wanajf kama kuna mtu ana habari za kinachoendelea kuhusu urejeshwaji wa wanyama waliotoroshwa maana isije kuwa makelele ya bungeni ndio mwisho! kama walitoroshwa kimagendo najua hata sheria za kimataifa zitakuwa upande wetu
wanajf kama kuna mtu ana habari za kinachoendelea kuhusu urejeshwaji wa wanyama waliotoroshwa maana isije kuwa makelele ya bungeni ndio mwisho! kama walitoroshwa kimagendo najua hata sheria za kimataifa zitakuwa upande wetu
COAL UNDER PRESSURE BECOMES DIAMOND
Subutu! Walishakwenda na maji na wajanja wameshaweka vyao mifukoni.
sio wajanja mkuu sema wezi! kagasheki yuko wapi? anafukuza walinzi wa mbuga anaacha kufuatilia ishu kubwa(au sina habari kuna kitu kinaendelea) watu wa haki za wanyama hii ishu haiwezi kuwahusu? bunge liko wapi? domo tu! wabunge wa CHADEMA nahisi hili liko ndani ya uwezo wenu komaeni hadi ile ndege irudishe wanyama wetu.
COAL UNDER PRESSURE BECOMES DIAMOND
nyinyiemu huwa wana msemo wao wa kiendacho kwa mganga hakirudi,na msemo mwingine wa kufanana na huo unaosema kuwa chatu akimeza huwa hatapiki..........kwa hiyo ndugu yangu hebu jiongeze na wewe
Kama damu inakusisimka unapoona haki ya mtu ikipokwa na uko tayari kuitetea kwa gharama yeyote, basi hakika wewe ni Comrade wangu-Che Guevara.
Kama hawarudishwi mbona wahusika yaani waliowauza hao wanyama mbona wanapeta tu mtaani na magari yao ya kifahari na chama tawala nacho kimefunga macho tu au ni ule msemo kuwa UKINIGUSA NAKUGUSA NA WEWE manake walioko ndani ya chama tawala asilimia kubwa ni majangili/mafsadi
Wewe ukowapi Tanzania hii inayoongozwa na wasanii boys 2men au? Hapa bwana ukiiba bila kukamatwa imetoka kama mzee wa kiwira. akijua sheria Hazifanyi kazi akasimama na kusema bila aibu ofisi ya ubalozi Yeye ndio anahusika mzee wa intelejensia naye akazidi pindisha sheria kutetea wazee wa Epa kuwa warudishe pesa kwanza sheria baadae mmh hapa inabidi tuuiombee CDM ije na sera mpya uwajibikaji ndio twiga warudi kama wako hair bado teh teh teh. J
Nani kakwambia twiga anaweza kutoroshwa?
Huwezi kumtorosha twiga kwa ukubwa wake ule, tena kwa kutumia ndege ya jeshi ya nchi nyingine.
inabidi wakati wa bajeti ya maliasili na utalii wabunge wapatikise ikiwezekana isipite bila twiga kurudi. bila shaka hao jamaa walianza long sana hizi deal ila juzi kati ndio yamewakuta. yaani inasikitisha kweli.
COAL UNDER PRESSURE BECOMES DIAMOND
kwa bongo hii sahau..watazaliana wengine ila hao ndo kwa heri
There is a thin line between madness and creativity
Hio ndo imetoka Hii ndo Tanzania ya ccm
COAL UNDER PRESSURE BECOMES DIAMOND
Sioni sababu ya msingi ya kutumia mamilioni ya walipa kodi kwa ajili ya kurudisha twiga 4 ambao tayari wamesha athirika kisaikolojia na kuacha twiga wengi wakizidi kuuawa. hizo fedha bora zitumike kzwalinda waliopo
hii ilikua ni kutapatapa tu baada ya kunyang'anywa kitumbua..hawezi kufanya lolote kwani wizi wa kule ni mwingi mno toka enzi za magji na usafirishaji wa magogo nje ya nchi..MUKULU mwenyewe kaanza ujenzi wa hoteli moja matata sana kule mbugani na ni wakati wa huyu maige ..sasa unategemea lolote hapo??
Labda tumuulize mzee wa meeeeeeeeeeeeeeeeeeee
kwenye mwanainchi ya leo kuna watu watatu wamefungwa miaka 20 kila mmoja kwa kosa la kuua pundamilia mbugani. TZ ni vidagaa tu ndio wanaoonewa!
Follow Us Here