Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 39
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,275
      Rep Power : 3570
      Likes Received
      3075
      Likes Given
      464

      Default Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Tuesday, 29 May 2012 21:17

      Joseph Zablon

      WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ameanza kutekeleza kwa vitendo kauli yake ya kuisafisha Idara ya Wanyamapori baada ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne na askari 28 wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mara ili kupisha uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa faru wawili na kung’olewa pembe.

      Faru hao ni miongoni mwa watano ambao Rais Jakaya Kikwete aliwapokea wakitokea Afrika Kusini, Mei 21, 2010 lakini Desemba 21, mwaka huo faru dume aitwaye george aliuawa na pembe zake zilinaswa Mwanza. Faru wengine wanne walipewa majina ya cleo, ethna, lunnar na dume pekee aliyebaki, benj.

      Wakati akipokea faru hao waliogharimu Sh7.5 bilioni kuanzia ununuzi hadi kuwasafirisha hadi nchini, Rais Kikwete alisema: “Afrika Kusini imeongeza uwezo kwa Tanzania kwa kuleta faru hao weusi na ongezeko hilo ni la manufaa kwa taifa. Hivyo, tutaimarisha huduma zao na ulinzi utakuwa wa kipekee zaidi yangu mimi.”

      Lakini tofauti na ulinzi huo alioahidi Rais, kumekuwa na taarifa za kuawa kwa faru wengine wawili hivi karibuni na mamlaka husika zikaficha tukio hilo hadi liliporipotiwa na vyombo vya habari. Takwimu zinaonyesha tangu mwishoni mwa 2009 hadi Desemba 2010, faru 15 wamekwishauawa.

      Balozi Kagasheki alisema jana kwamba amechukua hatua hiyo kutokana na wakurugenzi hao kukaa kimya baada ya tukio hilo na askari hao wakidaiwa kukiuka mkataba wao wa ajira ambao unawataka watoe ulinzi kwa wanyamapori.

      “Mkataba wao upo wazi kuwa wanapaswa kuwalinda wanyamapori hao na lolote linalowapata liwapate na wao pia, lakini wanyama wameuawa mwezi mzima umepita na wiki mbili baadaye gazeti linaandika ndipo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), wanachukua hatua,” alisema.

      Waziri Kagasheki pia alisema wahusika hao wameundiwa tume huru ambayo itafanya kazi ndani ya siku 60 na watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine, watachukuliwa hatua zaidi za kisheria na wale ambao watathibitika kuwa hawahusiki taratibu nyingine zitafuatwa.

      Aliwataja wakurugenzi ambao wamesimamisha kazi kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi, Justine Hando, Mkurugenzi wa Intelejensia katika Wizara hiyo, Emmly Kisamo, Mkurugenzi wa Hifadhi ya Serengeti, Mtango Mtahiko na Mkurugenzi Mratibu wa Mradi wa faru, Mafuru Nyamalumbati.

      Alisema anachukua hatua hizo ambazo ni tofauti na utaratibu wa kawaida kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ovyo ambavyo vinaichafua wizara yake.

      “Kwanza niliwauliza baada ya kupatikana kwa habari za kuuawa kwa faru hao walichukua hatua gani? Jibu likawa tumewapa siku 14 wajieleze,” alisema Kagasheki na kuongeza kuwa watendaji hao wakamwambia kuwa maelezo hayo yasiporidhisha hatua itakayofuata ni kuundwa tume.

      Kagasheki alifafanua kwamba alipohoji muda wa utendaji wa tume hiyo, aliambiwa ni siku 60 jambo ambalo alilikataa na kuchukua uamuzi wa kuwasimamisha ili kupisha uchunguzi huo na kudai kuwa watendaji hao kama wangeachwa wangeweza kuwa na athari zaidi kwa hifadhi na wanyamapori.

      Alisema wizara yake haiwezi kufanya kazi kwa woga na kusema yupo vitani akiahidi kupambana kuondoa uozo unaodaiwa kuigubika.

      Alisema anajua kuwa kuna mtandao wa ujangili ndani na nje ya nchi ambao una fedha nyingi lakini akasema hatarudi nyuma... “Faru ni moja kati ya viumbe hai ambavyo vipo hatarini kutoweka hivyo kilichotokea hakivumiliki.”

