Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

    Report Post
    Results 1 to 10 of 10
    1. Ptz is offline
      Ptz
      #1
      Ptz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd August 2011
      Location : SUMBAWANGA
      Posts : 266
      Rep Power : 600
      Likes Received
      87
      Likes Given
      39

      Default Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

      Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana vikao vya bunge letu la Tanzania live kwa kupitia tv. Nimeshuhudia baadhi ya wabunge na mawaziri wakiongea na simu bungeni huku kikao cha bunge likiendelea, ni mara kadhaa nimemshuhudia Mkuchika akiongea na simu na gazeti la mwanachi lilishamtoa kwenye front page picha yake huku akiongea na simu.

      Leo hii nimemshudia Davide Kafulia (mbunge Kigoma Kusini) akiongea na simu huku mzee Cheyo akitoa mchango wake, zaidi ya yote punde baada ya mzee Cheyo(Mbunge wa Bariadi) kumalizia mchango wake, kuna Mbunge wa Mbalali mh Kilufi akichangia kuna mbunge mmoja alikuwa kaketi kushoto kwake ghafla msg iliingia kwenye simu yake, niliisikia msg kwa ringtone ya Nokia, mbunge huyo alichukua simu na kuisoma msg na mara tu baada ya kusoma alionesha tabasamu zito (Source TBC leo saa 11 hadi moja jioni). Kwangu mimi nauita upumbavu. Nimekuwa pia nikifuatilia bunge la Kenya na Uganda, sijawahiona upumbavu huu.

      Ni bunge hili hili kuna mbunge mmoja alishathubutu kughushi hati na saini ya waziri mkuu Mizengo Pinda na kuachwa bila hatua yoyote ile. Je, ni harali kwa tabia kufanywa na hawa watu tunawaita waheshimiwa kuzitumia simu zao wakati wa kikao kikiendelea katika jengo tunaloliita tukufu kwani hata huku uraiani kuna vikao tumekuwa tukivifanya ni kulazimika kuzizima au kutoingia na simu kabisa,

      Kwa mifano ya mabunge ya wenzetu niliyoitaja mfano bunge la Kenya naona kwa Yule spika”sir Kenneth Marende, naibu wake “sir Farah Macalin” upumbavu ninaouona huukwa bunge letu Tanzania si rahisi kuuvumilia kwa bunge la Kenya, nilishashudia waziri akitolewa nje na kupigwa Ban ya vikao vitatu kwa kutojibu swali ipasavyo kwa ushahidi nilionao Bunge la Kenya ni Bunge la Kenya kweli “It’s a really Kenyans Parliament” ni vigumu kumjua hata mpinzani au mtawala ni ninani! Nawasilisha.


    2. #2
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,727
      Rep Power : 734
      Likes Received
      300
      Likes Given
      36

      Default Re: Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

      Haya tumeyataka wenyewe kama hatutaki mambo ya ovyo basi ikatae ccm kwa kuichagua CDM

    3. #3
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2888
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

      Hiko ni KIJIWE MDAU

    4. #4
      IPECACUANHA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th February 2011
      Posts : 1,114
      Rep Power : 644
      Likes Received
      229
      Likes Given
      51

      Default Re: Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

      Wabunge na viongozi wetu wamejaa mzaha katika utendaji wao. Mtu makini anayetambua umuhimu wake bungeni hawezi kutumia simu. Ni aibu yao na yetu wapiga kura tunaoshindwa kuwawajibisha wabunge wetu. Upuuzi unaofanyika Tanzania katika uongozi haupo mahali popote DUNIANI. Hapa hawara anahongwa cheo na wote tunaishia kuchangia kwa kodi zetu. Mhalifu anapata uteuzi wa Raisi. Ni ajabu na kweli.

