Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mwenyekiti wa sau amuunga mkono wenje suala la jemus mbatia!!!!!!!!!!

    Report Post
    Results 1 to 5 of 5
    1. #1
      KING KING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2011
      Posts : 251
      Rep Power : 733
      Likes Received
      25
      Likes Given
      0

      Default Mwenyekiti wa sau amuunga mkono wenje suala la jemus mbatia!!!!!!!!!!

      Mwenyekiti wa chama cha sau amemuunga mkono mhe wenje na kumutaka mbatia aachie ngazi nafasi ya mwenyekiti taifa -nccr ili kuimarisha upinzani. Amesema kwa sasa hawezi kumushirikiasha mbatia kama mpinzani na kupanga mikakatati ya kuwakomboa wanyonge na kuikosoa serikali ya kikwete ,kwa hofu kuwa taarifa za mikakati hiyo zinaweza kumufikia rais kikwete mara moja!!.

      Amesema kazi ya upinzani ni kukosoa serikali na mkosoaji lazima awe huru kimawazo na muonekano.muonekano wa mbatia baada ya kuteuliwa na rais kikwte unaonyesha dhahiri kuwa hayupo huru na maoni yake hayawezi kuwa huru!!

      Hata wananchi hawawezi kumuamini kama jinsi walipomwamini kabla wakati anashughulikia suala la korosho mtwara.
      "mimi kama mwenyekiti wa sau naona uamuzi uliochukuliwa na jemusi mbatia na kutangazwa na katibu mwenezi nccr(mh moses machali) unalenga kuua upinzani na ni ushahidi mzuri kuwa mbatia na nccr ni kibaraka wa ccm. Hata hivyo kauli hiyo inaharibu mahusiano mazuri yaliyotokana na muafaka wa hivi karibuni kati ya chadema na nccr na kupelekea mbatia , kufuta kesi ya kawe dhidi ya halima mdee.kama mbatia alifuta kesi hiyo bila hila moyono mwake ni bora akawa na hofu ya mungu na kuzingatia maslahi ya taifa ambapo nguvu ya umma ina taka movement for change inayohitaji kunganisha vyama badala ya kutishiana!!!!!!!!
      Ni bora mbatia akatazama upya athari za kukubali uteuzi wa rais kikwete ambaye ni mwenyekiti wa ccm huku yeye aendekee kubakia kuwa mwenyekiti wa nccr, hapa ndipo watu wanaona mwenyekiti wa ccm anaimani na mwenyekiti wa upinzani kuliko wanachama wa ccm wenyewe.anayekosolewa anaimani na anayekosoa hapa wananchi wanahofia kuwa huenda mipango hiyo imeanza siku nyingi.kwa kuwa mbatia amezingatia mslahi ya kuingia mbungeni baada ya kushindwa ubunge kwa kura na kwa kesi ni bora achague kuachia ngazi ya uenyekiti taifa ndani ya nccr vinginevyo kafulila mwingine ataibuka kudai kuwa nccr ni ccm -b.hiyo hekima ilitumika na kumusaidia sana mhe haji duni ambaye baada ya kuteuliwa kuwa waziri aliamua kuachia ngazi nafasi ya naibu katibu mkuu na kuepuka mgongano ndani ya cuf ,lakini seif alikiuka kanuni hii na kukumbwa na msukosuko hadi kumega cuf na kuundwa adc.
      Wananchi wa sasa wamezinduka na huwezi kuwalaghai na viongozi tunaweza kujikuta katika matatizo makubwa kama tutaendekeza kutumiwa na ccm huku nchi inaendelea kuliwa na wala rushwa ambao wameanza kukamatwa!!!
      Ingekuwa busara kwa mbatia kumupongeza mhe wenje kwa hoja yake badala ya kumutisha kama wakoloni walivyofanya huko nyuma.
      ni seme kweli kutoka moyoni mwangu kuwa sina imani kama jemusi mbatia anaweza kukaa kikao na wapinzani na mambo yakaenda vizuri"
      dkt paul hennry kyara (mweyekiti taifa sau 0755870601)

    2. Miaka 50

    3. #2
      Tewe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th January 2008
      Posts : 454
      Rep Power : 671
      Likes Received
      64
      Likes Given
      12

      Default Re: Mwenyekiti wa sau amuunga mkono wenje suala la jemus mbatia!!!!!!!!!!

      Yuyu JEMUS MBATIA ni nani?

    4. #3
      Mafuluto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th August 2009
      Posts : 797
      Rep Power : 2973
      Likes Received
      165
      Likes Given
      306

      Default Re: Mwenyekiti wa sau amuunga mkono wenje suala la jemus mbatia!!!!!!!!!!

      ....huyu bwabwa ni kuachana nae tu. Bila shaka kapewa ubunge ili kuendeleza libeneke la ku-camroniana !!

    5. #4
      Comi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2011
      Posts : 963
      Rep Power : 578
      Likes Received
      156
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By Tewe
      Yuyu JEMUS MBATIA ni nani?
      edditing error siyo jemus ila ni james mbatia mwenyekiti wa nccr-mageuzi

    6. #5
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,520
      Rep Power : 19793
      Likes Received
      4317
      Likes Given
      1306

      Default Re: Mwenyekiti wa sau amuunga mkono wenje suala la jemus mbatia!!!!!!!!!!

      Tumpe adhabu ya kumpuuza.

    7. RukaaJuu Final

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...