Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Madaktari Haydom nao wagoma

    Report Post
    Results 1 to 2 of 2
    1. #1
      Dingswayo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Location : Tanzania/Europe
      Posts : 2,628
      Rep Power : 5718
      Likes Received
      1054
      Likes Given
      2479

      Default Madaktari Haydom nao wagoma

      Thursday, 28 June 2012 20:18

      Joseph Lyimo,Mbulu

      MADAKTARI kumi wa Hospitali ya Haydom wilayani Mbulu katika Mkoa wa Manyara, wameungana na madaktari wa hospitali za Serikali nchini, katika mgomo wao unaondelea.

      Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, madaktari wa hospitali hiyo ya rufaa inayotoa huduma zake kwa wagonjwa kutoka katika Mikoa ya Manyara na Singida, walianza kugoma juzi.Hatua hiyo imesababisha madaktari wengine wanaoendelea na kazi, kuelemewa na wingi wa wagonjwa.

      Hospitali hiyo ya Haydom, inamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), lakini inapata vifaa tiba na dawa kutoka serikalini.Wakizungumza na waandishi wa habari kwa masharti ya kutotajwa majina, madaktari hao wanafanya masoma kwa vitendo katika hospitali hiyo, walisema hawataendea kutoa huduma hadi madai yao yatakapotimizwa.

      Pia walilaani vikali tukio la kutekwa nyara na kujeruhiwa vibaya kwa Dk Ulimboka ."Hata hivyo sisi tunaendeleza mapambano ya kudai haki zetu kwa njia ya mgomo. Kwa nini wanatumia mbinu chafu za kijasusi kushughulikia Dk Ulimboka," alisema mmoja wa madaktari hao.

      Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Anatory Choya, hatua ya madaktari katika Hospitali ya Haydom, kuingia katika mgomo.

      Alisema hata hivyo, ofisi yake inaendelea na jitihada za kuzungumza nao, ili warejee kazini na kuwahudumia wananchi.

      Choya alisema kwa sasa madaktari wanaoendelea na kazi ,wameelemewa na mzigo wa kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa."Tulijaribu kuwaita ili tukae nao katika meza moja, lakini walikataa. Hata hivyo tunamshukuru Mungu wamba tangu walipogoma hakuna madhara yaliyotokea kwa wagonjwa waliopo hospitalini ," alisema Choya.
      Semper fi!

    2. Miaka 50

    3. #2
      afrodenzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Location : sweet home
      Posts : 15,617
      Rep Power : 26573
      Likes Received
      5846
      Likes Given
      5721

      Default Re: Madaktari Haydom nao wagoma

      Hii Serikali yetu itatumaliza . Tunahitaji ma doctor kuliko hata wabunge. Cha ajabu wabunge ndo wanaolipwa kulikoni. Aibu kwa sana.
      samvande2002 likes this.
      Reply With Quote

    4. FemaTV & Radio

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...