Kizungumkuti cha migomo kinashika hatamu kwa taarifa za chini chini madaktari kukianzisha na wafanyakazi wa nssf kukianzisha ijumaaa
Kizungumkuti cha migomo kinashika hatamu kwa taarifa za chini chini madaktari kukianzisha na wafanyakazi wa nssf kukianzisha ijumaaa
hakuna sehemu wanatoa training ya Kulenga shabaha...
ni kweli kabisa ndugu Bufa..., migomo haina tija na inarudisha maendeleo nyuma. ila si kwa nchi kama tanzania. iweje uendelee kuumia na kazi wakati kinachopatikana hakifanyi kazi iliyokusudiwa????. kinaishia mikononi mwa wachache wanaojilimbikizia mali. tunalipwa kidogo n bado tunakatwa kodi kubwa ambayo hatuoni inachikifanya. UKITEKA MAJI MBALI NA KUYAMWAGA KWENYE PIPA LINALOVUJA, NA BADO UKAENDELEA TU, HAKIKA UTAKUWA MWENDAWAZIMU. ziba matundu kwanza ndo uendelee kuweka maji. Migomo inaweza saidia kidogo kwa hilo.
Bufa jiangalie sana, na jitathmini juu ya uwezo wako wa kufikiri........, otherwise great thinkers hapakufai.
Ndugu yangu siujui umasikini ni nini nasikia tu watu wakilalamika ila kwangu mm maisha na safi san. Pili, watu kua na jela zaidi ya bajeti ya serikali nje ya nchi haimaanishi kwamba basi nchi ni tajiri hizo ni pesa zao, ulivyompambe kama watu wengine utaanza kusema ooh tuna mbuga, madini, sijui ardhi na maji hivyo pekee havitoshi nchi kua tajiri dunia ya leo, singapore, tswana, swiss hawana yote hayo na wako mbelea yenu saaana sijui mtawaambia nini. TZ masikini sana sana na mbingu zishuke ndo itaendelea.
migomo ya wabongo kama mchezo wa kujificha wa watoto.
"watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema
Sikubaliani na migomo hata kidogo kwani bado kuna njia mbadala za kutafuta suluhu. Watanzania wenzangu ni lazima tuangalie faida na hasara za migomo katika jamii yetu. Daktari anapogoma nani anapata hasara/matatizo?.
Kudai malipo makubwa na kuboreshewa mazingira ya kufanyia kazi ni madai ya msingi kabisa, lakini pia tuangalie hali na uwezo uliopo wa serikali. Tusipende kulaumu na kudai kisichowezekana, huo ni uendawazimu wa hali ya juu.
Kwa upande wangu sioni sababu ya kuwa na migomo pamoja na maandamano yasiyo na tija.
Labda kwa sababu walisema watafanya kila liwezekanalo nchi isitawalike.
Kama hali ndiyo hiyo kuna raha kweli ya kutawala, au ndiyo dalili za nchi kutotawalika.
Busara zinahitajika hapo, waanze kupunguza kujilimbikizia mali wanasiasa kwanza ndipo hiyo migomo itakwisha, vinginevyo sahau.
naibu spika akihutubia watanzania waishiio Korea ya kusini siku moja alituasa tusitembelee jf kwani kuna upotoshwaji mkubwa. So wanalijua jukwaa hili na wanapitia hapa
Dhaifu ni Schizophrenia,
Kuhudhuria Harusi na kuhudhuria Msiba kwake hakuna tofauti.
Sasa watumishi wa serikali wakigoma,
anashindwa kuelewa yeye anahusika vipi,
Madakatari hawafanyi kazi Ikulu!
Walimu hawafanyi kazi Ikulu!
Migomo ya watu hawa inamhusu nini??
Ndiyo asii ya Dhaifu kutabasamu kila mahali,
brain yake haina uwezo wa kujitune na reality.
Raisi wetu ana tatizo la "hubris"
Which means extreme pride or arrogance. Hubris often indicates a loss of contact with reality and an overestimation of one's own competence or capabilities, especially when the person exhibiting it is in a position of power.(Wikipedia)
Madaktari mgomo wanini tena wakati wameshaambiwa asiyetaka aache?au wanakuja na madai mengine tofauti na yale ya kwanza?
WanaJF!
Kuna post nilichangia sometimes back, I remember to have told you thinking loudly that "Mgomo wa Madaktari" ulikuwa batili simply because ulivunja sharia za Kazi za Mwaka 2004.
Before rushing to open and post new posts on the subject matter Nyie vijana just let it go . Kasomeni sheria inasemaje and then come back.
Dhaifu alikwisha sema his hopeless govt of the day is no in position to offer more than fifteen percentum (15%)increase who ever is not willing to accept that offer should peacefully look for an employer of his choice. This was spoken openly and he didn't want to mince words pronto!
Sasa hizo ngonjera za kufufua mgomo wa Madaktari zinatoka wapi vijana . The train has gone and the President aliwaonea huruma kwani mlivunja sheria halali . Mimi tu nikemee hii Tabia mbaya ya Rais kuwa raisi na kuwasamehe watu hata kabla ya kuwapeleka mahakamani kumjibu tuhuma. If he had sober washauri sio hao akina Salva angengojea wakishahukumiwa then waende jela angojee siku ya siku kuu ya Uhuru awasamehe. Aliwasamehe akina Rostam and the Chenges,Msabaha, Ngeleja and the whole pack historian will judge him come 2016 dead or alive.
Msiote kugoma ila endeleeni na huo Mgomo baridi anyway hakuna sheria inayozuia mgomo baridi. But ushauri wangu why don't you simply pack and go anywhere except hell of course my dear Doctors!!!!
Ulichosema ni kweli kabisa,ninacho kiona mimi tatizo lipo kwa watunga SERA! kwanini? WANABAGUA WATUMISHI. idara ya kilimo mishahara yao ni mizuri sana lengo lilikuwa ni kuwashawishi waweze kukaa vijijini ambako ndio kwenye mashamba na wakulima pia. lakini wakasahau kuwa huko vijijini kuna walimu wengi tu ambao nao wanahitaji motisha.Jambo hili linaleta manung'uniko miongoni mwa watumishi wa umma.haiwezekani mwalimu alipwe tshs 300,000 mtu wa ugani akaanza na tshs 700,000/= na wote wanaishi kijiji kilekile na wote wana shahada za fani zao.
Tunaweza tukawa tumeweza kuwashawishi watu wa ugani kukaa vijijini lakini kwa upande mwingine tumewakatisha tamaa walimu.watu wa ngazi fulani ya elimu bila kujali fani zao basi tofauti ya mshahara isiwe kubwa kihivyo.kuwe na tofauti ya 100,000 hadi 200,000 lakini sivyo ilivyo sasa.mathalani katika sakata hili la walimu na serikali hata walimu wote walio goma wakifukuzwa tuna uhakika gani watakao kuja watakubali hiyo mishahara isiyo kidhi mahitaji?
ushauri wangu,NCHI hii ni yetu sote,tusibaguane,yatupasa kuona UAMZI WOWOTE UNAO HUSU WATU NA USTAWI WAO UNAZINGATIA MASLAHI mapana ya NCHI.UDUMISHE UPENDO,UMOJA WETU na MSHIKAMANO.
Follow Us Here