    5. #5
      Moony's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2011
      Location : Oshakati, Namibia
      Posts : 1,110
      Rep Power : 636
      Likes Received
      261
      Likes Given
      279

      Default Re: Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

      Quote By ptz View Post
      nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana vikao vya bunge letu la tanzania live kwa kupitia tv. Nimeshuhudia baadhi ya wabunge na mawaziri wakiongea na simu bungeni huku kikao cha bunge likiendelea, ni mara kadhaa nimemshuhudia mkuchika akiongea na simu na gazeti la mwanachi lilishamtoa kwenye front page picha yake huku akiongea na simu.

      Leo hii nimemshudia davide kafulia (mbunge kigoma kusini) akiongea na simu huku mzee cheyo akitoa mchango wake, zaidi ya yote punde baada ya mzee cheyo(mbunge wa bariadi) kumalizia mchango wake, kuna mbunge wa mbalali mh kilufi akichangia kuna mbunge mmoja alikuwa kaketi kushoto kwake ghafla msg iliingia kwenye simu yake, niliisikia msg kwa ringtone ya nokia, mbunge huyo alichukua simu na kuisoma msg na mara tu baada ya kusoma alionesha tabasamu zito (source tbc leo saa 11 hadi moja jioni). Kwangu mimi nauita upumbavu. Nimekuwa pia nikifuatilia bunge la kenya na uganda, sijawahiona upumbavu huu.

      Ni bunge hili hili kuna mbunge mmoja alishathubutu kughushi hati na saini ya waziri mkuu mizengo pinda na kuachwa bila hatua yoyote ile. Je, ni harali kwa tabia kufanywa na hawa watu tunawaita waheshimiwa kuzitumia simu zao wakati wa kikao kikiendelea katika jengo tunaloliita tukufu kwani hata huku uraiani kuna vikao tumekuwa tukivifanya ni kulazimika kuzizima au kutoingia na simu kabisa,

      kwa mifano ya mabunge ya wenzetu niliyoitaja mfano bunge la kenya naona kwa yule spika”sir kenneth marende, naibu wake “sir farah macalin” upumbavu ninaouona huukwa bunge letu tanzania si rahisi kuuvumilia kwa bunge la kenya, nilishashudia waziri akitolewa nje na kupigwa ban ya vikao vitatu kwa kutojibu swali ipasavyo kwa ushahidi nilionao bunge la kenya ni bunge la kenya kweli “it’s a really kenyans parliament” ni vigumu kumjua hata mpinzani au mtawala ni ninani! Nawasilisha.
      halali
      Lokissa likes this.


    6. #6
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 593
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

      Kwani hakukuwa na kiranja wa kuandika majina???

    7. #7
      Lokissa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Location : Goba
      Posts : 4,114
      Rep Power : 5815
      Likes Received
      1030
      Likes Given
      2878

      Default Re: Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

      bunge la kariakoo
      You may know me but you have no Idea who I am !

    8. #8
      gati's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st October 2009
      Posts : 76
      Rep Power : 506
      Likes Received
      13
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Bob G View Post
      Haya tumeyataka wenyewe kama hatutaki mambo ya ovyo basi ikatae ccm kwa kuichagua CDM
      naona hujaelewa vizuri hoja ya mtoa mada. Amefafanua vizuri na kutoa mfano hata wa David kafulila( ni CCM?!). Hapa hakuna hoja ya CCM wala CDM.

    9. #9
      Janjaweed's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 20th January 2010
      Posts : 3,700
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1416
      Likes Given
      1585

      Default Re: Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

      sio HARALI

    10. #10
      decruca's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 18th June 2012
      Posts : 166
      Rep Power : 386
      Likes Received
      34
      Likes Given
      14

      Default Re: Hivi ni harali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea

      Hapa mi sioni cha ajabu, hata wasipoongea na cm huwa wanapiga stori wenyewe kwa wenyewe huku hoja ikiendelea. na stori zinanoga hadi mtu anahama kiti chake anasogea kwa mwingine. wengine wanapiga usingizi tu kule mjengoni kipengele muhimu ni wakati wa kuandika majina kwa ajili ya sitting allowance,

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...