      Alisema kuwa mara baada ya kuandikwa kwa habari hizo, walikwenda hadi eneo la tukio na kukuta miili ya wanyama hao wakiwa wameondolewa pembe zao na jirani kukiwa na maganda ya risasi... “Tumewakuta mama na mwanaye wameuawa na pembe zao kuondolewa. Inasikitisha sana.”

      Mei 21 akizungumza Dar es Salaam katika uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Balozi Kagasheki alionya kwamba angeifumua Idara hiyo ya Wanyamapori huku akipiga marufuku usafirishaji wanyama hai nje ya nchi.

      Alisema kama idara hiyo itasimamiwa vizuri kukusanya mapato, inaweza kusaidia kupunguza matatizo ya wananchi.

    2. RukaaJuu Final

    3. #2
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,275
      Rep Power : 3570
      Likes Received
      3075
      Likes Given
      464

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Kagasheki ni Mchapa Kazi, Wakati akiwa Naibu Mambo ya Ndani na Waziri ni Lau; yeye ndiye aliyekuwa anafanya kazi zote

      Lau ni Makelele na kupenda kupigiwa Saluti

    4. #3
      Sniper's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2008
      Posts : 1,339
      Rep Power : 840
      Likes Received
      398
      Likes Given
      429

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Huko TANAPA kumeoza, kuna watu wanajionaga ni ma mungu mtu huko
      NYENJENKURU likes this.
      Kama kuoga ni usafi kwanini taulo linachafuka?

    5. #4
      Mkubwa ndevu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2011
      Posts : 357
      Rep Power : 490
      Likes Received
      35
      Likes Given
      0

      Default

      Comment removed by mods

    6. #5
      Kigogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 8,201
      Rep Power : 2096
      Likes Received
      1234
      Likes Given
      313

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      sina imani sana na Kagasheki.....ni upepo tu unapita ...
      August and Ndahani like this.
      ______________________________ _
      Niko tayari kufa huku nimesimama kuliko kuishi huku nimepiga magoti....

    7. Miaka 50

    8. #6
      Maarko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 490
      Rep Power : 509
      Likes Received
      82
      Likes Given
      29

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Tatizo la maliasili ni kupeana kazi kwa kufahamiana waajiriwa huku ni ndugu/marafiki wa viongozi wakubwa serikali ambao hawana weledi.Lazima muheshimiwa Kagasheki ajue vita alivyovianzisha ni vikubwa maadui wengi wapo humohmo serikali na ni viongozi wenzake wakubwa.

    9. #7
      KISAKA MORIS's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Posts : 367
      Rep Power : 430
      Likes Received
      30
      Likes Given
      42

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Mwache awang'oe maana hata yeye hatasalia maana muda si mrefu ataanza kuzitafuna.

    10. #8
      Baba Wilbur's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 6th June 2011
      Posts : 7
      Rep Power : 404
      Likes Received
      4
      Likes Given
      1

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Quote By Sniper
      Huko TANAPA kumeoza, kuna watu wanajionaga ni ma mungu mtu huko
      xxxxxxxxxxxxxx
      Last edited by Baba Wilbur; 30th May 2012 at 10:28.
      Edson likes this.

    11. #9
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,489
      Rep Power : 6171
      Likes Received
      3059
      Likes Given
      1020

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Quote By Baba Wilbur
      Maamuzi ya kukurupuka wakati mwingine si Mazuri. Protection ya faru ni vita na watu wameweka maisha yao rehani. Katika vita sio always unashinda tu, kwani maadui nao kila siku wanakua na mbinu mpya na silaha bora. Kuzidiwa na adui katika vita ni jambo la kawaida (Wanajeshi wanajua). Kwa watu walioko katika mapambano pale wanapozidiwa na adui basi hawana budi ku retreat na kujipanga upya then wanaendelea na vita.

      Kilichotokea Serengeti tuchukulie ni kuzidiwa na maadui (ingawa pia uwezekano wa kuhusika kwa mtu wa ndani upo). Mheshimiwa aliyechukua hatua hiyo angeliangalia swala hili kwa mapana zaidi. Ujangili (poaching) kwa sasa ni mkubwa sana nchini Tanzania. wanyama wanaoathirika zaidi ni Tembo hususan wale walioko katika maeneo ya wazi na mapori ya akiba (game reserves). Kinachotakiwa ni Wizara husika kuchukua hatua za kitaifa za muda mrefu kupambana na tatizo hili.

