Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Spika Makinda ang’ang’aniwa

    Report Post
    Results 1 to 17 of 17
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,209
      Rep Power : 3556
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      462

      Default Spika Makinda ang’ang’aniwa

      JUMATATU, JULAI 30, 2012 05:03 NA WAANDISHI WETU, DAR NA DODOMA

      *Atakiwa kutaja wabunge waliohusika
      *NCCR Mageuzi yampatia wiki moja
      *Watuhumiwa hatarini kupoteza ubunge wao
      *January Makamba apigilia msumari wa mwisho

      LICHA ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini na kamati nyingine kutokana na tuhuma za kukithiri kwa vitendo vya rushwa, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na watu wa kada mbalimbali, wameendelea kumng’ang’ania awataje kwa majina wabunge wote wanaotuhumiwa.

      Kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa vyama vya siasa waliitisha mikutano na waandishi wa habari na kusema hiyo ndiyo fursa pekee ambayo itarejesha imani kwa wananchi.


      Kutokana na hali hiyo, Chama cha NCCR-Mageuzi, kimesema kama Spika Makinda atashindwa kuwataja wabunge hao, basi chenyewe kiko tayari kutaja majina ya wabunge wanaotuhumiwa kudai na kupokea rushwa.


      Msimamo huo, umetolewa jana na wabunge wa chama hicho, walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.


      Katika mkutano huo, alikuwepo Mbunge wa Kuteuliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali na Mbunge wa Kasulu Vijijini, Zaitun Buyogela.


      Katika mkutano huo, Mbatia alisema wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa wanajulikana na kwamba hata juzi wakati wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, walishindwa kuhudhuria Bunge kutokana na aibu waliyokuwanayo.


      “Hawa watu wanajulikana kwa majina kwani hata jana (juzi), wakati tunapitisha bajeti ya Wizara ya Nishati, walitoroka bungeni na mimi niliwachunguza hadi nje sikuwaona.


      “Wakati wengine walitoroka, baadhi waliingia na hao ni wale wachache wajanja wajanja ambao wanapenda kupuliza huku na huko.


      “Kwa kuwa tabia hii imelichafua Bunge, tunamuomba Spika wa Bunge awataje kwa majina na kama atashindwa kuwataja kabla Bunge halijaahirishwa, basi sisi tutawataja kwa sababu tunawajua,” alisema Mbatia na kuungwa mkono na wenzake.


      Kwa mujibu wa Mbatia, wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa, wanatakiwa kutajwa kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kulirejeshea Bunge heshima iliyoshuka.


      “Hata Waziri Sospeter Muhongo, alipokuwa akihitimisha bajeti ya wizara yake ya Nishati na Madini, alisema kuna baadhi ya wabunge wanafanya biashara na TANESCO, hawa nao lazima watajwe kwa majina.


      “Lazima wachukuliwe hatua, kwani sisi tunaendesha Bunge letu wakati mwingine kwa kufuata nchi za Jumuiya ya Madola zikiwamo Uingereza na India, ambazo ziliwahi kuwachukulia hatua wabunge wake waliokumbwa na kashfa ya rushwa,” alisema.


      Akizungumzia kauli ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliyosema juzi, kwamba ameiagiza Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ili ichunguze tuhuma dhidi ya rushwa kwa wabunge, alisema baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ni watuhumiwa wa rushwa.


      Kutokana na hali hiyo, aliwataka wajumbe hao kujiondoa ndani ya kamati hiyo vinginevyo haki haitatendeka kwa kuwa nao ni watuhumiwa.


      “Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ni wachafu, kwa hiyo, ili uchunguzi ufanyike vizuri lazima kwanza wajitakase ili haki itendeke.


      “Bunge sasa limechafuka, kila mtu analishangaa na ili lionekane ni Bunge safi, lazima maamuzi juu ya kashfa hii yawe wazi na usifanyike upendeleo.


      “Pia mbunge yeyote anayeamini anatuhumiwa kwa rushwa, awe ni wa chama changu au wa chama chochote, uwe ni wewe Machali au wewe mama, ondoka na katika hili nitakuwa na sura nyingine kabisa pindi mtakapokuwa mkiwajibishwa.


      “Hata wabunge wale waliotajwa na Profesa Muhongo, wanafanya biashara na TANESCO, nao waachie ngazi.


