Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

    Report Post
    Results 1 to 18 of 18
    1. #1
      mzozaji's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th July 2010
      Posts : 248
      Rep Power : 501
      Likes Received
      8
      Likes Given
      2

      Default Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Wakuu nashangazwa sana na kasi ya hii serikali kushikilia kujenga mradi wa majumba ya kifahari Kigamboni kana kwamba ndio suruhisho la umaskini wetu. Nchi yetu haina maji safi sehemu nyingi na umeme wa mashaka kila siku lakini tunaona Mabilioni yakawekezwe kwenye majumba ambayo hatujui nani atapanga huku tukiwatimua watu toka makazi yao.Mimi kwa haraka naona kuna kitu kimejificha kwenye huu mradi mpaka unapelekwa puta hivi. Waziri wa ardhi katangaza bajeti ya mwaka huu kwenye huu mradi tena ni 10% ambayo ni Mabilioni na akasema hizo 90% zilizobaki 'watajua namna ya kuzipata'!! Hapa lazima kuna jambo.. Utaanzishaje mradi wakati hata fedha hujui utatoa wapi? Wenye kujua kidogo kuhusu huu mradi watujuze labda wengine tunashindwa kuelewa kwa akili ya kawaida.
      Babu Ubwete and Kamkuki like this.

    2. BAK is offline
      BAK
      #2
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,850
      Rep Power : 45019
      Likes Received
      8693
      Likes Given
      8761

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Nusu ya Bajeti ya Ardhi kujenga Kigamboni mpya
      Wednesday, 11 July 2012 20:36
      Florence Majani, Dodoma
      Mwananchi

      WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imetenga zaidi ya nusu ya bajeti yake kwa mwaka wa fedha, 2012/2013 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni, Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuendeleza mji huo ni Sh60 bilioni ambazo ni sawa na asilimia 59 ya makadirio ya matumizi ya wizara hiyo, ambayo ni Sh101.731 bilioni.

      Hata hivyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema Bungeni jana kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo ni sawa na asilimia 10 tu ya mahitaji ya kiasi cha Sh605.
      “Kwa hiyo tutatumia mbinu za kisasa (kupitisha bakuli letu la omba omba)kutafuta pesa nyingine Sh605 bilioni nje ya Bajeti kutekeleza mradi huu bila kuchelewa zaidi. Mradi huu unahitaji kiasi hicho cha fedha kwa miaka mitatu ya kwanza,” alisema Profesa Tibaijuka alipokuwa akiwasilisha makadirio ya matumizi ya wizara yake jana na kuongeza:

      “Nitasimamia mradi huu kwa kasi, ari na nguvu mpya. Ingawa pia sitakuwa nimetenda haki iwapo sitawashukuru wananchi wa Kigamboni kwa uvumilivu na ushirikiano wanaotuonyesha.”

      Katika Bajeti ya wizara hiyo ya Sh101.7 bilioni, matumizi ya kawaida ni Sh30.7 bilioni na Sh71 bilioni ni za maendeleo. Katika fedha hizo za maendeleo, Sh61 bilioni ni fedha za ndani na Sh10 bilioni ni fedha za nje.

      Kuhusu wananchi wanaoishi katika eneo hilo, Profesa Tibaijuka alisema hakuna mkazi yeyote wa Kigamboni atakayehamishwa kwani idadi ya wananchi waliopo ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya makazi mapya yanayotakiwa kujengwa katika eneo hilo.
      Alisema ni ushauri wake kwamba wakazi wote wa Kigamboni wachague kubaki katika mji huo kwani wawekezaji wa ndani na nje watapewa maeneo kwa ajili ya kujenga makazi ambayo yatatumika kuwahamishia wananchi watakaoamua kubaki.

      “Tunashauri wote wabaki kwa kuwa sasa hivi kuna wananchi takribani 82,000 wakati tunajenga mji mpya wenye uwezo wa wakazi 400,000. Hakuna sababu ya wananchi kuhama eneo hili ila makazi yao yatapangwa upya na kuboreshwa,” alisema.

