Ndugu yangu TUNTEMEKE,
Sijaangalia historia huko nyuma kuangalia kama kuna mtu aliwahi kuanzisha mjadala unaokuhusu, lakini napenda kuchukua fursa hii kuanzisha mada mahsusi dhidi yako.
Tangu nijiunge na rasmi JF (ingawa nimekuwa msomaji na mfuatiliaji wa forum hii tangu enzi za Jambo), nimekuwa nikisoma maandiko yako mbali mbali.
Ambacho kimekuwa kikinisikitisha ni aina ya uandishi ambao umekuwa ukiufanya. Kwamba, umekuwa ukiandika kwa hasira, kisasi, chuki na wivu. Ninashawishika kuamini kuwa, kati ya watu hawa, lazima kuna mbaya wako: Dr. Willbrod Slaa, Josephine Mushumbusi, Freeman Mbowe, John Mrema, John Heche na baadhi ya wakurugenzi ndani ya chama.
Uandishi wako, umejikita katika kuwasemea kwa hasira baadhi ya kundi la watu, ambao aidha wamekuwa wahanga wa kushindwa uchaguzi wa BAVICHA au wale ambao mfumo mpya wa Uhasibu (ambao tumeambiwa ulibuniwa na kuwa installed na Josephine).
Umevuka mipaka mpaka kwenda kwenye maisha binafsi kabisa na viongozi wa Chama: Slaa na Mbowe na Mrema pia.
Wakati umefika sasa ukaachana na siasa za chuki, wivu na hasira na kukumbatia siasa za ukweli, upendo na amani.
Kwa Moderators - forum hii ni credible sana. Nashauri posts za chuki kama hizi, zisiwe zinaachwa zivume mwanzo mwisho kwani zinahataisha amani, umoja na mshikamano.
Ni bora waandishi kama hawa, wakatupisha huku kwa Great Thinkers na kwenda kule kwenye FB - CHADEMA VS CCM, TANURU LA FIKRA ambako kuna mipasho, utoto, kejeli, udini, ukanda n.k.
Nabakia,
Mwanachama Mwaminifu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Reply With Quote


Follow Us Here