Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Take Care People!!!Men at Work.

    Report Post
    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast
    Results 21 to 40 of 59
    1. #1
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default Take Care People!!!Men at Work.

      Leo majira ya saa 8 mchana nimeshuhudia mwanamume mtu mzima(kama miaka 30 hivi) akiwa amekaa kitako kwenye mchanga huku akimwaga machozi kama vile mtoto mdogo aliyekosa kutimiziwa ahadi ya kununuliwa pipi na wazazi wake.
      Baada ya kusogea kidogo na kuuliza nini kimemsibu nikasikia akitamka kwa majonzi kwamba ''laptop ya kazini(akionyesha begi tupu),simu yangu na pesa taslimu Tsh.600,000 vyote vimekwenda na matapeli'' huku akisisitiza:''Jamaa wameniharibia kazi,jamaa wameniharibia kazi'', akirejelea laptop ya kazini ndiyo inayomtia mawazo zaidi.
      Kabla sijatafakari vizuri walinzi wa Supermarket ya TSN pale kona ya kuingia hospitali kuu ya Mhimbili wakanionyesha mabaki ya vitu vyenye mng'ao kama wa dhahabu huku wakiniambia kwamba jamaa ameingizwa mjini na wajanja wa mjini kwa kuuziwa kanyaboya.
      Lakini baada ya kumuuliza vizuri yule mtu aliyetapeliwa akijitambulisha kwa jina moja tu 'Josiah' na anafanya kazi kama Tax Consultant kwenye firm fulani mjini na akasema hakumbuki chochote kuhusu majadiliano yoyote ya kuuziana mali yoyote bali anachokumbuka ni kushikwa bega na kuitwa na sauti iliyosema:''Oya mkuu nakuomba tuongee kidogo'' kisha akaingia kwenye gari na kukuta vijana wawili na msichana mmoja waliovalia vizuri kisha wakamwambia ''Tuna dhahabu hapa tunaiuza kwa bei poa'' baada ya hapo hakumbuki kitu zaidi ya kujikuta hapo alipo bila ya vitu tajwa hapo juu.Jasho lilikuwa likimtoka sana huku ameinamisha kichwa kwa masikitiko baada ya kumaliza kujieleza.
      Baada ya muda kidogo kwa tukio zuri gari ya polisi ikakatiza na ikabidi tuisimamishe ili jamaa aliyetapeliwa akatoe maelezo polisi na pia tukamchangia kama Tsh.10,000 ya kwenda kokote atakapoelekea baada ya kutoka kituo cha polisi pale Mhimbili.
      Tahadhari kwa wote tuwe makini katika kuongea na watu tusio wafahamu kwa kuwa hili jambo la utapeli wa kiajabu-ajabu limeshamiri sana sehemu za katikati ya mji.Nadhani watu wameongeza speed ya kazi baada ya kusomewa bajeti ya 2012-2013.Men at work people..Watch Out!!

    2. Miaka 50

    3. #21
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default

      Quote By asigwa
      DUH......
      sasa na vilaptop vyetu hivi used mbona mwaka huu kazi ipo?? mpaka mwaka huu wa bajeti uishe tutakua tushakimbia mjini..
      Kikatie bima kilaputopu chako wasije kukuzidi mahesabu watoto wa jiji.

    4. #22
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default

      Quote By Godwishes
      Tunashkur mkuu,cc ambao 2ko mikoani huku huwa tunaonewaga!SASA hata nikija Tz,nakuwa carefu na sampo kama izo
      Karibu Tz ila macho yawe wazi kuna watu wamejiajiri kwenye sekta zisizo rasmi halafu pia kuna walioenda mbali zaidi wamejiajiri katika sekta isiyo rasmi plus haramu.

    5. #23
      denim kagaika's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th August 2011
      Posts : 229
      Rep Power : 637
      Likes Received
      27
      Likes Given
      11

      Default

      Quote By Ambitious
      Ha..ha..ha..ha Ajira millioni moja za Kikwete.
      Yeah hata mimi nimeona juhudi zake raisi wetu mdhaifu(kwa mujibu wa Mh Mnyika).
      Miss-Thang likes this.

    6. #24
      denim kagaika's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th August 2011
      Posts : 229
      Rep Power : 637
      Likes Received
      27
      Likes Given
      11

      Default

      Quote By Ambitious
      Wewe ulitaka fanya nini hapa?
      Huyo binti anajua kuchakachua thread alianza kuigeuza kijiwe cha salamu mtu chake njoo umchukue huyu asije kutandikwa huku.

    7. #25
      Kalumbesa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2010
      Location : Shamba
      Posts : 864
      Rep Power : 602
      Likes Received
      266
      Likes Given
      120

      Default Re: Take Care People!!!Men at Work.

