
By
Yericko Nyerere
Imenilazimu leo kutembelea hospitali hizi kubwa nchini na kujionea hali ya mambo ilivyo,
Nasikitika na kustaajabu ya Musa (serikali) kuona inaendesha propagana kuwa mgomo umekwisha ilihali hali ya mambo bado ni mbaya:
HAKUNA huduma zinazoendelea zaidi ya wauguzi tu ndio wapo tena nao wachache!
Nimefika Muhimbili Hospital saa tisa alasiri nikakaa mpaka saa kumi na moja jioni, nikaenda Hospitali ya Ocean Road, ambako nako nimekuta hali ni mbaya!
Anaedanganya umma kuwa huduma zimrejea halitakii mema taifa hili,
Nasema tena mgomo bado upo, labda madaktari warejee usiku huu au kesho!
Seikali ielewe kuwa kanuni ni ile ile watumiayo wa amini wa kiroho:
(waislamu) Huwezi kupata thawa za mwenyezi Mungu bila kuenenda na ktk utakatifu wake!
(Wakristo) Huwezi kwenda mbinguni bila kupita kwa Yesu kristu.
Njia pekee ya kumaliza mgogoro huu ni meza pana yenye kuratibiwa na ulimi wa busara tu!
Ubabe na vitisho havitafanikiwa kwa hili, kitakachoumia ni nyasi tu (wananchi)
Kama huamini nenda Muhimbili au UGUA kisha njoo jukwani hapa useme ulichoshuhudia au kilichokupata!
Mungu lisaidi Taifa na Waja wako!
Follow Us Here