      Kazi inayofanywa na askari wanaolinda faru ni ngumu sana tofauti na wengi wanavyoitazama. askari hawa kwanza hawaishi na familia zao, wanakaa porini muda wao wote wa kazi wakihama hama kulingana na movement ya wanyama hawa. wao ni silaha begani, hema mgongoni, jua lao mvua yao, hatari zote za wanyama wakali pamoja na nyoka na wadudu! ndio maisha yao. Inapotokea wanazidiwa nguvu na majangili tusikurupuke na kuanza kuwaita majina ya kila aina na kuwachafua.....wanahitaji moral support kutoka kwa viongozi wao na wananchi wote kwa ujumla. Badala ya kuwasimamisha kazi na kuanza kuwachafua kwenye vyombo vya habari, busara ingetumiaka, uchunguzi ufanyike ndo taarifa kama hizo zitolewe. Maamuzi katika maeneo sensitive kama uhifadhi wa faru yasiwe na msukumo wa kisiasa bali utaalam....Ni kweli tunahitaji kusafisha wizara ila pia tuangalie tunasafisha nini na tunasafisha wapi. Sidhani kama madudu na uchafu ulioainishwa na taarifa ya CAG pamoja na ile ya kamati ya bunge ni askari kuzidiwa nguvu na mbinu
      Mkuu Waziri amewasimamisha ili uchunguzi ufanyike siyo kwamba amewafuta kazi.

      Lakini pia suala la kushindwa kwenye medani na ku retreat kidogo hapo hauko sawa. Una retreat baada ya kupambana na katika mapambano kuna ushahidi wa kupoteza risasi na maisha siyo una retreat tu basi tunaamini kwamba umezidiwa nguvu. Ingekuwa hivyo wanajeshi wasingekuwa wanaenda mstari wa mbele.

      Hao wa Serengeti ni wapi wameonyesha kwamba walipambana na hao majangili na kuzidiwa nguvu. Najua unataka kusema kwamba majangili wana uwezo wa kuingia bila kuonekana na kuua hao wanyama. Lakini pia hii inatia shaka tena inatia aibu kwa kuwa mimi binafsi nilimsikia Rais akisema wale Faru waliotoka RSA watapewa ulinzi kuzidi hata ulinzi anaopewa yeye! Wanapouwawa na majangiri bila hao majangiri kukamatwa inatoa ujumbe gani?
      NYENJENKURU likes this.
      CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola.

    12. #10
      Ndekirhepva's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th May 2012
      Location : Lubumbash
      Posts : 304
      Rep Power : 414
      Likes Received
      27
      Likes Given
      77

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      mimi huyu waziri sina imani na mchakato alioanza kuuchukua kwa vile, kama ilivyo desturi, kamati itaundwa na itafanya uchunguzi na majibu yatapatikana, sema sasa issue inakuja nani wakumfunga paka kengele??????
      tuliona akina ngeleja, ngeleja hakuanza kupingwa kwenye hili bunge la juzi, alipingwa tokea bunge la february, lakini kwa shinikizo ndio bosi wake amempumzisha ila jamaa anaendelea kula bata mtaani, so mi naona ni mbwembwe tu, kwani Kagasheki hajui kwamba huo mradi ni wawatu wakubwa????
      JK atakua anahusika sana tu,haiwezekani faru wameuawa alafu hakuna taarifa iliyowafikia watu

    13. #11
      Kibanga Ampiga Mkoloni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th August 2007
      Location : Here! here!
      Posts : 4,800
      Rep Power : 1636
      Likes Received
      1195
      Likes Given
      1702

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Quote By nngu007
      Kagasheki ni Mchapa Kazi, Wakati akiwa Naibu Mambo ya Ndani na Waziri ni Lau; yeye ndiye aliyekuwa anafanya kazi zote

      Lau ni Makelele na kupenda kupigiwa Saluti
      Mzushi tu huyu nakumbuka alienda kule MGODINI akakuta maji yenye sumu na ALILIA KUPITA PINDA, Lakini wapi hakuna alichofanya.
      For the Holy Quran says in Sura 42, verse 41: 'All those who fight when oppressed incur no guilt, but Allah shall punish the oppressor, Come the day.

    14. #12
      King Kong III's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Enaboishu-Umenyeni
      Posts : 11,929
      Rep Power : 5064
      Likes Received
      3203
      Likes Given
      2661

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      TANAPA ni majangiri yani sawa na fisi kumkabidhi bucha.
      Kimbunga likes this.

