Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 34 of 34
    1. #1
      mwaJ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2007
      Location : Nowhere
      Posts : 3,458
      Rep Power : 14610
      Likes Received
      2294
      Likes Given
      1505

      Default Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Habari ni ndefu lakini naomba msome mpaka mwisho. Si maneno yangu bali nimeileta kama ilivyo. Ninatumaini watakaoguswa watamsaidia.

      ATHUMANI HAMIS AONGELEA MUSTAKABALIWA MAISHA YAKE NA AOMBA MSAADA


      ATHUMAN HAMIS alikuwa ni mpiga picha katika vyombo vya habari tofauti na alipata ajaliya gari iliyopelekea kushindwa kufanya kufanya kazi na bado anaugua anaishi kwakulala na kukaa kwenye kiti chake maalum sababu anasumbuliwa na Uti wa mgongo(Spinal Cord).
      Attachment 55614

      Mimi Athumani Hamisi Awali yayote, napenda kuwasalimia wote, wakubwa na vijana wenzangu Hii itakuwa mara yapili kuongea nanyi waandishi wenzangu, ndani ya miaka minne tokea nipate ajaliSeptemba 12, 2008 eneo la Kibiti Mkoani Pwani nikiwa na wenzangu Herry Makangeambaye kwa sasa ni marehemu na Anthony Siyame, tukiwa njiani kwenda Kilwamkoani Lindi kikazi. Mara ya kwanza niliongea nanyi 2010 baada ya kurejeakutoka Afrika kusini nilikopelekwa na Serikali kwa matibabu.

      Shukranizangu za awali, zimwendee Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete aliyenitembelea katika Hospitali ya Muhimbili nilikolazwa na kuagizanilipelekwe nje kwa matibabu zaidi. Katika ajali ile, nilivunjika shingo naku-damage spinal cord iliyopelekea kupooza mwili wote kuanzia shingoni. Katikaoperesheni iliyofanywa na madaktari wa hospitali ya Mil Park, Afrika Kusiniwalilazimika kuunganisha shingo kwa nyuma. Shukraniza pili ni kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kampuni ninayofanyia kazi yamagazeti ya serikali, wachapishaji wa Daily News, Sunday news, Habari LeoJumapili na Spoti leo, familia yangu iliyokuwa katika wakati mgumu wakati huohadi sasa watanzania wote wuamini wa dini zote waliokuwa wakiombea Pamoja namarafiki zangu waliokuwa wakihangaika huku na kule kwa namna moja ama nyingine.

      Niko mbeleyenu leo kuwaomba mnifikishie ujumbe kwa jamii kwa maelezo yafuatayo:- Ofisiyangu ya TSN ilinipangia nyumba ninayokaa Sinza Vatican, Wilaya ya Kinondonijijini Dar es salaam Mei 2010-2011 na mkataba ulikukwa kati ya mwenye nyumba naTSN ambao mimi sikuwahi kuuona hadi ninavyoongea na nyie leo. Mkataba uliishatena Mei 2011, mwenye nyumba alikwenda TSN kuomba kusaini mkataba mpya. Badalayake aliandikiwa mkataba mpya wenye jina langu na kupewa aniletee mimi nisaini.Nilipomuuliza mkataba wa kwanza uliingia na nani na ni nani alisaini. Alisemani TSN walisaini wakamwambia wana mgonjwa ambaye ni Staff wake atakuja kuishipale akitokea Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu.

      Mwenye nyumba akasema walimwambia gharama za nyumba ni za TSN, sasa nashangaa leo wameandika jinalako na mkataba ni kati yangu na wewe. Nikamwambia kaka, mimi sikutarajia kufikia hapa kwani mwaka 1999 ilipangwa mimi nifikie katika nyumba ya kampuni Upanga kuepusha gharama na ukaribu wa huduma za kitabibu, mpaka masuala yanguyatakapothibitishwa na Daktrari kama hali yangu itaruhusu mimi kuwezakufanyakazi ama vinginevyo. Rudi ofisini mkasaini kama mlivyofanya awali. Naumwambie kwa hali ya Athumani hawezi kusaini mkataba na mimi kulingana na haliyake. Isitoshe mi nilitiliana saini mkataba wa awali na TSN.
      Ukweli nilikataa kusaini zaidi ya mara tatu, mpaka Meneja Mwajiri siyo huyo wa sasa alipoingilia kati na kunithibitishia kuwa kampuni italipa nyumba mpaka uamuziwa madaktari utakapotoka, saini mimi nitakulinda.