      “Vyama vinavyojiita viadilifu viige mfano wa CUF, maana katika Bunge la nane wakati Msekwa ni Spika, kuna wabunge wanne wa chama hicho walikumbwa na kashfa ya rushwa na wakafikishwa mahakamani na pia CUF yenyewe ikawapiga marufuku kushika nyadhifa zozote ndani ya chama hicho.


      “Kwa hiyo, hawa watuhumiwa wajipime na kama hawajui, nawaambia Sheria namba 3 ya mwaka 1988 ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, inasema Mbunge anaweza kufungwa miaka mitano kama atapatikana na hatia ya rushwa.


      “Sisi tunayasema haya kwa nia njema, tunataka heshima ya Bunge irejee, pia tunamtaka Spika azitaje na kuzivunja kamati hizo alizosema atazivunja kwa kashfa hii ya rushwa, kwa sababu sisi tunajua ziko takribani kamati sita,” alisema.


      Alitoa mfano jinsi Bunge, lilivyokaa kimya juu ya hoja iliyowasilishwa bungeni mwaka jana na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), aliyewataja kwa majina baadhi ya wabunge wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, kwamba walikuwa na kashfa ya kudai rushwa.


      Naye, Machali alisisitiza kama Spika wa Bunge atashindwa kuwataja kwa majina wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa, watatajwa baada ya wiki moja. “Kama tulivyosema, Spika akishindwa kuwataja baada ya wiki moja, sisi tutawataja na pia tutawasilisha hoja binafsi bungeni kutaka jambo hili lijadiliwe.

      JANUARY MAKAMBA
      Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambaye awali alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, alisema ni sahihi kamati hiyo kuvunjwa, kwa sababu imekithiri vitendo vya rushwa.

      “Wakati mimi nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, vilikuwapo vitendo vya rushwa, si kwa wajumbe wote ila baadhi yao walikuwa vinara, kutokana na hali hiyo nilivipigia kelele na nimepata shida sana kupambana navyo,” alisema na kuongeza:

      “Tuliweka msimamo ndani ya Kamati kwamba vitendo hivyo havikubaliki hata kidogo na ilifikia hatua nilienda kuwashitaki kwa Spika, Anne Makinda, kuhusu tabia ya baadhi ya wajumbe kupokea rushwa na alikubaliana na mimi kisha naye alikemea vitendo hivyo.

      “Kusema ukweli tulifanikiwa kuvidhibiti kutokana na msimamo wa pamoja tuliokuwa nao. Baadhi ya wajumbe wa kamati wakalalamika kwanini nimeenda kusema kwa Spika, unajua ni wabunge wachache ndiyo wanaoharibu sifa ya wabunge wengine.

      “Kwa hiyo, wananchi wasidhani wajumbe wote wa Kamati ya Nishati na Madini ni wala rushwa, hapana, wanaofanya vitendo hivyo ni wachache kama nilivyosema hapo mwanzo.

      “Mimi nataka uchunguzi huo ufanywe haraka na wote wanaohusika wajulikane.”

      Katika hatua nyingine, alisema wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, kuna baadhi ya watu walikwenda kwa baba yake, Yusuph Makamba kwa ajili ya kumshawishi alegeze msimamo wake.

      “Unajua Kamati hii ina ‘deal’ na mambo makubwa na yenye maslahi ya watu, kwa hiyo usipokuwa makini kama kiongozi wa kamati au mjumbe wa kamati, watu wengi watakufuata na kukushawishi kwa fedha,” alisema na kuongeza:

      “Mimi nilikuwa na msimamo wangu na ndio maana hata watu wengine wakawa wanaogopa kuanza kunifuata na kunieleza wanayotaka niyafanye.

      “Nakumbuka siku moja, kabla ya kwenda katika mdahalo wa Star Tv kuna watu walimfuata mzee Makamba na kutaka anishawishi nisizungumzie mradi mmoja wa umeme ambao ulikuwa na walakini.

      “Lakini Mzee Makamba akawajibu kwamba mimi sikai kwake na nimehama tangu nikiwa na umri wa miaka 18, kwa hiyo hana namna yoyote ya kufanya. Kwa hiyo mtu unatakiwa uwe na msimamo na ifikie hatua wakuogope.”