      Gharama za mradi
      Profesa Tibaijuka alisema ujenzi wa Mji wa Kigamboni utafanywa kwa awamu tatu, ambazo zitatekelezwa kati ya mwaka huu na 2032 na gharama zinazotarajiwa kutumika hadi utakapokamilika ni Sh11.6 trilioni.

      Alisema awamu ya kwanza itakuwa kati ya mwaka 2012 na 2022, awamu ya pili kati ya 2022 na 2027 na awamu ya tatu ni kati ya 2027 na 2032.
      Profesa Tibaijuka alisema miongoni mwa kazi zitakazofanywa katika mwaka huu wa fedha ni kuundwa kwa wakala mpya wa kusimamia mradi huo anayejulikana kama Kigamboni Development Agency (KDA).

      Kazi nyingine ni kuidhinisha mpango na kuanza utekelezaji, kufanya uthamini wa mali zilizomo katika maeneo ya miundombinu, huduma za maji na eneo mbadala na kulipa fidia kwa mali zilizomo katika maeneo yaliyofanyiwa uthamini.
      Kuhusu fidia, Waziri Tibaijuka alisema wananchi ambao hawajakiuka maagizo ya mradi kwa kufanya maendelezo haramu, wasiwe na wasiwasi kuhusu fidia kwa sababu mradi utazingatia haki na ni endelevu... “Fidia itatolewa kwa mujibu wa sheria kwa tathmini ya kiujumla ambayo itakokotolewa kutokana na viwango vya soko na kuhusishwa ili iwe sahihi.”

      Alisema atafanya ziara ya mafunzo kwa wawakilishi kutoka Kigamboni kutembelea mji mpya ili uwepo uelewa wa pamoja juu ya jinsi mji huo utakavyokuwa.

      Hazina ya Ardhi
      Katika hatua nyingine, Profesa Tibaijuka alisema wizara yake inakamilisha uanzishaji wa Hazina ya Ardhi pamoja na Mfuko wa Fidia ya Ardhi.
      Alisema vyombo hivyo vitasimamia utoaji wa ardhi kwa wawekezaji wa ndani na nje kwa misingi ya kuingia ubia wa kumiliki pamoja hisa zitakazotolewa kwa uwiano kati ya wananchi na wawekezaji husika.

      Kuhusu kuweka na kutunza alama za mipaka ya Tanzania na nchi jirani, Profesa Tibaijuka alisema majadiliano ya kupima maeneo hayo yalishakamilika.
      Alisema majadiliano yalishafanyika baina ya Tanzania na nchi za Comoro na Msumbiji na mkataba wa kwanza kati ya Tanzania, Msumbiji na Comoro kwenye alama za utatu baharini inayotenganisha nchi hizo ulikamilika na kutiwa saini Desemba 5, mwaka jana.

      “Mkataba wa pili kati ya Tanzania, Shelisheli na Comoro ulitiwa saini Februari 17, mwaka huu. Hivyo basi, Tanzania imekamilisha upimaji wa mipaka katika Bahari ya Hindi na itatangaza eneo lake la ukanda wa kiuchumi baharini bila kipingamizi kwa nchi jirani,” alisema.

      Alisema wizara yake imewasilisha andiko la kudai nyongeza ya eneo ya ukanda wa kiuchumi baharini Januari, mwaka huu na Tume ya Mipaka ya Baharini ya Umoja wa Mataifa, inapitia andiko hilo.

      Profesa Tibaijuka alisema kupatikana kwa eneo hilo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 61,000 kutaiwezesha Tanzania kuvuna rasilimali za chini ya bahari kwa manufaa ya sasa na kwa vizazi vijavyo.

      Kurasini kulipwa fidia
      Kuhusu mradi wa uendelezaji wa eneo la Kurasini ulioanza 2006 kwa ajili ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka alisema wizara imetenga fedha chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi huo katika eneo la Kurasini na Shimo la Udongo.

      “Wizara itaendelea na malipo hayo kwani hata mwaka jana tulilipa kiasi cha Sh550 milioni kwa wakazi wa Mtaa wa Kurasini waliopo jirani na Mabwawa ya Majitaka,” alisema.

      Alisema wizara yake itaendelea kutatua migogoro ya ardhi, urasimishaji wa makazi holela, mikopo ya nyumba, ujenzi wa nyumba unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na ujenzi wa nyumba za biashara na makazi.