      Niliporejea nyumbani nikawe kwa wino katika dole gumba wakaweka saini. Mpaka yalipojitokeza ya sasa.Ndugu waandishi wa habari, hali yangu japo imeimarika zaidi kuliko awali, leonimekuja na jambo ambalo litahusisha jamii na nyie ndiye wahusika Wakuu katikasuala hili.


      KIKUBWA ZAIDI LEO NI SHUKRANI NAOMBI
      Ukweli ulio wazi, nashukuru kwa Mungu na kujivunia kuwa TSN. Nimelelewa na TSN kwa miaka sita sasa. Imenilea nikiwa mgonjwa kwa miaka mine, nikiwa bado niko ndaniya ajira jambo ambalo ni gumu sana sehemu nyingine. Imelipa nyumba kwa miaka miwili na imesitisha kulipa kodi ya 2012-2013 kwa barua ya Februari 3, 2012 nakutoa maelezo kwenye barua kuwa imefikia hatua hiyo kutokana na kuwapawafanyakazi wake asilimia 15 ya mishahara yao kulipa nyumba. Nyumba walionipangia ni ya vyumba viwili na kodi iliyolipwa kwenye mkataba wa mwaka jana ni Milioni 4.8 Nilipatwa na mshutuko kidogo, nafsi ikanishauri niite menejiment nyumbani tushauriane katika hili.

      Walikuja Machi 28, na wakanipa pole ya kampuni tokea nirudi 2010 Shs 50,000. Lakini mazungumzo hayakuisha kutokana na muda na kuahidi kurudi wiki inayofuata kwa mazungumzo zaidi. Nimepewa notisi na mwenye nyumba April 23, 2010.
      Nadhani kutokana na kubanwa na kazi, hawakupata nafasi ya kurudi tena kumalizia mazungumzo. Kwa mtazamo wa kifikira ni wazi msimamo ulibaki palepale. Barua yakusitisha kulipa kodi haikuja kwangu tu bali pia mwenye nyumba alipata.

      UFAFANUZIKabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani Tanzania, Netcare Rehabilitation Hospital,wanautaratibu mzuri sana. Kabla ya kuwa – discharged wanakuruhusu ukae nje ya hospital kwa miezi mitatu, kama una mke au mume na kama huna utatafutiwa nurse awe wa kike ama wa kiume mimi nilipata nurse. Baada ya hapo una hudhuria mazoezi na vipimo kadhaa kwa miezi mitatu. Ukifaulu kumaliza miezi mitatu wewe na mwangalizi wako hasa wewe mgonjwa bila kupata matatizo, hapo wanaku-discharge.

      Nilipiga simu kwa Katibu Kiongozi Ikulu wakati huo, Philemon Luhanjo na kwaKatibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii anahitajika nurse kuja kukaanami nje ya hospital kwa miezi mitatu, je mtanisaidiaje? Kwa kweli jibu laolilikuwa moja tu hatutatuma nurse kutoka huku, tafuta huko huko, fedha zakumlipa, nyumba ya kulala, chakula na usafiri, andika budget itume harakatutalipa na wasiliana na ubalozi waje kujua unakaa wapi na fedha zitatumwaubalozini watakuwa wanakuletea. Nilipata nurse na miezi mitatu ilipokaribiakwisha nilifanya mawasiliano kujua kama kutatumwa mtu wa kunifuata, wakanijibu njoo naye huyo huyo watanzania waliofanikiwa kuangalia vyombo vya habari wengiwalimuona kwani nilirudi Mei 28, 2010.

      Baada ya mwezi alimaliza mkataba namekutakiwa kutafuta nurse wa kukaa naye kwa saa 24. Akapatikana na akafundishwana M-South Africa jinsi ya kukaa na mgonjwa wa Spinal Cord.
      TSN,wakamlipa nurse wa South Africa Rand 12,500 alizokuwa anadai na palepale nikauliza vipi kuhusu malipo ya nurse mpya ambaye ataachwa na mimi? Kwa sababuserikali imemaliza jukumu lake na waliniambia kwa kuwa wewe bado ni mwajiriwawa TSN, jukumu lote sasa utakuwa chini yao na ndiyo mmepewa pia jukumu lakumlipa kama mlivyofanya leo. TSN walinijibu palepale kuwa suala la kumlipa nurse ni lako na familia yako ila nyumba tutalipa.