      CUF NAYO YANENA
      Nacho Chama cha Wananchi (CUF), kimevitaka vyama ambavyo wabunge wake wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa, kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), vijisafishe haraka kwa kuwachukulia hatua kali wabunge wao, ikiwa ni pamoja na kuwavua uanachama.

      Kauli hiyo, imetolewa mjini Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius Mtatiro, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yaliyoibuka nchini.

      Alisema CUF, kimesikitishwa na kitendo cha wabunge hao kupokea ‘milungula’, kwa ajili ya maslahi yao binafsi badala ya kuwatetea wananchi.

      “Inasikitisha kuona Bunge ndilo linalotakiwa kuielekeza Serikali na wabunge nao, lakini cha ajabu wabunge wake wanajihusisha na vitendo vya rushwa kwa maslahi yao binafsi…wanakuwa mstari wa mbele kuwatetea wafanyabiashara.

      “Hiki ni kitendo ambacho kinatia kinyaa na kichefuchefu kwa sababu hata Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, anasema vitendo hivi havijaanza leo, inaonekana vimeota mizizi.

      Akizungumzia kuhusu mkanganyiko uliojitokeza kuhusu mabadiliko ya muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Mtatiro aliitaka serikali iache kuwadanganya wananchi. “Hii ni sawa na danganya toto, kwa sababu kitendo cha Mkurugenzi wa SSRA kudai eti kuna miongozo na kanuni ambazo zitairekebisha sheria hii, ni jambo ambalo haliwezekani.


      KUVULIWA UBUNGE

      Taarifa za uhakika zilizopatikana jana kutoka mjini Dodoma, zinasema wabunge wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa, wako hatarini kupoteza ubunge wao.

      “Ndugu yangu mambo yako wazi, ngoja tume iliyopewa kazi hiyo ifanye kazi yake, lakini jambo kubwa ambalo naweza kukwambia ni kwamba wale wanaotuhumiwa wako hatarini kuvuliwa ubunge wao,” kilisema chanzo chetu.



      Last edited by nngu007; 30th July 2012 at 13:49.

    2. Miaka 50

    3. #2
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,209
      Rep Power : 3556
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      462

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa


      Kwanini Bunge letu liwe chombo cha kuchagua, kulinda, na kuficha Majina ya Majangili tuliowatuma kutunga Sheria na

      kutulinda. Speaker anawalinda Kuficha Majina yao? Kwanini kila kitu kikifika BUNGENI ni SIRI? Mabunge ya NCHI

      ZINGINE ndiko siri zinapotoka... Ina Maana Ma-Speaker wetu ni Madikteta???? HAYA BASI WAWAVUE UBUNGE...
      Last edited by nngu007; 30th July 2012 at 13:49.

    4. #3
      Asa79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th July 2012
      Posts : 591
      Rep Power : 462
      Likes Received
      162
      Likes Given
      10

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Makinda bado ni kinda ktk kusimamia masuala mengi mazito....anapwaya kupita kiasi ni hasara tupu kuwa na spika km makinda

    5. #4
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,657
      Rep Power : 716
      Likes Received
      291
      Likes Given
      36

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Wiki moja ya nini Mbatia Unampa ajenti wa Mafisadi huyo mama, Toa maasaa 5 tu leo tujue? Hio wiki ninavyowajua watahongwa wabunge na hio mada itakufa kifo cha mende na mtasikia waziri na katibu mkuu wake hawana kazi, hukuona mwingine alishaanza kujitangaza eti ni mwadilifu na anafaa kuwa amiri jeshi mkuu anawaza mambo ya jirani na kwao huko Burundi, congo na Rwanda vita 2

    6. #5
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,209
      Rep Power : 3556
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      462

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa


      * I failed to Understand why MODS moved this TOPIC from "HABARI ZA SIASA" to "HABARI MCHANGANYIKO"

      Is it really not a political Issue? I failed to understand their Intentions...


      WOW IT HIT'S ME... INAKATISHA TAMAA KWELI KAMA UHURU WAKO KIDOGO UNACHUKULIWA KIBABE...

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      BIG X's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2011
      Location : WHITE HOUSE
      Posts : 767
      Rep Power : 414
      Likes Received
      197
      Likes Given
      168

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Kama Spika naye anahusika????.
      GOOD JUDGEMENT COMES FROM EXPERIENCE, BUT EXPERIENCE COMES FROM BAD JUDGEMENT.

