Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

    Report Post
    Page 3 of 5 FirstFirst 12345 LastLast
    Results 41 to 60 of 81
    1. #1
      kadoda11's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Location : planet earth
      Posts : 1,385
      Rep Power : 702
      Likes Received
      355
      Likes Given
      183

      Default Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.
      Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.
      Vikundi vya Wachagga
      Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia Mashariki Tarakea, Rombo hadi magharibi ya Kilimanjaro Siha, Machame. Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Marangu, Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo, Wa-Uru, na Wa-Siha.
      Historia ya elimu kati ya Wachagga
      Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Kikristo walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.
      Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamishinari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi. Wakati wakazi wa mikoa mingine walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1,2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro vimezidi sana idadi ya shule katika miko mingine yote.
      Ni vema pia kusema kwamba shule hizi kuvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi wachagga tu
      Kilimo na chakula
      Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe,viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu
      Ndizi za Wachagga
      Ingawa wachaga wa leo wanakula vyakula mbali mbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi. Kuna ndizi za aina mbalimbali na hutumika kwa matumiza tofauti. Mfano ndizi kisukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda. Ndizi mshare kukatwa zikiwa mbichi na kupikwa chakula mbalimbali pamoja na nyama ya ngombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko,kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.
      Aina nyingine ni ndizi-ngombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
      Aina nyingine ni ndizi-mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Darisalamu utaona ndizi- mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku-vumbi au kiti-moto.
      Wachagga na muhogo
      Inasemekana kuwa "mchagga halisi, hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yao; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani hasa wa Machame walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba huko huko Kilimanjaro, majirani na watani wa wachagga yaani Wapare walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.
      Ulaji kiti-moto
      Pamoja na kilimo cha mazao, wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukupendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo waisalmu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".
      Majina ya Kichagga
      Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo. Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema,
      Mkenda, Massawe, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.
      Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.
      Utawala wa jadi ya Wachagga
      Watawala wa kichagga waliitwa "Mangi". Hawa walihodhi mashamba, ngombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa
      na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (wajerumani), Mangi Sina wa kibosho - anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na wamachame na kupora ngombe na mazao yao na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa ma-Mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa ni kama mabepari wa kwanza wa ki-jadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao. Usemi maarufu wa "u-Mangi-meza" inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa kichagga.
      Ardhi
      Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi. Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi uchagani ulipelekea wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya nk wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula. Ukienda kwenye mikoa hii utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta katika makusanyio ya wachaga mikoani mbali mbali.
      Maoni juu ya Wachagga
      Ingawa wanaume wa kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ngombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongon mwao. Wanawake wa kichagga (hasa kutoka
      Rombo) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa kipato cha wachaga ni kikubwa kulinganisha na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo kunatokana na wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa wototo ni wale ambao wazazi wao ni watu wapombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba uchagani kuna vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa nibiashara kubwa. Karibu kila kaya kumi natano kuna kila cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya dede sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchaggani kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi mchana na jioni. Sababu nyingi ni kazi; mama wa kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hawana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za kibiashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi. Pia baadhi ya wamama wa kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri tofauti na chakulawalichoandaliwa watoto japo ni chakula kilekile.

      CHANZO : Wachagga - Wikipedia, kamusi elezo huru
      Riwa, sirghanam, Mboko and 3 others like this.
      "The only true wisdom is in knowing you know nothing"

    2. RukaaJuu Final

    3. #41
      combra's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th May 2012
      Posts : 69
      Rep Power : 365
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default

      mtoa mada kuna kitu amesahau,kwanini wachaga wamefafanana yaani nirahisi sana kumgundua mtu anaetokea moshi,eidha kwa mwendo au sura.ufafanuzi plz

    4. #42
      dwight's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 288
      Rep Power : 491
      Likes Received
      20
      Likes Given
      3

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Chagga's run the country!
      Mtake msitake!