      Vodacom walijitokeza kubeba gharama za tiketi nilipopata ajali kwenda Afrika Kusini nawasindikiaji wote, tiketi ya nurse niliyekuja naye. Pia wakalipa tiketi yangu na nurse Desemba 8, 2010 kwenda na kurudi Afrika Kusini kwa ajili ya check up.Baada ya TSN kulipa nurse yule msouth afrika, nikawapigia Vodacom Foundation kuwa nurse amemaliza mkataba na ameshalipwa fedha naomba mumkatie tiketi. Hivyo ilikuwa Juni 25 na kesho yake Juni 26 2010 jioni wakaja watu wawili kutoka Vodacom Foundation na mmoja kutoka TSN waliniambia wamekuja na vitu vitatu. Wakamshukuru nurse kwa kazi nzuri, lakini wakamwambia, sisi ni kutoka Vodacom. Vodacom Foundation inakuomba uendelee kumhudumia Athumani. Na Vodacom watakulipa mshahara lakina tunaomba upunguze kiwango.

      Yule nurse akakubali akapunguza nusu ya mshahara aliokuwa akilipwa na serikali.Wakamwambia sasa Vodacom Foundation inakata tiketi ya kwenda nyumbani Afrikakusini kuaga. Akaomba siku 15, mkataba wa mdomo ukakubaliwa na yule nurse namshahara wa kwanza ukawa Julai 2010 kuendelea na kazi chini ya Vodacom. Julai 2010 wakamlipa. Kilichoendela naomba nisiseme.

      Muda wacheckup ulifika Desemba 2010, nikaitaarifu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Wakakubali wakaandika barua kwa kugawa majukumu. Afya wakasema watalipa gharamaza matibabu, Vodacom tiketi za kwenda na kurudi na TSN waliagizwa kulipa allowance kwa mgonjwa na nurse. Tukasafiri Desemba 8,2010 na tukarudi Februari28,2011. Malipo yaliyofanywa na TSN kidogo ni aibu naomba nisiseme. Hali hiyo ilinionyesha kuwa Vodacom Foundation walikuwa wanatambua uwepo wa yule nurse. Lakini hadi nurse anaondoka alilipwa mshahara mmoja tu na hata tiketi ya nurse kurudi Afrika Kusini Vodacom hawakulipa.

      Nililipa tiketi ya Business Class.Nikampa Rand 4,500 akakataa akachukua Rand 2,500 tu, akaniambia, Athumani nakuacha katika hali mbaya sana. Fuatilia haki zangu na zako, ukifanikiwa utaniambia na Account ya benki, First bank nakuachia utaniwekea.
      Vodacom Foundation hawajawahi kupokea simu yangu na Mkurugenzi wake hajawahi kupokea simu yangu wala kuongea na mimi tokea nipate ajali.

      Suala lingine waliniuliza nichague kitu kimoja, kujengewa nyumba au kusomeshewa watoto. Mimi nilichaguakujengewa nyumba. Walichukua chaguo langu. Tukamaliza mazungumzo. Baada yamwezi waliniambia suala lako limekubaliwa ila tumepata Mkurugenzi mpya, lakini usijali. Mpaka hapa ninavyoongea danadana ziliendelea mpaka ninavyoendelea kwenye nyumba, sijawahi tena kupata jibu kutoka Vodacom.
      La mwisho nilijibiwa na mmoja wa watu wa Vodacom Foundation aliniambia wewe uliingia mkataba na kampuni ya One Plass na si Vodacom Foundation.

