Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 27
    1. #1
      salosalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 528
      Rep Power : 538
      Likes Received
      133
      Likes Given
      36

      Default Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Kwa muda mrefu watanzania tumekuwa na tabia ya kusifu uovu unapofanyika.... sasa imekwenda hadi makazini. mtu akiajiriwa serikalini kwenye nafasi yoyote yenye mianya ya kuiba au kufisadi bila kufanya hivyo anatukanwa kila aina ya tusi na watz wenzake wanao mzunguka. Zaidi wale waliowahi kushika nafasi za namna hiyo serikalini bila utajiri mpaka kustaafu,wamekuwa wakinyooshewa vidole na kuambiwa Ugoigoi wao ndo uliowaponza.

      Lakini kwa wale waliopata kuliibia taifa(kufisadi) kwa namna yoyote wanaitwa wajaja, kwamba huyo sio boya kama maboya wengine. Maneno haya yanazungumzwa mbele ya watoto wanaokua. Wanajegwa kwa kuamini kuwa kuibia serikali ndio ujanja, kinyume na hapo ni uboya. Kumbe naomba jamii tubadilike, tuanye kusifu uchafu huku tukidhani tunajenga kumbe tunabomoa. Tena watu wakiwa kazini ukawazuia kuiba mali ya umma basi watakuundia mikasa ili ufukuzwe kazini kwa madai kuwa unaweka jam. Kwa serikalini kama wanamamlaka kubwa basi maramoja utahamishwa kituo cha kazi.

      Nashauri vita dhidi ya ufisadi ianzie nyumbani kwetu. Wazee wa busara semeni kitu hapa....
      katoto, fige and Ndukidi like this.

    2. Miaka 50

    3. #2
      Bornvilla's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 17th February 2011
      Posts : 634
      Rep Power : 0
      Likes Received
      141
      Likes Given
      0

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Aisee! We kumbe umeliona hili! Hii ndio halihalisi ndugu yangu. Hata wale wanaodai kuwa niwapambanaji wa ufisadi na wao ofisini kwao ni hayohayo,kifupi maadili hakuna. Nikweli kuwa vita ianzie nyumbani na kwenye taasisi za dini ili angalau watu wamwogope Mungu.
      Ndukidi likes this.

    4. #3
      Asa79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th July 2012
      Posts : 591
      Rep Power : 463
      Likes Received
      162
      Likes Given
      10

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Nasikia usipoiba serikali unaonekana bonge la *****.....iliwezekana kutokuiba kipindi cha nyerere tu

    5. #4
      Lokissa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Location : Goba
      Posts : 4,092
      Rep Power : 5807
      Likes Received
      1026
      Likes Given
      2876

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      ni waziri gani au mbunge gani ambe hajaibia serkali?
      tuwapime kabla hawajawa na vyeo walivo navyo walikuwaje?
      serikalini huko kuna allowance kibao zonatolewa bila hata kufanya kazi
      hata mini nipata hizo nachukua kwanini niobakie maskini kama sera ya chama ni ya kuchukua chak mapema?
      kama ulaji upo na uwezekano wa kula upo kwanini nife njaa? lol
      You may know me but you have no Idea who I am !

    6. #5
      Nov11's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 16th July 2012
      Posts : 4
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      6

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Nafikiri ifike mahali watanzania wapate madarasa ya uadilifu...ethics courses labda itasaidia lakini ianzie nyumbani toka mtoto mdogo afundishwe juu ya ubaya wa tamaa na rushwa na pia afundishwe kufikiria wengine na kuchukia ubinafsi....hasa unapokuwa na nafasi katika nchi hii. Kwa hawa walioko madarakani sasa nafikiri sijui tumechelewa ila kwa kweli tunahitaji kuwa na uelewa wa nini ni maadili ya kazi...

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Arushaone's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st March 2012
      Location : Arusha
      Posts : 6,438
      Rep Power : 40150
      Likes Received
      5085
      Likes Given
      16275

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Tanzania bila wizi inawezekana.

    9. #7
      fige's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2010
      Posts : 359
      Rep Power : 522
      Likes Received
      53
      Likes Given
      20

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Watanzania wanapoomba kazi huwa hawajali mshahara atakaopewa bali marupuprupu na hasahasa fursa za dili (wizi) kwenye kazi husika.

      Wivu ulio wa haki ,kutenda haki na kutowakatisha tamaa watenda haki ndiko kutakakotuokoa.SERIKALI ITIMIZE WAJIBU WAKE WA KUBORESHA MASILAHI YA WAFANYAKAZI NA KUPUNGUZA TOFAUTI ZA MISHAHARA.

      Inatia kinyaa kusikia sisi 30 tunaweza kulipwa na mfanyakazi mwenzetu wa serikali na bado akabakiwa na fungu la kutosha.

