Rep Power : 819
      Likes Received
      202
      Likes Given
      83

      Default Re: Pamoja na magari ya thamani; tanzania haina maabara ya kupimia ebola: Aibu ya nani?

      Mimi nina hakika vifaa vya kupimia viko (PCR machines) na wataalamu wako nchini hata hapo SUA and NIMR. Kinachohitajika ni primers za kupimia huo ugonjwa ambao fedha zake sio nyingi sana. Ni kujipanga tu.

      Au nimekosea molecular biologists? Hatuna maabara ya category 4 hapa Tz?

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...