      SIKU YA LEO Nimekujaleo kuutangazia umma hali ilivyo. Ukweli kwa sasa Account ya CRDB ilikuwamaalumu kwa ajili ya kusomeshea watoto, imekauka ya Postal bank ambayo yamshahara haina kitu. Pesa ya mshahara inayoingia benki ni 450,000 Nawalipanurse, msaidizi wake na mfanyakazi 370,000.
      Maisha yaulemavu ni ghali sikutarajia. Nina wanangu watatu, wa kwanza anamaliza darasala saba mwaka huu, wa pili yuko la nne na wa mwisho yuko la pili. Hawa wanasomaprimary za kulipia wote hawa nawalipia 200,000 kila mmoja kwa term jumla400,000 hizo shule zina term nne kwa mwaka. Gharama chakula, vifaa vyawanafunzi, gharama zao ndogondogo na za kifamilia Pamoja na chakula kwa mwezi,inakwenda kati ya 750,000 mpaka 900,000 kwa mwezi.

      Nimekuwa ombaomba mpaka watu kadhaa siwalaumu, wamechoka hawapokei simu wala kujibu sms.siyo siri ndugu wote wamekimbia waliobaki ni marafiki wa kweli wameniingiza katika familia zao. Hali yangu ni mbaya sana kiuchumi. Sina uwezo wa kulipa nyumba kwa gharama zozote zile. Mimi Athumani Hamisi, naomba watanzania watakaoguswa wanisaidie. Kubwa nyumba na ushauri wa madaktari walinishauri nisiishi mbali na mazingira ya hospitali kulingana na hali yangu. Makampuni, mashirika, wizara yoyote, shirikala nyumba la Taifa NHC, watu binafsi, serikali na Taasisi yoyote watakaoguswa na kilio changu nawaomba wanisaidie kwa njia yoyote. kwa waliotayari naomba misaada ipitie katika account No 01J2027048800 ya CRDB na Account No 010-00090488 ya Postal Bank Kwa wanaotumia mitandao ya simu, wanaweza kutumia M-pesa 0757 825 737, Tigopesa 0655 531 188 na Airtel Money 0784 531118; M-Pesa 0767 298 888 ya Chris Mahundi na Airtel Money 0686 710 977 ya Ephraim Mafuru.

      Habari kwahisani ya http://www.8020fashions.blogspot.com/
      Last edited by mwaJ; 6th June 2012 at 13:20.
      Azimio Jipya likes this.
      “Anyone who has never made a mistake has never tried anything new” -
      Albert Einstein

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      BabaDesi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2007
      Posts : 2,382
      Rep Power : 1085
      Likes Received
      251
      Likes Given
      1400

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      ...Aliporudi kutoka kwenye matibabu SAfrika walimpa jina la 'Mpiganaji' na kila mtu/taasisi mwenye jina mjini alijibainisha naye na kutoa ahadi kem kem. Miaka mitatu tu baadae wameishamsahau na kumuona sio Habari tena hadi yeye mawenyewe ameamua kuwa Habari ili kupata msaada. Pole Ndugu yetu Athumani Hamisi. Ndio binadamu walivyo. Mungu atakupitisha katika wakati huu mgumu unaopita. Nashauri pia uusome kwa makini Ujumbe muhimu wa muungwana Mtambuzi na ujaribu kuufanyia kazi. Utakusaidia. Pole Sana ndugu Yetu. Yote yatoka kwa Mungu.
      Sema Kwa Sauti, Mimi Ni Mweusi Na Najivunia Kuwa Hivyo!

    4. #22
      mwaJ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2007
      Location : Nowhere
      Posts : 3,458
      Rep Power : 14610
      Likes Received
      2294
      Likes Given
      1505