    5. #43
      roby2006's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th September 2011
      Posts : 315
      Rep Power : 450
      Likes Received
      45
      Likes Given
      12

      Default

      georgeallen rudia kuisoma vizuri utaielewa hakuna alichobakisha
      Quote By georgeallen
      aliyeleta mada hakugusia kabisa vitu vingine muhimu kwa wachagga: kusogeza mipaka, kupenda "ela" (kukwiba), kukaa mbali na wake zao, urithi kwa wanaume tu, kisusio.

    6. #44
      Mkereketwa_Huyu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2011
      Location : London | Dar Es Salaam
      Posts : 1,807
      Rep Power : 4586
      Likes Received
      577
      Likes Given
      413

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Quote By Vmark.
      Ok then! Hao wanawake wanaokucfia ts just they are hooking ua bucks buddy! They also want money. Pili cna cha kuniliza bse mie cio mchagga arifu.....i wanna know the facts only bse mengi yanapotoshwa kuhusu hawa watu.

      Naona bado hujanielewa, mimi siwapi pesa bali nguvu zangu za kiume. Soma mistari tena usikurupuke tu kunijibu.

    7. #45
      kadoda11's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Location : planet earth
      Posts : 1,385
      Rep Power : 702
      Likes Received
      355
      Likes Given
      183

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Quote By ARV
      Sifa moja aliyosahau kuiandika mtoa mada ni..........
      naona wadau mnasema nimesau kuandika hiki mara kile kuhusu wachagga.nilichokiandika sijakitunga mimi.nime-copy toka mtandao wa wikipedia na ku-paste hapa jamvini ndio maana nikaweka link chini ya thread kuonyesha source of information.kwa anaeteka kusahihisaha au kuongeza taarifa aingie katika mtandao wa wikipedia kuna option ya ku-edit.
      "The only true wisdom is in knowing you know nothing"

    8. Miaka 50

    9. #46
      Vmark.'s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd August 2011
      Location : Arusha/Moshi.
      Posts : 735
      Rep Power : 542
      Likes Received
      89
      Likes Given
      9

      Default

      Quote By Mkereketwa_Huyu
      Naona bado hujanielewa, mimi siwapi pesa bali nguvu zangu za kiume. Soma mistari tena usikurupuke tu kunijibu.
      Endelea kuwapa hizo nguvu bse humu jamvini wapo and soon watahamia kwako wote.......then i will bet my neck.

    10. #47
      Vmark.'s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd August 2011
      Location : Arusha/Moshi.
      Posts : 735
      Rep Power : 542
      Likes Received
      89
      Likes Given
      9

      Default

      Quote By combra
      mleta mada kuna kitu amesahau."kwanini wachaga wengi sura zao zimefafana?yaani ukimwaona sura tu, utajua huyu ametokea moshi,why?
      Kwasababu ni wachaga.Period!

    11. #48
      samilakadunda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th October 2011
      Posts : 792
      Rep Power : 543
      Likes Received
      102
      Likes Given
      13

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Nadeclea interest "mamsapu wangu mchaga tena wa rombo mashati" ukoo kimario! Hanipi shida walasioni uchagga wake juu yahaya yasemwayo, labda wale wa chagga wa kale(enzi za mwalimu).

    12. #49
      Vmark.'s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd August 2011
      Location : Arusha/Moshi.
      Posts : 735
      Rep Power : 542
      Likes Received
      89
      Likes Given
      9

      Default

      Quote By samilakadunda
      Nadeclea interest "mamsapu wangu mchaga tena wa rombo mashati" ukoo kimario! Hanipi shida walasioni uchagga wake juu yahaya yasemwayo, labda wale wa chagga wa kale(enzi za mwalimu).
      Hongera arifu...... Mie ni mkikuyu na namiliki eneo rombo an ma yf to be ni mchagga thts nice....