    10. #8
      Mwanahisa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Posts : 1,158
      Rep Power : 579
      Likes Received
      314
      Likes Given
      130

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Yani hii kitu ya kutumia mianya kujinufaisha imeshaingia kwenye damu ya watu wasiopenda kuangalia mbali,
      Hapa ofisini kuna mwanafunzi kapewa nafasi ya mafunzo kwa vitendo (field) ameshaanza kubeba rim paper za ofisi ya serikali kwa manufaa yake binafsi, Taifa la leo hilo.
      Success Requires No Explanations, Failure Permits No Alibis- Napoleon Hill

    11. #9
      salosalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 528
      Rep Power : 538
      Likes Received
      133
      Likes Given
      36

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By Bornvilla
      Aisee! We kumbe umeliona hili! Hii ndio halihalisi ndugu yangu. Hata wale wanaodai kuwa niwapambanaji wa ufisadi na wao ofisini kwao ni hayohayo,kifupi maadili hakuna. Nikweli kuwa vita ianzie nyumbani na kwenye taasisi za dini ili angalau watu wamwogope Mungu.
      Umenena la kunena Mja

    12. #10
      salosalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 528
      Rep Power : 538
      Likes Received
      133
      Likes Given
      36

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By Asa79
      Nasikia usipoiba serikali unaonekana bonge la *****.....iliwezekana kutokuiba kipindi cha nyerere tu
      Ni kweli ndugu yangu. Na kama kunawaliopata kuiba kipindi hicho, basi hawakupata kutumia mali hizo za wizi mpaka Mauti ilipowakuta la sivyo basi wanazitumia sasa. Maana wakati huo adhabu aliyoipata yeyote aliyebainika kuiba ilitosha sana kuwaogopesha wengine kufuata nyayo hizo mbaya. Big up Nyerere

    13. #11
      salosalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 528
      Rep Power : 538
      Likes Received
      133
      Likes Given
      36

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By Lokissa
      ni waziri gani au mbunge gani ambe hajaibia serkali?
      tuwapime kabla hawajawa na vyeo walivo navyo walikuwaje?
      serikalini huko kuna allowance kibao zonatolewa bila hata kufanya kazi
      hata mini nipata hizo nachukua kwanini niobakie maskini kama sera ya chama ni ya kuchukua chak mapema?
      kama ulaji upo na uwezekano wa kula upo kwanini nife njaa? lol
      mkubwa usemalo ni ukweli mtupu, lakini tunako kwenda hao wanaochukua chao mapema watalia juani baada ya kuchumia kivurini

    14. #12
      salosalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 528
      Rep Power : 538
      Likes Received
      133
      Likes Given
      36

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By kerusa
      Nafikiri ifike mahali watanzania wapate madarasa ya uadilifu...ethics courses labda itasaidia lakini ianzie nyumbani toka mtoto mdogo afundishwe juu ya ubaya wa tamaa na rushwa na pia afundishwe kufikiria wengine na kuchukia ubinafsi....hasa unapokuwa na nafasi katika nchi hii. Kwa hawa walioko madarakani sasa nafikiri sijui tumechelewa ila kwa kweli tunahitaji kuwa na uelewa wa nini ni maadili ya kazi...
      Zote pointi kaka ila hiyo ya blue imenigusa kipekee sana. Walioko madarakana hata wale wanaosubiri madaraka nje hawafai. Sasa najiuliza hawa watoto zetu watafundishwa Maadili/uadilifu na nani? au labda tanzie hapoo..

    15. #13
      salosalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 528
      Rep Power : 538
      Likes Received
      133
      Likes Given
      36

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By Arushaone
      Tanzania bila wizi inawezekana.
      Kweli mkubwa ila nadhani mvua hii inatuloanisha kwasababu paa lake linavuja. Tutahangaika sana kujenga kuta zinazobomoka kwa kuloana bila ukomu isipokuwa pale tutakapo ziba na kuezeka vizuri paa. Ninamaanisha ninacho kisema

    16. #14
      salosalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 528
      Rep Power : 538
      Likes Received
      133
      Likes Given
      36

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By fige
      Watanzania wanapoomba kazi huwa hawajali mshahara atakaopewa bali marupuprupu na hasahasa fursa za dili (wizi) kwenye kazi husika.

      Wivu ulio wa haki ,kutenda haki na kutowakatisha tamaa watenda haki ndiko kutakakotuokoa.SERIKALI ITIMIZE WAJIBU WAKE WA KUBORESHA MASILAHI YA WAFANYAKAZI NA KUPUNGUZA TOFAUTI ZA MISHAHARA.