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Quote By Mtambuzi
      Ndio nimeiona hii habari, naninakumbuka kwa usahihi kabisa juu ya ajali hiyo iliyompata mwenzetu.
      Mimi sipendi unafiki, ninachoweza kumshauri ndugu yangu huyu ni kujaribu kupunguza bajeti yake......... ingawa wazo hili limechelewa, lakini hata hivyo anaweza kuangalia bajeti yake na kuipunguza.
      Kitu cha kwanza ilitakiwa atafute nyumba za bei rahisi kidogo, Kukaa sinza kuna gharama kubwa sana, kwa mfano angeweza kuhamia Mwananyamala karibu na hospitali kwani pale anaweza kupata nyumba nzuri kwa bei nafuu kidogo, pili gharama za shule za watoto nazo zinamkamua sana, najua alikuwa na lengo la kuwasomesha wanae shule nzuri za English Medium, lakini kwa hali yake kwa sasa inabidi ageukie shule za akina Kayumba...... (najua utakuwa ni uamuzi mgumu),
      tatu, ajishughulishe na shughuli za kiuchumi, kuna namna nyingi za kujiongezea kipato, kwa mfano kwa kuwa taaluma yake ni mpiga pisha wa magazeti, basi angejifunza uandishi wa makala hata kwa njia ya mtandao na angekuwa anafanya kazi akiwa nyumbani....
      kingine labda angetafuta ujuzi wowote wa kazi za mikono, sidhani kama angetangaza kupitia vyombo vya habari kwamba anatafuta mwalimu wa kumfundisha kazi za mikono angekosa.... Naamini angepata na hata gharama za kumlipa wangejitokeza wafadhili....... Kutegemea wafadhili kwa misaada ya kila siku huku ukiwa na maisha ghali ni shida kidogo.....
      Naamini kamaatafuata ushauri wangu anaweza kuvuka mtihani huu mgumu.....
      Nakumbuka wakati fualni niliwahi kuandika makala kuhusu tajiri mmoja wa kule Colorado nchini Marekani, yeye alimudu kusimama na kuwa tajiri mkubwa nchini humo pamoja na misukosuko ajali alizowahi kupana na kuwa mlemavu kama alivyo Athumani.

      Ukitaka kusoma habari hiyo unaweza kubofya hapa:

      http://www.jamiiforums.com/jf-chit-c...ya-maisha.html
      Asante sana Mtambuzi nimeupenda ushauri wako, kuukwepa unafiki kunaweza kusaidia kupata ufumbuzi kwa urahisi zaidi. Natumaini hapa JF kuna watu wanaomfahamu kwa ukaribu na wanaweza kumpa ushauri ulioutoa.
      “Anyone who has never made a mistake has never tried anything new” -
      Albert Einstein

    5. #23
      Azimio Jipya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Location : Universal Space Station
      Posts : 3,282
      Rep Power : 5415
      Likes Received
      1006
      Likes Given
      1731

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Quote By mwaJ
      ... Watu wanaweza kuchangia pesa na hizo pesa badala ya kuzitumia zote ashauriwe namna ya kuzifanyia mradi ambapo pia atashauriwa namna ya kupata wasimamizi wa huo mradi maana yeye katika hali yake hataweza kusimamia na mawazo mengine ya kumsaidia ili mradi aondokane na huu utegemezi mkubwa aliyotumbukia baada ya ajali.
      mwaJ Ushauri huu nimeupenda sana! Uko very practice na unapungaza utegemezi! I hope atawezeshwa na wanahabari wenzake kupta michango hii inayotolewa hapa ya kiushauri na kumpa moyo! Ona mawazo yako yakiunganishwa na ya Mtambuzi hasa point no Nne na Tano yatakavyokuwa very enlightening!

      Quote By Mtambuzi
      Kitu cha kwanza ilitakiwa atafute nyumba za bei rahisi kidogo, Kukaa sinza kuna gharama kubwa sana, kwa mfano angeweza kuhamia Mwananyamala karibu na hospitali kwani pale anaweza kupata nyumba nzuri kwa bei nafuu kidogo,

      Pili gharama za shule za watoto nazo zinamkamua sana, najua alikuwa na lengo la kuwasomesha wanae shule nzuri za English Medium, lakini kwa hali yake kwa sasa inabidi ageukie shule za akina Kayumba...... (najua utakuwa ni uamuzi mgumu),

      Tatu, ajishughulishe na shughuli za kiuchumi, kuna namna nyingi za kujiongezea kipato, kwa mfano kwa kuwa taaluma yake ni mpiga pisha wa magazeti, basi angejifunza uandishi wa makala hata kwa njia ya mtandao na angekuwa anafanya kazi akiwa nyumbani....

      Nne, kingine labda angetafuta ujuzi wowote wa kazi za mikono, sidhani kama angetangaza kupitia vyombo vya habari kwamba anatafuta mwalimu wa kumfundisha kazi za mikono angekosa.... Naamini angepata na hata gharama za kumlipa wangejitokeza wafadhili.......