    9. #7
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 589
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Yes, ikibainika wavuliwe ubunge pasipo kujali wametoka chama gani.

    10. #8
      Mwita Maranya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2008
      Location : Ikorongo Game Reserve
      Posts : 7,976
      Rep Power : 12008
      Likes Received
      5307
      Likes Given
      5143

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Spika wa bunge hili asipoyataja majina ya wabunge wala rushwa ni dhahiri kwamba hata ka reputation kadogo ka bunge kalililikokuwa kamebaki kwa wananchi nako katapotea.

      Na asitegemee tena kwamba bunge hili litaweza kupata tena nafasi ya kujisahihisha na kujisafisha toka katika tope la rushwa zaidi ya hii ya sasa.

      Kafulila aliwahi kuzungumza "live" bungeni lakini mama makinda kwa kutumia busara za kamati yake ya uongozi akalitia kapuni, muda mfupi baadae mtuhumiwa mmoja wa Kafulila akabambwa ba Takukuru anachukua rushwa. Hiyo ilitosha kumzindua usingizi spika lakini kwa bahati mbaya ameendelea kuwalinda wabunge wala rushwa kwakuwa mara zote wamekuwa ni wabunge wa chama chake cha CCM.

      Kwakuwa safari hii kuna wabunge wa upinzani wanatajwa, basi nadhani anaweza kupata ujasiri wa kuwataja ili kujisafisha yeye binafsi pamoja na bunge na kujitenga na genge la wala rushwa.
      Honesty is a very expensive GIFT. Do not expect it from cheap people.

    11. #9
      Ndumbayeye's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2009
      Posts : 1,065
      Rep Power : 738
      Likes Received
      98
      Likes Given
      806

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Nafasi ya kuchafuana imewadia, kigezo gani kitatumika? wabunge lini wamezuiwa kufanya biashara na serikali au mashirika yake!

      Kila mtua atataja wa kwake, mi naanza na Mnyika...... nnavomuona ni mla rushwa mkubwa, spika andika jina lake.
      I HAVE SPOKEN

    12. #10
      NATA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2007
      Posts : 4,255
      Rep Power : 8416
      Likes Received
      1133
      Likes Given
      390

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Mh hebu nyie akina Mbatia wiki ndefu tutajieni mapema

    13. #11
      Sibhonike's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 87
      Rep Power : 428
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By webondo
      Yes, ikibainika wavuliwe ubunge pasipo kujali wametoka chama gani.
      Hakuna atakayebaki aiseee!!

    14. #12
      Duduwasha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Posts : 2,620
      Rep Power : 6249
      Likes Received
      523
      Likes Given
      418

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Ataje Kwani ile Sera ya Kulindana Imefutwa?

    15. #13
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,084
      Rep Power : 12251
      Likes Received
      6014
      Likes Given
      6851

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      KAFULILA ALIWATAJA AKINA ZABEIN MHITA.... nini kilifanyika??
      .....Ana sifa zote, nzuri na mbaya!!!

    16. #14
      Mbozib's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2012
      Posts : 358
      Rep Power : 430
      Likes Received
      43
      Likes Given
      5

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Hapo msishangae spika kuwataja wabunge wa CDM tu kwasababu ya ushabiki na chuki binafsi

    17. #15
      Borat69's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th June 2012
      Location : Global Citizen
      Posts : 698
      Rep Power : 488
      Likes Received
      279
      Likes Given
      77

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Mh. Mleta mada, hicho kichwa cha habari kimenifanya nikurupuke kuacha ugali wangu ukapoa nikifikiri Madame Supika amekamatwa na Puli za banji na tunguli Bungeni!!!! Au kang'ang'aniwa na yale mawig anayovaa kama nguchiro pale mbele Bungeni. Nitake radhi mkuu,kwa kuwa imenibidi nirudi kusonga ugali usiku huu na sufuria niiazime kwa mama mwenye nyumba.
      "Our Lives begin to End the Day We Become Silent About Things that Matter"-Dr Martin Luther King Jr.

    18. #16
      Kigogo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 8,195
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1232
      Likes Given
      313

      Default

      Spika hatuna bana mbona mnaumiza kichwa kwa mambo rahisi

    19. #17
      dizo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 30
      Rep Power : 366
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Spika Makinda ang’ang’aniwa

      Wahusika wanafahamika inachotakiwa spika awataje na wanyongwe adhrani

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...