      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    3. #3
      O-man's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 266
      Rep Power : 436
      Likes Received
      35
      Likes Given
      11

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Kigamboni, kama alivyozungumza mbunge wao jana, kimenuka. Yalitengenezwa na wenye madaraka ili bei ya maeneo ipae. Kwa kiasi fulani walifanikiwa, lakini wananchi wa kuburuza Kigamboni hakuna.

    4. #4
      muchetz's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th August 2010
      Posts : 237
      Rep Power : 496
      Likes Received
      62
      Likes Given
      1261

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Quote By BAK View Post

      Another CDA (Capital City Development) in progress. Hivi CDA imefikia wapi vile? Au tule tumiradi twetu?

    5. #5
      Elam's Avatar
      Member Array
      Join Date : 19th May 2009
      Posts : 45
      Rep Power : 523
      Likes Received
      10
      Likes Given
      0

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Goooo goo go go Prof. Tibaijuka hakuna wakuzuia maendeleo ya Watanzania...wakazi wakigamboni wanapaswa kujua Mjimpya sio kwaajili yao tuu, ni kwa ajili ya watanzania wote..tunataka maendeleo sio sumu za kisiasa toka kwa DR.Ndugulile, ya kwake tunayajua hivyo apishe maendeleo yaje...

    6. #6
      Wa Ndima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th August 2010
      Posts : 1,388
      Rep Power : 735
      Likes Received
      223
      Likes Given
      645

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      This is another silly season

    7. #7
      Mu-Israeli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2012
      Location : Jerusalem
      Posts : 1,203
      Rep Power : 606
      Likes Received
      435
      Likes Given
      191

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Quote By Elam View Post
      Goooo goo go go Prof. Tibaijuka hakuna wakuzuia maendeleo ya Watanzania...wakazi wakigamboni wanapaswa kujua Mjimpya sio kwaajili yao tuu, ni kwa ajili ya watanzania wote..tunataka maendeleo sio sumu za kisiasa toka kwa DR.Ndugulile, ya kwake tunayajua hivyo apishe maendeleo yaje...
      Hapo kwenye red,

      Maendeleo ya Watanzania yamezuiwa kwa miaka mingi sasa, labda kama wewe hujui.

      Maendeleo hayo yamezuiwa kwa namna zifuatazo:-
      • Mali na raslimali zote za Tanzania zinaliwa na wawekezaji ( Angalia migodi ya dhahabu, tanzanite, almasi, n.k)
      • Fedha zote za Tanzania zinaliwa na viongozi mafisadi (Angalia ulaji wa EPA, majengo ya BoT, Richmond, Dowans, n.k)
      • Mapato yote ya kodi za Tanzania zinaliwa na wetendaji serikalini (Angalia bajeti ya mwaka huu - chai na maadazi ya wafanyakazi serikalini zitagharimu Sh. 15 Billioni !!!, n.k)
      • Selikali haina pesa za kununulia CT scan kwa ajili ya hospitali zetu, ila ina pesa kwa ajili ya kujenga 'mji' wa Kigamboni !! ( Linganisha CT scan moja ni Sh. 200 million tu , ila mji wa Kigamboni Sh. 11,000 millioni !!!)

      Upo hapo ??? Hapo kuna maendeleo ???

      Kweli, mji wa kigamboni utajengwa, ila wewe na watanzania wengine mnaweza msiuone maana mtakuwa mmeshakufa kwa kukosa matibabu hospitali, maana hakuna vifaa vya kuwatibia kama vile CT scan na vifaa vinginevyo !!!
      Kamkuki, NAFIKA and KIJOME like this.
      "Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. " - Yakobo 04:17

    8. #8
      Bobuk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 2,181
      Rep Power : 949
      Likes Received
      889
      Likes Given
      1

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Jamani mimi naomba nifahamishwe, labda kuna kitu sielewi! Hivi Professor Anna Tibaijuka ni waziri wa Ardhi wa Tanzania? au ni Waziri wa Ardhi wa Dar es Salaam? Kutenga 59% ya budget yote ya Wizara ya Ardhi kwaajili ya Kigamboni tu THIS IS A BIG JOKE AND AN INSULT kwa Watanzania tusio wana Dar es Salaam.