      Tano Nakumbuka wakati fualni niliwahi kuandika makala kuhusu tajiri mmoja wa kule Colorado nchini Marekani, yeye alimudu kusimama na kuwa tajiri mkubwa nchini humo pamoja na misukosuko ajali alizowahi kupana na kuwa mlemavu kama alivyo Athumani. Ukitaka kusoma habari hiyo unaweza kubofya hapa:

      http://www.jamiiforums.com/jf-chit-c...ya-maisha.html
      Ushauri huu pamoja na Kuchangiwa na marafiki na ndugu amabako hakutadumu, utakuwa wa manufaa na wa dhati!

      Lets hope ushauri ataupata!
      Never Get Angry; Never Make Threat; Reason With People;
      "Napenda the logic of the words because in some ways it says about individual-not to use emotions-when scrutinizing something, whether it involves you or not" ...-by AshaDiii @ Jamiiforums 26th July 2011.


    6. #24
      mwaJ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2007
      Location : Nowhere
      Posts : 3,458
      Rep Power : 14610
      Likes Received
      2294
      Likes Given
      1505

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Quote By Mwali
      Sorry mpenzi, mi nipo ila naona mada imekaa ndefu sana
      Mi sipendi kusoma, hua nasinzia katikati, kabla sijamaliza
      Tafadhali nipe summary kwanza, kwa kifupi what is the issue?
      Acha uvivu Mwali somo tu, mie naona ngumu kutengeneza summary bana. Lakini shosti mbona kule MMU unajibu vikomenti hata mia hausinzii?
      Mwali likes this.
      “Anyone who has never made a mistake has never tried anything new” -
      Albert Einstein

    7. #25
      Mwali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2011
      Location : Ushongo Mabaoni
      Posts : 5,893
      Rep Power : 26887
      Likes Received
      4390
      Likes Given
      4662

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Quote By mwaJ
      Acha uvivu Mwali somo tu, mie naona ngumu kutengeneza summary bana. Lakini shosti mbona kule MMU unajibu vikomenti hata mia hausinzii?
      Nasoma vipost vifupi vifupi kule, sio kama hii.
      We hujanistukia tu, mwenzio ni chit chat zaidi
      Haya ya kufikiria sana naona niwaachie nyinyi
      But kwa vile umeniomba wewe ngoja nisome...
      mwaJ, Azimio Jipya and sweetlady like this.
      Creativity is the sudden cessation of stupidity.
      Edwin H. Land

    8. Miaka 50

    9. #26
      Mwali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2011
      Location : Ushongo Mabaoni
      Posts : 5,893
      Rep Power : 26887
      Likes Received
      4390
      Likes Given
      4662

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      mwaJ, Nimesoma thread mwanzo hadi mwisho
      Ila niseme tu ukweli si rahisi kuisoma yote

      Mchango wangu huu hapa (for what its worth):
      1. Aandike (aandikiwe) thread fupi zaidi watu waweze kusoma (I did this)
      2. Aipost jukwaa la sheria, na iwe intended for lawyers and legal advisers
      3. Aweke wazi matatizo yake, na aweke wazi anacho hitaji toka kwa viewers
      4. Binafsi sidhani kama anahitaji msaada wa kifedha ila ni legal advice zaidi


      Kwa kurahisisha usomaji na mchango nadhani ni bora tungeweka
      post kama hii jukwaa la sheria: kama ni sawa just copy-past it
      Kumbuka kuwaambia mods wasiunganishe hizi threads mbili
      ili misaada ya kisheria kwa ndugu Athumani ipatikane kirahisi:

      JF members, kuna thread nimesoma jukwaa la Habari na hoja mchanganyiko, nimeona nii lete huku:

      Kuna ndugu yetu anaitwa Athumani Hamisi. Sasa ni miaka minne tokea apate ajali, Septemba 12, 2008 eneo la Kibiti Mkoani Pwani akiwa na wenzanke, wakiwa njiani kwenda kazini Kilwa mkoani Lindi kikazi.Katika ajali ile, alivunjika shingo naku-damage spinal cord iliyopelekea kupooza mwili wote kuanzia shingoni. Ailipata msaada wa moja kwa moja toka Ikulu (Mhe Jakaya Kikwete), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kampuni alio kua akifanyia kazi yamagazeti ya serikali (TSN).