    15. #13
      Maundumula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 5,050
      Rep Power : 3122
      Likes Received
      1376
      Likes Given
      5834

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Hii inasikitisha sana, juzi juzi tulisikia mtu wa usalama na mtu wa serikali wamekamatwa wakinyemelea nyara za serikali. Hatujakaa vizuri faru wa JK nao wameuwawa wote na sisi hatujapata taarifa.

      Kumbe walikuwa wanasubiri JK aondoke eneo la tukio na ulinzi ukome hapo hapo! kweli hii nchi ni ya vilaza wa hali ya juu. Angalau kutupa information ya yaliyotokea hamna!. Sasa watatu convince vipi kama wao hawahusiki na mtandao huu wa ujangili hao vigogo wa TANAPA ? Si nilisikia hawa FARU waliwekewa vifaa maalum vya ku monitor popote pale walipo wanajulikana? kwanini wahusika hao wa usalama wa wanyama pori hawakuwa wanafuatilia nyendo zao? Sasa itabidi tutote tena another 7.5 Billion tununue FARU wengine kutoka SA!!!!
      Kimbunga and omujubi like this.

    16. #14
      omujubi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th December 2011
      Location : Bumbire Island
      Posts : 1,628
      Rep Power : 702
      Likes Received
      669
      Likes Given
      1686

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Quote By Maarko
      Tatizo la maliasili ni kupeana kazi kwa kufahamiana waajiriwa huku ni ndugu/marafiki wa viongozi wakubwa serikali ambao hawana weledi.Lazima muheshimiwa Kagasheki ajue vita alivyovianzisha ni vikubwa maadui wengi wapo humohmo serikali na ni viongozi wenzake wakubwa.
      kwenye red hapo ndilo tatizo la Watanzania sote, ni wachache kati yetu wanaoelewa madhara ya uharibifu wa urithi tulionao. Wenzetu Kenya wana matatizo kama haya lakini uelewa wa wananchi wa kawaida ni mkubwa kidogo katika kuhifadhi maliasili.

      Nenda Mikumi tu hapa mida ya saa mbili jioni uone jinsi nyama za swala, nyati, pofu nk zinavyouzwa hata kwa wapita njia na unaona wazi kuwa maaskari wanajua na wanapata mgao lakini ile sense kuwa wanyama wanaweza kutoweka haiko kabisa akilini mwao!
      “those who are so ready to take what is not theirs must be ready to loose what is theirs”

    17. #15
      posa's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th November 2010
      Posts : 28
      Rep Power : 438
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Quote By Ndekirhepva
      mimi huyu waziri sina imani na mchakato alioanza kuuchukua kwa vile, kama ilivyo desturi, kamati itaundwa na itafanya uchunguzi na majibu yatapatikana, sema sasa issue inakuja nani wakumfunga paka kengele??????
      tuliona akina ngeleja, ngeleja hakuanza kupingwa kwenye hili bunge la juzi, alipingwa tokea bunge la february, lakini kwa shinikizo ndio bosi wake amempumzisha ila jamaa anaendelea kula bata mtaani, so mi naona ni mbwembwe tu, kwani Kagasheki hajui kwamba huo mradi ni wawatu wakubwa????
      JK atakua anahusika sana tu,haiwezekani faru wameuawa alafu hakuna taarifa iliyowafikia watu
      Kama kadhamiria yeye mwenyewe ndio wa kumvika paka kengere. Tulimsikia Chami kuhusu suala la Mkurugenzi wa TBS, waziri anaweka visingizio kibao, mara hana uwezo wa kumsimamisha mpaka rais, mara ripoti haijafika kwangu, etc, mbona mwenzake hatukusia hayo ya rais aamue, mara alipoingia akachukua hatua.

      Kwa hiyo pia kama Kagasheki kadhamiria anatakiwa kuona mwisho wa jambo hili. Hasa tukinukuu maneno yake alipokuwa anaingia wizarai kwamba hatokuwa tayari kunyongwa yeye kabla hajamjonga mhusika.