    13. #50
      Rural Swagga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Location : Mars
      Posts : 622
      Rep Power : 555
      Likes Received
      161
      Likes Given
      640

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Kilimanjaro-Moshi-Old Moshi ndio kwetu,Proud 2b chagga,,,Safi sana,,Na kwa taarifa yenu Tumesambaa dunia nzima Napost hii kitu nipo Rio de Janeiro Brazil.Na tuna kikundi chetu cha wachagga mpaka sasa tuna memba 38
      A fool with a plan can outsmart a genius with no plan any day..!!!

    14. #51
      monyaichi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th May 2012
      Posts : 18
      Rep Power : 355
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Quote By Mkereketwa_Huyu
      Sioni umuhimu wake hata kidogo! Kwa zamani miaka ya 47 ilikuwa hivi ila siku hizi karibia kila kabila limesoma na wachagga wengi walisomeshwa na waseminari kwa bure enzi zile kwani wazazi wao walikuwa hawana uwezo na ni wafanyakazi wa seminari. Kwa hiyo wachagga walikuwa hawana budi kusoma.
      kwa hiyo unataka kusema wakati wachaga wanafanya kazi kwenye seminari makabila mengine walikuwa wapi? wasukuma walikuwa wakivua samaki? haihusu wachaga siku zote ni watu wakuona mbali

    15. #52
      Mkereketwa_Huyu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2011
      Location : London | Dar Es Salaam
      Posts : 1,807
      Rep Power : 4586
      Likes Received
      577
      Likes Given
      413

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Quote By monyaichi
      kwa hiyo unataka kusema wakati wachaga wanafanya kazi kwenye seminari makabila mengine walikuwa wapi? wasukuma walikuwa wakivua samaki? haihusu wachaga siku zote ni watu wakuona mbali
      Monyaiichi, sikia hizi habari za wachagga kuwa watu wa kuona mbali si za ukweli ila ni kasumba tu. Nakubaliana nawe to some extent kuwa wachagga wanapenda ku husstle, lakini I am telling you as I know si porojo wala nini...hakuna mtu asiyependa kuwa na pesa au amaisha mazuri. Watu wengi ni husstlers hapa bongo na ndiyo maana mpaka likazuka hili jina la wamachinga unafikiri ni kwa nini? wamachinga ni watu wa kusini, si ndiyo au nao ni wachagga kwa mtazamo wako?

    16. #53
      Ndechumia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2011
      Posts : 776
      Rep Power : 553
      Likes Received
      136
      Likes Given
      306

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      tafuta pesa mangi!! acha kulalamika

    17. #54
      matumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th July 2011
      Posts : 2,338
      Rep Power : 1445
      Likes Received
      649
      Likes Given
      500

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Mungu akunyime kila kitu lakini asikupe sura ya kichaga....yani ata iweje utabaki boya tu mbele ya wanyamwenga....sura ya kichaga!!!????aaaaarrrrgggghhh !!!

    18. #55
      UAMSHO TAKBIRI's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      2

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      kwa vitega uchumi vilivyopo kweli mkoa huu unastahili kuitwa jiji

    19. #56
      malema 1989's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2012
      Posts : 806
      Rep Power : 742
      Likes Received
      147
      Likes Given
      117

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Quote By UAMSHO TAKBIRI
      kwa vitega uchumi vilivyopo kweli mkoa huu unastahili kuitwa jiji
      inawezekana hata leo, ila tuongeze bidii zaidi katika kazi na tusisahau kurudi kwetu mara kwa mara kuona sehemu ya kusaidia.(MBUYA YA MCHAGA) NA ITARAMO MBE!