      Sasa tatizo lake kubwa ni kukabiliana na gharama za maisha zinazo sababishwa kwa kiasi kikubwa na ulemavu alo upata baada ya ajali ya kikazi. anahitaji pesa ya matibabu, pesa ya kuwalipa wahudumu, pesa ya kuwasomesha wanae watatu na pesa ya matumizi mbali mbali ya nyumbani, sikiongozwa na gharama za kodi ya nyumba pamoja na chakula mbazo kazikadiria kufika laki tisa kwa mwezi (900,00 Tsh)

      Kwa bahati mbaya, leo miaka minne baada ya kupata ajali hiyo inaonekana TSN na wafadhili wengine wameanza kuonesha dalili ya kugeuka wajibu wao wa kumsaidia mfanya kazi wao huyu, alie jeruhiwa katika safari ya kikazi. Nadhani hali hii inarahisishwa na kutokuwepo kwa makubaliano ya msingi (na yakuandikwa) kati ya Ndugu Athumani na tajiri wake (TSN). Leo amekua omba omba na msaada ulokua ukitoka kwa urahisi na kwa kufunika mahitaji ya mwaka au zaidi sasa unatoka kwa tabu, na unakuja kufunika mahitaji ya wiki kadhaa tu.

      Msaada anao hitaji ni wa kisheria (for a sustainable life, in the long term), na wa kifedha (to implement the legal advices and to cope with the daily expenses as he works on the long term plan)
      Msaada wa kisheria unao hitajika:

      1. Ufafanuzi wa haki zake kama mfanya kazi alie pata ajali akiwa kazini
      2. Ufafanuzi wa uwajibikaji wa TSN kama tajiri wake (ukizingatia walianza kulipia huduma na sasa wanaacha)
      3. Hatua za kuchukua ili haki na uwajibikaji vizingatiwe kwenda mbele
      4. Ufafanuzi wa compensation scheme inayo weza kutumika hapa (monthly allowances au one off package)
      5. Msaada wa kisheria (free of charge or at very accessible cost given the situation)
      6. Msaada wa kimawazo au kifedha toka kwa msomaji wowote atakae guswa na habari hii.


      Kwa walio tayari kuchangia kimawazo/kisheria, tafadhali weka mawazo yako kwenye thread hii au tembelea http://www.8020fashions.blogspot.com/

      kwa walio tayari kuchangia kifedha, misaada ipitie katika

      • account No 01J2027048800 ya CRDB na
      • Account No 010-00090488 ya Postal Bank


      ​Kwa wanaotumia mitandao ya simu, wanaweza kutumia

      • M-pesa 0757 825 737,
      • Tigopesa 0655 531 188 na
      • Airtel Money 0784 531118;
      • M-Pesa 0767 298 888 ya Chris Mahundi na
      • Airtel Money 0686 710 977 ya Ephraim Mafuru.


      Asanteni kwa michango.
      Creativity is the sudden cessation of stupidity.
      Edwin H. Land

    10. #27
      mwaJ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2007
      Location : Nowhere
      Posts : 3,458
      Rep Power : 14610
      Likes Received
      2294
      Likes Given
      1505

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Quote By Mwali
      Nasoma vipost vifupi vifupi kule, sio kama hii.
      We hujanistukia tu, mwenzio ni chit chat zaidi
      Haya ya kufikiria sana naona niwaachie nyinyi
      But kwa vile umeniomba wewe ngoja nisome...
      Mwali nimekupendajeeee? Yaani wewe ni zaidi ya "mwali"! Nadhani umenipata.
      Asante sana pia kwa kutengeneza summary. Ngoja niipost jukwaa la sheria kama ulivyoshauri.
      Azimio Jipya and Mwali like this.
      “Anyone who has never made a mistake has never tried anything new” -
      Albert Einstein

    11. #28
      Mwali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2011
      Location : Ushongo Mabaoni
      Posts : 5,893
      Rep Power : 26887
      Likes Received
      4390
      Likes Given
      4662

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Quote By mwaJ
      Mwali nimekupendajeeee? Yaani wewe ni zaidi ya "mwali"! Nadhani umenipata.
      Asante sana pia kwa kutengeneza summary. Ngoja niipost jukwaa la sheria kama ulivyoshauri.
      Pamoja sana (source: AshaDii )
      mwaJ and Azimio Jipya like this.
      Creativity is the sudden cessation of stupidity.
      Edwin H. Land

    12. #29
      sweetlady's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 24th December 2010
      Location : Tanzania
      Posts : 15,335
      Rep Power : 36534
      Likes Received
      7486
      Likes Given
      4604

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Quote By mwaJ
      Azimio Jipya ukiliangalia hili suala kisheria utajiuliza maswali mengi sana kuanzia kwenye malipo ya bima - ajali iliyosababisha kupoteza uwezo wa kufanya kazi, suala la kuumia kazini, je? bado yupo kwenye ajira ya TSN? Kama jibu ni ndio je, mwajiri wake anajukumu gani katika kumhudumia mfanyakazi wa aina yake in terms of accommodation (kumbuka amezungumzia nyumba za staff) n.k.

