Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

    Report Post
    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast
    Results 21 to 40 of 44
    1. #1
      Godfrey Electronics's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 13th March 2012
      Posts : 195
      Rep Power : 402
      Likes Received
      26
      Likes Given
      2

      Default Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      Katika nyimbo ya Solo Thang inayokwenda kwa jina la Miss Tanzania ni wazi kuwa aliyezungumziwa hapo Si Miss Tanzania bali ni nchi ya Tanzania. Katika wimbo huo ambao upo kwenye link hii hapa chini kuna mistari ifuatayo kwenye mashairi hayo

      http://www.hulkshare.com/dl/o7mepz38l1s4/?d=1

      Ubeti wa Kwanza
      Baba yake alikuwa mkoloni kipindi huyu Miss mwali
      Mchonga alikata utepe lakini hakuvinjari
      Sababu alikua busy kumlinda na geti kali
      Kumbe wenzake wanabinjuka, kushtuka akakaa mbali
      Demu alikua na heshima kabla haijatangazwa Rukhsa
      Chukua Chako Mapema ukimkonyeza tu umegusa
      Ana kifua kimebetuka sio maziwa ni madini
      Kayaacha wazi, watu wanashika hapo ndio anaponiudhi mimi
      Watu wanagonga tu Ikulu tena kwa mitindo huru
      Kavu kavu bila kinga hajali vinavyodhuru
      Kawa shangingi na amedata hana uwoga wa kunguru
      Anapenda sana chapaa haimtoshi kodi na ushuru
      Ana kijungu matata laini kama nyanya masalo
      Anatingisha Afrika nzima na mzigo Kilimanjaro
      Usimchezee kwa vidani sio pete sio hereni
      Anamiliki tanzanite kama ardhi ya Mererani
      Sura dhahabu inaita kama amezaliwa Geita
      Tatizo ndio kicheche kila mwanaume ndio amepita
      Hata Benja hakutoka Kapa huyu demu hajatulia
      Kama rushwa ndio kikwapa ananuka na kunukia

      Kiitikio

      Miss Tanzania
      Nakupenda ila hujatuliaa
      Vitendo vyako sitojivunia
      Sifa yako kubwa umefulia
      Miss Tanzania

      Ubeti wa Pili

      Bora angebaki kuwa modo kama Flavian Matata
      Ila demu amejiachia kisa anaendekeza bata
      Sitachoka kuwakilisha jinsi anavyoniacha hoi
      Juzi juzi kaopolewa na Handsome Boy
      Kabla hapo shoga zake wote kashawaona mabwege
      Sababu hawana dira na yeye ameshahongwa ndege
      Anafaa kuwa Miss Dunia maandalizi longolongo
      Tatizo anakula sana akijamba ni Songosongo
      Mara ghafla kanenepa kumbe mimba B.O.T.
      Kumbe demu aligawa EPA watu wamepiga hafu jii
      Alizugwa na akaunti hewa kuwadi Bwana Bilal
      Mara mdomo naye kazimwa bila hata picha ya kaburi
      Kinachomponza huyu shawty utulivu sifuri
      Ila hakuna anayepinga kwamba huyu demu ni mzuri
      Mixer siasa na biashara demu ameshakuwa chotara
      Mishe za Dar akimaliza Mjengoni anakwenda lala
      Kadri miaka inavyokwenda demu anazidi fulia
      Kumbe weupe ni mkorogo ona mwili sasa umefifia
      Demu kazidi umalaya wacha mabwana wamteme
      Haogopi kuliwa mtungo kisa anagawa umeme

      Ubeti wa Tatu

      Wadaku walishamfuma anakula denda na Richmond
      Dowans akazidi kete akamvisha pete ya diamond
      Binti masikini akanasa bwana mshenga ndio Lowasa
      Shemeji hataki hata picha ndio tabia gani sasa
      Ndoa ilifungwa kwa vifijo vigogo wakala pizza
      Keki nzima wale wao share yetu si ni giza
      Sio hayo demu ana mengi ya kuchukiza
      Malighafi ashazinadi for sale anajiuza
      Mtaani ilivuma rumor demu kawa mama huruma
      Uchumi umefungwa drip maendeleo ndio kali homa
      Mali asili ndio kitasa kila ufunguo ndio unapita
      Toka alipovunja ungo nusu karne imeshapita
      Mapenzi kafanya mradi anamegwa na mafisadi
      Amani kwa time bomb binti amekumbatia radi
      Vitendo vyake vibaya vinafanya adharaulike
      Tabia Katiba sio Msahafu ndio useme isibadilike
      Mikosi inayomkuta ndio kwanza anatabasamu
      Hajali waliomzunguka kama nao binaadamu
      Mbagala walimbaka mpaka akamwaga damu
      Na juzi Gongo la Mboto kaanza kujamba mabomu

