Wale wataalam wa hii mambo, hebu tuelezeni kwanini Tanzania ipo SADC. Na kwanini nchi zingine za East Africa ( Kenya, Uganda.... etc) hazipo.
Wale wataalam wa hii mambo, hebu tuelezeni kwanini Tanzania ipo SADC. Na kwanini nchi zingine za East Africa ( Kenya, Uganda.... etc) hazipo.
Vua GAMBA Vaa GWANDA
Nimeharibu kugoogle sipati jibu, tuendelee kungoja wataalam hapa.
HAKUNA NGUVU KUBWA KULIKO YA UMMA.
Swali lingine, Tanzania ilianza kuwa kwanza wapi, SADC au EAC!.
HAKI HAITAFUTWI UKIWA UMELALA KITANDANI...................
Tulianza kuwa EAC ambayo historia yake ilianzia toka ukoloni,baadae ikaanzishwa rasmi 1967 na kuvunjika 1977.(nikipata muda inshallah,siku moja ntaweka jamvini historia ya EAC). SADC ilitokana na kile kilichoitwa Front Line States ktk harakati za kudai uhuru kusini mwa Afrika. Kiukweli kutoka moyoni mimi nadhani SADC ndio ndg zetu wa ukweli na tungenufaika sana na ushirikiano huo kuliko hawa jamaa zetu wa EAC wanaowaza rasilimali zetu hususan ardhi kila siku. Hebu fikiri,kwa nn nchi zote nne za EAC zinailaumu TZ kwa kukwamisha maamuzi ya EAC.
Unajua zile nchi zilizokuwa zinajulikana kama frontline nations??? enzi zetu sisi shuleni kwenye somo la siasa tulikuwa tunafundishwa hizo, sasa sijui ilimu huko madarasani kwenu siku hizi ikoje, anyway nchi tano za kusini mwa Afrika, Tanzania, Zambia, Msumbiji,
Angola na Botwana zilijipa jukumu la kuzikomboa nchi za Afrika kusini, Nambia na Zimbabwe. Kwa muda mrefu mwalimu ndo alikuwa mwenyekiti wao, kuna wakati mabeberu waliwadhiaki viongozi hao kwa kumchora Nyerere amevaa koti la mifuko mitano na kila mfuko unakichwa cha kila kiongozi halafu kichwa cha habari kilikuwa ni swali lilikokuwa linauliza hawa ni akina nani na wanaenda wapi? Ha ha ha ha!!! mambo ya long time hayo!!
Any way baada ya uhuru kupatikana wazee watu wazima waliamua kuendeleza umoja na ushirikiano waliokuwa nao wakati wa mapambano, ndo ilizaliwa SADC ikihusisha nchi zilizokomboa na zilizokombolewa of course baadae kujumuisha nchi zingine zote za kusini mwa Afrika.
Sasa Kenya wao wakati sisi tunajitoa kwa hali na mali kuwaokoa ndugu zetu wao walikuwa wanajenga uchumi wao binafsi na kula bata!
Uganda walikuwa busy na alhaj field marshall akiwapa somo la kuiheshimu mamlaka. Tanzania chini ya mwalimu inamengi ya kujivunia, eti wale vikaragosi wa uamusho wanamtukana?????
Follow Us Here