      Hata ukisoma budget yako mipango yake yote aliyoongelea ni ya Dar es Salaam. Sijaona ukizungumzia watanzania tusio wana Dar es Salaam. Tangu ateuliwe ukifuatilia utendaji wake utaona yeye anashughulika na mamabo ya Dar es Salaam, kubomoa nyumba, viwanja vya wazi DSM tu?

      Sasa nimeanza kuelewa kwanini CDM wana advocate SERIKALI ZA MAJIMBO. Huyu Professor sisi watu wa mikoa hatufai kabisa. Mbona Magufuri tunamuona kila kona ya nchi hii. Yaani mimi huyu Mama ameni bore stiff, Yeye anafikiri Tanzania ni DSM tu.

      CDM tuleteeni serikali za majimbo tuachane na hawa WARASIMU wa DSM
      Kamkuki likes this.

    9. #9
      Original's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2012
      Posts : 325
      Rep Power : 431
      Likes Received
      66
      Likes Given
      265

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Naunga mkono hoja ni lazima mji ujengwe.

    10. #10
      wagaba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 600
      Rep Power : 484
      Likes Received
      123
      Likes Given
      92

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Tatizo kubwa la serikali ya CCM siku zote haina priority list ya projects zake. Sijui kwanini inapenda kukurupuka kila mara. Si lazima projects zote zianze kwa pamoja. tatizo kubwa hapa ni kuwa Kigamboni ina masilahi binafsi especially kwa viongozi wetu. Nani hajui kuwa wengi wao wameshakamata maeneo huko!
      Kinachofuata ni daraja la kigamboni kujengwa kwa haraka iwezekanavyo ili wasipate adha wanayoipata wakazi wake walalahoi sasa hivi.
      kujengwa Kigamboni ni maendeleo makubwa pia ila ndiyo kipaumbele kwa kipindi hiki kigumu cha uchumi?
      "Tanzania ni ya watanzania, na watanzania wenyewe ndo sisi"

    11. #11
      BADILI TABIA's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Location : DUNIANI
      Posts : 14,836
      Rep Power : 5674
      Likes Received
      6322
      Likes Given
      2418

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      waacheni wajenge kigamboni jamani, viwanja vyenyewe wanachukua wao vyote.....

      Wanajiandalia mji wao.....

    12. #12
      deny_all's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Posts : 415
      Rep Power : 661
      Likes Received
      9
      Likes Given
      5

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Quote By BADILI TABIA View Post
      waacheni wajenge kigamboni jamani, viwanja vyenyewe wanachukua wao vyote.....

      Wanajiandalia mji wao.....
      Oysterbay walishaiharibu kwa kujaza mabaa kila sehemu sasa wanaona wajitafutie makazi mapya ya hadhi yao na kuwaondoa watu wote wa kawaida.

    13. #13
      ALEYN's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th November 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 1,065
      Rep Power : 597
      Likes Received
      134
      Likes Given
      17

      Default

      Quote By mzozaji View Post
      Wakuu nashangazwa sana na kasi ya hii serikali kushikilia kujenga mradi wa majumba ya kifahari Kigamboni kana kwamba ndio suruhisho la umaskini wetu. Nchi yetu haina maji safi sehemu nyingi na umeme wa mashaka kila siku lakini tunaona Mabilioni yakawekezwe kwenye majumba ambayo hatujui nani atapanga huku tukiwatimua watu toka makazi yao.Mimi kwa haraka naona kuna kitu kimejificha kwenye huu mradi mpaka unapelekwa puta hivi. Waziri wa ardhi katangaza bajeti ya mwaka huu kwenye huu mradi tena ni 10% ambayo ni Mabilioni na akasema hizo 90% zilizobaki 'watajua namna ya kuzipata'!! Hapa lazima kuna jambo.. Utaanzishaje mradi wakati hata fedha hujui utatoa wapi? Wenye kujua kidogo kuhusu huu mradi watujuze labda wengine tunashindwa kuelewa kwa akili ya kawaida.
      safi sana umeongea kitu kizur ila Ngoja watu tulipwe ela zetu au hutaki maendeleo!? Kutokana na Thread yako nakupa 44%. Nakutania tu Mjomba

    14. #14
      cham's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th December 2011
      Posts : 24
      Rep Power : 383
      Likes Received
      5
      Likes Given
      1

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Hatujui kuchagua vipaumbele. Ujenzi wa mji si kipaumbele hata kidogo kwa nchi yetu maskini. Vipaumbele vinatakiwi viwe nishati, elimu, maji, mawasiliano, barabara na afya.