      Apelekewe rais Wimbo huu jamani akausikiepia Mwinyi, na Mkapa
      Last edited by Godfrey Electronics; 4th August 2012 at 08:04.
      Mtu Mzima and bayonamperembi like this.
      "Technology at the Speed of Life""Sharing The GoodThings Everyday"

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      Mwanaharakati Mkweli's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th June 2012
      Posts : 57
      Rep Power : 359
      Likes Received
      6
      Likes Given
      30

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      Safi sana solooooo nimekupata nilikuwa sijakuelewa vizuri ila baada ya kuisoma vizuri nimekupata saluti kwako

    4. #22
      Mtali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2011
      Posts : 376
      Rep Power : 469
      Likes Received
      70
      Likes Given
      73

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      I appreciate the work..... Kijana kaza buti hapa wapelekee salamu zaidi............ Na safari zao kwa Obama land.

    5. #23
      Kaunga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th November 2010
      Location : Wild wild west
      Posts : 8,443
      Rep Power : 13325
      Likes Received
      7672
      Likes Given
      6911

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      I wish tungekuwa na wasanii 10 tu kama huyu na Roma! Big up Solo T

    6. #24
      markj's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 1,006
      Rep Power : 548
      Likes Received
      164
      Likes Given
      143

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      mchonga alikata utupe japo hakuvinjari! anamaanisha nini,hapa solo kaniacha! ila kwingine tupo pamoja. mia
      MZUNGU AKIJICHUBUA HUJUE MOYONI ANA UAFRICA!.by stamina

    7. #25
      cmoney's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th October 2011
      Posts : 365
      Rep Power : 458
      Likes Received
      74
      Likes Given
      52

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      vp wadau hamna mwenye kamusi ya kiswahili maana kichwa hapa mi kinaniuma khs huyu dadangu
      Cmoney@

    8. Miaka 50

    9. #26
      Kertel's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2012
      Location : Motown
      Posts : 573
      Rep Power : 469
      Likes Received
      124
      Likes Given
      5

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      Big up kwa bro solo thang.Wengine kazi kuimba "oyoyo oyoyo" eti shombeshombe bebi,pumba*u

    10. #27
      Mkereketwa_Huyu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2011
      Location : London | Dar Es Salaam
      Posts : 1,820
      Rep Power : 4589
      Likes Received
      579
      Likes Given
      420

      Default

      Angetulia katika utunzi wake/mashairi yaliyoenda shule huu wimbo ungekuwa na maana lakini kama kawaida ya watunzi wa bongo fleva kajichanganya na utunzi wake kitu ambacho kinaonesha dhahiri kuwa hajuwi kutunga nyimbo za muziki ila ngonjera. Ushauri wangu, solo ukitunga ngonjera wape wanamuziki waliobobea wasahihishe, usikurupukie kuimba tu na kuchanganya vitu.

    11. #28
      Godfrey Electronics's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 13th March 2012
      Posts : 195
      Rep Power : 402
      Likes Received
      26
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By markj
      mchonga alikata utupe japo hakuvinjari! anamaanisha nini,hapa solo kaniacha! ila kwingine tupo pamoja. mia
      mchonga ndo nyerere

    12. #29
      Mkubwa ndevu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2011
      Posts : 357
      Rep Power : 490
      Likes Received
      35
      Likes Given
      0

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      cku ya kwanza nilifikiri kamwimbia wema du msafiri unatisha

    13. #30
      Mupirocin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th January 2011
      Location : Tanzania
      Posts : 1,562
      Rep Power : 806
      Likes Received
      523
      Likes Given
      408

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      Song limetulia sana, tunaomba tulipate haraka tupo Songea coz huu utafungiwa soon, coz umemponda m;kulu moja kwa moja wala hujiulizi kwa kweli mshikaji kafulia hana ishu tena.

    14. #31
      ablood8's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th August 2010
      Posts : 43
      Rep Power : 454
      Likes Received
      12
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By *****
      hizi ni tungo zilizotukuka!! dah safi sana solo, umeandika sijawahi fikiria!!
      Kweli kaka sio kila siku mara mwanayumba mara single boy na matamasha ya wizi ya Ruge

    15. #32
      Mupirocin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th January 2011
      Location : Tanzania
      Posts : 1,562
      Rep Power : 806
      Likes Received
      523
      Likes Given
      408

      Default

      Quote By markj
      mchonga alikata utupe japo hakuvinjari! anamaanisha nini,hapa solo kaniacha! ila kwingine tupo pamoja. mia
      hapa kwa tafsiri yangu anamrefer baba wa Taifa ambaye alizindua hili Taifa lakini hakujivinjali akawaachia wenzake ndo wanakula kwa mrija

    16. #33
      Apta Kayla's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2010
      Location : Dar es salaam
      Posts : 326
      Rep Power : 497
      Likes Received
      62
      Likes Given
      33

      Default

      Quote By markj
      mchonga alikata utupe japo hakuvinjari! anamaanisha nini,hapa solo kaniacha! ila kwingine tupo pamoja. mia
      Anamzungumzia Mwl Nyerere hapa. Aliikomboa nchi, hakuifaidi, ukiunganisha ni huo mstari wa ruksa unapata jibu.

