Tulimlaumu sana Mkapa kwa kukiuka maadili ya uongozi na kujiuzia mgodi wa Kiwira. Aliitwa fisadi na kuzomewa hadi na watoto wadogo, na wengi hata tukitaka afikishwe mahakamani, na moto wa madai haya ukizimika pale tu JK alipoibuka na kumtetea.
Lakini je, tumesahau kwamba Sea Cliff Hotel ilijengwa kwa kukiuka sheria zile zile zilizofanya nyumba za vigogo kuvunjwa hivi karibuni? Je, tumesahau kwamba Sea Cliff Hotel ilijengwa kwa mgongo wa Mwinyi ambaye naye alikiuka maadili ya uongozi kwa kutoa kibali kinyume na sheria za mazingira ili Sea Cliff ijengwe, ikisemekana kwa familia yake kupewa share katika hii hoteli?
Kwa hiyo swali ni kwamba, Sea Cliff Hotel itavunjwa kama zilivyovunjwa nyumba nyingine kwa kutumia sheria ile ile ya ujenzi unaokiuka sheria za kulinda fukwe?

Reply With Quote



Follow Us Here