    20. #57
      SinaChama's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 37
      Rep Power : 363
      Likes Received
      13
      Likes Given
      19

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      [QUOTE=Mkereketwa_Huyu;4127693]Kwa hii ya tatu ni kwa sababu wanaume wengi wa kichagga hawajui mapenzi, hii wala si siri. Utakuta jamaa yupo na demu/mke wake kitandani huku anawaza akaibe wapi ama akihamka asubuhi afanye kitu gani huku demu/mke anawaza akajitongoze kwa nani ili afurahishe nafsi yake. Na nafikiri hii pia inachangia kina Wolper, Uwoya, Lulu, na visichana vingine vya kichagga hapa Bongo kuwa viruka njia,[/QUOTE

      Mchango wako hauna uthibitisho. Ni dhana tupu.

    21. #58
      SinaChama's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 37
      Rep Power : 363
      Likes Received
      13
      Likes Given
      19

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Quote By Mkereketwa_Huyu
      Monyaiichi, sikia hizi habari za wachagga kuwa watu wa kuona mbali si za ukweli ila ni kasumba tu. Nakubaliana nawe to some extent kuwa wachagga wanapenda ku husstle, lakini I am telling you as I know si porojo wala nini...hakuna mtu asiyependa kuwa na pesa au amaisha mazuri. Watu wengi ni husstlers hapa bongo na ndiyo maana mpaka likazuka hili jina la wamachinga unafikiri ni kwa nini? wamachinga ni watu wa kusini, si ndiyo au nao ni wachagga kwa mtazamo wako?
      Mkereketwa_Huyu, Wachaga hawapo walipo kwasababu ya bahati tu. Kuna usemi unasema bahati inatokea fursa zinapokutana na maandalizi. Fursa nyingi zinawapita watu na wanaziangalia tu, kwa kuto kujua kwamba ni fursa au kwa uoga wa kujaribu. Wachaga wengi wana roho ya kuthubutu.
      Tatizo la ardhi ni moja ya sababu iliyowapelekea wachaga wengi kuhamia mijii ni kufanya kazi kwa kutumia elimu yao, na pia kufanya biashara. Mkoa wa Kilimanjaro ni mdogo. Na kwa mila za kichaga mzazi anawagawia watoto wake shamba linaloitwa kiamba, watoto nao wanawagawia watoto wanaowazaa, kwahiyo ardhi inaenda ikipungua jinsi vizazi vinavyoongezeka na kunakuwa hakuna tena mashamba ya kilimo kama zamani. hiyo imelazimisha wachaga wengi sana kuondoka kule vijijini na kwenda mjini kutafuta shughuli mbadala. Hiyo ndio iliyowafanya waonekane Hustlers.
      Sasa na kale kaelimu kadogo kanakopatikana kwenye vishule vyao kanawasaidia.
      Hili ni kabila maarufu katika kufanya biashara, Kuna wafanya biashara wakubwa na wadogo.
      Last edited by SinaChama; 1st July 2012 at 01:54.

    22. #59
      jmushi1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2007
      Posts : 14,376
      Rep Power : 16493
      Likes Received
      4301
      Likes Given
      5491

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Quote By combra
      mleta mada kuna kitu amesahau."kwanini wachaga wengi sura zao zimefafana?yaani ukimwaona sura tu, utajua huyu ametokea moshi,why?
      Unazungumzia "uniqueness"?
      Siyo mbaya kabisa, hata Mmasai unamjuwa, so as mgogo etc, shida ikwapi?
      Na si kila mtu/mchagga, ametokea Moshi **** wewe!
      "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

    23. #60
      SinaChama's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 37
      Rep Power : 363
      Likes Received
      13
      Likes Given
      19

      Default Re: Fahamu zaidi kuhusu Wachagga.

      Quote By Vmark.
      Ok then! Hao wanawake wanaokucfia ts just they are hooking ua bucks buddy! They also want money. Pili cna cha kuniliza bse mie cio mchagga arifu.....i wanna know the facts only bse mengi yanapotoshwa kuhusu hawa watu.
      Huyo anachuki na wachaga achana naye. Anataka kutuaminisha kwamba kabila zima la wachaga hawajui kufanya ngono. What is so special?

    Page 3 of 5 FirstFirst 12345 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...