      Hawa jamaa ni hatari, wamenijaribu mara kadhaa bila mafanikio..Huwa natumia principle yangu moja tu "I dont mess with anyone I dont know". Kuna siku jamaa alinisimamisha maeneo ya ubungo stand ya mkoa kwenye kituo cha basi kwenda mjini majira ya saa mbili kasoro usiku na kuanza mazungumzo nami
      Jamaa: Samahani za leo
      Mimi:Nzuri
      Jamaa: Hapa naweza pata gari za masaki?
      Mimi:Hapana,labda upande gari za msasani halafu ukapande gari nyingine mbele kwa mbele ,kondakta atakueleza zaidi

      Tukiwa tunaendelea na mazungumzo akajitokeza mshikaji aliyeonekana kufuatilia maongezi yetu na kudakia mazungumzo nitamwita rafiki

      Rafiki: ebwana vipi, anataka kwenda Masaki?
      Mimi: Ndio
      Rafiki: Sasa hapa unapanda gari za Msasani ukishuka unapanda bajaji,kwani unaelekea Masaki sehemu gani?
      Jamaa:Barrick
      Rafiki: Barrick saa mbili usiku huu? au una appointment na mtu pale?
      Jamaa:Ndio,nina madini nauza kuna mtu pale naenda kuonana nae anisaidie kunielekeza wapi nitauza kirahisi
      Rafiki: Ebwana angalia mjini hapa mzee,kuwa makini! Sasa hakuna shida mimi najua masoko tutakusaidia na mshikaji hapa utauza hayo madini ila na sisi itabidi ututoe.
      Jamaa: Sawa haina shida,nitashukuru sana
      Mimi: Sasa kwa sababu rafiki anajua mahali pa wewe kuuza madini yako atakusaidia mimi nina mambo yangu mengi nikasepa

      Nikaondoka kisha nikasimama mbele kidogo kuna jamaa anauza pweza nikanza gonga kipande moja baada ya nyingine huku nawacheki kwa kuibia,walikuwa wakiniangalia kwa makini na hasira hivi,kama watu wanaotafuta namna ya kuni attack.baada ya dakika chache nilipotupa jicho sikuwaona tena..

      Kuwa makini na matapeli na usisahau hawana alama usoni!!
      Ambitious likes this.

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default

      Quote By Mtanzania Imara

      Definitely men at work.Walikuwa wanataka kuku-set ili uingie kwenye mtego wao ila wewe ukawaponyoka kama kambale ukateleza.Wabaya sana hawa watu kwa muda wa dakika 30 unakuwa tayari umeshazidiwa mahesabu.
      Binadamu wabaya sana hasa wakiwa wanawinda mtu kwa minajili ya kujipatia fedha yaani hawana huruma hata kidogo,ubinadamu haupo kabisa.

    10. #27
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default

      Quote By denim kagaika
      Huyo binti anajua kuchakachua thread alianza kuigeuza kijiwe cha salamu mtu chake njoo umchukue huyu asije kutandikwa huku.
      Ha..ha..ha kumbe na wewe umemsoma ehhh!!

    11. #28
      wehoodie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2011
      Posts : 277
      Rep Power : 434
      Likes Received
      67
      Likes Given
      28

      Default Re: Take Care People!!!Men at Work.

      Damn....kama lagos

    12. #29
      asigwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Location : TANDHANIYA
      Posts : 4,388
      Rep Power : 1264
      Likes Received
      1208
      Likes Given
      1253

      Default Re: Take Care People!!!Men at Work.

      Quote By Ambitious
      Kikatie bima kilaputopu chako wasije kukuzidi mahesabu watoto wa jiji.
      kweli mkuu inabidi tukate bima..ila kwa upepo huu unaweza kukuta hata bima bado ukapewa ya kuchakachua

    13. #30
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default

      Quote By wehoodie
      Damn....kama lagos
      Yeah ni kweli watu wameanza kuwa na elimu + maarifa halafu kazi hakuna kwa hiyo wanajaribu plan B's.

    14. #31
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default

      Quote By asigwa
      kweli mkuu inabidi tukate bima..ila kwa upepo huu unaweza kukuta hata bima bado ukapewa ya kuchakachua
      Ha..ha bima feki zipo yaani watu wanatafuta hela kwa nguvu mpaka wanatishia amani.

    15. #32
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,572
      Rep Power : 16763
      Likes Received
      2480
      Likes Given
      1844

      Default Re: Take Care People!!!Men at Work.

      Hawa jamaa ni hatari sana maana hawana alama usoni. Ni kuwa makini tu.