    15. #15
      mizambwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2008
      Posts : 1,446
      Rep Power : 981
      Likes Received
      373
      Likes Given
      1825

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Quote By Elam View Post
      Goooo goo go go Prof. Tibaijuka hakuna wakuzuia maendeleo ya Watanzania...wakazi wakigamboni wanapaswa kujua Mjimpya sio kwaajili yao tuu, ni kwa ajili ya watanzania wote..tunataka maendeleo sio sumu za kisiasa toka kwa DR.Ndugulile, ya kwake tunayajua hivyo apishe maendeleo yaje...

      Wananchi wa Kigamboni hawajaukataa mji mpya, tatizo ni taratibu hazifuatwi na watendaji wa wizara ya ardhi katika kushughulikia mradi huu.

      Wamekuwa wakiwalazimisha wananchi kukubali pasipo kuwekwa wazi na hatima ya mali zao. Huwezi kuambiwa usaini kitu usichokielewa, na ndio yaliyofanyika Kigamboni.

      Lakini ni imani yangu kutokana na maelezo ya Waziri wa ardhi, wananchi wa kigamboni watakuwa wamemuelewa na endapo kama waziri hajaongea kisiasa, basi suluhisho litapatikana.

      MIZAMBWA
      NABII MTARAJIWA!!!
      SASA NIMEAMINI KUWA TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA!!!!, TUANDAE KABURI LA KUIZIKA MWAKA 2015

    16. #16
      mizambwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2008
      Posts : 1,446
      Rep Power : 981
      Likes Received
      373
      Likes Given
      1825

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Quote By wagaba View Post
      Tatizo kubwa la serikali ya CCM siku zote haina priority list ya projects zake. Sijui kwanini inapenda kukurupuka kila mara. Si lazima projects zote zianze kwa pamoja. tatizo kubwa hapa ni kuwa Kigamboni ina masilahi binafsi especially kwa viongozi wetu. Nani hajui kuwa wengi wao wameshakamata maeneo huko!
      Kinachofuata ni daraja la kigamboni kujengwa kwa haraka iwezekanavyo ili wasipate adha wanayoipata wakazi wake walalahoi sasa hivi.
      kujengwa Kigamboni ni maendeleo makubwa pia ila ndiyo kipaumbele kwa kipindi hiki kigumu cha uchumi?

      Tanzania jambo likifanyika kwa kuwekewa mkazo zaidi ujue lazima kuna 10% ya viongozi.

      MIZAMBWA
      NABII MTARAJIWA!!!
      SASA NIMEAMINI KUWA TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA!!!!, TUANDAE KABURI LA KUIZIKA MWAKA 2015

    17. #17
      mzozaji's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th July 2010
      Posts : 248
      Rep Power : 501
      Likes Received
      8
      Likes Given
      2

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Mbunge wao sasaa naye anawekewa zengwe kwa kuwatetea raia wake! Kuna jambo sio siri.

    18. #18
      WATANABE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 783
      Rep Power : 575
      Likes Received
      272
      Likes Given
      83

      Default Re: Hatuna maji, Umeme, CT scanner, tunakimbilia kujenga Kigamboni kwa Matrilioni!!!

      Kigambini ndio sehemu watakayoishi wamarekani watakaokuja kutwaa uranium yetu, ninyi wajinga si mnajengewa miundo mbinu kuelekea sehemu kutakakochimbwa uranium kama vile barabara za lami na umeme kupitia Millenium Challenge Account
      "Hatuwezi kutatua matatizo kwa akili ile ile ambayo ilisababisha yawepo"..Mch. Peter Msigwa

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...