      Njia za kumsaidia zaweza kuwa pamoja na hiyo aliyoomba mwenyewe yaani kumchangia pesa. Lakini hii kwa maoni yangu haitakuwa endelevu maana watu hawataweza kuchangia kila mara anapopungukiwa na ndio maana amesema baadhi ya watu aliowategemea wamechoka na hawapokei hata simu zake.

      Lengo la kuileta hii habari JF ni kupata michango ya wana JF ya hali, mali na mawazo pia namna huyu ndugu atakavyoweza kutoka katika hali aliyomo. Watu wanaweza kuchangia pesa na hizo pesa badala ya kuzitumia zote ashauriwe namna ya kuzifanyia mradi ambapo pia atashauriwa namna ya kupata wasimamizi wa huo mradi maana yeye katika hali yake hataweza kusimamia na mawazo mengine ya kumsaidia ili mradi aondokane na huu utegemezi mkubwa aliyotumbukia baada ya ajali.

      Najaribu tu kufikiria wako wapi wadada na akina kaka wa JF akina Bishanga Saint Ivuga Bujibuji Mtambuzi Pasco Senetor Mwali Preta sweetlady Kipipi kisukari Smile Michelle charminglady BADILI TABIA na wengineo waje wasaidie mawazo yao katika hili.
      mwaJ mpendwa nimeshindwa kumalizia kusoma habari......ni ndefu ntarudi baadae kusoma then ntachangia kile ntakachoelewa!
      Life without problems never make a strong and good person!

    13. #30
      Mama Mdogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st November 2007
      Posts : 1,361
      Rep Power : 860
      Likes Received
      685
      Likes Given
      73

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Nimesoma taarifa kwenye issamichuzi blogspot na kuona mwajiri wa Athumani (TSN) anatoa ufafanuzi na kuonyesha kuwa hawajamtelekeza Athumani, na wametumia fedha nyingi mpaka sasa na wanaendelea kumhudumia. Sasa sielewi nani ni mkweli Athumani au TSN. Ukisha soma mada katika post hii hapa JF ebu rejea link ifuatayo nawe ujisomee uone zipi mbivu na zipi mbichi.


      MICHUZI: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: TSN HAIJAMTELEKEZA ATHUMANI HAMISI
      mwaJ likes this.
      Anyone who has never made a mistake has never tried anything new - Albert Einstein
      No problem can be solved from the same level of consciousness that created it
      - Albert Einstein


    14. #31
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 589
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Inahuzunisha mno!

    15. #32
      trachomatis's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2011
      Location : Dar es Salaam,Tanzania.
      Posts : 3,460
      Rep Power : 1095
      Likes Received
      484
      Likes Given
      235

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Pole sana mkuu Athuman Hamisi... Tunazikumbuka picha zako baadhi yetu..!

    16. #33
      trachomatis's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2011
      Location : Dar es Salaam,Tanzania.
      Posts : 3,460
      Rep Power : 1095
      Likes Received
      484
      Likes Given
      235

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      Kuna wanaoshauri apunguze gharama za maisha yake.. Kwenye nyumba itashindikana maana anatakiwa kukaa karibu na hospitali...
      Labda kwa gharama za house girl,nurse,na gharama za ada za watoto wake maana wanasoma English Medium schools.. Haya anaweza kushauriwa cha kufanya kwayo..

      Once again.. Pole sana Athuman Hamisi

    17. #34
      pono's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2012
      Posts : 563
      Rep Power : 464
      Likes Received
      75
      Likes Given
      261

      Default Re: Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athuman Hamis kisha Chukua Hatua Kumsaidia

      hakuwa upande wa mafisadi ndio maana,angekuwa upande wao hangepata shida hivi

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...