    16. #33
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default

      Quote By Katavi
      Hawa jamaa ni hatari sana maana hawana alama usoni. Ni kuwa makini tu.
      Kweli mkuu wako kawaida sana na sio rahisi kuwatilia mashaka.Wana confidence sana na ni watu wanaoweza kujieleza bila kukwamakwama.Very smart people who make pre-calculated moves.

    17. #34
      stroke's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 17th February 2012
      Posts : 1,427
      Rep Power : 0
      Likes Received
      153
      Likes Given
      4

      Default Re: Take Care People!!!Men at Work.

      mbaya zaidi, hawa jamaa wanafuatilia watu tokea bank..hii ilitokea kwa mama flani ninayemfahamu ..ambaye alifuatiliwa na mwanamke mwenzake ambaye alimtapeli kwa staili kama hiyo ya dhahabu..na kuchukua laki 4 zake...nadhani wanatumia dawa pia..maana huyo mama kazubaa anakuja shtuka baadae hata hata senti kwenye pochi..ikabidi apigiewatu simu kwenda mchukua alipo maana hata nauli hakua nayo...so issue ya dhahabu au madini achaneni nayo....na si kila mtu ni wa kuongea nae....unatiririka tu,....wengine sio watu...

    18. #35
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default

      Quote By mkaliwakitaa

      Inawezekana kuna mbinu za kishirikiana au dawa fulani ya kupumbaza akili...Ni hatari sana na linaweza kumkuta mtu yeyote.

    19. #36
      Radhia Sweety's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 10th August 2011
      Posts : 1,333
      Rep Power : 0
      Likes Received
      639
      Likes Given
      4

      Default Re: Take Care People!!!Men at Work.

      Wanaoibiwa nao maboya sana. Yaani mtu anakuambia ana madini ya dhahabu halafu wewe unaamini kirahisirahisi tu.

    20. #37
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,572
      Rep Power : 16763
      Likes Received
      2480
      Likes Given
      1844

      Default Re: Take Care People!!!Men at Work.

      Quote By Radhia Sweety
      Wanaoibiwa nao maboya sana. Yaani mtu anakuambia ana madini ya dhahabu halafu wewe unaamini kirahisirahisi tu.
      Wengine wanakuwa na mambo ya ushirikina kwa hiyo unakuwa kama umepumbazwa vile. Ukishaibiwa ndio fahamu zinakurudia..

    21. #38
      Ambitious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2011
      Posts : 1,802
      Rep Power : 734
      Likes Received
      559
      Likes Given
      243

      Default

      Quote By Radhia Sweety
      Wanaoibiwa nao maboya sana. Yaani mtu anakuambia ana madini ya dhahabu halafu wewe unaamini kirahisirahisi tu.
      Dont go there binti.Hawa watu ni hatari sana.I think they have some kind of a voodoo spell or a brainwashing technique.By the time you are back to your senses,they are loooong gone.
      Last edited by Ambitious; 20th June 2012 at 10:25.

    22. #39
      Jaguar's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th March 2011
      Location : IRINGA
      Posts : 3,000
      Rep Power : 1085
      Likes Received
      677
      Likes Given
      256

      Default

      Quote By tizo1
      Hakuna cha sababu za kumcheka!hawa jamb ni noma siku hiz wanatumia mazingambwe....
      Kuna dada mmoja maeneo ya kimara mwisho naye yalimkuta hayo.Alijikuta anawapeleka matapeli waliodai ni waganga nyumbani kwake.Walimwambia kwamba walioteshwa kuhusu matatizo aliyonayo na kwamba wangempatia tiba.Dada alijikuta akiwapeleka home na kuwakabidhi bila hofu wala wasi TV,radio,woofer n.k.Ile jamaa wanampa kisogo tu ndo akastukia jina la mchezo kwamba keshapigwa na wajanja,i mean ameogeshwa roundabout saa 6 mchana kweupeeee bila ukungu.

    23. #40
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,572
      Rep Power : 16763
      Likes Received
      2480
      Likes Given
      1844

      Default

      Quote By Jaguar
      Kuna dada mmoja maeneo ya kimara mwisho naye yalimkuta hayo.Alijikuta anawapeleka matapeli waliodai ni waganga nyumbani kwake.Walimwambia kwamba walioteshwa kuhusu matatizo aliyonayo na kwamba wangempatia tiba.Dada alijikuta akiwapeleka home na kuwakabidhi bila hofu wala wasi TV,radio,woofer n.k.Ile jamaa wanampa kisogo tu ndo akastukia jina la mchezo kwamba keshapigwa na wajanja,i mean ameogeshwa roundabout saa 6 mchana kweupeeee bila ukungu.
      Sasa kesi kama hiyo utakwepa vipi....!!

    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...