    17. #34
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1826
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      safi sana

    18. #35
      alindae's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 25th June 2012
      Posts : 8
      Rep Power : 349
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      big up solo we ni nomaa vichwa km hivi vinahitajika sana kuleta mabadiliko

    19. #36
      markj's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 1,006
      Rep Power : 548
      Likes Received
      164
      Likes Given
      143

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      Quote By Apta Kayla
      Anamzungumzia Mwl Nyerere hapa. Aliikomboa nchi, hakuifaidi, ukiunganisha ni huo mstari wa ruksa unapata jibu.
      Na kweli! nilipata kuiona video ya vita vya kagera,kuna mahala benjamin w m! alikuwa yupo na nyerere baada ya vita kwisha! aisee, ukiambiwa makapa huyu ndo yule niliemuona pale, siamini machoyangu mpaka leo!
      MZUNGU AKIJICHUBUA HUJUE MOYONI ANA UAFRICA!.by stamina

    20. #37
      markj's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 1,006
      Rep Power : 548
      Likes Received
      164
      Likes Given
      143

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      anakifua kimebetuka! sio maziwa hadi madini! kayaacha wazi watu wanashika tu! HAPO NDO ANANIUZI MIMI.
      kama rushwa ndo kikwapa,ananuka na kunukia!
      kuadi bwana bilali nae kazimwa tu bila hata picha ya kaburi!(HIKI KIPANDE JIBU LIKO MABWEPANDE)
      bwana mshenga ndo lowassa! wao wanakula keki tu,shea yetu sisi ni giza(?)

      hivi uyu jamaa hayupo humu kwa magreat thinker? mkali sana! ivi huko nje aliko hamna mapori kama ya mabwepande kweli! mana yule jamaa asije akatumwa kwenda kule!
      MZUNGU AKIJICHUBUA HUJUE MOYONI ANA UAFRICA!.by stamina

    21. #38
      Azimio Jipya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Location : Universal Space Station
      Posts : 3,282
      Rep Power : 5415
      Likes Received
      1006
      Likes Given
      1731

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      Quote By Dauphine
      Katika nyimbo ya Solo Thang inayokwenda kwa jina la Miss Tanzania ni wazi kuwa aliyezungumziwa hapo Si Miss Tanzania bali ni nchi ya Tanzania. Katika wimbo huo ambao upo kwenye link hii hapa chini kuna mistari ifuatayo kwenye mashairi hayo

      http://www.hulkshare.com/dl/o7mepz38l1s4/?d=1

      Ubeti wa Kwanza
      Baba yake alikuwa mkoloni kipindi huyu Miss mwali
      Mchonga alikata utepe lakini hakuvinjari
      Sababu alikua busy kumlinda na geti kali
      Kumbe wenzake wanabinjuka, kushtuka akakaa mbali
      Demu alikua na heshima kabla haijatangazwa Rukhsa
      Chukua Chako Mapema ukimkonyeza tu umegusa
      Ana kifua kimebetuka sio maziwa ni madini
      Kayaacha wazi, watu wanashika hapo ndio anaponiudhi mimi
      Watu wanagonga tu Ikulu tena kwa mitindo huru
      Kavu kavu bila kinga hajali vinavyodhuru
      Kawa shangingi na amedata hana uwoga wa kunguru
      Anapenda sana chapaa haimtoshi kodi na ushuru
      Ana kijungu matata laini kama nyanya masalo
      Anatingisha Afrika nzima na mzigo Kilimanjaro
      Usimchezee kwa vidani sio pete sio hereni
      Anamiliki tanzanite kama ardhi ya Mererani
      Sura dhahabu inaita kama amezaliwa Geita
      Tatizo ndio kicheche kila mwanaume ndio amepita
      Hata Benja hakutoka Kapa huyu demu hajatulia
      Kama rushwa ndio kikwapa ananuka na kunukia

      Kiitikio

      Miss Tanzania
      Nakupenda ila hujatuliaa
      Vitendo vyako sitojivunia
      Sifa yako kubwa umefulia
      Miss Tanzania

