Chama cha wananchi (cuf) kimeandaa maandamano makubwa ya wakulima wa korosho tandahimba yatakayofanyika kesho tar-11/04/2012. Maandamano hayo yanalengo la kufikisha ujumbe kwa serikali kwamba wananchi wamechoka kusubiri ahadi zisizotekelezeka kuhusu malipo ya pesa za korosho ambapo serikali kupitia vyama vya ushirika ilikopa mwezi october mwaka jana. Maandamano hayo ni ya kisheria kwani wamepewa kibali na yataanzia ktk ofisi za cuf hadi ofisi ya mkuu wa wilaya tandahimba kesho saa 2 asubuhi.