    18. #16

      Na huo ndio utendaji tunaousbiri kwa muda mrefu, jambo linatokea hatua zinachukuliwa hapo hapo, sio visingizio kibao, mara haki za binadamu, mara tutashitakiwa, etc

    19. #17
      Olaigwanani lang's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th April 2012
      Posts : 337
      Rep Power : 818
      Likes Received
      52
      Likes Given
      375

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      ..MARA YA KWANZANZA KABISA WALIPOLETWA WATAALAM WA UHUFADHI WALIOMBWA WAPENDEKEZE NI WAPI WAWEKWE...WALIPENDEKEZA KATIKATI YA HIFADHI KWANI ITAKUWA NI VIGUMU KWA MAJANGILI KUPENYA NA KUHATARISHA MAISHA YAO..LAKINI SEREIKALI YETU ILIVO YA KINAFIKI..IKAWAPELEKA KULEE GURUMETI AMBAPO NI SEHEMU KARIBU NA VIJIJI VINGI VINAVYOZUNGUKA HIFADHI NA MIMI KAMA MHIFADHI WA ULINZI NINAJUA VIJIJI HIVO NI VIJIJI VYA MAJANGILI, CHAKUSHANGAZA NI KUWA SIJUI SERIKALI ILIKUWA INAOMBA USHAURI WA NINI MWANZONI WAKATI HAWATAKI KUFATA MAELEKEZO YA WAHIFADHI,NA HILI TUMEGUNDUA WANAPUUZA USHAURI HUKU WAKIFATA MASILAHI (INTEREST) ZA WALE MABWANA WENYE MAHOTELI MAARUFU YA KIFAHARI KULE GURUMETI..,ILI WAWAFANYIE BIASHARA ZAO KWA WATALII WAO...,KAMA MNAKUMBUKA SERIKALI ILIPUUZA USHAURI WA WATAALAM KUHUSU UJENZI WA SOPA LODGE TARANGIRE,SOPA LODGE NGORONGORO KWENYE UKUTA WA KRETA...HAYA MAMBO YAMEKUWA YAKIJITOKEZA SASA NA MADHARA YAKE NDO TUNAYAONA SASA..... HIVO MNATAKIWA MJUE KUWA SERIKALI HII HAIKO RADHI KUFATA USHAURI WA WASOMI WAKE..AMABAO WENGI WAO ILIWASOMESHA WAO ILI WAISAIDIE NCHI YAO LAKINI NDO HALI HALISI SASA ILIVO..... MWISHO WA YOTE NATAKA NITAHADHARISHE KUWA ITAKUJA KUBAKI HISTORIA TUU KWA WANYAMA WETU KWAMBA WALIKUWEPO.. (KWA KWELI SIASA NA UHIFADHI NI KAMA NYOTA NA BAHARI)kagasheki atakiwa ajue kuwa kuna hayo na ndoo aanze huko......badala ya chini
      Davie and Kindimbajuu like this.

    20. #18
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,489
      Rep Power : 6171
      Likes Received
      3059
      Likes Given
      1020

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Quote By Maundumula
      Hii inasikitisha sana, juzi juzi tulisikia mtu wa usalama na mtu wa serikali wamekamatwa wakinyemelea nyara za serikali. Hatujakaa vizuri faru wa JK nao wameuwawa wote na sisi hatujapata taarifa.

      Kumbe walikuwa wanasubiri JK aondoke eneo la tukio na ulinzi ukome hapo hapo! kweli hii nchi ni ya vilaza wa hali ya juu. Angalau kutupa information ya yaliyotokea hamna!. Sasa watatu convince vipi kama wao hawahusiki na mtandao huu wa ujangili hao vigogo wa TANAPA ? Si nilisikia hawa FARU waliwekewa vifaa maalum vya ku monitor popote pale walipo wanajulikana? kwanini wahusika hao wa usalama wa wanyama pori hawakuwa wanafuatilia nyendo zao? Sasa itabidi tutote tena another 7.5 Billion tununue FARU wengine kutoka SA!!!!
      Mkuu Maundumula sasa hao wanaoitwa game wakukamate na kakitoweo ka swala tu ndugu yangu umeisha! Kuna watu wamekula nyama ya swala ikiwa mbichi. Lakini kwa majangiri ati hawaonekani! Hawa TANAPA wana vifaa vya kisasa vya monitoring na hata ndge za patrol wanazo lakini Faru wanauawa.
      CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola.

    21. #19
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      huyu kagashek ni mtu hatari sana.....ni mla rushwa mkubwa na jizi lilokubuhu...hapo anataka kuinstall watu wake ili waanze kuiba sawa sawa
      Davie likes this.
      I'm Naturaly Evasive..

    22. #20
      Aswel's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 93
      Rep Power : 374
      Likes Received
      24
      Likes Given
      9

      Default Re: Faru wa JK wang’oa vigogo maliasili

      Safi sana wazembe lazima wawajibishwe, lakini tunaomba isiwe nguvu ya soda.

    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...