Hivi JamiiForums tunge-expose real ID zetu tungeondoka wangapi?
Kinachotusadia ni kwamba hakuna anayenijua jina langu halisi na wengi siwajui.
Hivi kila mmoja wetu angekuwa analazimika kuonekana ID yaani jina lake halisi na mahala unapokaa, hivi tungebaki salama kweli?
Au yangekuwa ndiyo yaleyale ya kuitwa na polisi watatu halafu unatokomoea kusikojulikana na kesho yake unakutwa mtaroni kama ilivyotokea kwa Robert Ouko kule Kenya.
...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}
Re: Hivi JamiiForums tunge-expose real ID zetu tungeondoka wangapi?
ingepunguza pumba humu ndani na kuwaacha watu wajadili kwa kina juu ya kuleta ukombozi wa kweli wa nchi hii. Unadhani ikiwa unatakiwa kabisa upatikane itashindikana?
Re: Hivi JamiiForums tunge-expose real ID zetu tungeondoka wangapi?
Mimi napingana nanyi.Ukijiamini na kama unaandika mambo ambayo umeyafanyia uchunguzi,au ambayo una uhakika huwezi kuogopa.Mimi naamini kuwa mtu ambaye hataki kujulikana na anaandika,anakua sio mkweli.Otherwise magazeti yangekosa waandishi.Tuache woga jitokezeni tuwe pamoja katika mapambano.
Re: Hivi JamiiForums tunge-expose real ID zetu tungeondoka wangapi?
Ni kweli ndg zangu, hata sisi tunaotumia ID na majina yetu, hatujui ni lini tutaokotwa, tuombeeni sana, huwa ninajiuliza hawa jamaa ni lini wataichomoa roho yangu? kisha najipa moyo bado bado. Tunaelewa kuwa tunamshika simba sharubu wakati yy yu macho. OOh..God be with us.
Kinachotusadia ni kwamba hakuna anayenijua jina langu halisi na wengi siwajui.
Hivi kila mmoja wetu angekuwa analazimika kuonekana ID yaani jina lake halisi na mahala unapokaa, hivi tungebaki salama kweli?
Au yangekuwa ndiyo yaleyale ya kuitwa na polisi watatu halafu unatokomoea kusikojulikana na kesho yake unakutwa mtaroni kama ilivyotokea kwa Robert Ouko kule Kenya.
Duh aisee wangetu ulimboka watu wengi tu humu ndani
Re: Hivi JamiiForums tunge-expose real ID zetu tungeondoka wangapi?
By Andrew Kellei
Mimi napingana nanyi.Ukijiamini na kama unaandika mambo ambayo umeyafanyia uchunguzi,au ambayo una uhakika huwezi kuogopa.Mimi naamini kuwa mtu ambaye hataki kujulikana na anaandika,anakua sio mkweli.Otherwise magazeti yangekosa waandishi.Tuache woga jitokezeni tuwe pamoja katika mapambano.
Uchunguzi wa uhakika? Wengine ni wafanyakazi wa hii serikali tena ofisi nyeti... Tungechinjwa zamani au tusingesema kitu hapa kama kule facebook, chezea serikali dhaifu wewe?
"Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa Rais Kikwete,Uzembe wa Bunge na Upuuzi wa CCM"
Re: Hivi JamiiForums tunge-expose real ID zetu tungeondoka wangapi?
mnajidanga nyote nyie
kuna mrundi mmoja,alikwenda ktk internet cafe na kutuma ujumbe kwa rafiki yake akimwelezea juu ya tishio la mlipuko utakaotokea huko shanghai,baada tu ya kuondoka na kuelekea chumbani,usiku ule alifuatwa hadi chumbani na sasa hajulikani alipo.
utumie jina halisi,ama usitumie jina halisi ni vyema ukawa makini na kile ukitumacho,kwani IP unayoitumia ndiyo itakayokumaliza.
"The person who says it cannot be done should not interrupt the person doing it."
Re: Hivi JamiiForums tunge-expose real ID zetu tungeondoka wangapi?
acheni woga, huna impact yoyote kwa harakati za kwenye keyboard, go out there and do something real ndio uanze kuhofia usalama wako. Kuficha id ni woga wa kijinga, kwa teknolojia hii watu wakitaka kukutafuta wanakupata tena haraka mno.
Follow Us Here