      Ubeti wa Pili

      Bora angebaki kuwa modo kama Flavian Matata
      Ila demu amejiachia kisa anaendekeza bata
      Sitachoka kuwakilisha jinsi anavyoniacha hoi
      Juzi juzi kaopolewa na Handsome Boy
      Kabla hapo shoga zake wote kashawaona mabwege
      Sababu hawana dira na yeye ameshahongwa ndege
      Anafaa kuwa Miss Dunia maandalizi longolongo
      Tatizo anakula sana akijamba ni Songosongo
      Mara ghafla kanenepa kumbe mimba B.O.T.
      Kumbe demu aligawa EPA watu wamepiga hafu jii
      Alizugwa na akaunti hewa kuwadi Bwana Bilal
      Mara mdomo naye kazimwa bila hata picha ya kaburi
      Kinachomponza huyu shawty utulivu sifuri
      Ila hakuna anayepinga kwamba huyu demu ni mzuri
      Mixer siasa na biashara demu ameshakuwa chotara
      Mishe za Dar akimaliza Mjengoni anakwenda lala
      Kadri miaka inavyokwenda demu anazidi fulia
      Kumbe weupe ni mkorogo ona mwili sasa umefifia
      Demu kazidi umalaya wacha mabwana wamteme
      Haogopi kuliwa mtungo kisa anagawa umeme

      Ubeti wa Tatu

      Wadaku walishamfuma anakula denda na Richmond
      Dowans akazidi kete akamvisha pete ya diamond
      Binti masikini akanasa bwana mshenga ndio Lowasa
      Shemeji hataki hata picha ndio tabia gani sasa
      Ndoa ilifungwa kwa vifijo vigogo wakala pizza
      Keki nzima wale wao share yetu si ni giza
      Sio hayo demu ana mengi ya kuchukiza
      Malighafi ashazinadi for sale anajiuza
      Mtaani ilivuma rumor demu kawa mama huruma
      Uchumi umefungwa drip maendeleo ndio kali homa
      Mali asili ndio kitasa kila ufunguo ndio unapita
      Toka alipovunja ungo nusu karne imeshapita
      Mapenzi kafanya mradi anamegwa na mafisadi
      Amani kwa time bomb binti amekumbatia radi
      Vitendo vyake vibaya vinafanya adharaulike
      Tabia Katiba sio Msahafu ndio useme isibadilike
      Mikosi inayomkuta ndio kwanza anatabasamu
      Hajali waliomzunguka kama nao binaadamu
      Mbagala walimbaka mpaka akamwaga damu
      Na juzi Gongo la Mboto kaanza kujamba mabomu

      Apelekewe rais Wimbo huu jamani akausikiepia Mwinyi, na Mkapa
      ... Its great Song

      ... Awamu zote wamo MCHONGA, RUKHSA, BENJA mKAPA, HANDSOME BOY

      ... Bila kusahau .. Lowasa, Bilal, Chukua Chako Mapema, EPA etc

      Jitihada zifanywe kwa wahusika kupata ... Huu mziki wausikilize wacheze na zaidi wauchukulie hatua ili uwe maarufu zaidi na zaidi ... Na ujumbe uende mabali zaidi na zaidi!!
      Never Get Angry; Never Make Threat; Reason With People;
      "Napenda the logic of the words because in some ways it says about individual-not to use emotions-when scrutinizing something, whether it involves you or not" ...-by AshaDiii @ Jamiiforums 26th July 2011.

    22. #39
      Godfrey Electronics's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 13th March 2012
      Posts : 195
      Rep Power : 402
      Likes Received
      26
      Likes Given
      2

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      nimemkubali solo

    23. #40
      Wamunzengo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd August 2012
      Posts : 500
      Rep Power : 443
      Likes Received
      126
      Likes Given
      4

      Default Re: Serikali inahusika 100% kwenye Miss Tanzania, Wasanii waichana live

      huu wimbo napendekeza uwe wa tatu baada ya zile mbili za taifa (Mungu ibariki...na TanzaniaTanzania...). utawasaidia sana hata hawa vijana wa kizazi cha bongo flava kujua umuhimu wa siasa safi kwenye nchi yao hasa kina Bushoke, Dokii, Hafsa Kazinja wanaokesha kuinadi ccm magamba.

      Halafu haya mashairi apewe cpt John Komba ayatengenezee kwaya moja nzuri hivi ili ujumbe uwafikie pia wapenda kwaya.

      Wabunge hasa hawa wa ccm ni bora waupate huu wimbo halafu watafakari na hizo kelele zao NDIYOOOOOO!! kwa kila kitu.

      Ningeweza ningependekeza upigwe kenye radio stations mfululizo japo wiki mbili labda hii inaweza ikasaidia kidogo watanzania kutafakari mustakabari wa nchi yetu na rasilimali zake. BIG UP SOLOOOOO!

    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...