      Inatia kinyaa kusikia sisi 30 tunaweza kulipwa na mfanyakazi mwenzetu wa serikali na bado akabakiwa na fungu la kutosha.
      Ndugu Fije, umenena kweli tupu.
      Siku hizi wanaita DILI kama ulivyosema, sio wizi tena. Mfano mzuri we fuatilia pesa za Radar zilizokuwa zimeibwa jinsi zinavyotajwa bungeni na popote serikalini. Zimepewa jina zuri sijapata kuona

    17. #15
      salosalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 528
      Rep Power : 538
      Likes Received
      133
      Likes Given
      36

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By Mwanahisa
      Yani hii kitu ya kutumia mianya kujinufaisha imeshaingia kwenye damu ya watu wasiopenda kuangalia mbali,
      Hapa ofisini kuna mwanafunzi kapewa nafasi ya mafunzo kwa vitendo (field) ameshaanza kubeba rim paper za ofisi ya serikali kwa manufaa yake binafsi, Taifa la leo hilo.
      Dah, imenibidi nicheke kidogo. Wewe umejua kuwa hilo ni kosa kama makosa mengine. Leo anabeba ream paper 7bu ndio ana-access nazo, akiendamahali akawa na access na mamillion ya pesa mwendo ndio huohuo. Mkanye tafadhali

    18. #16
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By Asa79
      Nasikia usipoiba serikali unaonekana bonge la *****.....iliwezekana kutokuiba kipindi cha nyerere tu
      Nani kakudanganya? Mbowe karithi mali ya kutoka wapi? Uliza lile jengo kwenye bar yake limepatikanaje na baba'ke alikuwa na wadhifa gani Serikalini?
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    19. #17
      salosalo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 528
      Rep Power : 538
      Likes Received
      133
      Likes Given
      36

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By zomba
      Nani kakudanganya? Mbowe karithi mali ya kutoka wapi? Uliza lile jengo kwenye bar yake limepatikanaje na baba'ke alikuwa na wadhifa gani Serikalini?
      Tupo hapa kujuzana yale tusio yajua.. Tafdhali tuambe ilipatikanaje na wadhiwa wa baba yake ulikuwa upi?

    20. #18
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By salosalo
      Tupo hapa kujuzana yale tusio yajua.. Tafdhali tuambe ilipatikanaje na wadhiwa wa baba yake ulikuwa upi?
      Taboo!
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    21. #19
      Borat69's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th June 2012
      Location : Global Citizen
      Posts : 707
      Rep Power : 490
      Likes Received
      280
      Likes Given
      77

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      Quote By kerusa
      Nafikiri ifike mahali watanzania wapate madarasa ya uadilifu...ethics courses labda itasaidia lakini ianzie nyumbani toka mtoto mdogo afundishwe juu ya ubaya wa tamaa na rushwa na pia afundishwe kufikiria wengine na kuchukia ubinafsi....hasa unapokuwa na nafasi katika nchi hii. Kwa hawa walioko madarakani sasa nafikiri sijui tumechelewa ila kwa kweli tunahitaji kuwa na uelewa wa nini ni maadili ya kazi...
      Mkuu,
      Hii nadhani itakuwa ngumu kidogo. Mimi nakumbuka nilipokuwa mdogo(6-7yrs) huko kipindi cha nyuma nilikuwa nikipita jikoni nyumbani na kukuta nyama inachemshwa nilikuwa nanyakua Kama paka jizi na kukimbilia uwani kula..bila kujali nilikuwa naihujumu familia yetu,huku lawama zote zikienda kwa dada (house girl) kwamba ndiye aliyekuwa akifanya ufisadi wa mboga. Arobaini zangu zilifika nikakamatwa na mfupa uwani,nikatandikwa na fimbo ya mpera na tabia ya uhujumu mboga ikakomea hapo.

      Kwa hiyo kuna uwezekano kabisa hivi vitabia tunavyo tokea utoto. Inahuzunisha lakini ndio ukweli.
      "Our Lives begin to End the Day We Become Silent About Things that Matter"-Dr Martin Luther King Jr.

    22. #20
      Choi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th July 2012
      Posts : 59
      Rep Power : 355
      Likes Received
      11
      Likes Given
      39

      Default Re: Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

      mafisadi sio serikalini tu, hata kwenye sekta binafsi. nilikuwa na kiduka changu cha dawa baridi nimemuweka mdada aniuzie nikienda kazini anaenda kkoo anachukua dawa zake ndio anauza hapo dukani zangu haziuziki mpaka nikafunga duka ndio jirani akaja kunipa hiyo siri. ukienda posta kwenye maduka ya wahindi wauzaji wanakwambia hii bidhaa inauzwa 300000,lakini nenda pale mlangoni umpe mlinzi 150000 na bidhaa utaikuta hapohapo! ukikaa ofisini unaletewa saa ya 300000 unaambiwa lete 150000, ukiuliza imetoka wapi unaambiwa imeibiwa airport! usiache mafundi wakutengenezee matofali wakati haupo watabadilisha ratio bila kujali ubora utajijua mwenyewe na nyumba yako
      hayo ni machache niliyokutana nayo, sasa niambieni tunaanzia wapi kurekebisha hii hali!!

    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...