ally kombo, nimekusoma mkuu. Kwa bahati ninajua ninachokiongea maana nimepitia darasani. Hapo kwenye red ndipo pa kuanzia. Kumbuka kwenye post yangu nyingine nimesema Islamic Banking wanatumia mfumo wa
ku-share profit & loss, I hope unaelewa hili maana sio techinical. Sasa turudi hapo kwenye red; unajuwa ni kwanini Islamic Banking haikopeshi 'CASH?
Under Islamic banking ukitaka gari hawakupi cash, au ukitaka mkopo wa nyumba hawakupi cash, watanunua nyumba then wanapiga mahesabu na mnakubalina utalipa how much na kwa muda gani mtakaobaliana. Hivyo hayo makubaliano yanayofanyika between the bank and customer ni malipo ya hiyo nyumba (mortage) plus mgao wa faida (interest rate?). Kinachofanyika hapa ni kutotumia neno 'interest rate' lakini bado customer ana-incur cost, na ndio maana hapo kwenye blue bank wana-calculate before hand kujua faida ni kiasi gani ili mjadiliano marejesho yanayojumuisha mgao wa hiyo faida. Ni sawa na kusema bank wanakuwa 'partner' kwenye hiyo shughuli yako.
Kwenye kijani, kama nilivyosema ni kwa sababu ni mfumo wa ku-share profif & losss. Lakini bank sio wajinga, they are not there to make whatever loss ili wagawane na wateja! Vinginevyo wasingekuwa kwenye market.
Really, you have to seat down and analyse kwa makini ndio utaona ni jinsi gani hakuna tofauti. Kwa sababu mmoja (conventional banking) anakupa hela unalipia tenda yako lakini unarudisha mkopo plus interest rate (share ya profit). Huyu hataki kujua utapata faida au hasara kiasi gani. Take the money, do your thing but pay back with charges.
Lakini mwingine (Islamic banking) anakuwa involved moja kwa moja kwenye tenda yako, anailipia, anafanya mahesabu kujua faida, then mnagawana. Na ungeniuliza binafsi, hapa ukopeshaji chini ya Islamic banking ni kwamba bank inakuwa na uhakika zaidi kuhusu hela zake maana wanakukopesha baada ya kujua profit/loss. Wanakuwa part of whatever walichokukupesha.
Najua tunajadiliana mambo ya imani ambayo kusema kweli yanaweza kuwa very sensitive, lakini pia ni muhimu sote tukatambua maandiko ya vitabu vitakatifu either Quaran au bibilia vimeandikwa miaka mingi. Na wakati tunasoma inakuwa na maana zaidi kukumbuka context ya maandiko hayo kwa kutiliana maanani mazingira ya wakati huo. Kwa mfano, miaka 1,000 iliyopita, ni vigumu kumkopesha mtu usiyemfahamu, hujawahi kukutana naye, hujui anaishi wapi, huna uhakika anafanya nini. Katika mazingira kama haya, ukitumia taratibu za Islamic banking basi unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuhakikisha hela yako inarudi. Hata hizi conventional banking ukiangalia historia ya 'lending' huko nyuma mikopo ilikuwa under different set of rules. Science & technology imesaidia maana ni rahisi kwa bank kujua mteja anatoka wapi, anafanya nini na hata kufuatilia shughuli zake.
Follow Us Here